Maswali ya Biblia Kutoka

 

S: Kwenye Kutoka, tunajuaje kuwa kitabu cha Kutoka kinatakiwa kuwemo kwenye Biblia?

J: Pamoja na sababu nyingine, Yesu pamoja na watu wengine wengi kwenye Biblia walilithibitisha Agano la Kale kuwa kweli na walikitaja kitabu hiki kuwa sehemu ya Maandiko. Kwa maelezo zaidi angalia mwisho wa sehemu ili kuona waandishi wa Kikristo na Kiyahudi walioongelea Kutoka. Tazama pia maswali yanayohusu Mat 22:32 na Luk 2:23.

 

S: Je kitabu cha Kutoka kina umuhimu gani?

J: Kitabu cha Kutoka kinatakiwa kisomwe na kufanyiwa kazi, na si kusomwa tu kwa kufahamu mambo yaliyo ndani yake. Ingawa vitabu vya Kutoka na Kumbukumbu la Torati vina amri kumi, kitabu cha Kutoka ni cha pekee kwani kinaelezea mapigo na kukombolewa kwa toka utumwa wa Misri. Mambo haya si historia yenye kufurahisha tu; yanaonyesha tabia ya Mungu na jinsi ambavyo Mungu anashughulika na watu wake. Mungu hawaepushi watu wake na nyakati ngumu, bali huwawezesha kupita nyakati ngumu. Mungu alitumia njia za kawaida (wakunga), njia za kawaida zenye mkazo wa kiroho (baadhi ya mapigo), na njia za kimiujiza (kugawanywa ka Bahari ya Shamu katika muda uliotakiwa) kuwakomboa watu wake.

Kitabu cha kutoka kinaonyesha jinsi Mungu anavyohusiana kipekee na Musa na Haruni na hata Farao. Mungu alimvumilia Musa kwa mashaka kuhusu uwezo wake wa kuongoza, lakini pia alikuwa "mkali" kwa kupandisha kwake hasira mbele ya Waisraeli wote.

Matukio ya kwenye Kitabu cha Kutoka yalikuwa muhimu katika kuwabainisha Waisraeli kama watu waliochaguliwa na Mungu. Walikuwa pamoja kwenye nyakati ngumu, waliuona ukombozi mkubwa na baraka, lakini kitu cha maaana zaidi ni kuwa walimwona Mungu akifanya kazi katika maisha yao kupitia mambo hayo yote.

Bila matukio ya Kutoka tusingekuwa na fununu kuhusu Pasaka, na kukosa uanishi wa karamu ya mwisho. Kama jinsi Waisraeli walivyowezeshwa kupita kwenye maangamizo kwa damu ya mwana kondoo, sisi pia tunawezeshwa kupita kwenye maangamizo kwa damu ya Mwana Kondoo anaye chukua dhambi za ulimwengu.

 

S: Kwenye Kutoka, kuna njia zinazoweza kusaidia kukifahamu kitabu hiki?

J: Kitabu cha Kutoka kina kina kirefu sana na kinaweza kueleweka kwa viwango vingi tofauti.

1) Licha kuimarisha imani yetu kwa jumla, Kutoka inatoa ufumbuzi wa mafumbo kadhaa kama kwa nini kulikuwa na vielelezo vingi vya Usemitiki huko na Misri na baadaye viliondoka, baada ya hapo kwa nini Thutmose IV alikuja kuwa Farao ingawa alionyesha kuwa hakuwa wa kwanza kuzaliwa, na ni watu gani ambao walikuja kuwa "Wahabiru waliokimbia kwa kucharuka" ambao baadaye waliiharibu baadhi ya miji wa Wakaanani.

2) Ni historia sahihi ya Waisraeli, na jinsi gani walikuja kuwa taifa kutoka kuwa ukoo.

3) Ni kitabu kinachomhusu Mungu, chenye kufunua tabia yake ya namna anavyowatendea wanadamu. Kinaonyesha jinsi alivyotumia njia za kawaida na kimiujiza kwenye historia na kuwatenda watu wake na watesi watu waliokuwa wanawakandamiza.

4) Ni kitabu cha sheria, mambo ambayo Mungu amewaagiza watu wakewayafanye.

5) Kama Nehemia, ni kitabu kinachohusu uongozi wa kiungu, jinsi ambavyo mtu mmoja akiwa na Mungu anavyoweza kuliangusha jeshi na kuwaongoza watu wengi sana kwa mafanikio kwa miaka 47.

6) Ni kitabu kinacho wahusu watu wote wa Mungu, kwamba sisi nasi tunaweza kutiwa moyo kuwa Mungu atatukomboa, nasi pia tunaweza kukutana naye, na kwamba Mungu anaweza kufanya makazi yake kwenye hema la mioyo yake.

7) Ni kitabu cha mifumo (Kut 25:40), ya ukombozi, mapambano, maisha ya uchaji na vitu vyenye kumpemdeza Mungu na vile visivyo mpendeza Mungu.

 

S: Je muhtasari wa kitabu cha Kutoka ukoje?

J: Kwa kuwa njia mbalimbali za kukiangalia Kitabu cha Mwanzo, vitabu tofauti vya maoni ya Biblia (commentaries) vina mihtasari tofauti. Ufuatao ni muhtasari wa jumla.

I. Utumwa wa Misiri (Kutoka 1-14)

A. Njia ya kwenda kwa Farao (Kutoka 1-4)

1. Utumwa wa Israeli (Kutoka 1)

2. Musa hatarini (Kutoka 2)

3. Kuitwa na Mungu (Kutoka 3,4)

B. Ukombozi – Wape watu wangu ruhusa waende (Kutoka 5-14)

1. Mapambano mawili (Kutoka 5-7:13)

2. Pigo la kwanza – Damu (Kut 7:14-25)

3. Pigo la pili – Vyura (Kut 8:1-15)

4. Pigo la tatu – Chawa (Kut 8:16-19)

5. Pigo la nne – Nzi (Kut 8:20-32)

6. Pigo la tano – Mifugo kufa (Kut 9:1-7)

7. Pigo la sita – Majipu (Kut 9:8-12)

8. Pigo la saba – Mvua ya mawe (Kut 9:13-

35)

9. Pigo la nane – Nzige (Kut 10:1-20)

10. Pigo la tisa – Giza la siku tatu (Kut 10:21-

29)

11. Pigo la kumi – Mzaliwa wa kwanza na

Pasaka (Kut 11:1-12:30)

12. Kuvuka Bahari ya Shamu (Kut 12:31-

14:31)

II. Maisha jangwani (Kutoka 15-40)

A. Kuelekea Sinai: Safari ya kumtegemea Mungu (Kut 15:1-18:27)

1. Wimbo wa Miriam – Kukumbuka

ukombozi wa Mungu (Kut 15:1-21)

2. Mara na Elim – Je Mungu atatoa kwenye

nchi kavu (Kut 15:22-27)?

3. Mana na kware – Je Mungu atawalisha kwenye sehemu kame namna hii (Kutoka 16)?

4. Masa – Kushindwa mtihani wa imani (Kut

17:1-7)

5. Waamaleki – Je Mungu atatulinda (Kut

17:8-15)?

6. Naweza kufanya vitu vyote mwenyewe –

fikra zaidi zinazobadilika Kutoka 18)

B. Kukutana na Mungu Sinai (Kutoka 19-

24)

1. Kukutana na Mungu (Kutoka 19)

2. Amri kumi, madhabahu, hakuna sanamu

(Kutoka 20)

3. Sheria za madai (Kut 21-23:10)

4. Sabato na sikukuu (Kut 23:11-19)

5. Ahadi ya Mungu ya ukombozi (Kut 23:20-

33)

6. Chakula cha jioni na Mungu (Kutoka 24)

C. Kuabudu katika hema la kukutania – Kujiandaa kwa ajili ya Mungu miongoni mwenu

1. Kujenga ufahamu wetu

a. Vifaa – Kumtolea Mungu (Kut 25:1-9)

b. Safina – mahali kukutana na Mungu (Kut

25:10-22)

c. Uwepo wa Mungu kwenye hama la

kukutania (Kut 25:23-30)

d. Kinara cha taa – Nuru ya Mungu maishani

mwetu (Kut 25:31-40)

e. Hema la kukutania – uhusiano binafsi wa

karibu na Mungu (Kutoka 26)

f. Madhabahu ya dhabihu za kuteketeza –

Kabidhi vitu kwa Mungu (Kut 27:1-8)

g. Ua wa hema la kukutania – Kukutana

pamoja kwa ajili ya Mungu (Kut 27:9-19)

h. Usiache ibada yako iishiwe mafuta – (Kut

27:20-21)

2. S

Kujiweka wakfu

a. Mavazi ya makuhani wa Mungu (Kutoka

28)

b. Kuwaweka wakfu makuhani wa Mungu

(Kutoka 29)

3. Makuhani wanafanya nini

a. Madhabahu ya kufukizia uvumba – je

maombi yako ni manukato (Kut 30:1-

10)?

b. Usisahau kuwa tulinunuliwa kwa gharama

(Kut 30:11-16)

c. Mabirika ya kuogea – hitaji letu la kuoshwa

kila siku (Kut 30:17-21)

d. Mafuta ya kutiwa matakatifu (Kut 30:22-

33)

e. Uvumba (Kut 30:34-38)

f. Mafundi (Kut 31:1-11)

g. Ishara ya kuitunza sabato (Kut 31:12-18)

D. Uasi, toba na matengenezo (Kut 32-33)

1. Ndama wa dhahabu – Wangewezaje?

Tutaweza (Kut 32)?

2. Matengenezo – Je tunaweza (Kutoka 33)?

3. Utiifu na kukutana na Mungu tena (Kutoka

34)

E. Maelezo tena ya ibada kwenye hema la kukutania baada ya kutubu (Kut 35:1-39:43)

F. Mungu pamoja nasi – Je hema lako limejengwaje (Kutoka 40)?

1. Kujiandaa kwa ajili ya Mungu (Kut 40:1-

33)

2. Kuja kwa Mungu kwa utukufu (Kut 40:34-

38)

S: Je nani aliyejibu kwa mara ya kwanza maswali kuhusu Kitabu cha Kutoka?

J: Kwa kadri ninavyokumbuka, mtu wa kwanza kuandika majibu ya maswali kuhusu Kitabu cha Mwanzo alikuwa Philo, Myahudi mwenye kuufahamu utamaduni wa Kigiriki toka Alexandria, aliyeishi kati ya mwaka 20 KK hadi 50 BK. Kwa bahati mbaya, vipande vichache tu vya kazoo yake vimeweza kupatikana sasa.

 

S: Kwenye Kutoka 1, iliwezekanaje kuwa na watu wengi kiasi hicho kwa muda wa miaka 430?

J: Ili kupata jibu la swali hili, angalia maelezo ya Kitabu cha Hesabu 1.

 

S: Kwenye Kutoka 1, ni kwa jinsi gani Mungu mwenye upendo aruhusu Waebrania wawe watumwa kwa miaka 400?

J: Urefu wa maisha ya mtu, au hata miaka 400, ni mweko mfupi tu ukilinganishawa na maisha ya milele mbinguni. Mungu huruhusu watu wake wateseke hapa duniani, hata mateso yasiyo ya haki, kwa sababu hiki ni kipindi cha muda tu, naye atatulipa mbinguni.

Hata hivyo, Mungu si tu kuwa ameruhusu jambo hili litokee, bali pia kuwa jambo hili liwe Baraka kubwa kwa Waisraeli. Kulikuwa na vita vingi sana Kaanani kipindi hicho: ifuatayo ni orodha ya baadhi ya vita hizo:

 

Mwaka 1500 KKMwaka 1485 KK

Thutmose III wa Misri anaiteka Arvad ya Foenikia

Mwaka 1483-1437 KK

Mapambano 17 ya kijeshi ya Thutmose III wa Misri - Napoleon wa Misri

Mwaka 1483 au 1468 KK

Huko Megido Thutmose III awashinda Wakaanani

Karibu mwaka 1454 KK

Qadesh aiasi Misri

 

Kwa kuwa watumwa Misri, na wachungaji kasi ambayo Wamisri waliichukia, hawakuweza kuchangamanishwa na Wamisri. 735 Baffling Bible Questions Answered uk.49 inaeleza vizuri sana: "Mara nyingi vitu vinavyoonekana kutuumiza sana maishani mwetu huwa ni baraka za Mungu kwetu ambazo zimefichika, zenye kutambuliwa hivyo tu baada ya mapenzi ya Mungu aliyoyakusudia kufunuliwa katika muda wake."

 

S: Je watawala wa Kihiksosi waliwezaje kuendana na Kut 1:8 kwa mujibu wa elimukale?

J: Wahiksosi walikuwa watu wa Kiasia walioitwaa Misri kutokana na magari yao bora ya farasi toka mwaka 1760 hadi 1640 KK. Waliitawala misri kwa muda mfupi, na waliondolewa kidogo kidogo kuanzia mwaka 1573/55 hadi 1540 KK. Wakati Yakobo na familia yake walipohamia Misri, Wamisri waliokuwa maarakani walikuwa ni wale waliowatangulia Wahiksosi kulingana na Mwa 46:34 na 32:32.

Mwa 46:34 inasema Wamisri hawakupenda kuwa wachungaji, na Wahiksosi waliitwa "wafalme wachungaji."

Mwa 32:32 inasema kuwa hawa Wamisri hawakuwa wanakula pamoja na Waebrania [wenye asili ya Asia].

Hivyo, kama Wahiksosi wasingekuwa ndio watawala wa Misri wakati familia ya Yakobo ilipokuwa inakwenda Misri, "Mfalme mya" angekuwa na mashaka na watu waliokuwa kwenye nafasi za juu wakati wa wafalme walitangulia. Isitoshe, wakati Wahiksosi walipoondolewa, Wamisri wazawa wangeweza kuendelea kuwa na mashaka na watu wenye asili ya Asia wasiokuwa Wamisri, kama vile Waebrania.

 

S: Kwenye Kut 1:8-10, kwa ufupi, je ni kweli kuwa hakuna ushahidi wa elimukale wenye kuthibitisha kuwepo kwa Waisraeli Misri, kama mtu asiyeamini uwepo wa Mungu, Capella, alivyodai?

J: Hapana, kuna ushahidi wa kutosha. Si tu kwamba "Wahabiru" wameongelewa, lakini pia Papyrus Brooklyn 35.1446 inaonyesha mifano mingi ya watu wenye asili ya Asia waliopewa majina ya Kimisri. Baadhi ya watu hawa wenye asili ya Asia wanatoka kwenye makabila ya Isakari na Asheri. Tazama pia swali linalofuata na Kut 11:5-12:30 kwa maelezo zaidi.

 

S: Kwenye Kut 1:8-10, mbali ya Biblia, je kuna ushahidi wowote wa Waisraeli kuwa utumwani Misri au kutoka Misri?

J: Baadhi ya "wanazuoni wamakinifu" (wale walio tayari kutafsiri maandishi kinyume cha mapokeo yao na jinsi wanavyopendelea na kuacha ushahidi uongoze fikra zao hata kufikia uamuzi) bado wanaiamini dhana iliyopitwa na muda kuwa hapakuwa na ushahidi wa Waisraeli ama kuwepo au kutoka Misri. Huenda wanatakiwa kusoma "maandishi yaliyo ukutani." Michoro kwenye ukuta wa kaburi la Khnumhotep (mwaka 1892 KK) huko Beni Hasan, Misri inaonyesha "watu 37 wenye asili ya Asia", au watu wasiokuwa Wamisri waliotokea Mashariki ya Kati. Walikuwa na nywele nyeusi, ndevu ndefu, majoho marefu yenye rangi, pinde na fimbo iliyopinda ambayo ikirushwa humrudia mtu aliyeirusha.

Wanazuoni Wakristo walioandika kwenye Wycliffe Dictionary of Biblical Archaeology, The Expositor's Bible Commentary, na vitabu vingine wamekusanya ushahidi mwingi sana kuwa Waisraeli walikuwa Misri. Si tu kuwa wanazuoni Wakristo wanafundisha kuwa Waisraeli walikuwa Misri toka karibu mwaka 1875 hadi 1445 KK, lakini mwanaelimukale asietenda kwa kufuata dini, David M. Rohl, kwenye kitabu chake Pharaohs and Kings: A Biblical Quest (Crown Publishers, 1995) pia ametoa ushahidi unaoendana na Waissraeli kutoka Misri. Ifuatayo ni oridha ya "Vitu kumi muhimu zaidi" vyenye kuthibitisha Waisraeli kutoka Misri.

10. Viunzi vya mifupa vya kondoo wenye manyoya marefu walio na asili ya Kiasia vinaonyesha kuwa walionekana kwa mara ya kwanza kabisa kwenye ukanda wa Delta wa Misri karibu na wakati wa Yusufu (mwaka 1900-1800 KK). Jina la Yusufu la Kimisri "Safena-panea" huenda lilikuwa "Zat-en-afu" (aliyeitwa) na "Ipiankhu" (Ipu ni aliye hai). Jina "Ipiankhu" na namna mbalimbali lilivyoitwa yalitumika sana wakati wa Yusufu lakini hayakutumika sana kabla na baada ya wakati huo. Majina mengi mengine ya Kiebrania yanapatikana kwenye karatasi la mafunjo la Kimisri kwenye jumba la makumbusho la Brooklyn, New York (35.1446). Chini ya utawala wa Sobekhotep III (karibu mwaka 1540 KK), idadi kubwa ya watumwa walihamishiwa kwenye eneo la Thebes. Kati ya majina 95, zaidi ya nusu yake yalikuwa majina yenye asili ya Kiasia, na majina ya Kimisri yalikuwa yametolewa baada ya hayo. Mengi ya majina ya Kimisri yana maneno "anayeitwa" kama sehemu ya kwanza ya jina. Baadhi ya watu hawa walirekodiwa bayana kuwa wametoka kwenye makabila ya Isakari na Asheri.

