Waislam Wauliza Wakristo

Swali la 1: Kwa nini mnaliamini Agano la Kale?

Jibu: Maandiko na elimukale (archaeology) vinaonyesha kuwa hakuna mabadiliko makubwa kwenye nakala za sasa kwa sababu angalau tano:

1. Mungu aliahidi kulinda neno lake katika Isaya 55:10-11; 59:21; 1 Petro 1:24-25, Mathayo 24:35. Hatima ya yote tunapaswa kuamini kuwa ama Mungu anaaminika au haaminiki. Lakini kama Muislam anaamini kuwa Mungu hakulinda neno lake katika Agano la Kale, na kwamba hakulinda neno lake katika Agano Jipya, ni kwa nini abadilishe na kulinda neno lake kwenye Kurani?

2. Yesu na Agano Jipya limethibitisha maandiko ya Agano la Kale katika Mathayo 19:4; 22:32,37; 39; 23:35; Marko 10:3-6; Luka 2:23-24; 4:4; 11:51; 20:37; 24:27,44

3. Ushahidi wa Elimukale: Kwenye Septuagint, Torati ilitafsiriwa kwenye Kiyunani/Kigiriki karibu mwaka 400 K.K. Hati toka Bahari ya Chumvi (Dead Sea Scrolls) yaliandikwa kuanzia karibu mwaka 100 K.K hadi baada ya Kristo, na tunaweza kuyalinganisha na Biblia zetu za leo. Tafsiri za Kiaremi (Aramaic Targums) zilitolewa karibu na muda Yesu alipokuwepo duniani. Maandiko toka Bahari ya Chumvi yana vipande karibu 95,000 kutoka kwenye nyaraka 867 zilizoandikwa kwa mkono za Agano la Kale na maandiko mengine. Karibu 1/3 ya nyaraka zilizoandikwa kwa mkono za Hati toka Bahari ya Chumvi ni nyaraka za Agano la Kale kwa mujibu wa NIV Study Bible uk.1432. Elimukale inaonyesha kuwa Biblia ambayo Yesu aliijua ilikuwa imehifadhiwa. Nahal Hever ni pango karibu na Engedi, ambalo lina kipande kilichoandikwa kati ya mwaka 50 K.K. na 50 B.K. cha Manabii Wadogo katika lugha ya Kiyunani. Huko Masada, kulikuwa na nakala ya kitabu cha Yoshua iliyoandikwa mwaka 169-93 K.K. Mafunjo ya Nash (Nash Papyrus), yaliyoandikwa mwaka 150 K.K., yana amri kumi. Hati ya wadi Muraba'at ya Manabii Wadogo iliandikwa karibu mwaka 132 B.K.

4. Waandishi wa kanisa la awali, kuanzia kama mwaka 97/98 B.K, walilitumia Agano la Kale mara nyingi sana. Angalia www.MuslimHope.com/Bible/ot.html kwa orodha ya angalau waandishi 15 wakristo hadi mwaka 258 B.K waliotumia Agano la Kale.

5. Waandishi wa Kiyahudi, ingawa walikuwa maadui wa ukristo, walilihifadhi Agano la Kale lile lile lililomo kwenye Biblia za kiprotestant za leo. Kipekee, waandishi wa kiyahudi Philo na Josephus walitumia Agano la Kale mara nyingi sana.

Kwa muhtasari, Mungu ni Mwenye enzi, ajuaye yote, na asiye na uzembe wa aina yoyote ile. Tunaweza kuamini kuwa ameweka muelekeo sahihi kwa wote wanaotafuta kumfuata kokote anakowaongoza.

 

Swali la 2: Je tunaweza kuliamini Agano Jipya?

Jibu: Ndiyo, kuna sababu tano zinazofanana na zile zilizotangulia, kuanzia na tumaini kuwa Mungu hataruhusu watoto wake wadanganywe kabisa, hadi kwenye ushahidi mkubwa wa nyaraka zilizoandikwa kwa mkono.

1. Mungu ameahidi kulinda neno lake katika Isaya 55:10-11; 59:21; 1 Petro 1:24-25, Mathayo 24:35. Tunaweza kumwamini Mungu.

2. Nyaraka za zamani zaidi zilizoandikwa kwa mkono zilizolindwa ni pamoja na:

100 B.K. uk.6 (kipande cha Luka)

117-138 B.K. John Rylands (Yohana 18:31-33,37-38)

100-150 B.K. Chester Beatty II (uk.45)

125-175 B.K. - Bodmer II (uk.66)

125-175 B.K. uk.104 (kipande cha Mathayo)

Zaidi ya nyaraka 30 zilizoandikwa kwa mkono zilizoandikwa kabla ya mwaka 300 B.K.

Nyaraka hizi za kale zinaonyesha vitu vitatu:

1. Uthibitisho wa ziada kuwa Agano Jipya lilisambazwa kwenye ulimwengu wote wa Rumi mapema sana.

2. Hakuna mabadiliko makubwa na maandiko tuliyonayo leo

3. Mafundisho ya msingi, kama vile uungu wa Yesu, nk. Kwenye Biblia zetu leo yalikuwepo kwenye Biblia za kale zaidi pia.

Tofauti na Uislam, kuna Kurani chache sana zilizohifadhiwa kabla ya kufanywa kuwa ya aina moja na 'Uthman. Hata moja ya hizi ina sura mbili pungufu ya Kurani za leo.

3. Idadi kubwa ya nyaraka zilizoandikwa kwa mkono zilizohifadhiwa ni pamoja na

Nyaraka 8 au zaidi zilizoandikwa karibu mwaka 300 B.K.

Jumla ya nyaraka 10,000 za Kiyunani

Nyaraka 14,000 za ziada kwenye lugha nyingine

Jambo hili linaonyesha vitu viwili:

1. Tunafahamu kabisa kila neno la Agano Jipya la awali kwa uhakika wa karibu 97.3%.

2. Hata 2.7% tofauti inaonyesha kuwa hapakuwa na mabadiliko ya muhimu yaliyoathiri mafundisho ya kikristo.

Tofauti na uislam, Bukhari, Sahih Muslim, al-Tabari, na Fihrist kwenye Sura na aya zilizokuwemo kwenye Kurani lakina hazipo tena sasa.

4. Waandishi wa kanisa la awali, walilitumia Agano Jipya sana. Kwa mfano, Clement wa Rumi, alipoandika mwaka wa 97/98 B.K, alitumia vifungu vingi vya kitabu cha Waebrania. Angalia www.MuslimHope.com/Bible/nt.html kwa orodha ya angalau waandishi 22 wa kikristo hadi mwaka 258 B.K. waliotumia na kunukuu vitabu vya Agano Jipya.

5. Hata waalimu wa uongo wanaunga mkono usahihi wa maandiko. Mmoja wa waalimu wa uongo wa kinostikia (Gnostic heretic) aliyeitwa Tatian (mwaka 170 B.K.) aliandika "ulinganifu" (a "harmony" of the gospels) wa injili, ambamo aliziweka zote pamoja. Aliziacha sehemu ambazo zilionyesha kuwa Yesu alikuwa mtu. Mwalimu wa uongo wa kiarian (Arian heretic) aliyeitwa Ufilas aliitafsiri Biblia kwenda kigothi karibu mwaka 250 B.K. Alikuwa na kila kichocheo cha kupunguza sehemu nyingi za Biblia zilizoonyesha mtazamo wa juu kuhusu Yesu, lakini hakufanya hivyo. Toleo la Ufilas ni tafsiri sahihi.

Kama angalizo la pembeni kwa Waislam, Sura 4:150-151 inasema, "Wale wote wanaomkana Mungu na wajumbe wake, na wanataka kumtenganisha Mungu na wajumbe wake, wakisema: 'Tunawaamini baadhi yao lakini tunawakataa wengine': na wanataka kuchukua msimamo wa nusu kwa nusu, (151) Si waumini kwa ukweli . . ."

Sura 3:48 inasema, "Na Mungu atamfundisha [Yesu] kitabu cha Hekima, , Torati, na Injili." Kama Yesu alifundishwa Agano la Kale, na tunalo Agano la Kale toka wakati wa Yesu, basi Yesu alifunzwa Agano la Kale tulilonalo.

Sura 3:50 inasema, "'(Mimi [Yesu] nimekuja kwenu), kuithibitisha Torati ambayo ilikuwepo kabla yangu. . . . Nimekuja kwenu na Ishara toka kwa Bwana wenu. Kwa hiyo mcheni Mungu na mnitii mimi."

Kama kila nakala ya Biblia ilikuwa potofu wakati wa Muhammad, je Mungu angewadanganya watu kwa kutoa hii Sura 5:47?

Sura 5:47 inasema, "Watu wa Injili na waamue kwa kutumia maneno ambayo Mungu amesema ndani yake . . ." Kama watu wa Injili wanapaswa kuamua kwa kutumia maneno ambayo Mungu ameyafunua kwenye Injili, je ni vipi Injili ambayo kwayo wanatakiwa kuamua isiwe Injili ambayo Mungu aliwaambia waamue kwayo?

Sura 5:48 inasema, "Kwenu (Watu wa Kitabu) tulituma maandiko kwa ukweli, tukithibitisha andiko lililokuja kabla yake, na kulilinda kwa usalama: kwa hiyo amueni kati yao kwa yale ambayo Mungu ameyafunua, na msizifuate tamaa zao zisizofaa, hata kwenda mbali na kweli iliyokuja kwenu . . ."

Sura 15:9-10 inasema "Tumetuma, bila mashaka, Ujumbe; Na tutaulinda kwa hakika [dhidi ya upotofu]. Tulituma wajumbe kwenu Miongoni mwa madhehebu ya zamani:" Sura 15:9 haisemi kwamba ni Kurani tu iliyolindwa, bali hata "ujumbe."

 

Swali la 3: Kwenye Mwanzo 16:1, kwa kuwa Abraham na Sarai hawakuwa na watoto, Abraham aliwezaje kuwa na watoto zaidi baada ya Isaka?

Jibu: Tunaweza kumwachia mwanahistoria wa kiislam al-Tabari (aliyekufa mwaka 923 B.K.) ajibu hili swali katika juzuu ya 2 uk.127: alisema kwamba Abram alioa tena na akawa na watoto wengi. Mwanzo 16:1 inaonyesha kuwa ni Sarai, si Abraham, aliyekuwa tasa. Kwa hiyo Abraham alikuwa na watoto zaidi, lakini Sarai hakuwa nao.

Kwa hakika Abraham alikuwa mtu wa kufurahisha. Aliishi kwenye tamaduni ambayo iliabudu miungu ya uongo, aliitwa na Mungu wa kweli kuondoka na kumfuata Yeye kwenda kwenye sehemu isiyojulikana, na Abraham aliacha kile alichokijua na kumfuata Mungu wa kweli. Watu wa dunia ya leo wanatakiwa kuwa tayari kufanya hivyo hivyo.

 

Swali la 4: Kwenye Mwanzo 16:1-4, kwa nini Abraham [kama inavyodaiwa] alizini na Hajiri?

Jibu: Hapana, Ishmael hakutokana na zinaa. Na kama kuwa suria ni zinaa, basi Muhammad naye alikuwa na Masuria. Mambo manne ya kuyazingatia katika kujibu swali hili.

Masuria waliruhusiwa: Kuoa mke zaidi ya mmoja kuliruhusiwa wakati wa Agano la Kale, na Sara alimtoa Hajiri kwa Abraham ili awe suria. Kwa hiyo jambo alilofanya Abraham liliruhusiwa na Mungu aliyejifunua kwake na baadaye kwenye sheria ya Musa, pia na sheria ya Mesopotamia ya wakati ule.

Mifano inayofanana na huo: Zaidi ya hayo, jambo hili halikuwa la ajabu kama linavyoweza kuonekana kwa baadhi ya wasomaji wa leo. Kwa mujibu wa Misemo Migumu ya Biblia uk.121-122, mifano inayofanana na huu wa kijakazi kuchukua nafasi ya mke mgumba inapatikana kwenye sheria za Hammurabi, vibao vya Nuzi, vibao vya Alalakh na vibao vya Mari. Lakini hata kama jambo linafanywa na watu wengi na ni "halali", haimaanishi kuwa linampendeza Mungu. Mwanzo 16:4-5 inaonyesha kuwa muda mfupi baadaye Sara alijuta kwa kitendo chake hicho.

Hajiri alijivunia hadhi yake: Zaidi ya hayo, Hajiri alipokuwa mke wa Abram hakukataa. Kwa hakika, Hajiri alijivunia ujauzito wake na kumdhihaki Sarai (Mwanzo 16:4,5). Ingawa kumuoa mateka kuliruhusiwa kwenye Agano la Kale, tendo la ndoa nje ya ndoa halikuwahi kuthibitishwa kuwa halali bali ni uovu mbaya.

Tofauti na hivyo, Waislam wanaruhusiwa kuwalazimisha mateka wao kufanya nao tendo la ndoa, japokuwa hawajaolewa nao. Tazama Bukhari Hadith juzuu ya 3 kitabu cha 34 sura ya 113 kabla ya na.437 uk.239; juzuu ya 3 kitabu cha 34 sura ya 111 na.432 uk.237 kwa maelezo zaidi. Pia mwanahistoria Muislam wa zamani al-Tabari juzuu ya 2 uk.72 anadai kuwa Sara alimruhusu Abraham kumuoa Hajiri.

Kwa muhtasari, Mungu ni mtakatifu, Abraham hakuwa mzinifu, na wakristo wana viwango vya juu zaidi vya utakatifu kuliko vile alivyokuwa navyo Muhammad kwa wafuasi wake kwenye Hadithi.

 

Swali la 5: Kwenye Mwanzo 22:1-18, je inawezekana kuwa mvulana ambaye Abraham alikaribia kumtoa kafara awe ni Ishmael, siyo Isaka, kama ambavyo Waislam wanadai? Vinginevyo, inawezekanaje Isaka awe "mtoto pekee wa kiume" wa Abram?

Jibu: Ni Isaka aliyetolewa kafara na si Ishmael kwa sababu angalau nne:

Hata Kurani haisemi kuwa alikuwa ni Ishmael: Mwanzo 22:2 inasema alikuwa ni Isaka. Kwa Waislam, ingawa Kurani ya kiislam inazungumzia jambo hili kwenye Sura 37:99-111, hakuna sehemu yoyote kwenye Kurani nzima inayosema kuwa huenda alikuwa Ishmael au Isaka. Kwa hakika, wanazuoni wengi wa awali wa kiislam walifundisha kuwa alikuwa ni Isaka, wakati wengine walifundisha kuwa alikuwa ni Ishmael. Tazama al-Tabari juzuu ya 2 uk.68. al-Tabari juzuu ya 2 uk.82-97 inasema mabingwa 16 wa kiislam walisema kuwa ni Isaka wakati mabingwa 23 wa kiislam walisema kuwa ni Ishmael.

Abram alikuwa na mtoto mmoja tu wa kiume wakati ule: Ishmael alikuwa na miaka 14 wakati Isaka alipozaliwa. Hajiri na Ishamael walifukuzwa na kwenda sehemu nyingine Isaka alipoachishwa kunyonya kwenye Mwanzo 21:8-10. Abraham alijaribiwa "kwa muda mrefu" baada ya hapo kwenye Mwanzo 21:34, na "mtoto wa kiume" alikuwa kwenye meza ya kutolea kafara kwenye Mwanzo 22:12.

Mrithi pekee: Isaka alikuwa mirthi pekee, na mtoto pekee wa kiume, pia inamaanisha "mtoto wa kiume mpendwa". Ingawa utamaduni wa wakati ule uliruhusu watu kuwa na masuria kwa ajili ya kupata watoto, urithi na haki ya mzaliwa wa kwanza vilienda kwa watoto wa kiume wa mke halisi, siyo watoto wa kiume wa masuria. Tazama Mambo Magumu kwenye Biblia na Mambo Yanayoonekana Kupingana uk.141 kwa maelezo kamili.

Mwana pekee wa ahadi: Mwanzo 21:12 inasema, "katika Isaka uzao wako utatajwa." Abraham alikuwa na watoto wengine pia wa kiume, lakini walizaliwa baada ya ahadi hii.

 

Swali la 6: Kwenye Mwanzo 32:24-30, je Mungu wa Wakristo ni mnyonge sana hata anachukua usiku mzima kupigana mieleka na Yakobo?

Jibu: Kwanza kabisa alikuwa ni malaika wa Mungu (ambaye Yakobo alimwita mtu), siyo Mungu mwenyewe aliyepigana naye mieleka. Yakobo alisema kuwa amemwona Mungu uso kwa uso, lakini Yakobo alikutana na Mungu kupitia malaika. Hata bila kujali hilo, Mungu alimtuma huyu malaika, ambaye alikuwa na nguvu yakumwangamiza Yakobo.

Kama baba anapigana mieleka na mtoto wake wa miaka miwili mwenye msimamo wa nguvu, na hata kama atamwacha ashinde wakati mwingine, hiyo haitamaanisha kuwa yeye ni baba mnyoge. Kwa namna hiyohiyo, lengo la Mungu lilikuwa ni kupambana na usumbufu wa Yakobo, siyo kumwondoa Yakobo au ung'ang'anizi wake. Mungu alitaka kumfanya Yakobo ajue yeye ni nani, siyo kumuua.

Fikiri ingekuwaje kama mwili wako ungekuwa hivyo hivyo ila uwe na nguvu mara 100 zaidi. Ungeweza kufanya vizuri sana kwenye michezo, kuvunja kuta, na kukimbia haraka sana. Lakini kila unapojaribu kuchuma ua unalivunja, kila unaposhika mkono wa mtoto mdogo unauvunja, na kila unapomshika mwenzi wako inabidi apelekwe hospitali. Huenda kuwa na misuli yenye nguvu mara 100 si jambo jema kabisa.

Mungu ni mwenye nguvu zote, lakini pia ana upole na mwenye maarifa. Mungu ana nguvu mara nyingi zaidi zisizohesabika kuliko sisi, lakini anaweza kuthibiti nguvu zake kuliko tunavyofanya sisi. Zefania 3:17 (NIV) inatupa mfano wa upole wa Mungu: "Bwana, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa; atakushangalia kwa furaha kuu, atatulia katika upendo wake. Atakufurahi kwa kuimba."

Katika 1 Wafalme 19:11-13 Mungu anamwambia Elia atauona uwepo wa Bwana. Haukuwa kwenye upepo mkali, tetemeko la nchi, au moto, bali kwenye sauti ndogo ya utulivu.

Kwa muhtasari, Wakristo wanamwabudu Mungu ambaye ni mpole lakini pia Mwenye nguvu zote.

 

Swali la 7: Kwenye Kutoka 19:11, Mlima Sinai ulikuwa Maka, kwa sababu Gal 4:25 inasema ilikuwa Arabuni?