Isitoshe, baadhi ya majina ya Kiebrania ni Menahem na Shifra. (Hata hivyo, hapa ilikuwa miaka 100 kabla ya Shifra kwenye Kutoka 1). Walt Kaiser kwenye A History of Israel, uk.84 na The Expositor's Bible Commentary juzuu ya 2, uk.307 anasema kuwa majina mawili ya Kisemitiki, Shifra linaweza kuwa linatokana na jina "Sp-ra" (mwenye haki), na jina "Puah" huenda lilitokana na neno la Kigariti (lugha iliyoumika maeneo ya Syria ya kale kwenye karne za 14 hadi 12 KK) "Pgt" lenye kumaanisha "msichana" au "mwenye kutukuka."

Pia, Leiden Papyrus 348 inatoa amri "kugawa nafaka kwa askari na kwa Waapiru wanaoafirisha mawe kwenda kwenye mnara mkubwa wa Rames[s]es."

9. Mtu wa pili kwa madaraka asiyekuwa Mmisri inaleta maana nzuri zaidi. Kama Yusufu angejaribu kuasi, Wamisri wasingemfuata. Imerekodiwa kuwa Wakaanani, kama Meri-Ra na Ben-Mat-Ana walikuwa na nafasi za juu sana kwenye mahakama ya Misri.Msemitiki mmoja aliyeitwa Yanhamu alikuwa msaidizi wa Amenhotep III aliyekuwa anaishi Gaza.

8. Matofali yalitumika kujenga baadhi ya miji ya Misri kama vile Pithom. Hapo Pithom, yamepatikana matofali yaliyotengenezwa kwa majani makavu kwenye ngazi ya chini kabisa. Kwenye ngazi ya kati matofali yalikuwa na vishina vya mabua tu. Kwenye ngazi ya juu, wanaelimukale wamekuta kuwa matofali yalitengenezwa bila kitu chochote cha kugundishia. Kaburi la Mmisri mashuhuri aliyeitwa Rekhmere/Rek-mi-Re lililokuwa Thebes kwenye karne ya 15 KK lina mchoro wa watumwa wanaotengeneza matofali.

7. Palikuwa na ushahidi wa majanga makubwa yaliyopelekea miili ya watu wengi kuzikwa kwa haraka. Hata hivyo, idadi kubwa ya vifo haithibitishi wala kukanusha kuwa jambo hili lilisababishwa na tukio lililotokea ghafla usiku mmoja.

Pia, Tacitus kwenye Histories Kitabu cha 5 anaorodhesha mawazo mbalimbali ya kukisia kuwa Wayahudi walitokea Krete, au Misri, au Ethiopia, au Ashuri, na kisha anasimulia habari yenye kufurahisha sana. "Hata hivyo, waandishi wengi wanakubaliana kuwa kuliwahi kutokea ugonjwa, ambao uliharibu sana mwili, ulioanzia Misri, kiasi kuwa Mfalme Bocchoris, akitafuta kupona, alikwenda kwa kuhani muuguzi wa Hamoni, na alizuiliwa kuisafisha milki yake, na kuipeleka kwenye nchi nyingine ya kigeni jamii ya watu wanaochukiwa na miungu. Watu ambao walikusanywa baada ya kutafutwa kwa bidii, walijikuta wameachwa jangwani, waliishi kwa sehemu kubwa katika hali ya kutokujitambua kwa huzuni, hadi mmoja wa watu hao waliokuwa uhamishoni, aliyeitwa Moyses, alipowaonya kuwa wasitafute msaada toka kwa mungu yeyote au binadamu, wakiwa wameachwa kiasi kikubwa kama walivyokuwa, bali wajiamini, huku wakimchukulia kiongozi wao aliyetumwa toka mbinguni mtu ambaye anapaswa kuwasaidia kuepukana na shida inayowakabili wakati ule . . . Moyses, ambaye anataka kujipatia mamlaka juu ya taifa hilo hapo baadaye, aliwapa njia mpya ya kuabudu, iliyotofautiana na nyingine zote zilizotumiwa na watu wengine . . . Walimchinja kondoo, kitu ambacho kilionekana kuwa kejeli kwa Hamoni, na walimtoa ng'ombe dume kuwa kafara, kwa sababu Wamisri walikuwa wanamwabudu kama Apis." (Imenukuliwa kutoka The Annals and The Histories, kazi ya P. Cornelius Tacitus, Encyclopedia Britannica, Inc. 1952).

6. Maandishi ya Kimisri ya karibu mwaka 1350 KK yanaelezea tukio la kushangaza lililotokea kabla ya hapo: "Jua limefunikwa na halitoi mwanga wenye kuwawezesha watu kuona. Maisha hayawezekani jua linapofunikwa na mawingu. Ra [mungu] amegeuza uso wake mbali na wanadamu. Endapo litaangaza kwa saa moja! Hakuna anayejua mchana unapofika. Kivuli cha mtu hakitambuliwi. Jua la mbinguni linafanana na mwezi . . ." Maneno haya yanaweza kuwa yanaongelea giza lililotanda juu ya nchi, au yanaweza kuwa yanaongelea mlipuko wa volkanokwenye kisiwa cha Thera.

5. Farao Thutmose IV hakuwa mtoto wa kwanza wa kiume. Kwenye Dream Stela of Thutmose IV (mwaka 1421-1410 KK) iliyopatikana kati ya nyayo za mbele za makucha ya sanamu ya Kimisri ya jiwe (yenye mwili wa simba na kichwa cha mwanamke) huko Giza, mungu Harmakhis alimwahidi Thutmose masaada maalum ilia je kuwa mfalme aada ya huyo aliyekuwepo madarakani kwa malipo ya kuondoa mchanga uliojilundika kwenye sanamu hiyo. Huenda asingehitaji msaada maalum kama angekuwa mtu wa kwanza kutakiwa kumrithi baba yake Amenhotep II (mwaka 1450/1447-1401/1385). Walt Kaiser kwenye A History of Israel, uk.90 anasema kuwa kaka mkubwa zaidi wa Thutmose IV aliitwa Webensenu. Webensu alizikwa kwenye kaburi la kifalme, na huenda akawa ndiye aliyekufa wakati wa pigo la kumi Mtoto wa pili wa kiume wa Amenhotep II alikuwa Khaemwaset, aliyeoa kabla ya kufa. Kwa mujibu wa Kaiser, "Hivyo, ingawa Sphinx Stele haiwezi kuchukuliwa kuwa ni kithibitishoo cha moja kwa moja cha mzaliwa wa kwanza, ushahidi wa kutosha umetolewa na wataalamu wa mambo ya Misri wenye kuthibitisha tarehe ya mapema (karne ya 15 KK) ya kutoka utmwani wa Misri kwa Waisraeli na ukweli kwamba Thutmose IV hakurithi kiti cha enzi cha baba yake."

4. Maandishi yenye mchanganyiko wa Kimisri na Kiebrania kwenye mapango yaliyo karibu na mlima Sinai yanaelezea kugawanyika kwa bahari, Musa na kukamata kware. Kitu cha kufurahisha zaidi ni lugha: ilikuwa ni mchanganyiko wa Kimisri na Kiebrania. Mwana historia Diodorus Siculus (mwaka 10 KK) pia alifahamu jambo hili. Pia kwenye lango la migodi ya shaba ya Sinai kuna mamia ya maandishi. Mengi kati ya hayo yameandikwa kwa herufi za kale za Kimisri, lakini karibu maandishi 40 yameandikwa kwa aina ya mwandiko wa herufi zilizotangulia Kisinai za karne ya 15 KK. Hata hivyo, ushahidi huu "wenye mashaka", kwa sababu haiwezekani kutambua muda ambao maandishi haya yalipoandikwa.

3. Jeshi la Misri, ambalo kabla ya muda huu lilikuwa linaidhibiti Kaanani, halikuwemo kabisa. Hatusikii sana kuhusu jeshi la Misri tena hadi wakati wa Farao (Mfalme) Seti I, aliyeiangamiza Hazor mwaka 1300 KK.

2. Huko Yeriko, Bryant G. Wood alizikuta kuta imara, kiasi kikubwa cha nafaka (cheny kumaanisha uvamizi uliochukua muda mfupi), na hapakuwa na uporaji (kwa kuwa nafaka zilikuwa bado zipo). John Garstang ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kuona kiasi kikubwa cha nafaka iliyogeuzwa kuwa kisukuku. Hard Sayings of the Bible, uk.182-183 inataja ushahidi wa tetemeko la ardhi lenye kiasi cha 8 kwenye kipimo cha Richter, ambalo linaweza kuwa liliacha nyufa kwenye kuta. Kuta za matofali mabichi ziliuangukia ukuta wa mawe ulikuwa nje, na kufanya mteremko mzuri wa kupandia au kushukia. Je utekaji huu ulitokea lini? Chombo cha kufinyangwa cha kauri toka Cyprus kinaonyesha kuwa kilitengenezwa kati ya mwaka 1450 hadi 1400 KK. Hirizi za Kimisri ziliandikwa jina la mfalme aliyekuwa anatawala wakati huo hadi kipindi cha Yoshua. Mwazoni mwa karne hii, John Garstang alikosea kukadiria muda wa kuta za Yeriko kujengwa katika kipindi cha Yoshua, lakini Kathleen Kenyon ameonyehsa kuwa Garstang hakuwa sahihi kwa mujibu wa Wycliffe Bible Dictionary, uk.575. Njia ya kupima umri wa vitu vya kale ya Carbon-14 inaonyesha kuwa anguko la Yeriko lilitokea mwaka 1410 KK au miaka 40 kabla au baada ya hapo.

1. Kuhusu kuangamizwa kwa miji ya Kanaani, kitabu cha Yoshua tu kinasema kuwa ni miji hii tu iliyoangamizwa: Debir, Eglon, Hazori, Hebroni, Yeriko, Lakishi, Libnah, Makadeh, na Ai. Wataalamu wa elimukale wametambua kuwa miji ifuatayo iliangamizwa wakati ule: Aradi, Debiri, Hazori, uwanja uliopo el-Khalil (Hebroni?), Yeriko na Lakishi. Uwanja uliopo Beitin (Bethel?), mji wa Gibeoni na uwanja uliopo Khirbeti Nisya ilitelekezwa. Mji mdogo wa Ai huenda uliharibiwa sana hata usiweze kuonekana. Ni nani aliyeiangamiza miji hii? Mbao zenye maandiko za Amarna zinatueleza wazi kabisa. Hizi zilikuwa barua zilizoandikwa toka Kanaani kwenda wa mfakme wa Misri karibu mwaka 1500-1400 KK. Mbao hizi zinawataja "Wahabiru wenye kukimbia kwa kucharuka" walioogopwa sana. Kitu cha kufurahisha ni kuwa, mbao hizi zinamtaja pia mfalme Lab'ayu wa Shekemu, aliyekuwa msaliti kwa kuwa alikuwa mshirika wa wavamizi wa Wahabiru. Baadaye, pande la jiwe la Farao Merenpta (mwaka 1225 KK) pia linawataja watu walioitwa Israel kaskazini mwa Kanaani.

Mbali ya hii, Julius Africanus (aliyeandika mwaka 235-245 BK) anawataja wanahistoria Wagiriki wa zamani walioandika kuhusu Kutoka kwa waisraeli Misri. "Polemo, kwa mfano, kwenye kitabu chake cha kwanza kiitwacho Greek History, anasema: ‘Wakati wa Apius, mwana wa Phoroneus, divisheni moja ya jeshi la Wamisri iliondoka Misri na kufanya makazi Palestina kwenye sehemu iitwayo Shamu, ambako si mbali na Arabia: hawa kwa vyovyote vile walikuwa watu waliokuwa na Musa. Na Apion mwana wa Poseidonius, mwana sarufi mwenye kuchosha sana, kwenye kitabu chake kiitwacho Against the Jews, na kwenye kitabu chake cha nne kiitwacho History, anasema kuwa wakati wa Inachus mfalme wa Argos, wakti Amosis alipotawala Misri, Wayahudi waliasi chini ya uongozi wa Musa. Na Herodotus pia anataja uasi huu, na ule wa Amosis, kwenye kitabu chake cha pili, na kwa namna fulani pia Wayahudi wenyewe, akiwajumuisha na watu waliotahiriwa, na aliwaita Waashuru wa Palestina, huenda kupitia kwa Abraham. Na Ptolemi wa Wamisri wa kale, aliyeelezea historia ya Wamisri kutoka nyakati za mwanzo zaidi, anatoa maelezo hayohayo ya vitu hivi vyote; kwa hiyo kati yao, kwa jumla, hakuna tofauti inayostahili kutajwa kwenye historia" (Ante-Nicene Fathers juzuu ya 6 Julius Africanus, kipande cha 13, uk.124.

Hii si mara ya kwanza wanazuoni wamakinifu hawakufahamu elimukala. Kwa mfano, wataalamu wa elimukale wamegundua Wahiti mwaka 1892. Hata hivyo, baadhi ya wanazuoni bado wanatia shaka uwepo wao miaka kumi baaday (1902, E.A.W. Budge.)

Hitimisho: Ni vigumu kuogelea kinyume cha mkondo wakati kanuni hii yenye kushuku inazama kwenye bahari ya ukweli. Hivyo, elimukale leo hii inaonyesha kuwa rekodi za Biblia zinadhihirisha jinsi Biblia inavyoaminika. Kwa kuwa Biblia iko sahihi katika kuwasilisha maelezo mengi madogo madogo, tunaweza kuiona kuwa sahihi katika maelezo kuhusu Biblia yenyewe: ujumbe wa Mungu kwetu.

Vyanzo vingine vyenye kufurahisha vya maelezo ya elimukale kuhusu Waisraeli wakiwa Misri ni: Encyclopedia Britannica, Can Archaeology Prove the Old Testament? iliyoandikwa na Ralph O. Muncaster, Encyclopedia of Bible Difficulties iliyoandikwa na Gleason Archer (Zondervan), Evidence for Faith iliyoandikwa na John Warwick Montgomery, The New International Dictionary of the Bible iliyoandikwa na Douglas, J.D. na Merrill C. Tenney, 735 Baffling Bible Questions Answered, uk.53, The New Evidence That Demands a Verdict iliyoandikwa na Josh McDowell, na Biblical Archaeology Review.

 

S: Kwenye Kut 1:8-10, je ni kweli kuwa "imethibitishwa kwamba Wamisri walijijengea wenyewe miji yao na minara yao yote", kama mtu asiyeamini uwepo wa Mungu (Capella) alivyodai?

J: Si hivyo kabisa. Ili kupata jibu ya swali hili tazama swali lililotangulia.

 

S: Kwenye Kut 1:8-10, kwa nini Mungu aliruhusu watu wake wateswe?

J: Wakati mwingine Mungu huacha watu wake wateseke kwa sababu mbalimbali: adhabu (Waamuzi), kuchambua watu ambao hawakutaka kumfuata, kamaa vile uhamisho, n.k. Lakini katika jambo hili, ingawa Biblia haisemi kwa uwazi, tunaweza kukisia.

Fikiria kuwa watu wangekuwa mafunzi washi wanaolipwa vizuri na wanatendewa vema wakati Musa alipotokea na kusema kuwa Mungu anataka kuwakomboa. Kitu gani kingewafanya watake kumfuata Musa endapo Farao angekuwa rafiki wao mzuri sana? Hata kama uhuru katika nchi ya ahadi ungekuwa mzuri zaidi, wengi wao wasingependa kuacha hali njema waliyokuwa nayo. Fikiri jinsi ambavyo baadhi yao wangekuwa wanafungasha mizigo yao tayari kuondoka huku wakijiuliza jinsi ambavyo watakwenda kuishi maisha magumu jangwani wakati waliyafahamu maisha ya raha tu. Fikiria jinsi ambavyo wangepaswa kumtumaini Mungu kupata maji na chakula vyao wakati vitakapokuwa havipo jangwani, ilhali walikuwa na raha asana hata hawakutakiwa kumtumaini Mungu kwa kitu chochote kile. Hivyo tunaweza kuona baadhi ya sababu za Mungu kuruhusu wapitie hali hizi ngumu.

Hata hivyo, bado kuna watu waliolalamika jangwani, wengine walitaka kurudi Misri na wengine waliyakataa mamlaka ya Musa.

Huenda tusipende kusikia jambo hili, lakini wakati mwingine Mungu hutufanya tupitie kwenye hali ngumu ili twende na kufanya kitu ambacho anataka tukifanye.

 

S: Kwenye Kut 1:11 tunajua kitu gani kuhusu wasimamizi wa watumwa wa Misri mbali ya vile Biblia inavyosema?

J: Neno la Kimisri "ser" limo kwenye michoro ya ukutani kwenye kaburi la Kithebe (jina la Kigiriki la mji wa kaskazini ya Misri ya zamani) la Rekhmire, aliyekuwa msimamizi wa utengenezaji matofali wa Mfalme Thutmose III. Michoro hii inawaonyesha wasimamizi wa watumwa wakiwa na mijeledi mikubwa sana. Hieroglifu (picha inayowakilisha neno iliyotumika katika maandishi ya kale ya Kimisri) inafurahisha: kichwa na shingo vya twiga.

 

S: Kwenye Kut 1:11, je Waisraeli walijenga "miji ya kuwekea akiba?"

J: Msemo huu unaweza kutafsiriwa vizuri zaidi kama "niji ya usambazaji" au "miji ya kuhifadhia." "Hazina" zilikuwa nafaka na vyakula vingine, siyo fedha na dhahabu. Miji ya kuwekea akiba ilikuwa mashariki mwa Misri ili kuweza kusambaza vizuri zaidi kwa majeshi ya Kimisri yaliyokuwa yanakwenda kwenye mapambano Palestina na Shamu.

 

S: Kwenye Kut 1:11, je miji miwili ya Pithomu na Ramesesi ipo wapi?

J: Pithom (nyumba ya [mungu] Atum), upo kwenye korongo kavu la mto Tumilat lililo mashariki mwa delta ya Naili. Korongo hili linaweza kuwa ama ni mabaki ya Tell er-Rababeh au Tell el-Maskhuta karibu km 13-14 mashariki. Pale Tell el-Maskhuta matofali yalikutwa yaliyotengenezwa bila majani makavu. Septuaginti (tafsiri ya Kigiriki ya Agano la Kale) inaongeza kusema huu ni mji huohuo wa "Oni" au Heliopolisi.

Mji wa Ramesesi ulikuwa ukidhaniwa kuwa ulikuwepo Tanisi/Zoani. Hata hivyo, kwa sasa unadhaniwa kuwa karibu na Qantir kwa mujibu wa Hans Goedicke kwenye Biblical Archaeologist Review juzuu 7 (Sept-Okt 1981). Kuna ushahidi wa mabaki ya Shamu ya Palestina kutoka mwaka 1700-1500 KK.

 

S: Kwenye Kut 1:11, je neno "Farao" lilianza kutumika lini?

J: Mara nyingine maana za maneno hubadilika toka muda mmoja hadi mwingine. Kutoka mwaka 2,500 hadi 2,000 KK neno "Farao" kwa mara ya kwanza lilimaanisha "nyumba kubwa" (mahali) lakini lilibadilika polepole na kumaanisha mfalme wa Misri aliyeisha pale.

 

S: Kwenye Kut 1:15, je wazalishaji wa Kiebrania waliwezaje kuhudumia wazazi wengi kiasi hili?

J: Ni dhahiri kuwa hawakumhudumia kila mzazi, lakini walisimamia yao walipokuwa wanajifungua. Wasimamizi wa ujuzi wa aina mbalimbali walidhibiti jamii ya Kimisri.

 

S: Kwenye Kut 1:15-19, je kuma ushahidi wowote mbali ya Biblia wa majina Shifra na Pua?

J: Sifahamu ushahidi wowote wa jina Pua. Lakini maandiko ya Kimisri yaliyo kwenye mafunjo yaliyohifadhiwa Brooklyn Museum (35.1446), yaliyoandikwa karibu mwaka 1540 KK, yanamtaja Shifra. Shifra huyu aliishi zaidi ya miaka miamoja kabla ya Shifra aliyetajwa kwenye kitabu cha Kutoka.

 

S: Kwenye Kut 1:16-19, Mungu aliwezaje kuwabariki wazalishaji wa Kiebrania Shifra na Pua kwa kudanganya Farao?

J: Wakristo wanatoa maoni tofauti katika kujibu swali hili.

1. Wengi wanasema kuwa Mungu aliwabariki kwa ajili ya imani yao iliyowasukuma kusimamia haki, na aliwasamehe kwa kudanganya. (Pia, Amri Kumi zilikuwa bado kutolewa wakati ule).

2. Wengine wanasema kuwa waamini hawapaswi kuwaambia ukweli watu waovu wasiostahili kuambiwa kwenye mazingira yanayohatarisha maisha.

3. Shifra na Pua hawangeweza kuwazalisha wanawake wote hao: badala yake inaawezekana walikuwa wanalisimamia "jeshi" la wazalishaji lilikuwa likifanya kazi hii. Wazalishaji hawa waliokuwa chini yao wanaweza kuwa ndio waliodanganya au walichelewa kwa makusudi.

 

S: Kwenye Kut 1:16, je mpango wa Farao wa kuwaua watoto wa kiume wa Kiisraeli haukuwa wa kijinga kwani watoto hawa wangekuja kuwa watumwa wazuri?

J: Palikuwa na Wamisri kama milioni 4.1 hivi. Ikiwa Waisraeli walikuwa wakiongezeka kwa kasi kubwa kuliko Wamisri, idadi yao huenda ilikuwa milioni 2, Farao aliingiwa na hofu.

Kama wazo la ziada, ingawa Farao aliagiza kuuawa kwa watoto wa kiume wa Kiebrania, kinyume chake, Mungu alimfanya mmoja wa hao watoto alelewe kwenye nyumba ya Farao mwenyewe.

 

S: Kwenye Kut 1:16, kwa nini Musa alikuwa hatarini kuuawa na Farao kwani Haruni kaka yake haonekani kukabiliwa na hatari hiyo?

J: Kwa mujibu wa Walter Kaiser kwenye A History of Israel uk.89, kama Musa alizaliwa mwaka 1526 (miaka 80 kabla ya Kutoka kwa Waisraeli Misri), atakuwa alizaliwa mwaka wa kwanza wa ufalme wa Thutmose I (mwaka 1526-1512 KK), na anaelekea kuwa ndiye mfame wa Misri (Farao) aliyetoa agizao hili.

Kama wazo la ziada, Farao aliyetaka kumuua Musa baada ya kumuua Mmisri anaelekea kuwa Thutmose III (mwaka 1504-1450 KK). Hakuna Farao mwingine aliyeishi muda mrefu, hivyo huenda habari iliyoandikwa kwenye Kutoka si sahihi, au palitokea "bahati kubwa sana" kuwa Farao pekee aliyeishi muda mrefu alitokea kutawala muda unaoendana na tukio hili.

 

S: Kwenye Kut 1:17, je waamini wanapaswa kumuogopa Mungu?

J: Ndiyo. Tazama sehemu ya pili ya jibu la Kutoka 9:30.

 

S: Kwenye Kut 2:1, je hadithi ya Musa kwenye kikapu inafananaje na hadithi ya Sargon?

J: Sargon wa Akadi (karibu mwaka 2355-2279 KK) kwa mujibu wa hadithi za kale zisizothibitishwa Sargon aliwekwa kwenye kikapu kilichotengenezwa kwa matete na kupakwa lami na kuwekwa mtoni. Aki, mtunza bustani, alimuokoa na kumlea kama mtoto wake. Lakini, mama yake Musa alifany hivyo kwa sababu ya mfalme, na hakumwacha, bali alimtuma Miriam kumwangalia.

 

S: Kwenye Kut 2:3, kama Mungu alimpenda Musa, kwa nini alimruhusu kupitia kwenye hatari kubwa namna hii ya a kuzama, kuonekana, na mamba?

J: Mungu anaona mambo yote, na ni dhahiri kuwa anaona mambo mengine tofauti na sis. Mungu Mwenyezi alikuwa na wa kutosha kunfanya Musa awe salama. Hata tukiwa kwenye mafuriko yenye kutisha, mahali salama zaidi kuwepo ni katika mapenzi yake.

Nina uhakika kuwa jambo hili lilikazia fikra hii kwa Musa kuwa aliokolewa kwa kusudi maalumu. Watu wengine wanaweza kuona kuwa kwa jinsi Mungu alivyomhifadhi Musa atawahifadhi na wao pia.

 

S: Kwenye Kut 2:5, kwa nini binti wa Farao alikwenda kuoga kwenye Mto Naili, na vipi kuhusu mamba?

J: Leo hii, mamba hawapatikani kaskazini mwa Aswan, lakini kwenye nyakati za kale walipataka mbali zaidi hata Memphis. Inaelekea kuwa binti wa mfalme alipenda kuoga kwenye ukanda wa delta ulio kaskazini (ambako Waebrania waliishi), ili awe mbali na mamba. Binti Farao anaweza kuwa alizoea kuoga kwenye kijiti kidogo, si lazima uwe mkondo mkuu wa Mto Naili. Pia, kuoga huku kunaweza kuwa kulikuwa kwa ajili ya utakaso wa kidini si kuwa msafi tu.

 

S: Kwenye Kut 2:10, je jina Musa ni la Kimisri au Kiebrania?

J: Jina Musa si la kawaida kwa sababu ni la Kimisri na Kiebrania. Kwa Kiebrania jina Moseheh linatokana na kitenzi masah, lenye kumaanisha "kuchukua kutoka." Kwa Kimisri, kitenzi ms/mes, chenye kumaanisha "kuchukua kutoka, kuzaliwa", au "(mungu huyu na yule) amwzaliwa." Kisarufi, ni muundo wa Kimisri cha kale wa ki ‘pafektive' ambao unahusiana na aspekti yenye kuonyesha kitenzi kikamilifu kwa mujibu wa The Expositor's Bible Commentary uk.310. ms ni muisho wa kawaida kwenye Ptahmose, Thutmose, Ahmose, na Ramose. Jina la Kimisri ms' linaweza kumaanisha "mtoto au mtoto wa kiume."

 

K: Kwenye Kut 2:14,15 Musa aliondoka Misri akihofia hasira ya mfalme, lakini kwenye Ebr 11:27 Musa aliondoka Misri bila kuwa na hofu ya mfalme.

S: Kwenye Kut 2:14, 15, alipokuwa na miaka 40, Musa aliondoka kwa mara ya kwanza akihofia hasira ya mfalme. Kwenye Kutoka 13-14, alipokuwa na miaka 80, Musa aliondoka mara ya pili bila kuhofia hasira ya mfalme, na Ebr 11:27 inaongelea kuondoka kwa mara ya pili. Musa mara ya pili kukabiliana na hofu yake, lakini wakati huu alijua kuwa ana lengo la kulitimza, na kuwa Mungu atamlinda.

 

S: Kwenye Kut 2:18, ilikuwaje baba mkwe wa Musa aliitwa Reueli, kwani alikuwa ni Yethro kwenye Kut 3:1 na 4:18?

J: Baba mkwe wangu mwenyewe ana majina mawili ambayo hayahusiani (Kichina na Kiingereza), kwa hiyo nafikiri jambo hili si ajabu. Jambo pia halielekei kuwa lilionekana kuwa la ajabu kwa Abram/Abraham, Sarai/Sara, Yakobo/Israeli, Ben-Oni/Benjamini, Zafenathi-Panea/Yusufu, Hoshea/Yoshua, Gideoni/Yerubaali, Hanania/Shedraki, Mishaeli/Meshaki, Azaria/Abednego, na Danieli/Belteshaza.

Mara nyingi watu huwa na majina tofauti kwa lugha tofauti, na inaonekana lilikuwa jambo la kawaida mtu kupata jina lingine miaka yake ya baadaye, kama ambavyo Gideoni/Yerubaali na Hoshea/Yoshua wangeweza kukueleza. Kuhusiana na baba mkwe wa Musa, Walter Kaiser kwenye A History of Israel uk.92, anataja Ugaritic Textbook cha Cyrus H. Gordon (1965) kama chanzo cha taarifa, anasema kuwa majina Yethro, (na Hobab) yapo kwenye lugha ya Kigariti (lugha iliyoongelewa maeneo ya kaskazini ya Siria ya kale). Re'u'el linamaanisha "rafiki au mchungaji wa Mungu."

Kwenye jamii nyingine, ilikuwa kawaida mtu kuwa na majina zaidi ya moja. Huko Misri, Osiris, Wennofer, na Khent-amentiu yalikuwa majina ya sanamu moja. Sebek-khu na Djaa yalikuwa majina ya mtu mmoja. Huko Mesopotamia, Ahiqar ni mtu aliyeitwa pia Aba'enlil-dari, na Tiglath-pileser ni Pul pia. Sheria za Lipit-Ishtar zinamwita mungu mmoja Enlil na Nunamnir, na sheria za Hammurapi zina Inana/Ishtar/Telitum na Nintu/Mama. The Expositor's Bible Commentary juzuu ya 2 uk.313 inasema kuwa vyanzo vya kusini mwa Arabia pia vina watu wenye kuwa na majina mawili. Isitoshe, akitoa mifano hii kwenye Ancient Orient and Old Testament (IVP 1966) uk.121-124, Kenneth Kitchen anasema kuwa majina mawili yalikuwepo Kanaaani, Arabia ya Kusini ya Kale, Wahuria, na Wahiti.

Josephus ana maelezo tofauti. Anadhania kuwa Reueli lilikuwa jina lake, na Yethro cheo chake.

 

S: Kwenye Kut 2:21-22, tuna haja gani ya kumheshimu Musa ambaye [kama inavyodaiwa] alikuwa na mtoto aliyemzaa nje ya ndoa?

J: Maandiko hayasemi kuwa Musa alikuwa na mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa. Kutoka 2:21 inaposema kuwa Reueli alimpa Musa binti yake, Sipora, alimpa awe mke wake. Kama ushahidi wa jambo hili, Kut 4:20 inamwita Sipora mke wake, na Kut 4:25, Sipora mke wake anamtaja Musa kuwa "bwana arusi wa damu" kwake.

 

S: Kwenye Kut 3:2, malaika wa BWANA alikuwa ni nani hasa kwenye mwali wa mot uliotoka katikati ya kijiti?

J: Neno "malaika" linaweza kumaanisha mjumbe. Kuna mambo matatu yanayowezekana, hebu na tuyaangalie yote haya.

Kiumbe mwema wa aina ya malaika aliyeumbwa na Mungu: Kut 3:2 inasema "malaika wa BWANA." Hata hivyo, kwa nini Musa alilzimika kuvua viatu vyake, kwa sababu pale palikuwa mahali pale palukuwa patakatifu kwenye Kut 3:6?

Mungu (ama Utatu Mtakatifu auma Mungu Baba): Anayesema, "Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa YakoboI." Licha ya hayo kujifunua kwa Mungu katika Agano la Kale kunaitwa ‘theophany.'

Yesu Kristo: Kanisa la awali lilichukulia kwa pamoja kuwa huku kulikuwa ni kutokea kwa Yesu, Neno la Maungu, kabla ya kufanyika kwake kuwa mwili duniani. Yesu alisema "Mimi ni Mungu . . ." na Yesu alikuwa ni mjumbe pia, au Neno la Mungu Baba. Licha ya hayo, kutokea bayana kwa Mungu Mwana kwenye Agano la Kale kunaitwa ‘Krtistofani.'

 

S: Kwenye Kut 3:8, Wahiti waliwezaje kuwepo Kanaani nyakati za Musa na Yoshua?

J: Tazama maelezo kwenye Mwanzo 23 kwa ajili ya jibu la swali hili.

 

S: Kwenye Kut 3:8,17 na Yos 25:6, kwa nini Kanaani inaitwa nchi iliyojaa maziwa na asali?

J: Kwa Waisareli waliokuwa wafugaji, Kanaani ilikuwa ni nchi yenye milima na mabonde yenye rutuba yafaayo kutunzia mifugo iliyonona nan a maua kwa ajili ya nyuki.

 

S: Kwenye Kut 3:10 na 6:10-13, je Musa aliitwa na Mungu alipokuwa Midiani au Misri?

J: Musa aliitwa na Mungu kwa mara ya kwanza kabisa alipokuwa Midiani. Hata hivyo Musa alianza kuwa na mashakabaada ya kurudi Misri, na Mungu alithibitisha wito wake kwa Musa alipokuwa Misri. Mara nyingine hata siku za leo, watu huhitaji uthibitisho wa mambo ambayo wanayajua kuwa kweli.

 

S: Kwenye Kut 3:18, je Musa aliongea uongo alipomwomba Farao awaruhusu Waisraeli waende jangwani kwa muda wa siku ili kumtolea Mungu wao sadaka?

J: Hapana. Kuna mambo sita ya kuyazingatia, kisha sababu yenye uwezekano kuwa ndiyo inayofanya maneno haya ya Musa yasiwe uongo.

1. Mungu alisema angewatoa Waisraeli Misri na wasirudi tena (Kut 3:17), na baadaye Mungu alifanya hivyo.

2. Ilikuwa ni amri ya Mungu, siyo maneno ya Musa kuwa wakati huu aombe tu ruhusa ya kwenda jangwani kwa siku tatu, badala ya kuomba ruhusa ya kuondoka Misri (Kut 3:18)

3. Mungu alifahamu hakika, na alimwambia Musa kuwa Farao hatawapa ombi lao hili dogo (Kut 3:19)

4. Kinadharia tete, kama Farao angempa Musa ombi lake, hakuna kitu chenye kuonyesha kuwa Musa angemdanganya Farao na kutorudi Misri.

5. Kinadharia tete, kama wangeenda na kurudi, jambo hilo lisingewazuia kuomba tena kuondoka moja kwa moja.

6. Kutosema jambo si kuongopa. Tukiongea kibayana zaidi, kuomba jambo dogo na kuwa kutokusema kuhusu jambo kubwa ambalo utaliomba badaye si kudanganya.

Kwa nini Mungu alitaka Musa aombe jambo hili dogo kwanza? Yaelekea kuwa haikuwa uongo bali neema. Mungu alimpa Farao na Wamisri nafasi ya kukubali ombi dogo na kujizoeza polepole kuwaacha Waisraeli waondoke. Hata hivyo, wakati huohuo Mungu alipowapa nafasi hiyo, alikwishajua, kwa uhakika kabisa, matokeo ya matendo huru ya Farao. Leo hii, Mungu hutoa nafasi ya wakovu kwa watu wote, lakini Mungu tayari anajua matokeo ya matendo huru ya kila mtu.

 

S: Kwenye Kut 3:22 na Kut 12:33-36, kwa nini Mungu aliwaambia Waisraeli wawaombe Wamisri vitu vya thamani?

J: Neno la Kiebrania sa'al linamaanisha "omba" siyo "kopa." Kuna mambo matatu ya kuzingatia katika kujibu swali hili.

1. Hapakuwa na uongo: Wamisri walijua kuwa Waisraeli walkuwa wanaondoka na vitu watakavyowapa (Kut 12:31-6). The Expositor's Bible Commentary juzuu ya 2, uk.324 inasema neno la Kiebrania lenye kumaanisha kuchukua kitu kwa nguvu, nissaltem, halimaanishi kibayana kuiba, ulaghai wenye lengo la kujinufaisha kifedha, au uongo. Pia inasema kuwa "kopesha/kuazima" hudhaniwa mara nyingi tokana na athari ya tafsiri mbaya katika kipindi ambacho Kiebrania hakikufahamika au, kama ilivyo sasa, tokana na mtazamo usio na sababu wa imani kuwa maoni na matendo yote yanatakiwa yatokane na mantiki na ufahamu badala ya imani za kidini au maitikio ya kihisia."