Jibu: Mlima Sinai upo kwenye rasi ya Sinai; isipokuwa Musa angekuwa na magari makubwa au matreni, Maka pangekuwa mbali mno. Mambo manne ya kuzingatia katika jibu hili.

1. Haidhuru: Kama Mlima Sinai ungekuwa Maka, pasingekuwa na tofauti yoyote kwa Wakristo, isipokuwa hatua za safari za Waisraeli zisingeeleweka. Hata hivyo, inaonekana kuwa ingekuwa muhimu kwa baadhi ya Waislam kwani kungelifanya wazo la kuwa Maka ilishiriki kwenye kazi ya Mungu kabla ya Muhammad la kuaminika. Hata hivyo, Waislam wengine, kama rejeo chini ya ukurasa 2504 kwenye Kurani Takatifu: Toleo la Kiingereza la Maana na Ufafanuzi (Holy Quran: English Translation of the Meanings and Commentary) linalinganisha Mlima Sinai na Jabal Musa, sawa na wengi wa Wakristo.

2. Arabuni tofauti: Katika Wagalatia 4:25 "Arabuni" si nchi ya leo ya Kiislam ya Saudi Arabia, bali jimbo la Kirumi la Arabuni. Jimbo la Kirumi la Arabuni lilikuwa ni rasi ya Sinai, sehemu ya kaskazini magharibi ya Jordan ya leo, na sehemu ndogo ya Syria. Tazama ama The Roman World uk.107 au Encyclopedia Britannica sehemu ya Historia ya Rumi ili kuiona ramani inayoonyesha hili. Kama rejeo la pembeni, Warumi hawakuwahi kutwaa sehemu ya karibu na Maka , kwa hiyo jimbo la Kirumi la Arabuni halingeweza kuhusisha Maka.

3. Siyo Maka: Watu wenye kondoo na ng'ombe wangeweza kutembea maili 6 tu kwa siku; hata kama wangekuwa na ngamia tu kwa kawaida wangeweza kwenda maili 12 kwa siku. Safari ya siku 11 umbali wa karibu maili 800 kutoka Maka kwenda Kadesh Barnea kwa miguu, pamoja na ng'ombe na kondoo, na watoto wadogo, ingekuwa ya kasi kubwa sana, isipokuwa kama wangekuwa na magari wakati huo. Tazama ama The Roman World uk.107 au Encyclopedia Britannica sehemu ya Historia ya Rumi ili kuona ramani.

4. Kwenye Rasi ya Sinai: Rasi ya Sinai ni pembetatu inayotazama kusini yenye milima upande wa kusini ambayo Kutoka 19:2 na Hesabu 3:14; 9:1,5; 10:12 vinaiita Nyika ("Jangwa") la Sinai. Jangwa la Sin linaitenganisha Elim na Sinai. Hesabu 33:3-50 inataja kila sehemu walipopiga kambi Waisraeli. Kwa bahati mbaya hatujui maeneo ya sehemu hizi za kambi, lakini kwa kuziangalia, tunaweza kuona ipi ipo kati ya wapi.

Ndani ya nyika ya Sinai, kuna milima miwili iliyo karibu karibu, yenye kulingana na mlima Sinai.

Gebel Musa/Mousa (futi 7,363) Haya ni maoni yaliyotokea zamani, angalau kuanzia karibu mwaka 500 B.K. Ina miteremko mirefu sana. Nyumba kubwa ya utawa ya Mt. Catherine ipo sehemu ya chini ya mlima huu. Wengi wa Waislam, lakini siyo wote, wanaona kama huu ndio mlima Sinai pia. New International Dictionary of the Bible uk.674 ina picha ya Jebel Musa.

Ras es-safsafeh (futi 6,540 mita 1993) ipo maili mbili (km 3.2) kaskazini mwa Gebel Musa kwenye mgongo huo huo. Ina uwanda mpana chini.

Gebel Serbal (haielekei kuwa hivyo): Eusebius (mwaka 325 B.K.) alidhani hivi. Lakini New Bible Dictionary (1978) uk.1193-1194 inaeleza kuwa hakuna nyika karibu na sehemu yake ya chini.

Kwa muhtasari, wakati ambapo Wakristo na hata baadhi ya Waislam wanaafiki kuwa mlima Sinai upo Sinai, tunaweza kuwa karibu na Mungu sehemu yoyote ile, na hatuhitaji mahali maalumu, sanamu za vyuma, au hata mawe meusi ili kuweza kuwa karibu naye.

 

Swali la 8: Kwenye Hesabu 36, kwa nini [inadhaniwa] wanawake hawakuweza kurithi kwenye Biblia? Kwenye uislam, kwa mfano, mabinti wanayo haki ya kurithi.

Jibu: Mambo manne ya kuzingatia katika jibu hili.

Kwenye Biblia, mabinti wa Selofehadi walirithi toka kwa baba yao. Jambo hili lilikuwa sahihi na lenye kufaa kama mapenzi ya Mungu, kwa mujibu wa Hesabu 27:7-8. Pia Hesabu 36:8 inasema kwa wakati ujao wa kila binti atakayerithi ardhi, kwa hiyo waliweza kurithi. Mabinti wa Ayubu walirithi pia kwenye Ayubu 42:15.

Urithi unaoenda toka kabila moja hadi jingine kwenye Hesabu 36:9 ndilo jambo linaloongelewa hapa, siyo mafanikio ya mabinti wa Selofehad.

Azimio likawa mabinti warithi ardhi, ila walitakiwa kuolewa kwenye kabila la Manase. Baadaye, wanawake wote waliorithi ardhi walitakiwa kuolewa na watu wa kabila lao.

Katika Agano Jipya, 1 Petro 1:3-4 inaonyesha kuwa watu wote wanaoamini wana urithi muhimu zaidi kuliko yote, urithi wa mbinguni uliowekwa kwa ajili yetu.

Kama rejeo la pembeni, katika uislam wa kweli mabinti walipata nusu tu ya urithi wa kaka zao. Sura 4:11 inasema, "Allah (kwa hiyo) anakuagiza kuhusiana na (urithi) wa watoto wako: kwa mtoto wa kiume, sehemu iliyo sawa na ile ya watoto wawili wa kike . . ." (Tasfiri ya Yusef Ali uk.209).

Kwa ufupi, kwa kuwa Hesabu 36:8 inaongea kuhusu mabinti kurithi ardhi, na Hesabu 27:7-8 inaongea kuhusu urithi wa mabinti kwa jumla, itakuwa kinyume cha Agano la Kale kutowaruhusu mabinti kurithi. Wagalatia 3:28 inasema kuwa hakuna mwanaume au mwanamke ndani ya Yesu, na katika sehemu zilizobaki za Biblia, Agano la Kale na Jipya, hakuna kitu kinachozuia haki ya urithi ya mwanamke, au ya nafasi za kiuchumi kwa ujumla. Kinyume na uislam, wanawake katika ukristo wana matumaini ya mbinguni sawa na wanaume.

 

Swali la 9: Katika Kumbukumbu 18:17-18; 33:1-2, na 34:10-11, ni Muhammad aliyetabiriwa hapa, kama baadhi ya Waislam wanavyodai?

Jibu: Kumbukumbu 18:15-18 inasema Mungu atamwinua nabii, kuwa watamsikia, kama Musa kutoka miongoni mwao, miongoni mwa ndugu zao. Je Yesu alikuwa nabii? Je Wayahudi walio wengi walimsikia Yesu? Je Yesu alikuwa mmoja wa Wayahudi? Je Yesu alikuwa Myahudi? Waislam wanapaswa kutokuwa na shida kuafiki kuwa mistari hii inamfaa Yesu kuliko Muhammad. Kama angalizo la kihistoria, kabla ya Nicea Archelaus (262-278 B.K.) pia alizungumzia jinsi ambavyo Kumbukumbu 18:15 isivyoweza kuwa inamwongelea mtu mwingine yoyote yule isipokuwa Yesu Kristo kwenye Disputation with Manes sura ya 43 uk.219.

Yafuatayo ni maoni zaidi.

a. Kumbukumbu 33:1-2 inasema "Bwana", na Waislam hawamwiti Muhammad Bwana wao. (Waislam wa 'Alawite na makundi mengine ya Ghulat wanamchukulia Muhammad kuwa Mungu, lakini maoni hayo siyo kawaida kwa Waislam.)

b. Kumbukumbu 34:10 kwamba "Wala hakuinuka tena katika Israeli nabii kama Musa." Wasifu huu uliandikwa, huenda na Yoshua, muda mrefu kabla Yesu hajaja.

c. Kumbukumbu 34:10 inasema "uso kwa uso", na Muhammad hajawahi kusema kuwa alipata maneno yake moja mwa moja kutoka kwa Mungu, bali kupitia malaika (Sura 2:97). Yesu aliwasiliana moja kwa moja na Mungu Baba kwa mujibu wa Yohana 1:18 na vifungu vingine.

d. Mstari unaofuatia, 34:11, unasema kuwa hakuna nabii mwingine yoyote aliyefanya miujiza hiyo mikubwa kama Musa. Muhammad, kama ilivyoandikwa kwenye Kurani (Sura 17:90-93) hakuwahi kufanya miujiza kama hii, isipokuwa kusema Kurani. (Kurani inapingana na jinsi mapokeo ya baadaye ya Hadithi yanavyosema.)

e. Kwenye Kurani yenyewe, Sura 29:27 inasema unabii umekuja kupitia Isaka na Yakobo. Kwenye tafsiri ya Yusuf Ali ya Kurani, anasema, "Na tumewapa (Abraham) Isaka na Yakobo, na tumeagiza miongoni mwa wazao wake unabii na ufunuo . . ." Wakati ambapo mabano kwenye jina la Abraham yapo kwenye tafsiri ya Yusuf Ali, neno lote "Abraham" halimo kwenye Kurani ya Kiarabu, na Yusuf Ali aliona haja ya kuongeza neno "Abraham" kwenye maandiko ambayo Waislam wanayaona kuwa ni neno la Mungu.

f. Mwisho, Petro, mtume wa Yesu, alisema andiko hili lilitimia kwa Yesu kwenye Matendo 3:22-26. Mtume Petro alikuwa na nafasi kubwa sana ya kuweza kujua jambo hili.