2. Hapakuwa na kutumia nguvu: Wamisri walipendezwa nao, na walikuwa wanawasihi kuondoka kwenye Kut 12:33-36.

3. Hapakuwa na dhuluma: Vitu vilivyotolewa vilikuwa ni malipo kidogo ya kosa la kuua watoto wadogo na miaka 400 ya utumwa. Wazo hili la tatu (kama yalivyokuwa mawili ya kwanza kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja), yalielezwa na Tertullian kwenye Against Marcion kitabu cha 2, sura ya 21, uk.313-314, mwaka 207/208 BK. Jibu hili pia limo kwenye Against Heresies kitabu cha 5, sura ya 30 aya ya 2, kitabu kilichoandikwa na Irenaeus mwaka 182-188 BK.

Muhtasari: Waisraeli waliomba, na Wamisri, ambao kwa wakati huo walikuwa wanawahurumia, waliwapa ombi lao.

 

S: Kwenye Kut 3:22 na Kut 12:33-36, je Mungu angewezaje [kama inavyodaiwa] kuwafundisha Waisraeli kutokuwa waaminifu na kuiba? Mtu asiyeamini uwepo wa Mungu aliuliza swali hili.

J: Je umewahi kuomba kupata kitu chochote kile? Kama umewahi, je jeambo hilo linakufanya uwe mwizi? – Hakika sivyo hivyo, kufikiri kwa jinsi hii ni ujinga. Vivyo hivyo:

1. Wamisri walijua kuwa Waisraeli walikuwa wanaondoka. Ukweli ni kwamba, Wamisri walikuwa wanawaomba Waisraeli waharakishe kuondoka kwenye Kut 12:33.

2. Waisraeli waliwaomba Wamisri wawape vitu hivyo vya thamani (Kut 12:35-36).

3. Wamisri walipendezwa na Waisraeli na waliwapa (si kuwakopesha) vitu hivyo (Kut 3:22; 21:36).

Kama ilivyoelezwa kwenye jibu la swali lililotangulia, The Expositor's Bible Commentary juzuu ya 2, uk.324 inasema neno la Kiebrania lenye kumaanisha kuchukua kwa nguvu, nissaltem, kibayana halimaanishi kuiba, ulaghai wenye lengo la kujinufaisha kifedha, au uongo.

 

S: Kwenye Kutoka 4, je tunaweza kujifunza nini kuhusu itikio la Musa kwa wito wa Mungu?

J: Kwanza kabisa, Mungu alimwonyesha Musa nguvu zake za ajabu (Kut 3:2), kisha uvumilivu wa kufanya kazi na Musa aliyekuwa visingizio vingi vilivyotokana na kukosa imani (Kut 4:1-13), na mwishoni hasira yake ikawaka kwa Musa. Tunao wajibu wa kuitikia wito wa Mungu, na kujiepusha na kutokutii kwa sababu uoga, uasi, au imani katika udhaifu wetu. Natumaini kuwa hufiki hatua ya kumfanya Mungu kuwa mkali kabla ya kuitikia wito wake.

Wakati Musa aliposema kuwa hawezi, tunaweza kuona mambo mawili ya kweli na jambo moja lililotokana na kutokuwa na imani.

1. Musa alisema ukweli kabisa kuwa watu wanaweza wasipende kumwamini mtu toka nje ambaye hawamfahamu, na kuwa hakuwa mwepesi wa kusema.

2. Musa alifahamu kwa uaminifu wote kuwa kwa nafsi yake mwenyewe hangeweza kufanikiwa katika jukumu hili.

3. Musa aliamini uongo uliotokana na kutokuamini kuwa Mungu hakuwa na nguvu za kutosha kutimiza mapenzi yake kupitia udhaifu wa Musa. Ninaomba kuwa ikiwa una uongo huu moyoni mwako uuweke wazi, utubu dhambi hii kwa Mungu, na kuamua kuamini kuwa ukuu wa Mungu ni mkubwa kuliko udhaifu wako mbaya zaidi.

 

S: Kwenye Kut 4:3-5, je fimbo isiyokuwa na uhai inawezaje kuwa nyoka?

J: Jambo hili si ujanja tu, kwani kwenye Kut 7:12 nyoka alikuwa na uwezo wa kumeza. Mungu ni mkubwa kuliko kanuni za kiasili za kimwili na za kibiolojia, na si kinyume chake.

 

S: Kwenye Kut 4:11, je Mungu haruhusu tu lakini pia huwafanya watu kuwa bubu, viziwi, na vipofu?

J: Upende usipende, Mungu huuruhusu kila uovu na ulemavu unaotokea. Pia, nyakati nyingi Mungu huwa na kusudi maalumu la kuwafanya watu namna fulani. Kwa hiyo miujiza mingi sana mikubwa ilifanywa kupitia Musa, lakini Mungu alichagua kumfanya awe na kigugumizi (Kut 4:10-13, 6:12,30) na kutokukiondoa. Vivyo hivyo, miujiza mingi sana ilifanyika kupitia kwa Paulo, lakini kwenye 2 Kor 12:7-9, Mungu alichagua kutokuuondoa mwiba wa Paulo.

 

S: Kwenye Kut 4:18, kwa nini jina "Yethro" linaandikwa kwa njia tofauti?

J: Baadhi ya lugha, kikiwemo Kiarabu, zina miisho tofauti ya majina kulingana na jinsi linavyotumika kwenye sentensi. Sehemu nyingine, jina Yethroe lilitafsiriwa kwa Kiebrania kwa mfumo tofauti likiwa mwisho mmoja mahali fulani na mwisho tofauti mahali pengine. Jambo hili lilifanyika pia kwa Geshemu/Gashmu, Mwarabu wa Ne 2:19; 6:1-2,6. Jambo lenye kufarahisha zaidi kuhusu Kut 4:18 ni kuwa miisho yete imetumiwa kwenye aya moja. Inaonekana waandishi hawakutafutiza sana kuwa tahajia zinazofanana za majina, na hivyo basi nasi hatupaswi kufanya hivyo.

 

S: Kwenye Kut 4:18, kwa nini Musa alisem anatake wkenda Misri "kuona kama bado wapo?"

J: Endapo sababu zake zilikuwa sahihi au si sahihi, Musa alichagua kutokusema bayana na kuficha sababu yake kuu ya kurudi kwake Misri. Biblia haiutetei usiri wa Musa, inaurekodi tu.

 

S: Kwenye Kut 4:22, je Israeli alikuwaje mzaliwa wa kwanza wa Mungu?

J: Mzaliwa wa kwanza ana haki, upendeleo, na majukumu maalumu. Waisraeli walikuwa watu waliochaguliwa na Mungu, kupitia kwao neno la Mungu lingeenea duniani kote. Walikuwa:

Wameasiliwa kuwa watoto (Rum 9:4)

Wamekabidhiwa maneno ya Mungu (Rum 3:2), kupokea sheria (Rum 9:4)

Mababu (Rum 9:5)

Uzao wa Yesu kwa jinsi ya kibinadamu (Rum 9:5)

 

S: Kwenye Kut 4:24, kwa nini Mungu alikaribia kumuua Musa?

J: Kuna mambo manne ya kuzingatia katika kujibu swali hili:

Mandhari: Ingawa Mungu alijua kuwa Musa hatakufa, mambo yalionekana kukatisha tamaa sana kwa upande wa Sipora.

Sababu: Aya hii haisemi ni kwa jinsi gani Musa alikuwa karibu ya kufa, huenda kwa ugonjwa, lakini wanafahamu kuwa Mungu alifahamu si tu kuwa aliruhusu jambo hili, lakini pia alilifanya litokee kwa makusudi kabisa.

Adhabu: Sipora na Musa hawakuwa wamelitimiza agano la tohara na Ibrahim, na Mungu aliwaadhibu hadi wakati Musa alipolitimiza.

Tahadhari: Kama Musa alivyotambua, hakuna mtu alinayeweza kuwa mkubwa sana hata asiwe na wajibu wa kumtii Mungu tena.

 

S: Kwenye Kut 4:30, je watu wanatakiwa kuamini kwa ajili ya miujiza?

J: Watu hawapaswi kumwamini Mungu tu kwa sababu ya miujiza. Miujiza ina nafasi yake inayofaa katika kuthibitisha imani kwa wajumbe wa Mungu. Miujiza hii haikuwa na lengo la kuthibitisha uwepo wa Mungu kwa watu hawa; badala yake, miujiza ilikuwa na lengo la kuthibitisha kuwa Musa alitoka kwa Mungu aliye hai.

 

S: Kwenye Kut 4:31 na Kut 6:9, je watu walimwamini Musa au la?

J: Walimwamini Musa mwanzoni kwenye Kut 4:31, lakini baadaye walikuwa na shaka kwenye Kut 6:9 baada ya Farao kuwaongezea uwingi wa kazi.

 

S: Kwenye Kut 5:2, nani aliyekuwa mfalme wa Misri na Waisraeli walitoka lini?

J: Farao aliyekufa hapa anaelekea kuwa Thutmose III. Malkia wake mkuu alikuwa Hatshepsut Meritre (tofauti na mama yake, Hatshepsut aiyekuwa maarufu sana). Waisraeli walitoka Misri karibu mwaka 1446/1445 KK. Sababu ya kuchukua tarehe hii 1446/1445 ni 1 Fal 6:1, ambayo inasema kuwa Sulemani alianza kujenga hekalu miaka 480 baada ya Waisraeli kutoka Misri, na wana elimukale wanaamini kuwa mwaka huo utakuwa ni 966 KK.

Kama wazo la ziada, Eusebius anasema kuwa jinal la binti wa Farao aliyemtoa Musa mtoni ni Merris kwenye Praeparatio Evangelica 9.27. Josephus anasema ni Thermuthis kwenye Antiquities 2. 224 (9.5), na Kitabu cha Jubilees 47:5 kinasema jina lake lilikuwa Tharmuth.

Wakati huu ulikwa chini ya ama Thutmose III, au kuna uwezekano mkubwa zaidi kuwa Farao Amenhotep II (mwaka 1450/20-1401/1385 KK). Malkia wake mkuu aliitwa Tia. Wakristo wengine walikuwa wakidhani kuwa Waisraeli walitoka Misri baadaye sana wakati wa utawala wa Rameses II (1290-1224 KK). Mwaka 1446/1445 KK unachukuliwa kwa sababu:

1. Kwenye 1 Fal 6:1 Biblia inasema miaka 480 kabla ya hekalu la Sulemani.

2. Wakati wa utawala wa Amenhotep II, Wasemiti walilazimishwa kutengeneza matofali.

3. Dream Stela wa Thutmose IV. Tazama maelezo kwenye Kut 12:29.

4. Amu 11:26 inasema miaka 300 kabla ya Yeftha.

5. Mji wa Hazori haukukaliwa baada ya karne ya 13 KK.

6. Mbao za Amarna zilizoandikwa mwaka 1400 KK zinasema kuwa waliogopa "Wahabiru" au "Abiru" hata walicharuka.

7. Clement wa Alexandria, kwenye Stromata 1:21 (mwaka 183-217 BK), anasema miaka 450 kutoka wakati wa Yoshua hadi Daudi.

8. Jina la Rameses lilitumiwa kabla ya karne ya 13 KK. Ramose lilikuwa jina la mtu mwenye cheo kikubwa wakati wa Amenhotep III.

Ingawa watu wengine wana maoni kuwa "Kutoka [kwa Waisraeli Misri] kulitokea wakati ule (mwaka 1449 KK) ni jambo lisilofikirika." Hata hivyo, njia ya kupima umri wa vitu kwa kutumia kiasi cha kaboni imeonyesha tarehe ya kuangushwa kwa Yericho karibu mwaka 1410 KK. Farao aliyetawala miaka 40 kabla ya muda huo atakuwwa Thutmose III.

 

S: Kwenye Kut 5:2, je Farao huyu alikuwa ni yule yule wa kwenye Kutoka 15?

J: Kwa mujibu wa The Bible Knowledge Commentary : Old Testament, uk.115-116, hakuwa mtu mmoja. Farao wa Kutoka 1, huenda alikuwa Thutmose III, alitaka ama kuwaondosha kabisa ama kuwapunguza Waisraeli. Farao wa wakati Waisraeli walipokuwa wanatoka Misri, hunda Amenhotep II (mwaka 1450/1420-1401/1385), alijishughulisha zaidi na kuwatumia kama watumwa. Kumbuka, kulikuwa na kipindi cha miaka 80 kati ya Kutoka 1 na Kutoka 5.

 

S: Kwenye Kut 5:3; 8:26-27 na 10:26, je Musa alikuwa anatoa sababu tu za kuondoka?

J: Maandiko hayasemi endapo Mungu alimwambia Musa amweleze Farao sababu hizi za kuondoka, au endapo Musa aliziongea kwa kujiamulia yeye mwenyewe tu. Kama alijiamulia yeye mwenyewe, tazama kuwa Maandiko hayasemi endapo Musa alisema kila kitu kwa usahihi.

 

S: Kwenye Kut 5:6, kwa nini wanatumia majani makavu (mabua) kutengeneza matofali?

J: Majani makavu yaliyafanya matofali yawe na nguvu zaidi, kwa sababu udongo unaokuwa umeshikwa humo hauna uwezekano mkubwa wa kutoka.

 

S: Kwenye Kut 5:6-7, je Waisraeli waliwezaje kukabiliana na kazi ya ziada ya kukusanya mabua yao wenyewe?

J: Kwanza inabidi kufahamu kuwa majani makavu (mabua) yalikuwa muhimu katika kuyafanya matofali yawe imara, kwa sababu yalikuwa kitu chenye kushikilia kinachopunguza matofali kupukutika. Pia ingawa matofali yalikuwepo zaidi Mesopotamia kuliko Misri, baadhi ya miji ya Misri kama vile Pithomu ilijengwa kwa matofali. Kaburi la kiongozi wa ngazi ya juu nchini Misri aliyeitwa Rekhmere/Rek-mi-Re aliyeishi Thebes kwenye karne ya 15 KK lina michoro ya watumwa wakiwa wanatengeneza matofali. Picha ya mchoro huu imo kwenye The New International Dictionary of the Bible, uk.174.

Mabaki yaliyopo Pithomu yanaonyesha matofali yakiwa na majani makavu kwenye ngazi za chini za kuta, matofali yenye mashina ya nyasi/mabua yaliyokatika kwenye ngazi za kati, na matofali yasiyo na nyuzi nyuzi kwenye ngazi za juu. Matofali yalitofautiana ukubwa kutoka sm 33 kwa 33 kwa 9 (inchi 13 kwa 13 kwa 3 ½) had ism 41 kwa 20 kwa 15 (inchi 33 kwa 33 kwa 9).

 

S: Kwenye Kut 6:1, kwa nini mkono wa Mungu wenye nguvu umetajwa bayana hapa?

J: Ubashiri unaofurahisha unasema kuwa katika wakati huu, wafalme wa Misri walikuwa wakitumia mara kwa mara msemo "mmiliki wa mkono [wenye nguvu]" kama sehemu ya majina ya vyeo vyao. Kut 6:1 inasistiza kuwa mikono yao yenye kujivuna haikuwa kitu ikilinganishwa na mkono wa Mungu.

 

S: Kwenye Kut 6:3 na vifungu vingine, je nadharia ya JEPD ina matatizo gani?

J: Nadharia ya JEPD ilifikiriwa kwa mara ya kwanza kabisa karne ya kumi na tisa kabla ya wanazuoni kuhakikisha kuwa watu wa kawaida walikuwa wanaweza kuandika wakati wa Musa. Inasema kuwa vitabu vitano (au wakati mwingine sita) vya kwanza vya Biblia vilihaririwa pamoja kutoka kwenye vyanzo vyake vya awali vilivyoitwa J (Jehovah, Yehova), E (Elohim), P (Priestly, ukuhani), na D (Deuteronomy, Kumbukumbu la Torati).

Kuna matatizo mengi kwenye nadharia hii ya JEPD, yafuatayo ni mawili kati ya hayo.

1. Wanazuoni wenye utayari wa kufuata maoni mapya na kutilia shaka/kutoafiki msimamo wa asili au mapokeo hawakubaliani juu ya aya zilizo kwenye J, E, P, na D.

2. Aya nyingi zinalazimika kugawanywa katikati. Kwa mujibu wa Evidence that Demands a Verdict volume II, uk.134, the Interpreter's One-Volume Commentary toleo la Biblia la nadharia ya JEPD linagawanya mistari hii na kuiweka kwenye vyanzo viwili au zaidi.

Mwa 2:4; 7:16, 17; 8:2, 3, 13; 10:1; 12:4; 13:11, 12; 16:1; 19:30; 21:1, 2, 6; 25:11, 26; 31:18; 32:13; 33:18; 35:22; 37:25, 28; 41:46; 42:28; 45:1, 5; 46:1; 47:5, 6, 27; 48:9, 10; 49:1, 28

Kut 1:20; 2:23; 3:4; 4:20; 7:15, 17, 20, 21; 8:15; 9:23, 24, 35; 10:1, 13, 15; 12:27; 13:3; 14:9, 19, 20, 21, 27; 15:21, 22, 25; 15:13, 15; 17:1, 2, 7; 19:2, 3, 9, 11, 13; 24:12, 15, 18; 25:18; 31:18; 32:8, 34, 35; 33:5, 19; 34:1, 11, 14

Hes 13:17, 26; 14:1; 16:1, 2, 26, 27; 20:22

(Kumbukumbu la Torati halitajwi kwa kuwa inachukuliwa kuwa kitabu chote kimo kwenye chanzo "D").

Je ni mistari mingapi inatakiwa kugawanywa katikati kabla hata nadharia hii haijajitetea? Mistari tisini na moja ni mingi kupita kiasi.