1. Ama, Yesu alifanya makosa ya kumruhusu mtu mwongo kama Petro kuwapotosha watu, kwa kwa karibu miaka 2,000, ambao wamekuwa wakijaribu kumfuata Mungu, na Mungu hakuinua kidole kuwaambia watu ukweli.

2. Au, Yesu alijua alichokuwa anafanya wakati alipomchagua Petro, na Mungu hakusahihisha kitu ambacho hakikihitaji masahihisho yoyote yale.

3. Vinginevyo, Petro hakusema hivyo, na kitabu cha Matendo ya Mitume kilipotoshwa kabla ya maelezo ya maneno hayo ya kwanza tuliyo nayo toka nje ya Biblia yanayoturejesha kwa Yesu, karibu mwaka 138 B.K.

Viongozi wa awali wa kanisa walisema kuwa mstari huu ulimwongelea Yesu. Baadhi yao ni

Justin Martyr 138-165 B.K.

Irenaeus 182-188 B.K.

Tertullian 220-220 B.K.

Origen 225-254 B.K.

Chrysostom 407 B.K.

Justin Martyr alizaliwa karibu mwaka 114 B.K., ingawa watu wengine hudhani mwaka 110 B.K. Apology yake ya kwanza iliandikwa kati ya mwaka 138 B.K. na mwaka 165 B.K. wakati wa kifo chake. Ni dhahiri kuwa alitakiwa kusoma unabii huu unaomwongelea Yesu kabla ya kuandika.

Muislam anaweza kusema kuwa Justin hakukosea tu bali pia manuscripts zote za Agano Jipya ziliunukuu usemi wa Petro kimakosa.

Pia, tafsiri kwenye lugha nyingine zilifanywa mapema sana; tarehe za hapo juu si za tafsiri za kwanza, bali ni tarehe za manuscripts za zamani zaidi ambazo zipo leo hii. Hizi zinaaminika kwa sababu zimepita kwenye mtiririko huru ambao watu wanaweza kuutumia kuthibitisha manuscripts za Kiyunani. Mtiririko wote wa manuscripts hizi, kutoka Afrika kwenda Asia, unaafiki kuwa Petro alisema hivi akimwongelea Yesu.

Tazama When Cultists Ask uk.43-44,45-46 na When Critics Ask uk.125-126, uk.131-132, na uk.133 kwa habari zaidi.

 

Swali la 10: Kwenye 1 Sam 1:2; Mwa 16:2; 25:1; 29:23-24;28-29, 2 Sam 20:3, nk., kwa nini Mungu aliruwahusu Abraham, Yakobo, Daudi na watu wengine kuoa wake wengi?

Jibu: Mambo manne ya kuzingatia kwenye jibu hili.

1. Kuoa wake wengi haukuwa mpango kamili wa Mungu, kama ilivyodokezwa wakati alipowaumba Adam na Hawa. Alisema wawili (siyo wengi) watakuwa mwili mmoja.

2. Mungu aliruhusu vitu kama talaka (Mathayo 5:31-32; Mark 10:2-12), kwa sababu mioyo yao ilikuwa migumu. Baadhi ya vitu, kama kuoa wake wengi na viapo vya haraka haraka, Mungu aliwaachia watu kutambua kuwa havikuwa vyema.

3. Hata katika nyakati za Agano Jipya, kuoa wake wengi hakukuwa kwa kawaida sana. Kuna mifano kumi na tano tu ya Agano la Kale mpaka wakati wa Suleiman, na minne au mitano baada ya muda huo.

4. Kuanzia wakati wa Paulo, na leo, wazee wa makanisa na mashemasi wacha Mungu hawatakiwi kuwa na mke zaidi ya mmoja (1 Timotheo 3:2,12; Tito 1:6).

 

Swali la 11: Kwenye 1 Sam 13:14, Daudi angewezaje kuwa mtu anayeupendeza moyo wa Mungu, kwani baadaye Daudi alifanya dhambi kubwa sana?

Jibu: Swali hili ni kwa Waislam na Wakristo pia, kwa sababu Kurani pia inamwelezea Daudi kuwa nabii wa kweli. Lakini, ingawa wengi wa Waislam wanafikiri kuwa manabii wote, akiwemo Daudi, hawakuwa na dhambi, Biblia inaonyesha kuwa Daudi alifanya dhambi kiasi kikubwa tu. Daudi aliupendeza moyo wa Mungu, si kwa sababu hakuwahi kufanya dhambi, bali kwa sababu, alipotokea kufanya dhambi alitubu. Waislam pia wanaamini kuwa Adam alikuwa nabii, na ni kweli kwamba Adam alianguka dhambini wakati alipokiuka agizo la Mungu na kula tunda la mti.

 

Swali la 12: Kwenye 1 Sam 25:4-35, Daudi alikuwa [kama inavyodaiwa] anatafuta kulinda ili kujipatia mali kwa njia ya ulaghai?

Jibu: Hapana, ila mwenye kuuliza swali atakuwa sahihi ikiwa hatataka kufuata dini ambayo nabii na viongozi wake walinufaika kwa kuwalinda walaghai. Mambo manne yanafaa kuzingatiwa katika jibu.

1. Daudi hakuwa anatafuta kulinda ili kujipatia mali kwa njia ya ulaghai, kwa vile Daudi, yeye aliyekuwa analinda watu wengine, alikuwa anatoa mali kwa wale aliokuwa anawalinda, kama alivyofanya kwenye 1 Samuel 30:26-31.

2. Daudi hakumwomba Nabal 1) malipo ya mara kwa mara, au 2) dhahabu, au kitu chochote cha thamani. Daudi aliomba tu chakula chochote ambacho Nabal angeweza kuwa amehifadhi. Nabal hakulalamikia ombi lolote la hela au vitu vya thamani. Badala yake, 1 Samuel 25:11 inaonyesha kuwa Nabal alifahamu ombi hili kuwa ni la mkate, maji na nyama tu.

3. Daudi alikiri baadaye, kwa masikitiko, angekuwa ametenda uovu kama angemuua Nabal na watu wake, kwa mujibu wa 1 Samuel 25:13,33-34, 39.

4. Daudi hakuchukizwa na Nabal kwa kuwa alikiuka makubaliano yoyote ya ulinzi. Badala yake, Daudi alichukizwa na majibu yake ya dharau kwenye 1 Samuel 12:10-11.

Tofauti na hivi, Waislam toka wakati wa Muhammad na kuendelea wamekuwa na kodi maalum kwa Wakristo na Wayahudi tu (na hata Wazoroastria/Wamagia) inayoitwa Jizya. Kwa mujibu wa Bukhari Hadith juzuu ya 2 uk.7, kwenye farahasa, Jizya ni "Kodi ya kichwa iliyowekwa na Waislam kwa watu wa Maandiko na watu wengine wenye kitabu kilichofunuliwa (wasio Waislam) wakati walipokuwa chini ya utawala wa kiislam." Waislam hata wanasema kuwa Wakristo na Waislam na Wayahudi wanapaswa kushukuru kuwepo kwa Jizya, kwa sababu bila hiyo, hawangekuwa na haki ya kuishi kwenye nchi za kiislam bila kuuawa.

 

Swali la 13: Kwenye 1 Fal 11:1-3, kwa nini Suleiman alikuwa na wake 700 na Masuria 300, kinyume cha amri ya Mungu ya kwenye Kumb 17:17?

Jibu: Kumbukumbu 17:17 inasema mfalme asiwe na wake wengi, na kwa kitendo hicho, Suleiman alifanya dhambi. Kuoa wake ilikuwa ni njia ya kuimarisha ushirikiano na falme nyingine, lakini pia ilikuwa ni makosa kutokumtii Mungu. 1 Fal 11:1-4 inasema kuwa Suleiman alifanya dhambi kwa kuoa hawa wake wageni, na kuugeuzia moyo wake kuwa mbali na Mungu.

Hard Sayings of the Bible uk.229 inalitumia jambo hili kwa njia ya kupendeza sana. Ingawa Suleiman angeweza kuweka viwango vya juu kama mfano, alianza kujiona kama hana haja ya kuzuiliwa na Mungu kwa njia hii. Leo hii kama kiongozi wa kikristo anajiona kuwa hayumo kwenye mipaka ambayo Mungu ameiweka kwa Wakristo wa kawaida, kiongozi huyu atakuwa kwenye shida kubwa sana ya kiroho. Kwenye Kurani, hakuna mwanaume anayeruhusiwa kuwa na zaidi ya wake wanne, isipokuwa Muhammad tu, ambaye alitokea kuwa na wake karibu 15 baada ya Khadija, na Masuria wawili.

Zaidi ya hayo, Muhammad na Waislam wengine walikuwa na wasichana mateka na watumwa, na Kurani inawaruhusu Waislam kufanya tendo la ndoa na wanawake ambao wanawamiliki kwa nguvu ya mikono yao. (Sura 4:24; 23:5-6; 70:29-30; 33:50,52 Abu Dawud juzuu ya 2 na.2150 uk.577)

 

Swali la 14: Kwa nini Wakristo wanakula nyama ya nguruwe wakati ambapo Biblia yao wenyewe inasema kuwa wasile?

Jibu: Kwa nini kuzungumzia nguruwe tu? Agano la Kale linazuia kula nyama ya nguruwe, nyama ya ngamia, kamba wadogo, na vitu vingine. Hata Muhammad aliruhusu kula nyama ya ngamia (Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 na.261 uk.162 na sehemu nyingine), hata kwa kutambua kuwa Wayahudi hawakupaswa kuwa wanakula nyama ya ngamia (Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 14 na.524 uk.333). Yesu alitangaza kuwa vyakula vyote ni safi kwenye Marko 7:14-15. Muhammad alijaribu kubatilisha utanguzi ambao Yesu aliuweka kuhusu nyama ya nguruwe, lakini alipenda ngamia.

 

Swali la 15: Kwenye 2 Fal 2:23-25, kwanini Elisha, nabii mkubwa aliyechukuliwa na kupelekwa mbinguni moja kwa moja, aliwafanya dubu wawaue watoto 40 kwa sababu hakutaka aitwe 'mwenye upaa'?

Jibu: Mambo matatu ya kuzingatia kwenye jibu.

1. Elisha hawajabiki na dubu; dubu walitumwa na Mngu.

2. Neno la kiebrania lililotumiwa hapa kwa "vijana" linaweza kumaanisha watu wenye umri wa hadi miaka 20 hivi. Yusufu alikuwa "kijana" kwenye Mwanzo 37:2, sawa na askari wa jeshi la Abram kwenye Mwanzo 14:25.

3. Makundi ya uhalifu ya vijana yaliweza kuwa na ukatili wakati ule sawa na leo hii.

 

Swali la 16: Je Zab 45:3-5 inamwongelea Muhammad, kama baadhi ya Waislam wanavyodai?

Jibu: Hapana, hata Waislam hawawezi kusema hivi, isipokuwa baadhi yao wa dhehebu la Ghulat, ambalo wanafikiri kuwa Muhammad ni Mungu. Zaburi 45:6 inasema, "Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele." Licha ya Muhammad kutokudai kuwa Mungu, Muhammad hakuwahi kuwa na kiti cha enzi au fimbo ya kifalme.

 

Swali la 17: Kwenye Isa 21:7, anayepanda "punda" ni Yesu, na anayepanda "ngamia" ni Muhammad?

Jibu: Hapana. Mambo matatu ya kuzingatia katika jibu hili.

1. Hawa walikuwa ni wajumbe wa wakati ule waliokuja kutoa taarifa kuwa Babeli imeanguka. Kitu pekee cha maana labda ni kwamba wapanda ngamia walikuwa wapelelezi, wapanda punda walikuwa raia wa kawaida, na waendesha magari yaliyokuwa yanakokotwa na wanyama walikuwa askari.

2. Pia askari Wamidiani waliokuwa waovu walipanda ngamia, lakini jambo hili halina maana yoyote sawa na kuongelea kuhusu Muhammad hapa.

3. Mwisho, hao walikuwa wapanga ngamia (uwingi), hivyo hata kama mmoja wao alikuwa Muhammad, hii ingemaanisha kuwa mpanda ngamia mwingne angekuwa anakuja baada yake.

Hakuna maana yoyote kujaribu "kuchuja mbu na kumeza ngamia" kwa kujaribu kutumia mstari huu kuonyesha kufanana na uislam wakati ambapo kuna vitu vingi sana kwenye Biblia (Ubaba wa Mungu, Utatu Mtakatifu, kuokolewa kwa neema, Roho Mtakatifu, nk.) ambavyo vinapingana na uislam.

Tazama vitabu vya When Cultists Ask uk.79 na When Critics Ask uk.269 kwa maelezo zaidi.

 

Swali la 18: Je Hab 3:3 inaweza kuwa utabiri kuhusu Muhammad?

Jibu: Ni baadhi ya Waislam Waghulat tu wanaoweza kufikiri hivyo, kwa sababu mstari huu unamwongelea "Mungu", siyo "Muhammad." Baadhi ya Waislam wa madhehebu ya Ghulat wanaamini kuwa Muhammad ni Mungu, ingawa jambo hili ni upotofu kwenye masikio ya Waislam Wasuni. Hata hivyo, endapo Waislam Wasuni wenyewe wangejiuliza swali hili kwa uzito kabisa, wangetakiwa kuamini kuwa Muhammad ni Mungu, kwa sababu "Mungu alitoka Teman".

Sababu nyingine za kuonyesha kuwa mstari huu hauwezi kuwa unaongelea kuhusu Muhammad, ni kwamba "Sifa yake" hazielekei kwa Muhammad, kwani sifa ni ya Mungu." Mlima Paran ni mahali ambapo Waisraelii walipiga kambi, na ni mbali na Maka. Kitabu cha When Cultists Ask uk.89 kinatoa jibu hili hili kwa ujumla. Tazama kitabu cha When Critics Ask uk.315 kwa maelezo zaidi.

Mwisho, baadhi ya Waislam wametokea kupendelea kutafuta muendelezo kati ya Muhammad na Biblia, kama palivyo na muendelezo kati ya Yesu na Masihi aliyeahidiwa kwenye Agano la Kale. Hata hivyo, baadhi ya Waislam wanatafuta muendelezo huu sehemu ambazo hazina uelekeo kabisa, Habakuki 3:3, katika kutafuta kitu cha kutabiri kuhusu Muhammad.

 

Swali la 19: Je kwenye Injili, ni kweli kuwa Yesu alikufa msalabani, au Mungu alimweka mtu mwingine kwa njia ya miujiza na bila kufahamika kama ambavyo Kurani ya kiislam inavyodai kwenye Sura 4:157-158?

Jibu: Hii ni tofauti ya msingi kati ya uislam na ukristo.

Wakristo wanasema alikuwa Yesu halisi kwa sababu maelezo yote ya kikristo na yasiyokuwa ya kikristo yanasema kuwa alikuwa ni Yesu. Allah wa Waislam ni tofauti na Mungu wa kwenye Biblia, na Allah amewadanganya na kuwafanya watu wake wajinga kwa kuwafanya wafikiri kuwa Allah alimweka mtu mwingine.

Waislam wanasema Allah ni Mungu yule yule wa kwenye Biblia. Kitendo cha Allah cha kumbadilisha Yesu hakingeweza kutambuliwa na mtu yoyote, na kwa ajili hiyo kusingeweza kuwepo ushahidi wowote wa kihistoria wa jambo hilo.

Wote (Wakristo na Waislam) wanaweza kukubali kwamba kuna wakati mmoja ambapo Allah wa Waislam aliwadanganya kwa makusudi na kuwafanya watu wote wa Allah mwenyewe kuwa wajinga.

 

Swali la 20: Kwa kuwa Mungu hana mwili, Yesu anawezaje kuwa Mwana wa Mungu?

Jibu: Wakristo HAWAAMINI kuwa Yesu alikuwa Mwana wa Mungu kwa maana ya kimwili au kingono. Badala yake, neno hili ni kielelezo cha maana ya kina ya jinsi Yesu alivyokuwa tofauti na viumbe vyote vilivyoumbwa. Waislam wa madhehebu Shia wana dhana inayofanana na hiyo kiasi. Wanaposema 'Ali ni kidole cha Mungu, hawaamini kuwa Mungu ana vidole kumi kama watu. Badala yake, hiki ni kielelezo chenye maana kubwa zaidi kwao.

 

Swali la 21: Kama Yesu si kiumbe kilichoumbwa, anawezaje kutokana na Mungu?

Jibu: Kutokana kunamaanisha "kutokea toka kwa" bila ya kuumbwa, sawa kidogo na Waislam wengi wanavyoamini Kurani kuwa imetoka kwa Mungu lakini haikuumbwa. Kabla ya mwanzo wa wakati, Yesu, ambaye pia anaitwa Neno la Mungu, alitoka kwa Mungu Baba. Kwa hiyo, kwa njia tofauti, Waislam na Wakristo wanasema kuwa Neno la Mungu lilitoka kwa MUngu lakini halikuumbwa.

 

Swali la 22: Kwenye Mt 5:17 na Matendo 10:10-16, kwa kuwa Yesu alisema hatatangua kitu chochote kwenye sheria, kwa nini Wakristo hula nyama ya nguruwe na hawazifuati sheria za vyakula za Agano la Kale kama Waislam wanavyodai kufanya?

Jibu: Ingawa si Wakristo wala Waislam wenye kuzifuata sheria za vyakula, Wakristo hawafanyi hivyo kwa sababu wanamsikiliza Yesu. Mambo matano ya kuzingatia kwenye jibu hili.

Wakati huu, wafuasi wa Yesu walizifuata sheria za vyakula za Agano la Kale. Yesu alisema kuwa sheria haitapita kabisa mpaka itakapotimizwa yote.

Ukweli wa ufufuko wa Yesu, umebadilisha kimsingi njia ambayo Mungu anashughulika na watoto wake. Malaika alimtaarifu Petro, mwanafunzi wa Yesu, kuwa Mungu alivitakasa vyakula vyote kwenye Matendo 10:9-16. Angalia kuwa mstari huu hausemi kuwa wanyama wote walikuwa safi siku zote, lakini kuwa Mungu amewatakasa.