 

S: Kabla ya Kut 6:3, kwa nini vifungu 197 vinatumia jina "Yahweh", kwa kuwa Kut 6:3 inasema kuwa Mungu hakujifunua kwa jina hilo kwa Ibrahimu, Isaka na Yakobo?

J: Tuangalie kwanza kitu ambacho siyo jibu, kisha jibu la swali hili.

a) Mambo ya kweli yasiyo sehemu ya jibu.

a1. Kwa kuwa Musa aliandika Kitabu cha Mwanzo wakati wa uhai wake, siyo wakati wa Yakobo, Musa angeweza kutumia jina lolote alilopenda kutumia. Kwa mfano, watu wanaandika kwa usahihi kabisa kuwa Columbus aliigundua Marekani, hata kama Columbus hakujua jina "Marekani au Amerika." Jambo hili pekee linaelezea sehemu zote isipokuwa 53 ambazo ni nukuu za moja kwa moja au zile zinazofanana.

a2. Kwa kulinganisha Septuajinti (tafsiri ya Kigiriki ya Agano la Kale) na Toleo la Kimasoretiki (toleo rasmi la Kiebrania la Agano la Kale) inaonyesha kuwa watu waliokuwa wakinakili vitabu hivi wanaonyesha kuwa walikuwa huru katika kubadilisha majina ya Mungu. Julius Wellhausen alidai kuwa wazo hili lilikuwa ni udhaifu mkubwa zaidi wa nadharia yake mwenyewe ya vyanzo vya Pentatiuki.

a3. Jina la Mungu lilifahamika na Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, lakini Mungu hakufahamika kimsingi kama Yahwe. Mungu alikuwa anafunua maana kwa Musa ambayo hakuwa ameifunua kwa mababu hawa watatu wa taifa la Israeli.

b) Jibu la swali hili limo kwenye Kut 6:3 yenyewe

b1. Kut 6:3 haisemi nilijifunua [kwao] "kabla ya wakati wa Musa." Inasema tu "nilimtokea Ibrahimu, Isaka, na Yakobo."

(This eliminates 5 of the 53 passages.)

b2. Kutoka haisemi kuwa mababu hawa watatu hawakulifahamu jina la Mungu. Inasema tu kuwa "nilimtokea . . . bali kwa jina langu sikujulikana kwao." Ingawa Mungu aliongea au alitokea kwa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo mara zisizopungua 15, hakutokea kwao kwa njia maalumu inayohusiana na jina lake kama alivyotokea kwa Musa. Kwa kweli, wakati Yakobo alipouliza jina la mtu aliyeshindana naye usiku kucha kwenye Mwa 32:29, hakujibiwa.

Angalia pia swali linalofuata kwa maelezo zaidi.

 

S: Kwenye Kut 6:3, kwa kuwa Mungu hakujifunua kama Yahwe kwa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, tunaweza kusemaje kuhusu sehemu zifuatazo ambazo Mungu alijiita Yahwe? Mwa 15:7 "Mimi ni BWANA (Yahwe/Yehova), niliyekuleta kutoka Uru"; Mwa 18:14 "Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA?" Mwa 28:13 "Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka . . ."

J: Haya yanaweza kuwa mabadiliko yaliyofanywa baaaye na watu waliokuwa wananakili Maandiko. Vifungu vyote hivi kwenye Septuajinti (tafsiri ya Kigiriki ya Agano la Kale), neno Mungu (theos) limetumiwa, wala si neno la Kigiriki lenye kumaanisha "MIMI NiKO" kwenye Kut 3:14 (ho ōn), au neno la Kigiriki kwenye Kut 6:3 (kurios). Angalia pia maelezo kwenye swali lililopita.

 

: Kwenye Kut 6:16-20, je Waisraeli waliwezaje kuwa Misri miaka 430 kwani kulikuwa na vizazi vitatu tu vilivyotajwa kati ya Lawi na Musa?

J: Kulikuwa na vizazi zaidi ya vitatu, kwa sababu mara nyingi orodha za vizazi huwa na mapengo kwani mtoto anaweza kumaanisha mzao, na baba inaweza kumaanisha mhenga.

 

S: Kwenye Kut 6:20, kwa nini Amramu alimuoa Yokebedi shangazi yake kwani kufanya hivyo kulizuiliwa kwenye Law 18:11?

J: Kuna mambo mawili ya kuzingatia katika kujibu swali hili.

1. Kitabu cha Mambo ya Walawi kilikuwa bado kuandikwa wakati huo.

2. Pia, Biblia haikatazi jambo hili, bali inaripoti kwa uaminifu kitu kilichotokea.

 

S: Kwenye Kut 6:20, je Yokebedi na Amramu walikuwa wajukuu wa Lawi, wazazi wa Musa?

J: Siyo lazima iwe hivyo kwani neno ‘mtoto' linaweza kumaanisha ‘mzao', na Yokebedi hakutajwa kwa jina kwenye Kut 2:1-9. Kwa kuwa Kohathi alikuwa na wazao wa kiume 8,600 wakati wa Musa (Hes 3:28), haielekei kuwa Amramu, mtoto wa Kohathi, alikuwa Amramu, baba yake Musa. Tazama See When Critics Ask, uk.69-70, Encyclopedia of Bible Difficulties, uk.111, The Bible Knowledge Commentary: Old Testament, uk.117, 247, na The NIV Study Bible, uk.94, kwa maelezo haya

 

S: Kwenye Kut 6:26-27, je Musa aliandika kitabu hiki kwani kimeandika kuhusu Musa jwa kutumia nafsi ya tatu?

J: Hakuna sababu ya kutia shaka kuwa Musa aliandika kitabu hiki. Kuandika kwa kutumia nafsi ya tatu kulikuwa jambo la kawaida kwenye maandiko ya kale. Mifano mingine ni pamoja na hii ifuatayo:

1. Julius Kaisari, Gallic Wars.

2. Julius Kaisari, writing Civil Wars.

3. Xenophon, Anabasis.

4. Josephus, Wars of the Jews.

5. Mtume Yohana, Injili ya Yohana.

 

S: Kwenye Kutoka 7-11, kwa nini Mungu aliwapiga Wamisri kwanza badala ya kuwashawishi wawaruhusu Waisraeli kuondoka?

J: Kut 9:16 (na Rum 9:17) zinasema kuwa Mungu alifanya hivi ili kuuonyesha nguvu zake na kwamba jina lake litangazwe duniani kote. Kuna mambo sita ya kuzingatia.

a) Mungu ni mwenye enzi yote na anayo "haki" ya kuchagua njia yoyote anayopenda kutumia.

b) Mungu hakuwadhukumu Wamisri waliokuwa na miaka 400 ya "desturi ya kijamii" ya kuwatumikisha waebrania.

c) Mara nyingi watu walio chini ya kiongozi wanaathirika na maamuzi ya viongozi wao.

d) Mungu aliwapa nafasi ya kuwaruhusu watumwa wao waondoke. Hata hivyo, wao walichagua manufaa ya kiuchumi ya kuwaatumikisha watu wengine badala ya kuwafanyi watu wengine jinsi ambayo wao wenyewe wangependa wafanyiwe.

e) Jambo hili lilikuwa ni hukumu si kw Misri tu bali pia kwa miungu ya Kimisri. Jambo hili lilionyesha kuwa miungu hiyo ilikuwa ya uongo, na kwamba Yahwe ndiye Mungu pekee aliye wa kweli na mwenye nguvu.

f) Jina la Mungu lilitukuzwa duniani kote. Kwa kweli, Wamisri leo hii wanamwona Musa kama shujaa na nabii wa Mungu.

 

S: Kwenye Kut 7:1, je Musa aliwezaje kuwa kama Mungu kwa Farao?

J: Ufananisho huu hausemi kuwa Musa alikuwa Mungu, bali kwamba mawasiliano yote na vitu vyote vitakavyofanyika baina ya Farao na Mungu wa kweli vitapitia kwa Musa, akisaidiwa na Haruni. Tazama pia 2 Kor 3:20, ambapo tunawmbiwa kuwa sis tu barua nyaraka (barua) za Mungu kwa watu wengine. Kama mwanamke mmoja alivyosema, "Tunapaswa kuwa Biblia pekee ambazo watu wengine watazisoma."

 

S: Kwenye Kut 7:11,22 na Kut 8:7, je waganga wa Farao walionyeshaje uwezo wao wa kiganga?

J: Kama wazo la ziada, moja ya mbinu za kimazingaombwe zinayofanywa siku hizi, yenye kutumia vikombe vitatu vinavyofunika mipira, ilitumiwa Misri ya kale pia. Ingawa watu wanaweza kuwadanganya wenzao kwa kutumia mbinu za ujanja na zisizokuwa miujiza, shetani ana nguvu za kimiujiza kama 2 The 2:9 na Ufu 13:13 zinavyoonyesha. Waganga hawa wanaelekea kuwa walikuwa wanafanya vitu mbalimbali kwa kutumia nguvu za shetani.

 

S: Kwenye Kut 7:17-22, maji yaliwezaje kubadilika na kuwa damu?

J: Ingawa Wamisri wanaelekea kuwa walifahamu takataka nyekundu zilizokuwa zinatoka Ethiopia, takataka hizi nyekundu hazikuwa zinayachafua maji yaliyokuwa kwenye mitungi na ndoo za mawe. Kuna maoni mawili. Kwa kuwa hakuna jambo lisilowezekana kwa Mungu, hakuna haja ya kuuliza kuwa Mungu ‘alitakiwa kutumia' njia gani. Badala yake, inaweza kufaa kuuliz kuwa ni maoni gani yaliyo na ushahidi bora zaidi wa namna ambayo Mungu alichagua kufanya.

1. Damu ni damu halisi.

2. Maji yalikuwa mekundu, kama yale yaliyosababisha michipwi yenye sumu iliyosababisha kubadilika kwa rangi ya maji ya mto kunakoonekana kwenye bahari mbalimbali na Mto Naili. Michipwi huua samaki na kuyafanya maji yasinyweke.

 

S: Kwenye Kut 7:19 na 8:16, 24 je mapigo yalikifanywa katika "nchi yote" ya Misri, au yaliiacha Gosheni kwenye Kut 8:20, 22?

J: Kut 9:6 inajibu swali hili kwa kunyesha kuwa waliposema nchi yote ya Misri ilimaanisha kuwa Gosheni haikuwemo.

 

S: Kwenye Kut 7:20, je waganga waliwezaje kubadilisha maji kuwa damu kwani Musa alikuwa amekwisha badilisha maji ya mtoni kuwa damu?

J: Kut 7:20 inasema ni maji ya kwenye mto yaliyokuwa mbele ya Farao ndiyo yaliyobadilika mara moja kuwa damu. Maji mengine yanaweza kuwa yalibadilika muda mfupi baadaye.

Wakati mwingine, shetani anapofahamu muda wa Mungu anaweza akataka kusifiwa kwa jambo ambalo Mungu anafanya. Angalia maelezo kwenye Kut 12:29 au mfano mwingine unaowezekana. Tazama When Critics Ask, uk.73 na Haley's Alleged Discrepancies of the Bible, uk.434-435 kwa maoni tofauti, kuwa "yote" ilimaanisha sehemu kubwa ya maji.

 

S: Kwenye Kut 7:22 na 4:21, ni nani aliufanya moyo wa Farao kuwa mgumu?

J: Farao alikuwa mtu wa kwanza kufanya hivyo, na Mungu aliufanya mgumu pia. Mistari hii inamtaja aliyeufanya moyo kuwa mgumu:

Bwana ataufanya mgumu moyo wake (Kut 4:21)

Farao mwenyewe aliufanya mgumu moyo wake (Kut 8:15, 32; 9:34; 1 Sam 6:6)

Ulijifanya kuwa mgumu (yaani moyo wa Farao wenyewe ulijifanya kuwa mgumu (Kut 7:13-14, 22; 8:19; 9:7; 9:35)

Bwana alifanya mgumu (Kut 9:12; 10:1, 20, 27; 11:10; 14:4-5, 17)

Kwa muhtasari, Wakristo kama vile Clement wa Rumi (aliyeandika mwaka 96-98 BK kwenye 1 Clement, sura ya 51) hakuliona hili kuwa jambo la kuchagua moja ya vitu viwili bali vitu vyote viwili vilihusika.

Hali inayofanana na hii ipo Rum 1:21-32, ambapo Mungu aliwapa ukengeufu mkubwa zaidi watu wasioamini na waliokengeuka. Mungu hata aliufanya mgumu moyo wa Israeli kwenye Isa 63:17. Tazama pia maelezo kuhusu Rum 9:18 kwa habari zaidi.

Kama wazo la ziada, Mungu pia aliifanya migumu mioyo ya Wakanaani kwenye Yos 11:20.

 

S: Kwenye Kut 8:10, kwa nini Farao alimwambia Musa awaondoe vyura kesho na si leo?

J: Huenda siku ilikuwa imeenda sana, lakini hata hivyo wangeweza kuondolewa mara moja. Jambo linaweza kuonyesha namna ambayo moyo wa Farao ulikuwa mgumu. Alitaka kuhakikisha kuwa vyura hawaangamii zaidi wakati alipokuwa anaongea na Musa.

 

S: Kwenye Kut 8:16-19, hawa "chawa" walikuwa ni nini?

J: Hawa wanaweza kuwa wadudu ambao kwa siku hizi tunaweza kuwaita visubi, hawa wanasumbua sana ingawa hawaumi. Kwa upande mwingine, inawezekana pia kuwa walikuwa mbu. Watu hawana uhakika wa maana halisi ya neno la Kiebrania kinnim, kwa sababu kama Bible Knowledge Commentary: Old Testament, uk.122, inaonyesha kuwa hapa ni mahali pekee kwenye Biblia ambapo neno hili limetumika.

 

S: Kwenye Kut 8:19; 31:18; Kumb 9:10; Zab 8:3 na mingineyo, je Mungu ana kidole?

J: Hapana. Huku ni kueleza kwa kunakotumia umbo la binadamu kwenye kuonyesha nguvu ya Mungu. Kama wazo la ziada, msemo wa kiisimu (sayansi ya lugha) wenye kuonyesha utumiaji wa sehemu ya kitu kimoja kuelezea kitu kizima ni lugha ya picha inayoitwa sinekdoke (synecdoche). Kwa habari zaidi angalia maelezo kwenye Zab 91:4. Kwa mfano unaofanana na huu kwenye dini nyingine, Uislamu, Bukhari Hadith, juzuu ya 9, kitabu cha 93, sura ya 26 na.543, uk.409 inataja kidole cha Allah.

 

S: Kwenye Kut 8:19; 31:18; Kumb 9:10; Zab 8:3, na mingine, kwa kuwa haikuwa sahihi kutengeneza sanamu ya aina yoyote ile ya Mungu, kwa nini Biblia inatumia anthropomofisimu ya Mungu, kama vile kuwa na mkono, n.k.? (John L. MacKenzie aliuliza swali hili miaka kadhaa iliyopita)

J: Tofauti kati ya mambo haya mawili ni tofauti ya mawasiliano na ibada. Mungu alichagua kuwasiliana kwa kutumia njia ambazo wanadamu wanaweza kuelewa, ikiwa ni pamoja na kutumia mashairi, na maelezo ya kianthrofomia, kama vile "Mkono wake wa kiume."

Hata hivyo, Mungu yuko wazi kabisa katika kutuzuia kutengeneza sanamu au kuchora picha kwa lengo la kumwabudu au kumtukuza Mungu.

 

S: Kwenye Kut 8:20-32, je hawa walikuwa ni nzi wa aina gani?

J: Kuna nadharia kadhaa. Kwa mujibu wa The Bible Knowledge Commentary: Old Testament, uk.122-123, hawa wanaweza kuwa waliitwa "nzi wenye kushambulia mbwa" ambao wanauma na kuumiza sana. Hawa wanaweza kuwa waliwakilisha mungu wa Kimisri aliyeitwa Re. Kwa upande mwingine, wanaweza kuwa nzi mwenye kutagia mayai kwenye mabuu ya wenzao, waliomwakilisha mungu wa Kimisri aliyeitwa Uatchit. Nzi hawa wanaweza kuwa walivutiwa na vyura waliokuwa wanaoza.

 

S: Kwenye Kut 9:4; 11:23 na 12:13, je mapigo yaliwezaje kutowadhuru Waisraeli kwani yaliwadhuru Wamisri?

J: Mungu anao uwezo wa kutenda kwa kadri apendavyo. Pia kwenye Kut 15:26, ikiwa ‘Waisareli watamtii Mungu ameahidi kuwa hawatakuwa na magonjwa siku za mbele pia, kwenye Kut 15:26.

 

S: Kwenye Kut 9:6, 19-20, kwa kuwa ng'ombe wote na farai walikufa, je farasi waliweza kuishije kwenye Kut 14:9?

J: Kwenye Kut 9:6, neno ‘wote' linamaanisha ama ng'ombe walio nchi yote ya Misri, au ng'ombe wote walio kwenye mashamba ya Misri, au maana zote mbili. Katika mandhari hii, ukaribu wa Kut 9:19-20 na 9:6 unadhihirisha kuwa mwandishi hakukusudia kulifanya neno hili lieleweke kama kila mnyama, ndani au nje, bali wanyama walia mashambani.

 

S: Kwenye Kut 9:6, 19-20, je tunafahamu nini kuhusu ufugaji mifugo Misri?

J: Mifugo ya Misri ilitunzwa kwenye mabanda kuanzia mwezi wa tano hadi wa kumi na mbili wakati wa mafuriko ya Mto Naili ambapo malisho yanakuwa yamejaa maji. The Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 2, uk.357 inasema pigo hili linaweza kuwa lilitokea mwezi wa kwanza, wakati ambao baadhi ya mifugo ilikuwa inatolewa nje kula. Kwa sababu mafuriko yalikuwa yanachelewa kuisha kwenye delta kuliko sehemu nyingine za Misri, mifugo iliwekwa kwenye mabanda hadi baadaye zaidi. Ikiwa mnyama alikufa kwa sababu ya ugonjwa wa miguu na midomo kwa sababu vyura waliokuwa wanaoza, shida hii ingewadhuru zaidi wanyama walioko mashambani.