Hata Waislam wanaobishia jambo hili, wao wenyewe wanapaswa kukubali kuwa baadhi ya sheria za vyakula za Agano la Kale hazipaswi kufuatwa. Waislam wanaona kuwa wanaweza kula nyama ya ngamia (na Muhammad alifanya hivyo), lakini Walawi 11:3-8; Kumbukumbu 14:6-8 vinazuia kuila. Muhammad pia alisema inaruhusiwa kula mafuta. Ibn-i-Majah juzuu ya 4 na.3274 uk.437, lakini Ibn-i-Majah juzuu ya 4 na.3383 uk.495 inasema kwamba Muhammad alijua kuwa Wayahudi hawaruhusiwi kula mafuta au damu (Law 3:17)

Msikilize Yesu kwenye Mathayo 15:10, 17-20 na Marko 7:14-15. Yesu alisema kile kimtokacho mtu ndicho kimfanyacho najisi, si kile kimwingiacho. Mark 7:19 inaonyesha kuwa kwa usemi huu Yesu alivitakasa vyakula vyote. Kama tunamwita Yesu nabii, tunapaswa kusikiliza maneno yake.

Sauti kutoka mbinguni ilimwamuru Petro kula kwenye Matendo 10:10-16, ikimwonyesha kuwa sheria za vyakula zilitumika hadi wakati wa kafara ya Yesu, si baada ya hapo. Tunapaswa kuitii sauti ya malaika wa Mungu na mtume wa Yesu.

Kwa kuhitimisha, tunapaswa kutokupuuzia maneno ambayo manabii wa Mungu wamesema, bali kuyasikiliza.

 

Swali la 23: Kwenye Lk 3:23-33, Mariamu angewezaje kuwa wa uzao wa Yuda, kwa sababu Elisabetii alitokana na mabinti wa Haruni kwenye Lk 1:5, na Mariamu na Elisabeti walikuwa mtu na binamuye kwenye Lk 1:36?

Jibu: Biblia haijataja bayana kabila la mama zao.

Kwa hiyo, Mariamu na Elisabetii wangeweza kuwa mtu na binamu yake kwa kutegemea mambo haya yawezekanayo:

Mama zao walikuwa mtu na mdogo wake: Kama mama zao walitoka kwenye kabila ambalo halijaelezewa bayana.

Mama wa Mariamu na baba wa Elisabeti walikuwa mtu na dada yake: Kama mama yake Mariamu alikuwa dada wa baba yake Elisabeti, kwa ajili hiyo, mama yake Mariamu atakuwa alikuwa wa kabila la Haruni na Lawi.

Baba yake Mariamu na mama yake Elisabeti walikuwa mtu na dada yake: Baba yake Mariamu alikuwa kaka wa mama ya Elisabeti, kwa hiyo, mama yake Elisabeti atakuwa anatoka kabila la Yuda.

Muislam aliona kuwa jambo hili linathibitisha kuwa Mariamu alikuwa anatoka kwenye ukoo wa Haruni. Jambo hili ni muhimu kwa Waislam kwani kama Mariamu hatokei kwenye ukoo wa Haruni basi Kurani itakuwa imekosea. Kwa ujumla, Waislam wanaamini kuwa Kurani hapa duniani ni nakala ya neno kwa neno ya ubao wa Kurani [mbinguni] Sura 85:20-22.

Tazama kitabu cha When Critics Ask uk.381 kwa jibu linalofanana na hili.

 

Swali la 24: Kwenye Yoh 14:16-26; 15:26; 16:5-15, je Muhammad alitabiriwa kwenye Agano Jipya kama Msaidizi au Roho Mtakatifu, kama ambavyo baadhi ya Waislam wanadai?

Jibu: Hapana. Kama jambo hili lingekuwa kweli, basi Waislam wangeamini mambo haya matano (ambayo hawayaamini)

1. Muhammad alimtukuza Yesu. (Yoh 16:14)

2. Mungu alimtuma Muhammad kwa jina la Yesu. (Yoh 14:26)

3. Muhammad alikuwa ametumwa na Yesu pia. (Yoh 16:7)

4. Muhammad alitwaa hekima ya Yesu na kuifanya ifahamike kwetu. (Yoh 16:15)

5. Muhammad alikuwa "ndani ya" mitume. (Yoh 16:17)

Kwa hiyo, hakuna Muislam mwenye ueleo wa mambo atakayeamini kuwa mistari hii inamuongelea Muhammad. Mistari hii lazima iwe inamwogelea mtu mwingine aliyetumwa na Mungu.

Kwa upande mwingine, pengine Waislam wanapaswa kumtukuza Yesu, kama wanadhani kuwa Muhammad alifanya hivyo, kulingana na mistari hii.

Kama wazo la kihistoria, kabla ya Nicea Archelaus (262-278 B.K.) naye alizungumzia jinsi ambavyo Msaidizi kwenye Yohana 14-16 ni Mungu Roho Mtakatifu kwenye Disputation with Manes sura ya 34-35 uk.208-209

Tazama When Cultists Ask uk.182-183 na When Critics Ask uk.419-420 kwa maelezo zaidi.

 

Swali la 25: Kwenye Matendo 4:36, kwa nini kanisa la kikristo [inadaiwa] linaondoa Injili ya Barnaba toka kwenye Biblia?

Jibu: Haikuondolewa; Mungu hakukusudia vitabu vya mafundisho ya uongo, vilivyoandikwa zaidi ya miaka 1,000 baadaye kujiingiza. Injili ya Barnaba inapingana na wazo kuu la Biblia na Kurani, kwa kusema kwamba Yesu HAKUWA Masihi. Injili ya Barnaba ni udanganyifu wa karne ya 15 wa italia wenye makosa ya ya tarehe za kihistoria.

Mambo ya msingi yanaonyesha kuwa hiki si kitabu kilichoandikwa zamani. Injili ya Barnaba inafahamika Italia tu, na hakuna mwanndishi wa zamani aliyewahi kuizungumzia. Inaongelea mambo ambayo hayakutumika mpaka karne kadhaa baadaye. Pia, injili nyingine za udanganyifu zilizoandikwa kwa lugha ya kiarabu zilikutwa Granada. Ziligunduliwa baada ya mwaka 1588, na waliodanganya walikuwa Wamoo. Ingawa mwandishi mmoja wa kiislam, Ata ur-Rahman, aliichanganya injili hii ya uongo na Barua/Waraka wa Barnaba, hakuna kitu chochote inachofanana nacho isipokuwa jina.

Nani aliyeiandika? Uchambuzi wa mwandiko unaonyesha kuwa Injili ya Barnaba inaweza kuwa imeandikwa na Fra Marino, aliyewahi kuwa baba mchunguzi wa uasi asiyekuwa na fikra nadhifu wa Venice tokea mwaka 1542 hadi 1550. Kwa upande mwingine, Mhispania Anselmo Turmeda (aliyekuja kuitwa Abd-Allah ibn Adb Allah baadya ya kubadili dini kuwa Muislam) alisema kuwa aliwahi kuwa padre na alisoma Bologna, Italia kwa muda wa miaka kumi. Mwalimu wake huko alikuwa Muislam wa siri. Kutajwa kwa sarafu za kihispania kwenye Injili ya Barnaba kunathibitisha jambo hili.

Inapingana na Biblia na Kurani: Yesu si Masihi. Sura ya 83 uk.181 sura ya 97 uk.223 sura ya 42 uk.97

Masihi ni Muhammad. Sura ya 97 uk.225-227

Mungu aliumba vitu vyote kwa ajili ya Masihi. Sura ya 191 uk.427.

Mungu aliumba vitu vyote kwa ajili ya Muhammad sura ya 39 uk.91 "[Muhammad] atakuwa mjumbe wangu, ambaye kwa ajili yake nimeumba vitu vyote; ambaye atatoa nuru kwa ulimwengu wakati atakapo kuja; ambaye nafsi yake iliwekwa kwenye fahari ya mbinguni miaka elfu sitini kabla sijaumba kitu chochote."

"mjumbe wa Mungu [Muhammad] atajibu: 'Bwana, nakumbuka wakati uliponiumba, ulisema kuwa umekusudia kuufanya ulimwengu na Paradiso vinipendezeshe mimi, na watu, kwamba wakutukuze wewe kupitia mtumishi wako.'" Sura ya 55 uk.131. Pia sura ya 56. uk.133

Tofauti nyingine na Kurani zinawafanya Waislam wachukue tahadhari kutaka kuitumia "Injili" hii kama kithibitisho. Kwa mujibu wa Bukhari Hadith juzuu ya 4 kitabu cha 56 sura ya 5 na.712 uk.467, Muhammad alisema kuwa moja kati ya vitu vitatu vya uongo zaidi ni "kusema kuwa nimesema maneno ambayo sikuyasema."

Waislam waaminifu ambao hawatakuwa na matendo watakaa jehanamu miaka 70,000. Sura ya 137 uk.319

Muhammad atakwenda jehanamu and ataogopa kuona adhabu za watu wengine sura ya 135 uk.315

Mungu ni baba. Sura ya 133 uk.307

Mungu ni baba yetu. (ingawa hana watoto) sura ya 17 uk.31, 33

Makosa ya jumla - Kusafiri majini kuelekea miji ya bara: Haya si makosa madogo tu, bali yanaonyesha kuwa mwandishi alikuwa na ufahamu kidogo sana wa jiografia na historia ya Palestina.

Yesu alikwenda kwenye bahari ya Galilaya, na baada ya kupanda chomboni alisafiri kuelekea mji wa Nazareti. Sura ya 20 uk.41 (Nazareti ipo bara.)