 

S: Kwenye Kut 9:16; 11:9, je Mungu alimwinua Farao kwa lengo la kumwadhibu tu?

J: Hapana, Maandiko hayasemi hivi. Yanasema kuwa Mungu alimwinua Farao pamoja na uovu wake uliokuwa unasumbua ili kuonyesha uwezo wake wa kuwatoa Waisraeli kwenye utumwa. Pamoja na kutumia uovu kuwaonyesha watu wengine nguvu na hukumu zake, Mungu pia aliuruhusu uovu kukua kwa muda, na Mungu analihukumu tunda linalozalishwa.

 

S: Kwenye Kut 9:19 na 9:27, Musa aliwezaje kusafiri kwenda kumwona Farao wakati wa pigo baya asana la mvua ya mawe?

J: Ni dhahiri kuwa mvua haikuwa kila mahali wakati wote. Hata wakati wa tufani huwa panakuwa shwari machoni pa dhoruba. Musa huenda alikwenda kwa Farao wakati mvua imetulia kwa muda mfupi kwenye sehemu baadhi ya maeneo ya Misri. Inawezekana pia kuwa Mungu alimlinda Musa wakati alipokwenda kwa Farao.

 

S: Kwenye Kut 9:20; Isa 28:5 na Ezek 4:9, je ni aina gani ya chakula kilicho limwa na wakulima wa wakati ule?

J: Chakula cha watu wa wakati ule kilikuwa tofauti sana na chakula cha kwenye jamii zenye maendeleo ya viwanda za siku hizi, kikiwa na aina nyingi zaidi za vyakula vya asili. Ulimwengu wa kale haukuwa na mahindi au viazi kwa sababu vyakula hivyo vilitokea Bara la Amerika. Walikuwa na ngano na shayiri kama tulizo nazo leo, lakini walilima kiasi kikubwa zaidi cha nafaka nyingine za kale ambazo tunalima kama vyakula vinavyoliwa zaidi sehemu fulani fulani tu. Kwa mfano, Einkorn, Emmer, na aina ya ngano ya zamani (spelt) mara nyingine huwa zinaitwa "ngano zilizofunikwa"; hazipurwi vema kama ngano. Shayiri, ulezi, na mtama hazina virutubisho vingi kama ngano, ingawa mtama na ulezi vingali vinatumika Afrika kama chakula cha binadamu. Nafaka iitwayo ‘Kamut', yenye radha nzuri sana, pia ilizalishwa. Nafaka nyingine za kale ni amaranth and quinoa. Hawakuwa na nafaka nyingine, triticale, inayotakana na kuchanganya mbegu za ngano na shayiri, kwa kuwa ililimwa kwa mara ya kwenza huko Scotlandmwaka 1875. Kwa habari zaidi angalia http://www.hort.purdue.edu/newcrop/proceedings1996/V3-156.html#EINKORNOrigin.

Kwa ajili ya vitu vyenye kuongeza utamu, mbali ya viazisukari na miwa toka kwenye nchi za kitropiki, kimsingi watu walitumia asali tu. Asali ina namba kubwa ya kemikali tofauti ndani mwake, na kila bechi ya asali ya porini ni tofauti kwa kuwa inategemea na maua amabayo nyuki wameyatembelea. Kuna mtu aliyewahi kusema kuhusu asali kuwa, kama chakula leo kitakuwa mchanganyiko wa vitu mbalimbali visivyofahamika, na vina kemikali mbalimbali ndani mwake kila wakati kinapotengenezwa, hapangekuwa na namna yeyote ya kukubaiwa na idara ya vyakula na madawa!

 

S: Kwenye Kut 9:23, inawezekanaje kuwa na moto uliochanganika na mvua ya mawe?

J: Jambo hili hutokea kwa kawaida mara nyingi tu wakati wa ngurumo kali za mvua yam awe zinazoambatana na radi. Hiki kinawezakuwa ndiyo chanzo cha moto kwenye Kut 9:29. Hata hivyo, Mungu angeweza kuuffanya kwa namna yeyote ambayo angependa.

 

S: Kwenye Kut 9:30, watu wanapaswa kumcha Mungu kwa namna gani?

J: Hatumchi Mungu kwa njia ifananayo na mtu anayemwogopa mtu mdhalimu na mwovu. Hata hivyo, tunapaswa kumcha Mungu kwa njia mbili.

1. Watu wasio amini wanapaswa kuhofia hukumu na ghadhabu vya Mungu.

2. Hofu pia inamaanisha heshima. Watu wote tunapaswa kumheshimu Mungu aliyetuumba, Yeye aliye sababu ya kuwepo kwetu, na Yeye ambaye atawahukumu watu wote na kuwapa watu uzima wa milele au kuwahukumu kwa kuwapeleka jehanamu kwenye mateso ya milele, jalala la ulimwengu. Kuna Wakristo wanaodhani kuwa Mungu anashindwa kuwa kama wanavyotaka mungu awe. Mungu wa kweli anafanana na tabia yake mwenyewe, lakini huenda hata asijisunbue kufanana na viwango vyako. Tazama pia jibu la swali la Kut 20:20.

 

S: Kwenye Kut 10:21-23, je ingewezekanaje kuwa na giza juu ya nchi ya Misri tu?

J: Mungu aliumba nuru na anaweza kuithibiti. Endapo hili lilikuwa ni badiliko la muda mfupi kwenye jua, kanuni asilia, au wingu jeusi, majivu ya volkeno, vizuizi vingine, au kitu kingine chochota ambacho hakijatajwa hapa, Mungu anaweza kufanya kitu chochote anachotaka.

 

S: Kwenye Kut 10:21-33, je kuna ushahidi wowote wa elimukale wa giza lililoikumba nchi ya Misri?

J: Huenda. Biblical Archaeology Review ya Januari/Februari 1991, uk.50 inasema "Maandishi ya Kimisri yaliyo andikwa baada ya kumalizika kwa Utawala wa Kinasaba XVIII (karibu mwaka 1350 KK) yanaelezea shida hii kama ifuatavyo:

"Jua limefunikwa na halitoi mwanga kwa watu. Maisha hayawezekani tena jua linapokuwa limefunikwa na mawingu. Ra [mungu] amegeuza uso wake mbali na wanadamu. Kama tu lingeangaza japo kwa saa moja! Hakuna anayejuaye mchana unapokuja. Kivuli cha mtu hakitambuliwi. Jua linafanana na mwezi mbinguni . . ."

Maneno haya yanaweza kuwa yanaongelea giza lililokumba nchi, au yanaongelea volkeno iliyotokea kwenye kisiwa cha Thera.

 

S: Kwenye Kut 10:29, Musa anasema hataonekana tena usoni pa Farao. Lakini, Farao anawaita Musa na Haruni waende kwake kwenye Kut 11:31. Jambo hili linawezekanaje? Je Musa alikuwa amekosea kwenye Kut 10:29 na kama ni hivyo, ni Mungualiyekuwa amemtuma kusema hivi au alisema yeye mwenyewe tu?

S: Kwenye Kut 10:29, ni dhahiri kuwa Farao alikuwa amechoka kumwona Musa, na kwa ajili hiyo lengo la Musa lilikuwa kwamba asiende kwa Farao tena. Lakini wakati Farao alimwagiza aende kwake, Musa alipaswa kwenda. Hebu tuliangalie jambo hili kwa njia tatu:

a) Ikiwa maneno haya yalikuwa unabii basi haukuwa unabii wa kweli.

b) Ikiwa maneno haya yalionyesha nia ya Musa basi yalikuwa ya kweli; Musa hakuja kwa kukusudia kwake mwenyewe; aliitwa.

c) Ikiwa maneno haya yalikuwa ni ahadi basi hii ahadi ya kibinaddamu (siyo ya Mungu) iliingiliwa kwa kutakiwa afuate amri ya Farao.

Kwa ufupi, Musa hakuwa anadanganya lakini alikuwa anategemea wazi kabisa kuwa hatakwenda tena kwa Farao na Musa hakuwa sahihi katika jambo hili.

Jambo la muhimu kuangalia ni kwamba manabii walikuwa wanadamu, na wangeweza kusema na kufanya vitu visivyo sahihi pia. Mfano mzuri zaidi ni Nathani alipokuwa anamwambia Daudi kuwa atajenga hekalu na kisha Mungu akimrekebisha Nathani kwenye 2 Sam 7:3-17. Nabii wa Mungu huwa hana makosa anapoongea kama nabii, yaani "asema Bwana" au misemo mingine inayofanana na huu. Wakati Musa ameshikwa na hasira na akaugonga mwamba mara kadhaa na kuwaita Waisraeli waasi, huenda alisema maneno mengine pia ambayo aliyajutia.

 

S: Kwenye Kut 11:3 na Hes 12:3, je Musa aliandika mwenyewe kuwa alikuwa mkuu na mnyenyekevu sana?

J: Kuna maoni matatu tofauti kuhusu swali hili:

a) Musa alikuwa anatoa mandhari ya kweli ya sifa yake.

b) Wakati maneno haya yalipokuwa yanaandikwa na mwandishi wa Musa, mwandishi aliyaongezea kwa uvuvio wa Mungu.

c) Maneno haya yalifanya kuongezwa na watu waliokuwa wananakili Maandiko, na Mungu aliruhusu nyongeza hiyo iendele kuwepo kwa miaka na miaka. Tazama pia maelezo ya Hes 12:3.

 

S: Kwenye Kut 11:5-12:30, mbali ya Biblia, kuna ushahidi wowote wa mapigo kutokea Misri kipindi hiki?

J: Huenda ni hivyo. David M. Rohl kwenye Pharaoh's and Kings: A Biblical Quest (1995), uk.278-279, anasema kuwa kulikuwa na ushahidi wa maafa makubwa na idadi kubwa ya miili ya watu iliyozikwa kwa haraka. Hata hivyo, idadi kubwa ya vifo haithibitishi au kukanusha kuwa vilitokana na tukio la ghafla la usiku mmoja. Hili liligunduliwa na Manfred Bietak huko Tell ed-Daba Habari hii ipo kwenye Avaris and Pramesse: Arhcaeological Exploration of the Eastern Nile Delta (London), 1979, uk.295.

Isitoshe, Josephus anamnakili Manetho kuwa "Pigo toka kwa Mungu limetuangamiza." Hata hivyo, maneno haya yamo kwenye mandhari ya wavamizi toka mashariki waliivamia Misri, hivyo huenda yakawa yanaelezea tukio lisilohusiana na mapigo haya, au huenda walikuwa wavamizi wa Misri katika kipindi cha Musa ambao Kitabu cha Kutoka hakiwaongelei.

 

S: Kwenye Kut 12:19, je maneno "atakatiliwa mbali na mkutano wa Israeli" yanamaanisha kuondolewa toka kwenye jamii na huenda kifo, au adhabu ya kifo?

J: Wanazuoni wa Kikristo hawakubali kama Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 2, uk.375 anavyosema.

Kuondilewa: The Bible Knowledge Commentary: Old Testament, uk.128. Believer's Bible Commentary, uk.98 inasema, "yaani, kuondolwa toka kwenye kambi na marupurupu yake. Kwenye mandhari nyingine, maneno "kukatiliwa mbali" yanamaanisha kuuawa."

 

S: Kwenye Kut 12:29, je Mungu mwenye upendo wote [kama inavyodaiwa], ambaye anapenda kiasi kikubwa zaidi, anaweza kuwaua watoto wa kwanza wa kiume wa Wamisri?

J: Hakuna mstari wa kwenye Biblia unaosema kuwa Mungu ana upendo wote, na hakuna mstari unaosema Mungu anapenda zaidi. Upendo wa Mungu unawiana na tabia zake nyingine. Kuhusiana na Mungu wa kwenye Biblia kuua watoto wa kiume wa kwanza wa Wamisri, tazama jibu la swali linalofuata.

 

S: Kwenye Kut 12:29-30, kwa nini Mungu alikuwa na haki [kama inavyodaiwa] kuwaua wazaliwa wa kwanzo wote wa Misri badala ya Farao mwenyewe, kwa kuwa Farao ndiye aliyefanya dhambi?

J: Kuna mambo matatu ya kuzingatia katika jibu la swali hili.

Wamisri wote waliwatumikisha Waisraeli. Farao mwenyewe hakuwatandika watumwa bali wasimamizi wa Kimisri ndio waliofanya hivyo. Kwa miaka 400 jamii ya Kimisri ilichukuliwa kuwa ni kawaida kunufaika na watumwa wa Kiebrania.

Watu mara nyingi hupata matokeo ya matndo ya watu wengine. Wakina mama anayetawaliwa na madawa ya kulevya huzaa watoto wenye ubongo mdogo, wanaotawaliwa na madwa ya kulevya. Mamilioni ya watu wamekufa kwa sababu uuaji wa kikatili sana wa Hitler na watu wengine. Mambo haya yametokea kwenye ulimwengu usio wa haki. Hata hivyo angalia jambo linalofuata.

Haki kamilifu imacheleweshwa hadi siku ya hukumu. Kwa mfano, kwenye Luk 13:1-5, Yesu aliambiwa kuhusu watu wa Galilaya ambao Pilato alichanganya damu yao na kafara zao. Yesu alisema kuwa jambo hili halikutokea kwa sababu walikuwa wabaya kuliko Wagalilaya wengine, lakini kuwa kama hawatatubu wao pia wataangamizwa. Kuna watu wanaadhibiwa zaidi kuliko wengine kwa jambo hilohilo kwenye maisha haya. Hata hivyo, kwenye siku ya hukumu Mungu atahukumu kwa haki na kurekebisha mambo yote.

 

S: Kwenye Kut 12:29, kuna ushahidi gani wa elimukale unaoonyesha kuwa mtoto wa kiume wa Farao alikufa muda mfupi kabla ya Waisraeli kutoka Misri?

J: Kwenye stela ya ndoto ya Thutmose IV (mwaka 1421-1410 KK) inayopatikana kati ya nyayo za mbele za mnyama zenye makucha za sanamu la jiwe la huko Misri (lenye mwili wa samba na kichwa cha mwanamke) la Giza, mungu Harmakhisi alimwahidi Thutmose msaada maalumu kuja kuwa Farao kwa malipo ya kuondoa mchanga uliojikusanya karibu na sanamu hili la jiwe. Huenda asingehtitaji msaada maalumu endapo angekuwa mtu wa kwanza kwenye mlolongo wa kumrithi baba yake Amenhotep II (mwaka 1450/1447-1401/1385).

Walter Kaiser anasema kuwa kaka mkubwa kabisa wa Thutmose IV aliitwa Webensenu. Webensu alizikwa katika kwenye makaburi ya kifalme, na huenda ndiye aliyeuawa wakati wa pigo la kumi. Mtoto wa pili wa kiume Amenhotep II alikuwa Khaemwaset aliyekuwa ameoa kabla ya kufa. Kama Kaiser anavyosema, "Hivyo, ingawa sanamu ya jiwe haiwezi kuchukuliwa kuwa uthibitisho wa moja kwa moja, wa kufa kwa mtoto wa kwanza, ushahdi wa kutosha umetolewa na wataalamu wa mambo ya Misri kuunga mkono tarehe ya kale ya Waisraeli kutoka Misrini na ukweli kuwa Thutmose IV hakutarajia kumridhi baba yake kwenye kiti cha enzi."

 

S: Kwenye Kut 12:29-30, je Mungu wa haki na mwenye upendo aliwezaje kuwawaua wazaliwa wa kwanza wa Wmisri wakati hawakuwa na mamlaka na maamuzi ya Farao?

J: Kuna mambo manne ya kuzingatia katika kujibu swali hili.

1. Vifo havithibitishi kuwa Wamisri na wanyama hawakuwa na hatia ya uamuzi wa Farao.

2. Watu wa Misri hawakupinga wala kufanya kitu chochote dhidi ya mauaji ya watoto wadogo na ukandamizaji hadi Kut 12:33. Hata kwenye Kut 14:5, watu wa Misri waliwataka Waisraeli warudi kuwa watumwa.

3. Ni muhimu kupinga kwani watu, wakiwemo watoto wadogo, mara nyingi hupata madhara makubwa kupita kiasi kwa sababu ya maamuzi ya viongozi wa kisiasa.

4. Kuna vitu vingi visivyo vya haki katika maisha haya. Lakini kuna siku inakuja, siku ya hukumu, ambapo kila kitu kitakuwa cha haki. Mungu ni wa haki, na matajiri na maskini, waonezi na wenye kuonewa, Wanazi, Wakambodia, Wasudani, na watu mtu mwingine yeyote atapata haki kamilifu mwisho wa dunia — ingawa hakuna mtu anayeweza kusema kitu pekee anachotaka ni haki bila neema?

Tazama Encyclopedia of Bible Difficulties, uk.113-114 na When Critics Ask, uk.74-75 kwa majibu mengine.

 

S: Kwenye Kut 12:30, je ingewezekanaje kutokuwa na nyumba ambayo haikuwa na mtu aliyekufa, kwani Waisraeli hawakuguswa ni pigo hili?

J: Kwenye mandhari hii, maneno haya yanaongelea nyumba za Misri ambazo Pasaka haikusherehekewa.

 

S: Kwenye Kut 12:35, kwa nini Mungu aliwaamuru Waisraeli "wawaambie Wamisiri wawatake" vyombo vya fedha na dhahabuwakati walijua kuwa hawatavirudisha?

J: Neno hili la Kiebrania linaweza kutafsiriwa kuwa "kuomba bila kuwa na lengo la kurudisha", na lilieleweka na kutafsiriwa hivyo kwenye Septuajinti.

Kuhusu sababu ya Waisraeli kutaka na kuchukua vyombo toka kwa Wamisri, tazama maelezo ya Kut 3:22 ili kupata jibu.