Mafarisayo wa wakati wa Yesu walikuwa wanajinyima vitu mbalimbali kwa njia ya ajabu sana. Sura ya 145 uk.337-339

Mungu alimwacha Yesu apate mambo mabaya kwa sababu watu wengine walimwita Mungu. Sura ya 112 uk.257

Makosa ya tarehe za kihistoria: Jambo linalosemwa hapa si kwamba Injili ya Barnaba ilikuwa na mambo kadhaa ambayo si sahihi kihistoria. Jambo linaloongelewa ni kwamba makosa mengi yanathibitisha kuwa kitabu hiki kiliandikwa Ulaya wakati wa Enzi ya Kati.

Sarafu kwenye sura ya 54 (dinari ya dhahabu iligawanyika katika sehemu sitini) zilikuwa za Kihispania.

Baba yake alidai kuwa kulikuwa na idadi isiyokuwa na kikomo ya miungu. (Wasumeri hawakuwa na dhana ya kutokuwa na kikomo) sura ya 26 uk.57

"Baadaye, wakati chakula kilikuwa kikienda chini [ya koo la Adam], alikumbuka maneno ya Mungu; kwa sababu hii, akitaka kuacha kula chakula, aliweka mkono wake kwenye koo hili, ambapo kila mtu ana alama." (Msemo "kikoromeo, au 'Adam's apple'" ulikuwa mseomo wa Ulaya ya Enzi ya Kati) sura ya 40 uk.93

Pilato alikuwa gavana wa Uyahudi, wakati Yesu alipozaliwa. Sura ya 3 uk.7

Jubilei sasa ni kila baada ya miaka 100. Sura ya 83 uk.191-193

Waungwana wa wafalme. (Waungwana, 'Barons' walikuwa wa Enzi za Kati) sura ya 131 uk.301

Unataka farasi kama mashujaa wa koo bora waliopewa daraja la juu tokana na ushujaa wao waliouonyesha. (Mashujaa hawa hawakuwepo wakati wa Yesu.) sura ya 69 uk.159

Mzigo wa umma. Sura ya 69 uk.161

Mnara mrefu juu ya paa la nyumba ambapo waandishi walikuwa wakisimama kuhubiri. Sura ya 127 uk.291; sura ya 129 uk.297; sura ya 12 uk.19

Mwana mpotevu, soksi [mguu] mpya. Sura ya 147 uk.241

Lazaro na dada zake wawili walikuwa wamiliki mali kwenye miji mingine ya Magdala na Bethania, sawa tu na wakati wa Enzi za Kati! Sura ya 194 uk.433

Yesu (ukweli ni Yuda) alivaa kama mcheza kiinimacho. Sura ya 217 uk.475

Pia za misonobari (Hapakuwa na pia za misonobari mahali Yesu alipokuwa anaishi.) sura ya 113 uk.259

Nasuri (Fistula). (Neno la kiganga ambalo halikutumika kwa ajili ya uwazi wenye lengo la kupitishia maji mpaka Enzi za Kati.) Sura ya 120 uk.275

Yesu hakuwa anajua kusoma wakati alipokuwa na umri wa miaka 12. Sura ya 9 uk.15

Yesu alifanya maombi kwa ushirikiano na mjumbe wa Mungu, na Yesu alisikia sauti ya Muhammad, [Je Muhammad aliishi kabla ya kuzaliwa?] sura ya 84 uk.195

Makosa haya "mengi kiasi" yanathibitisha kuwa kitabu hiki kiliandikwa Ulaya wakati wa Enzi za Kati.

Hitimisho: Fikiri wewe ungekuwa Muislam ambaye aliambiwa kuwa kuna mtu ameeokota "kitabu" kilichopotea toka kwa Mungu. Pamoja na mambo mengine, "Sura" hii imeeleza kuwa Muhammad alisafiri kwa mtumbwi kwenda Maka, na sura hii imetofauitiana na mafundisho ya Biblia na imetofautiana na Kurani kwenye mambo kadhaa. Manuscript ya zamani zaidi ya sura inayodaiwa iliandikwa Italia, ambayo si tu lugha isiyokuwa ya mashariki ya kati, bali pia haikuwepo wakati wa Muhammad. Mwisho, sura hii inayodhaniwa kuwa na desturi za kihistoria, ambazo hazikutokea Ulaya mpaka baada ya miaka 1,000.

 

Swali la 26: Je Biblia ilipotoshwa?

Jibu: Hapana. Kurani na Biblia vinafundisha kuwa Mungu huhifadhi neno lake. Kwa mujibu wa Kurani, wakati wa Muhammad wakristo walikuwa na Injili. Tuna nakala nyingi za Agano Jipya zilizoandikwa tokea mwaka 100 hadi 200 B.K., na Hati toka Bahari ya Chumvi (Dead Sea scrolls) za Agano la Kale zilizoandikwa kabla ya muda wa Muhammad. Tazama jibu la kwanza kwa habari zaidi kuhusu Agano la Kale.

Baadhi ya tofauti kwenye maandiko hazionyeshi upotofu wa jumla, kwa sababu The Fihrist, Sahih Muslim, na vianzo vingine vya kiislam vilivyotolewa humo, na sura tatu zinaelekea kuwa ziliongezwa. Kurani ya 'Ubai bin Ka'b na Ibn Mas'ud zina mabadiliko mengi zaidi.

 

Swali la 27: Kwa nini hakuna uhakika kwenye baadhi ya mistari ya Biblia?

Jibu: Mungu aliahidi kutunza neno lake, na limetunzwa kiasi kwamba hakuna upungufu wa uhakika unaoathiri mafundisho ya Mungu. Hata hivyo, Mungu aliruhusu makosa yasiyo na maana sana wakati wa kuipitisha Biblia toka kizazi kimoja hadi kingine. Hata hivyo, Mungu anapendezwa zaidi na jinsi tunavyoamini na kutenda kuliko silabi moja moja. Vivyo hivyo, kuna mabadiliko kwenye Kurani yaliyotokana na mistari iliyobatilishwa na uhariri alioufanya 'Uthman.

Hata leo, kuna tofauti katika matoleo mbalimbali ya kiarabu ya Kurani. Kwa mfano, Geisler na Saleeb katika kitabu cha Answering Islam uk.193 wanaonyesha tofauti kadhaa katika kiarabu: Sura 28:48 [sahirani/sihrani], Sura 32:6 [ummahatuhum/ummahatuhum wa hyua abun lahum] Sura 34:18 [rabbana ba'id/rabuna ba'ada], Sura 38:22 [tis'un/tis'atun]. Sura 19:35 [tantaruna/yamtaruna]. Tazama W. St. Clair-Tisdell A Manual of the Leading Muhammedan Objections to Christianity (London: Society for Promoting Christian Knowledge, 1904 uk.60.). Pia kuna tofauti kubwa kati ya Kurani ya 'Uthman na Kurani inayotumiwa leo. Kwa nini kuna mabadiliko haya, na kwa nini hawaibadilishi ili iwe kama ilivyokuwa zamani?

 

Swali la 28: Kwa nini Wakristo walifanya vita vya msalaba (Crusades), uchunguzi wa Kihispania (Spanish Inquisition), Wakatoliki na Waprotestant huko Ireland, Wasebu (Greek Orthodox) na wa Kroati (Wakatoliki), na Waislam wa Bosnian?

Jibu: Yesu alikuwa mfalme wa amani, na hakuwahi kuagiza kuua mtu yoyote yule kwa kuwa ana dini tofauti. "Vita vya msalaba" vya kikristo havikuwa sehemu ya ukristo wa Biblia. Vita vya msalaba (au Jihadi za kikristo) vilikuwa ni kitu kiovu ambacho wazungu wa Ulaya walijifunza toka kwenye Jihadi za kiislam.

 

Swali la 29: Je naweza kuingia mbinguni bila kumkubali Yesu kama Bwana na Mwokozi wangu?

Jibu: Hapana, huwezi kwenda mbinguni kama unakataa kumkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako. Mambo manne ya kuzingatia kwenye jibu hili.

Haki: Mungu ni mwema, Mtakatifu, mwenye haki kwa watu wote (Waebrania 6:10). Mungu huwahukumu watu kwa kuzingatia ufahamu walio nao (Warumi 4:15; 5:13). Abraham hakujua jina la Yesu, lakini alimfuata Mungu na bado aliokolewa kupitia Yesu. (Yohana 8:56, Waebrania 9)

Njia moja tu: Hatuwezi kwenda mbinguni kwa kutegemea haki yetu wenyewe; tunahitaji rehema na neema za Mungu kupitia kwa Yesu. Yesu siyo tu njia ya kwendea kwa Mungu bali pia ni njia pekee ya kwendea kwa Mungu. (Yoh 14:6; 15:5; Matendo 4:12). Njia pekee ya kuifikia mbingu ya Mungu ni kupitia njia ya Mungu.

Ukimkataa Yesu kama Mwana wa Mungu utakuwa umeikataa mbingu: Hata kwa mtu anayeshika dini sana, Farisayo wa kiyahudi, Yesu alisema kuwa kama ukinikataa utakufa kwenye dhambi zako. (Yohana 8:24)

Mungu hutafuta: Mungu hapendi mtu yoyote aangamie (2 Petro 3:9), lakini kama Yeremia alivyowalilia watu wake (Yeremia 13:17; 14:17) na kama Yesu alivyoililia Yerusalem (Luka 19:41-44) na kama Petro alivyowasihi watu waliokuwa wanamsikiliza (Matendo 2:40), Mungu, huwatafuta watu wake kwa haja hiyo hiyo.