 

S: Kwenye Kut 13:2, 13 je Waisraeli walitakiwa kuwatakasa wazaliwa wao wa kwanza (wa kike na wa kiume), au ni wazaliwa wa kwanza wanaume tu kama Kut 22:29 inavyosema?

J: Kiebrania na tafsiri za kisasa vinasema watoto wa kiume:

Kut 13:2 "yeyote anayefungua mimba miongoni mwa wana wa kiume wa Israeli"

Kut 13:13 "kila mzaliwa wa kwanza wa wanadamu miongoni mwa wanao wa kiume"

Toleo la zamani la ‘King James', linasema tu mzaliwa wa kwanza.

 

S: Kut 13:4, je mwezi wa kwanza ulikuwa mwezi wa Abibu, au Nisani kama kwenye Neh 2:1?

J: Wakati ule (mwaka 1445 KK) Waisraeli waliuita Abibu. Karne kadhaa baadaye (karibu mwaka 500 KK) chini ya utawala wa Waajemi uliitwa Nisani.

 

S: Kwenye Kut 13:19, je kuhifadhiwa kwa mifupa ya Yusufu kunamaanisha kuwa Wakristo wawe wanazitukuza maiti za waumini kama Wakatoliki wanavyosema?

J: Hapana. Si kwamba kila wakati mifupa ilipohifadhiwa ilimaanisha kuwa ilikuwa inatukuzwa. Hakuna ushahidi kwenye Biblia kuwa mifupa ya Yusufu, au mtu mwingine yeyote kwa jinsi hiyo, ilichukuliwa kuwa na kitu chenye utukufu kinachopaswa kuabudiwa.

Amri ya pili inazuia kuwa sanamu yeyote ile mbele ya Mungu. Kipindi chote cha Enzi ya Kati, Wakatoliki mbalimbali walijaribu kuweka madaraja ya dhambi huku "dhambi mbaya zaidi saba" zikiwa maarufu zaidi. Jambo la kufurahisha zaidi kuhusu orodha hizi mbalimbali ni kuwa karibu zote zinaisahau amri ya pili.

 

S: Kwenye Kut 13:21-22; 14:19-20; 40:38, Mungu aliwezaje kuwafuata Waisraeli kama wingu na nguzo ya moto?

J: Kwa kuwa Mungu aliishatokea kama wageni watatu kwa Abram na moto kwenye kichaka kwa Musa, kutokea kama wingu au nguzo ya moto hakingekuwa kitu kigumu kwake. Inaweza kuwa vigumu kwetu kubadilisha miundo yetu ya namna tunavyomfikiria Mungu anapaswa kufanya, kuliko namna Mungu kutokea kama kitu fulani.

 

S: Kwenye Kut 14:6-7, kwa Farao aliwafuata Waisraeli wote akiwa na magari/vibandawazi ya kukokotwa na farasi 600 tu?

J: Ingawa magari ya kukokotwa na farasi yalikuwa ni silaha nzuri sana za vita nyakati za kale, na wengi wa Waisraeli hawakuwa na silaha, jibu ni kuwa Kut 14:7 inasema kuwa Farao alichukua magari yanayokokokwa na farasi 600 bora zaidi kati yay ale aliyokuwa nayo, na magari yote ya kukokotwa na farasi, na Kut 14:9 inasema na jeshi. Kut 15:4 pia inataja magari ya Farao yanayokokotwa na farasi na jeshi lake.

 

S: Kwenye Kut 14:6-7, magari yenye kukokotwa na farasi ya Wamistri yalikuwaje wakati ule?

J: Wataalamu wa elimukale wanatuambia kuwa magari yanayokokotwa na farasi kaskzini mwa Mesopotamia yalikuwa kama mikokoteni iliyokuwa na watu watatu au wane ndani yake, na hadi punda au farasi wanne. Wamisri walikuwa na magari yenye kukokotwa na farasi kama haya, hadi Wahiksosi (watu watokanao na mchanganyiko wa Kisemitiki na Kiasia waliivamia Misri miaka ya 1600 KK na kuishi kwenye delta ya Mto Naili) walitwaa sehemu kubwa ya Misri, baada ya mwka 1586 KK kwa magari yao bora zaidi yakokotwayo na farasi. Baada ya muda huu, magari yakokotwayo na farasi ya Kimisri yalikuwa mepesi sana, yakiwa na farasi wawili na watu wawili. Mtu mmoja alikuwa dereva na mwingine alikuwa mpiga mishale. Magurudumu yake yalikuwa makubwa na yakiwa na spoko (njiti) sita kwa kawaida. Hapakuwa na misumari kwenye ekseli hadi wakati wa Waajemi. Magari yanayokokotwa na farasi yalikuwa silaha muhimu sana za vita kwenye maeneo ardhi kavu na tambarare lakini hayakuwa yanafaa sana kwenye milima au sehemu zenye maji mengi.

 

S: Kwenye Kut 14:9-28 na Yos 24:6, wafalme wa Maisri waliwezaje kuwa na "wapanda farasi" kwani majeshi ya wakai ule hayakuwa na askari wa farasi?

J: Kama maelezo chini ya ukurasa kwenye tolea la Biblia la NIV yanavyosema, wapanda farasi wanaweza kuwa ni "madereva wa magari yanayokokotwa na farasi", siyo askari wa farasi. Neno hili linapotumika, mara nyingi huwa ni kinyume na jeshi la kawaida.

 

S: Kwenye Kut 14:14, kwa kuwa Mungu alipigana kwa ajili ya Waisraeli wakati ule, kwa nini Mungu hakupigana kwa ajili ya Waisraeli baadaye?

J: Mungu hakulazimika kupigana kwa ajili ya Waisraeli kila wakati. Angeweza kupigana kwa ajili yao na kuacha kuoigana kwa ajili yao wakati wowote alipotaka kufanya hivyo. Mara nyingi, Mungu alitokea kuwaacha wapigane vita vyao wenyewe.

 

S: Kwenye Kut 14:17 na 15:21, kuzama kwa Wamisri kunamwinuaje Mungu na kumpa utukufu?

J: Kulionyesha kwa macho ya Waisraeli kuwa Mungu ana nguvu ya kuwaokoa hata kutoka kwenye jeshi, na kwamba Mungu atawachunga.

 

S: Kwenye Kut 14:17 na 15:21, kwa nini Mungu alikuwa dhalimu sana hata akalizamisha jeshi la Misri kwenye Bahari ya Shamu, wakati askari walikuwa wanatii amri tu?

J: Kuna somo muhimu hapa: askari hawapaswi kuwatii viongozi waovu. Wakati ule, wakata askari wa Kimisri walipoamrishwa kuwaaua watu watu wanaomwabudu Mungu ambao hawakuwa wanapigana vita, walistahili kuadhibiwa kwa ajili ya "utiifu wao wa uovu." Leo hii, "wapambanaji watakatifu" wa Kiislamu wanapoamriwa kuwaua watu wasiopigana vita wanaomwabudu kwa sababu tu ni Wakristo, wao pia wanastahili hukumu ya jehanamu ya moto.

 

S: Kwenye Kut 14:18, je Waisraeli walivuka Bahari ya "Shamu" (the Red Sea), au Bahari ya "Matete" (the Sea of Reeds)?

J: Neno la Kiebrania lililotumika hapa ni Yam Suph, na linaweza kumaanisha kitu chochote kati ya hivyo viwili; hatufahamu sehemu hasa waliyovuka. When Critics Ask, uk.75-76 inasema inaweza kuwa Ziwa Ballah, ambalo lilikuwa ni "bahari" yenye kina kifupi na upana wa karibu km. 16-24 (maili 10-15). (Ziwa Ballah liliharibiwa wakati Mfereji wa Suezi ulipokuwa unajengwa).

Hata Bahari ya Matete huenda haikuwa na kina kifupi wakati ule. Kut 14:22 inasema maji yalifanya "ukuta" pande zote, hivyo ni lazima kuwa palikuwa na kiasi kikubwa cha maji mahali hapo. Kama bahari waliyoivuka ilikuwa na kina kifupi, na Waisraeli waliivuka, basi kama mtu mmoja alivyosema kwa mzaha, itakuwa ni muujiza mkubwa zaidi endapo waliivuka Bahari ya Matete yenye kina kifupi na kuwafanya farasi na magari yanayokokotwa na farasi yazame kwenye maji yenye kina cha inchi chache tu.

 

S: Kwenye Kut 14:21-29, je Mungu aliwezaje kuigawa bahari?

J: Mwenyezi ana uwezo wa kufanya vyovyote anavyotaka. Kut 14:21 inarekodi upepo wa nguvu utokao mashariki, lakini kunaweza kuwa na vitu vingine pia.

 

S: Kwenye Kut 14:21-29, je mlipuko mkubwa wa Thera unaweza kuwa ndio ulisosababisha kugawanyika kwa Bahari ya Shamu?

J: Maoni haya yalisemwa na kitabu kiitwacho The Bible as History kilichotungwa na Hans Goedicke. Nadharia hii ilikuwa maarufu sana kipindi fulani, kwa sababu mlipuko wa volkeno wa Kisiwa cha Nadharia hii iliwahi kuwa maarufu sana kipindi fulani, kwa sababu mlipuko wa volkeno wa Kisiwa cha Thera ulichukuliwa kutokea karibu mwaka 1500 KK, muda ambao ni karibu na maoni ya Goedicke kuwa Waisraeli walitoka Misri mwaka 1477 KK. (Siku hizi, kutoka kwa Waisraeli Misri kunaaminika kutokea mwaka 1445 KK). Hata hivyo, utafiti wa makini zaidi wa kupima umri wa vitu vya kale kwa kutafuta kiasi cha kaboni wenye kutumia miali uliofanywa katika miduara ya mashina ya miti ya mwaloni huko Ireland na msonobari huko California (Marekani) umeonyesha kuwa kulikuwa na kupungua joto duniani kote kwa kiasi kikubwa sana karibu mwaka 1628 KK, +/- 20. Muda wa kupungua joto wa barafu ya Greenland unaonekana kuwa karibu mwaka 1645 KK. Kwa hiyo, mlipuko wa volkeno kwenye Kisiwa cha Thera ulitokea karibu miaka 200 kabla ya hapo. Angalia Biblical Archaeology Review Januari/Februari 1991, uk.41-51 kwa maelezo zaidi.

 

S: Kwenye Kut 14:21-29, je Waisraeli milioni 2 wangewezaje kuvuka Bahari ya Shamu kwa muda wa masaa 24 tu?

J: Chukulia kuwa wanaume 602,000 wanamaanisha idadi ya watu wote ni karibu milioni 2 hadi 2.5. Ikiwa sehemu waliyovuka ilikuwa na upana wa karibu km. 3.2 - 4 (maili 2- 2.5), na walikuwa karibu mita/yadi mbili toka mtu mmoja hadi mwingine watafanya safu 1,760 za mistari yenye watu 1,136 kila moja. Ikichukuliwa kuwa mikokoteni na wanyama vilikuwa umbali wa karibu mita kumi toka kwa mtu aliyekuwa mbele yao, na watu walitembea mwendo wa polepole wa km 1.6 (maili moja) kwa saa, wangeweza kuivuka sehemu hiyo kwa muda wa masaa 6.5.

 

S: Kwenye Kutoko 15, je kuna ushahidi wowote wa Waebrania kuzunguka zunguka kwenye rasi ya Sinai?

J: Ndiyo, kuna ushahidi wa kiasi fulani. Can Archaeology Prove the Old Testament, uk.30 inasema palikuwa na maandishi kwenye mapango yaliyogunduliwa kwenye Mlima Sinai yanayoelezea kugawanyikaa kwa Bahari ya Shamu, Musa na kukamata kware. Kitu chenye kufurahisha zaidi ni lugha iliyotumika: ilikuwa mchanganyiko wa Kimisri na Kiebrania. Mwana historia Diodorus Siculus (mwaka10 KK) pia alifahamu jambo hili. Hat hivyo, Can Archaeology Prove the Old Testament, uk.30 pia inasema kuwa uhalisi wa maandishi haya hauwezi kuthibitishwa au kukanushwa. Hii inaweza kuwa ni kwa sababu hakuna namna ya kutafuta muda wa maandishi kwenye kuta za miamba.

Wycliffe Dictionary of Biblical Archaeology, uk.535 inasema kuwa kwenye lango la machinbo ya shaba ya Sinai kuna maandishi mengi kwa mamia. Mengi kati ya hayo yapo kwenye hieroglifu (maandishi ya kale ya Kimisri), lakin maandishi karibu 40 yapo kwenye herufi zilizozitangulia zile za Kisinai za karne ya 15 KK. Haya ni moja ya vitu vya kubuniwa vyenye herufi za kialfabeti vya kale zaidi vilivyopo leo.

 

S: Kwenye Kut 15:1-21, je sehemu hii iwekwe pamoja na ie inayotangulia ya Kutoka au ile inayofuata?

J: Kwa kuwa haya ni masimulizi, inaweza kufuatana na sehemu yeyote kati ya hizo. Watu wengi wenye kutoa maoni ya vitabu vya Biblia wanaiweka panoja na sehemu inayotangulia, kwa kuwa sehemu inaweza kuwa iliimbwa muda mfupi sana baada ya kukombolewa. Hata hivyo, katika kupanga kitabu cha Kutoka, mimi huwa napendelea kuiweka kwenye sehemu inayofuata kwa sababu nusu ya kwanza ya Kutoka 15 na nusu ya pili ya Kutoka 15 kwa pamoja vinatengeneza taswira nzuri sana. Tunapaswa kukumbuka kuwa wakati Waisraeli walipokuwa wanasafiri jangwani hawakuweza kusoma kwenye Kitabu cha Kutoka kabla hakijaandikwa na kujua walikokuwa wanaenda au kitu kitakachotokea kwao. Walipokuwa wanasafiri, kimsingi kulikuwa na mambo mawili tu ambayo waliweza kuyafanya. Wangeweza kuukumbuka ukuu na neema vya Mungu kwao, au kulalamikia hali iliyokuwa inawakabili wakati huo.

Katika maisha yetu leo, kimsingi haya ndiyo mambo mawili tu tunayoweza kuyafanya pia: kumtukuza Mungu na kumtii kwa moyo wa shukrani, au kupendezwa na dunia na kumlalamikia au kwenda njia yetu wenyewe, kutilia shaka upaji wake na jinsi anavyotutunza.

 

S: Kwenye Kut 15:1, iliwezekanaje kuwa na "wapanda farasi" kwani jeshi la Misri halikuwa na askari waliokuwa wakipigana toka juu ya farasi wakati ule?

J: Neno "wapanda farasi" halielezi kitu kilichokuwa kilichokuwa kinaendeshwa. Majeshi ya wakati ule yalitegemea sana magari ya kukokotwa na farasi, na hawa walikuwa watu wenye kuyaendesha magari haya ambao pia waliitwa madereva wa magari yanayokokotwa na farasi.

 

S: Kwenye Kut 15:2, Miriamu aliwezaje kuimba kuwa ataandaa makazi ya Mungu?

J: Mahali ambapo toleo la King james la Biblia ya Kiingereza (King James Version, KJV) linasema "nitamwandalia makazi", tafsiri za kisasa zinasema "nitamtukuza." Neno la Kiebrania navah, kimsinig linamaanisha kusherehekea (kwa kusifu) lakini linaweza pia kumaanisha kuandaa makazi. Neno la Kiebrania lifananalo nalo, naveh/navah, linamaanisha nyumba.

Zab 22:3 (KJV) inasema kuwa says that God "Uketiye juu ya sifa za Israeli." Ingawa hili ni neno tofauti la Kiebrania, yashab, linalomaanisha kukaa ua kuishi, wazo linafanana.

Kwa mtu mmoja mmoja, kwenye Agano Jipya Mungu anafanya makazi yake ndani ya moyo wa kila mwamini. Yoh 14:23 inasema, "Yesu akajibu akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake." Ingawa hatutakuja kuwa kama Mungu (uongo ambao Shetani alifundisha kwenye Mwa 3:4-5), ni ukweli unaofurahisha kuwa hatukai ndani ya Yesu (Yoh 15:7), lakini Mungu anakaa ndani yetu (1 Yoh 4:13-16).

Kwa pamoja kutoka wakati wa Agano la Kale hadi sasa, waamini ni mawe ambayo kwa pamoa yanafanya hekalu la Mungu aliye hai (1 Pet 2:5; Efe 2:20-21).

 

S: Kwa kuwa Kut 15:11 inasema "Ee BWANA, katika miungu ni nani aliye kama wewe", je kuna Mungu zaidi ya mmoja?

J: Hapana. Mstari huu, kama Isa 40:18, unaonyesha kuwa Mungu hana wa kulinganishwa naye. Kwenye 1 Kor 8:1-7 inaonyesha kuwa kuna sanamu nyingi, lakini kuna Mungu mmoja tu wa kweli, kama inavyoonyeshwa kwenye Kum 4:35-39; 6:4; Mak 12:29-33; Isa 43:10-12; 44:6, 8; 45:5-6, 14, 21; 46:9; Yoel 2:27; 1 Tim 1:17; 2:5 na 6:15-16.

 

S: Kwenye Kut 15:16, je Mungu "aliwanunuaje" Waisraeli?

J: Moja ya namna ambazo wao ni maliyake ni kuwa Mungu aliokoa maisha yao.

 

S: Kwenye Kut 15:22-27, je tunaweza kujifunza kitu gano kutokana na maji ya Mara na Elim?

J: Mungu alikuwa anawajaribu kwa mujibu wa Kut 15:25. Watu walihitaji sana maji, na walipata maji mengi sana pale Mara, lakini jambo hili liliweza kuonekana kama utani mkubwa sana, kwa sababu yalikuwa maji machungu na yasiyoweza kunywekwa. Maji machungu yanakuwa hivyo kwa sababu yana alkali nyingi sana. Kwa hayawi na radha mbaya tu, bali pia ni hatari kwa mwili wako. Mungu siyo tu kwamba aliyafanya maji machungu yastahimilike na yenye afya ya kutosha kunywewa, lakini aliyafanya matamu na yenye radha nzuri.