 

Swali la 30. Je Wakristo wanasalije?

Jibu: Biblia ina sala nyingi ambazo tunaweza kuzitumia kama mifano, lakini Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kibayana namna ya kusali kwenye Mathayo 6:9-13. Wakristo wanayaona maombi kuwa ni kuongea na Mungu; kwa ajili hiyo maombi machache ya Wakristo yamekaririwa. Maombi ya kikristo mara nyingi huishia na msemo "kwa jina la Yesu", kwa sababu ni kupitia njia ya kafara aliyoitoa Yesu tunayo njia ya kumwomba Baba. (Yohan 16:26)

Wakristo wanapaswa kuomba bila kukoma, kama ilivyoamriwa kwenye 1 Thess. 5:17; Efe 6:18; Fil 4:4;6; Ebr 13:15; na kwa mfano Warumi 1:9-10 na Wakolosai 1:9, 1 Wathesolanike 1:2-3; 3:10. Hii si kama katika uislam, ambako kuna muda maalum ambao maombi yamezuiliwa kwenye Bukhari juzuu ya 2 kitabu 21 sura ya 38 na.283 uk.158. Waislam wanazuiliwa kusali wakati wa jua kuzama, na kati ya swala ya alfajiri na magharibi (Bukhari juzuu ya 1 kitabu 10 sura ya 30 na.558 sura ya 31 na.559-561, sura ya 32 na.563 uk.323-325). Nyakati ambazo sala zimezuiliwa zimeelezwa kwenye Abu Dawud juzuu ya 1 kitabu cha 3 na.1272-1273 uk.336. Wanawake wanapaswa "kuacha sala" wakati wa siku zao za mwezi. Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 3 na.652 uk.188-189, juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.142 uk.48; Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 6 na.322 uk.194, kitabu cha 6 na.327 uk.196; Sunan Nasa'i juzuu ya 1 na.355-361 uk.281-284; juzuu ya 1 na.364-368 uk.285-286.

 

Swali la 31. Ukristo si dini ya utamaduni wangu au wazazi wangu.

Jibu: Ukirudi wakati wa nyuma kiasi, labda kila mmoja ana mababu ambao walikuwa waabudu sanamu, wauaji, wala watu, waliochoma wajane, au walifanya mambo mengine mabaya kama haya. Je unapaswa kuifuata mifano yao? Hapana! Kwenye Luka 16:19-31 Yesu anaongea na mtu aliye jehanamu ambaye anapenda mtu mmoja aende kuwaonya ndugu zake kuwa wasifanye kama alivyofanya yeye. Labda baadhi ya mababu zako, huko jehanamu sasa, wanatumaini utabadilika na kutokufanya kama walivyofanya wao.

Hata kama ilikuwa ni dini ya utamaduni, bado unapaswa kuchagua kati ya kufuata utamaduni wako wa asilia na kumfuata Mungu. Wakati wa Yesu, watu walikuwa na tamaduni na sheria nyingi za kidini za ziada, hata Yesu alisema kuwa hawakuwa na nafasi ya neno lake (Yohana 8:37). Hii ni moja ya sababu walitaka kumsulubisha Yesu.

Imani kwa Mungu wa kweli haikuwa dini ya wazazi wa Abrahamu pia. Abraham alipaswa kuchagua: ama kumfuata Mungu ama kuufuata utamaduni. Hata kama utamaduni hauna makosa, kama unaupenda utamaduni wako na kuufuata kuliko Mungu, utamaduni wako ni kikwazo kwako. Kwenye 2 Wakorintho 11:1-4, Paulo aliandika kuhusu hangaiko lake kuhusiana na kitu chochote kitakachotupotosha toka kwenye kujitoa kwetu kwake.

 

Swali la 32: Je ni kwa nini unaupinga sana uislam?

Jibu: Tunawapenda Waislam na tunawatakia mema zaidi - kwamba waje kuishi kwa furaha mbinguni milele. Kwa kuwa uislam umewapotosha watu kutoka kwa Mungu, tunaupinga uislam kwa faida yao. Hata hivyo, hatuupingi uislam sawa na kuwapinga Waislam wenyewe. Kumfanya uporaji Madina kungeonekana kuwa kitu kibaya, lakini hivi ndivyo Waislam walivyofanya kwa Waislam wenzao kwenye vita vya Harrah mwaka 683/684 B.K. al-Tabari juzuu ya 19 uk.217. Wafuasi wa 'Ali waliunguza nyumba ili kuwaua kwa moto Waislam walio ndani yake wenye kumuunga mkono Mu'awiyah (al-Tabari juzuu ya 17 uk.170). Katika nyakati za sasa, wakati waamini kwenye msikiti nchini Pakistan walipigwa bunduki tu kwa sababu wao siyo Washia, hili ni jambo baya. Tamerlane, ambaye alijenga msikiti mweupe wa Samarkand, alifanya lundo la mafuvu 70,000 ya Waislam waishio Isfahan. Hili likikuwa jambo la ajabu mno.

Wakristo hawapaswi kuwachukia Waislam (au mtu mwingine yoyote yule) kwa njia hizi tatu.

1. Tusiwalaani Waislam hata kama Muhammad alitulaani sisi. Mwishoni mwa maisha yake, Muhammad alisema, "Mungu na awakane Wayahudi na Wakristo kwa kuwa wamejenga sehemu za kuabudia kwenye makaburi ya manabii." (Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 8 sura ya 55 na.427 uk.255). Tazama kuwa hakutofautisha kati ya Wakristo wa kweli na wanafiki; aliwalaani wote tu.

2. Hatupaswi kusema kitu chochote cha "kashfa" (= uongo + ubaya). Kwa mfano, Wayahudi waliitwa waovu kwa sababu walimwita Ezra ('Uzair) mwana wa Allah, kama Kurani inavyosema kwenye Sura 9:30. Wayahudi walimwabudu Ezra kwa mujibu wa Bukhari juzuu ya 6 kitabu 60 sura ya 80 na.105 uk.86. Maneno haya yanawakashfu Wayahudi.

3. Muhammad aliwashutumu wapagani kwenye mstari kwa mujibu wa Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 72 sura ya 91 na.174 uk.113.

Kwa hiyo tunaweza angalau tukaafikiana na Waislam wa kisasa (nategemea) kwamba kuwa mbaya kiasi hiki sivyo mtu wa Mungu anavyopaswa awe.

Kwa ajili yetu, Yesu alitumia zaid ya 1/3 ya maneno yake yote yaliyorekodiwa ama akikemea, akitahadharisha watu maalum, akitahadharisha kwa jumla, au akirekebisha mambo ya uongo. Pia alikuwa anatia moyo, nasi pia tunapaswa kufanya hivyo. Si kwamba tu tujiulize, "Yesu angefanyeje?", bali pia tunapaswa kujiuliza, "Yesu angependa tuseme nini?" Ndio, sisi tu "waonyaji" kama Yeremia, Yohana Mbatizaji, Paulo, na hata Yesu, lakini tunataka mjue kwamba pia tunapenda watu wengine. Tusingependa kuwaumiza nyinyi, hata kama Waislam wanawaumiza Wakristo, na tunatafuta tu jambo lililo jema zaidi kwenu.

 

Swali la 33: Kwa nini Wakristo [inadaiwa] wanawashambulia Waislam?

Jibu: Tunawajali Waislam; hatuwashambulii. Maneno matatu yanajibu swali hili: Wabosnia, Yesu, na wanavijiji.

Wabosnia: Wakati Wasebu walipokuwa wanawaua kikatili Waislam wa Bosnia, Wamarekani waliwapinga. Wasebu wanawezakuwa waliwaona Wamarekani kama watu waliokuwa wanawapinga, lakini hatukuwa tunawapinga Wasebu. Tulikuwa tunawalinda watu walioonewa, na tulipinga ukatili uliofanywa na baadhi ya Wasebu (sio wote). Kwa jinsi hiyohiyo, hatuwapingi Waafghanistan, kama ambavyo meli zetu za misaada zinavyoonyesha, lakini raia wetu waliposhambuliwa, tuliitikia kwa lengo la kujilinda ili jambo hili lisitokee tena.

Yesu alisema tunapaswa kugeuzia shavu lingine, na tunafanya hivyo kama mtu mmoja mmoja. Hata hivyo kwa ngazi ya serikali, Warumi 13:4 inasema kuwa (serikali) haishiki upanga bure. Utamaduni wa magharibi si wa kikristo ingawa ukristo umeuathiri sana. Jambo hili si jema moja kwa moja lakini tuna wajibu wa kupinga vitu ambavyo sio sahihi, bila kujali utamaduni. Kuna mambo mengine yasiyokuwa mazuri zaidi ya kuua watu. Kuwafanya wanawake kuwa kama raia wa daraja la pili, kuwazuia kufanya kazi nje ya nyumba zao, kuuona ushahidi wao kuwa ni kama nusu ya ushahidi wa mwanaume, na ni yupi asiyetakiwa kwenda nje ya nyumba, mawazo yote haya si sahihi. Mungu anatukanwa wakati mambo haya yanapofanyika kwa jina lake.

Wanavijiji huko Indonesia na Sudan wanachinjwa leo hii tu kwa sababu si Waislam. Je unaweza kuniambia kwa nini Waislam ulimwenguni kote wahisi kuwa wanapaswa wawe wanafanya hivi, na bado Waislam wanafikiri kuwa ukosoaji wowote wa amani na akili wa desturi za kiislam ni "kuwashambulia?"



For more info contact www.MuslimHope.com