Je Mungu anaweza kukupa kwenye nchi kavu na yenye kiu? Mungu anajua mahitaji yako, lakini kama inakuwaje endapo una uhitajina njia pekee ya kupata inaonekana kuwa kituko kikubwa. Je utaendelea kuwa mwaminifu, na ama umngojee Mungu kukupatia kimiujiza pamoja na maji mengine, au kama ilivyo hapa, afanye jambo linaloonekana kuwa "siyo ufumbuzi" wa shida yako kuwa ufumbuzi unaotosheleza.

Waisraeli walijaribiwa mara nyingi, kama alivyokuwa Daudi, Wayahudi wa miaka iliyofuata, Yesu, na Wakristo wa awali. Hatupaswi kushangazwa tunapoona kuwa nasi pia tunajaribiwa.

 

S: Kwenye Kutoka 16, tunaweza kujifunza kitu gani toka kwenye mana na kware?

J: Hitaji la watu la maji lililotakiwa kutimizwa haraka sana lilitimizwa, lakini vipi kuhusu kuishi kwao muda mrefu zaidi? Badala ya kumwomba Mungu mahitaji yao, walimlalamikia Musa. Unafanyeje unapokuwa na hitaji la kweli na Mungu bado hajalitimiza? Unalalamika, au unaendelea kumwomba Mungu?

Je Mungu anaweza kukulisha kwenye sehemu kame. Je panapokuwa hakuna virutubisho, ama chakula cha mwili, au kihisia, urafiki, kiroho, ambayo unadhani Mungu ana uwezo wa kutosha kukutimizia kwa muda mrefu? Tunapaswa kupanga kwa ajili ya hali yetu ya baadaye (kama chungu wenye busara kwenye Mit 30:25), lakini unaweza kuiangalia hali yako ya baadaye kwa kwa kumwamini Yeye, siyo uoga?

 

S: Kwenye Kut 16:23-30, kwa nini Waisraeli walitakiwa kuitunza sabato mahali palipoitwa jangwani la Sini, kwani agizo lilitolewa baadaye pamoja na amri kumi kwenye Mlima wa Sinai?

J: Mungu aliwapa amri hii kabla ya kuwapa amri kumi.

 

S: Kwenye Kut 16:23, je jangwa la Sin ni hilohilo la Zini?

J: Hapana. Jangwa la Sini lilikuwa mashariki mwa Mlima Sina wakati jangwa la Zini lilikuwa kusini mwa Yuda na kusin mashariki mwa Kadeshi Barnea. The Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 2, uk.404 inasema konsonanti ya kwanza ya Kiebrania ni tofauti.

 

S: Kut 16:31; Hes 11:7-9; Kumb 8:3, 15 Yos 5:12; Zab 78:24, 25; 105:40 na Neh 9:15, je mana ni nini hasa?

J: Maandiko yanasema tu kuwa hiki kilikuwa ni chakula kilichotolewa kimiujiza na Mungu.

Watu wengine wanakisia kuwa vitu vyenye kuliwa vinavyotolewa na vichaka au miti midogo kwenye jangwa la Sinai, vitu vyenye kutolewa na wadudu, n.k. lakini maelezo ya kawaida hayatoshelezi. Mana ilitokea siku sita katika juma, lakini si kwenye siku ya sabato. Isitoshe hapangeweza kuwa na vitu vya kutosha vyenye kutolewa na wadudu au vichaka/miti modogo kuilisha idadi kubwa namna hii ya watu.

Ebr 9:4 inasema kuwa sehemu ya mana ilihifadhiwa kwenye sanduku la agano.

 

S: Kwenye Kut 17:1-7, kwa nini Mungu alikasirishwa na watu wanaomtii?

J: Kut 17:1 inasema watu walisafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kama Bwana alivyowaamuru. Lakini walinung'unika walipokwa wanamtii. Utiifu peke yake hautoshi; tunatakiwa kuwa na utiifu wenye furaha, bila kulalamika wala kubisha, kama Fil 2:14 inavyoonyesha.

 

S: Kwenye Kut 17:2 na Kumb 6:16, je watu wanawezaje kumjaribu Mungu, kwani Mungu hawezi kujaribiwa na maovu kwenye Yak 1:13?

J: Tafsiri nzuri zaidi kuliko "kumjaribu Mungu" ni "kumweka Mungu majaribuni." Ni kweli Mungu hawezi kujaribiwa na uovu, lakini bado watu wanaweza kujaribu kufanya hivyo. Jambo hili linaonyesha dhambi ya watu wanaomwambia Mungu "Fanya namna hii na tenda muujiza huu vinginevyo . . ."

 

S: Kwenye Kut 17:8, wakati Waisraeli walipokuwa wanashinda pale tu Haruni na Huri walikuwa wanainua mikono ya Musa je jambo hili halionekani kuwa kama ushirikina?

J: Watu wote walijua kuwa nguvu ilikuwa ni ya Mungu si mikono. Mungu mara nyingine hutumia matendo ya kimwili kupitishia nguvu zake. Kwa mfano, tazama 2 Fal 13:21 (mifuoa ya Elisha), Hes 21:4-9 (nyoka wa shaba), na Yoh 9:6-7 (Yesu akitfanya tope na kuweka kwenye macho ya kipofu).

 

S: Kwenye Kut 17:15-16, je jina la Mungu lina umuhimu gani hapa?

J: Ni jambo kubwa kuwa Musa alimwita Mungu Yahweh Nissi, "Bwana ni beramu yangu." Katika lugha ya mapambano ya kijeshi, beramu ilikuwa ni heshima ya jeshi au divisheni, na askari walipigana hadi mwisho ili waweze kuiokoa kwa gharama yeyote ile. Maneno haya yana maana zaidi ya Mungu kuwa mwenye nguvu. Wakati jeshi kubwa lililokuwa limedhamiria kuwashinda Waisraeli lilipowajia, Waisraeli HAWAKUAMINI tu kuwa Mungu alikuwa mwenye nguvu, anaweza kuwapa msaada wa kiasi fulani kama angependa kufanya hivyo. Badala yake, waliamini kuwa Mungu sit u alikuwa na nguvu lakini pia kuwa alifanikiwa katika muda wa uhitaji wako zaidi na kuwaokoa lwale walioliitia jina lake. Leo hii Wakristo wote wanaamini kuwa Mungu ana nguvu, lakini je unaishi kwa jinsi unavyomwamini Mungu atakufanikisha wakati wako wa uhitaji zaidi? Kama ni hivyo, basi siyo tu kuwa unaamini kuwa Mungu ni beramu yako, na utapambana hadi mwisho kusimama imara kwa ajili yake, lakini pia unafahamu kuwa wewe ni beramu ya Mungu, kwa maana kuwa unabeba jina lake na u mboni ya jino lake (Kumb 32:10; Zab 17:8), na kuwa Mungu atakuwa nawe hakika. Hata kama utauawa kwa ajili ya Mungu, unajua kuwa "Ina thamani machoni pa BWANA mauti ya wacha Mungu wake" (Zab 116:15).

 

S: Kwenye Kut 18:7 kwa kuwa tunapaswa kumwabudu Mungu tu, kwa nini Musa alimsujudia baba mkwe wake?

J: Kuinama kwa ajili ya kuonyesha heshima si kuabudu. Hata leo hii watu kuinama au kukunja magoti kwa Malkia wa Uingereza kwa heshima. Ibrahimu aliinama kwa heshima ya wafalme, na kusujudu ni kitu sahihi ili mradi tu hakichukuliwi kuwa ni ibada. Tofauti na jambo hili, inakadiriwa kuwa karibu Wakristo 50,000 waliangamia wakati wa mateso ya Warumi na watu wengi walielewa vibaya kuwa ya kuwa hivyo. Warumi hawakuwa na shida na Wakristo kumwabudu Yesu. Warumi hawakuweza kuvumilia Wakristo kukataa kumwabudu mtu yeyote isipokuwa Mungu, hasa mfalme.

 

S: Kwenye Kut 18:17-26, kwa nini Musa alichukua ushauri wa Yethro badala ya ushauri wa Mungu?

J: Ushauri wa Yethro haukuwa kinyume cha mapenzi ya Mungu, lakini Musa aliutambua kuwa ni mzuri katika kumfuata Mungu. Tunapaswa kuwa kuangalia hali halisi na kupokea mashauri toka kwa watu wengine na Mungu pia.

 

S: Kut 19:3,20; 24:9, 13, 15, 18; 34:4, Kwa nini Musa alikwenda mlimani mara saba, na akarudi kumwona Bwana (Kut 32:31) lakini Mungu anaripotiwa kushuka mara nne tu kwenye Kut 19:14, 24; 32:15; 34:29?

S: Kuna watu ambao wametumia jambo hili kuunga mkono hoja ya watunzi wengi wa Kitabu cha Kutoka, lakini The Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 2, uk.416 inasema kuwa halisaidii kujibu swali. Kitabu cha Kutoka hakitakiwi kuwa masimulizi yanayofuata mfuatano wa kutokea kwa matukio yanayoripotiwa, hakuna shiida ya kitabu hiki kufuata mfuatano wa kutokea kwa matukio hapa; mfuatano wa matukio ni dhahiri kabisa.

Kut 19:3 Musa alikwea peke yake

Kut 19:14 Musa alishuka peke yake

Kut 19:20 Musa alikwea kileleni peke yake

Kut 19:24 Musa alishuka mara moja kuja kumchukua Haruni

Kut 24:9 Musa na watu wengin 73 wanakwea

Kut 24:12-13 Mungu anamwambia Musa akwee, Musa anawaacha wazee mahali walipokuwepo, na Musa na Yoshua wanaenda mbali zaidi.

Kut 24:15 inasema kuwa Musa alipokwea, yaelekea alikuwa peke yake, alikwea zaidi.

Kut 24:18 inasema kuwa kisja Musa aliingia katika wingu alipokuwa anakwea, kwa hiyo safari hii ilikuwa ni ileile ya Kut 24:15.

Kut 32:15 Musa alikuja hadi chini akiwa na mbao mbili, akamkuta Yoshua. (Musa anazivunja mbao kwenye Kut 32:19).

Kut 32:31 Musa anarudi kwa Bwana. Hii haimaanishi kuwa ni lazima awe amekwea na kushika mlima ingawa anaweza kuwa alifanya hivyo.

Kut 34:4 Musa akwea na mbao mbili zisizoandikwa

Kut 34:29 Musa ashuka mlima na mbao mbili.

Tunapoongelea Musa na milima, mfuatano kama huu ulitokea wakati wa kubadilika kwa sura ya Yesu. Alipokuwa anasafiri na mitume wake kumi na mbili, alijitenga nao na alikwea mlimani na watatu tu. Luk 9:32-33 inaonyesha kuwa Yesu alikuwa umbali kiasi toka kwa hao wanafunzi watatu wakati alipobadikia. Kisha wingu liliwafunika. Luk 9:36-37 inaonyesha kuwa wanafunzi wengine walimfuata Yesu kabla ya makutano kuja chini ya mlima.

Muhtasari: Kuwa kutambua kuwa safari pamoja na kundi kubwa la watu hiyo inaweza kuwa sehemu ya safari safari ya kwenda mbali zaidi na watu wachache, na kwa kutambua kuwa hapakuwa na ulazima wa kutaja kila mara alipokuwa anashuka, namba ya safari ambazo Mus alizifanya kukwea mlima hazina shida.

 

S: Kwenye Kut 19:4, je watu wangewezaje kuwa na mbawa za tai?

J: Hii ni sitiari ya namna Mungu alivyotenda kuwafikisha kwenye nchi aliyowaahidia, bila ya nguvu zao wenyewe. (Leo hii tunapokuwa na mapambano makubwa, Mungu hutubeba kwenye mbawa za tai).

 

S: Kwenye Kut 19:11, je Mlima Sinai ulikwa wapi hasa?

J: Ukanda: Rasi ya Sinai ni pembetatu inayoelekea kusini huku milima ikiwa upande wa kusini, ambao Kut 19:2 na Hes 3:14; 9:1, 5; 10:12 zinauita jangwa (nyika) ya Sinai. Jangwa la Sin linaitenga Elimu kutoka Sinai. Hes 33:3-50 inataja kila sehemu ambayo Waisraeli walifanya kambi. Kwa bahati nzuri, hatufahamu sehemu halisi makambi haya yalipofanyika, lakini kwa kuyaangalia tunaweza kuona lipi lililokuwa kati ya lingine.

Ndani ya Nyika ya Sinai, kuna vilima viwili vilivyo karibu karibu vinavyoendana sawa na mahali Mlima Sinai ulipowepo.

Gebel Musa (mita 2,244 au futi 7,363). Haya ni maoni yaliyotokea zamani, angalau kuanzia mwaka 500 BK. Una miteremko mikali. Nyumba ya watawa ya Mt. Katherina (St. Catherine Monastery) ipo chini ya mlima huu. Waislamu wengi lakini si wote nao wanauona huu kuwa Mlima Sinai. New International Dictionary of the Bible, uk.674 ina picha ya Gebeli Musa.

Ras es-safsafeh (mita 1993 au futi 6,540) uko km. 3.2 (maili 2) kaskazini mwa Gebeli Musa kwenye safu hiyo hiyo. Una uwanda mkubwa sana kwa chini.

Gebel Serbali (haina uwezekano mkubwa): Eusebius (mwaka 325 BK) alifikiria hivi. Hata hivyo, The New Bible Dictionary (1978), uk.1193-1194 hakuna nyika maeneo ya karibu na chini ya mlima huu.

Watu wachache wanafikiri Mlima Sinai upo Mebel al-Lawz, Arabia huenda kwa sababu

a) Wamefikiri kwa makosa kuwa rasi ya Sinai ilikuwa sehemu ya Misri wakati Waisraeli walipokuwa wanatoka Misri.

b) Wanasahau kuwa Mlima Sinai ulikuwa nje ya nchi ya Midiani kwa mujbu wa Kut 18:27 na Hes 10:29-30.

c) Paulo alisema Mlima Sinai ulioko Arabia (Gal 4:25), na wanasahau kuwa rasi ya Sinai ilikuwa kwenye jimbo la Rumi la Arabia.

www.christiananswers.net/abr/scoop.html, baada ya kutoa sababu zilizotangulia, pia anasema kuwa umbali wa kuelekea Arabia ungekuwa mrefu sana kutoka Kadeshi Barnea. Kwa kuwa watu wenye makundi ya mifugo walikuwa wanaweza kusafiri karibu maili 6 tu kwa siku. Ingawa umbali toka Jebel al-Lawz kuelekea Kadeshi Barnea ni karibu km. 240 (maili 150), na walikwenda kutoka Sinai kuelekea Kadeshi Barnea kwa siku 11 tu.

Waislamu mara nyingine wanajaribu kusema kuwa Mlima Sinai ni Maka. Isitoshe Gal 4:25 inasema kuwa Mlima Sinai uko Arabia. Hata hivyo, hii siyo nchi ya siku hizi ya Saudi Arabia, lakini rasi ya Sinai ilikuwa sehemu ya jimbo la Rumi la Arabia. Pia safari ya karibu km. 1,300 kwa siku 11 kutoka Maka hadi Kadeshi Barnea wakiwa pamoja na makundi ya mifugo wanyama wachanga, na watoto wadogo, kwa miguu isingesadikika. Tazama ama The Roman World, uk.107 au Encyclopedia Britannica kwenye Historia ya Rumi kuona ramani.

Kama Mlima Sinai ungekuwa Maka kweli usingebadilisha kitu chochote kwa Wakristo, isipokuwa kwamba hatua za sfari ya Israeli isingendeeleweka. Hata hivyo, ni muhimu kwa baadhi ya Waislamu, kwani inafanya dhana ya kuwa Maka ilikuwa na sehemu katika kazi ya Mungu kabla ya kuzaliwa kwa Muhammad isadikike. Hata hivyo, Waislamu wengine, kama maelezo chini ya uk. 2504 kwenye Holy Quran: English Translation of the Meanings and Commentary inauchukulia Mlima Sinai kuwa Jabal Musa, sawa na wengi wa Wakristo.

 

S: Kwenye Kut 20:4-5, je ni SAHIHI kwa Wakristo kuwa na kuvaa misalaba na vitu vingine vya sanaa vya kidini?

J: Kama vitu vya kukumbushia ni sawasawa, kama Wayahudi walivyonakiri Maandiko kama kitu cha kuwakumbusha kwa kufuata Kumb 6:8-9. Hata hivyo, si misalaba wala Maandiko wala kitu kingine chochote kinachotakiwa kuabudiwa badala ya Mungu.

 

S: Kwa kuwa Kut 20:4-5 inakataza kufanya sanamu, kwa nini kulikuwa na sanamu nyingi kwenye hema la kukutania (Kutoka 25-27) na baadaye hekaluni (1 Fal 6:1-38; 7:13-51)?

J: Ilikuwa SAWASAWA kufanya sanamu ambazo Mungu aliagiza kwa ajili ya mapambo na si kuabudu. Lakini, hata wakati sanamu ambazo Mungu aliamuru kutengeneza zilitumiwa kuabudu zilitakiwa kuharibiwa. Kama mfano, soma kuhusu nyoka ya shaba kwenye Hes 21:4-9 na 2 Fal 18:1-4. Tazama kazi ya Tertullian, Against Marcion (mwaka 207 BK), kitabu cha 2, sura ya 22 kwa maelezo zaidi.

 

S: Kwenye Kut 20:5; Kumb 4:24; 6:15; Yos 2:18; Zef 1:18; 3:18, je Mungu ni mwenye wivu, kwani 1 Kor 13:4 inasema kuwa upendo hauhusudu?

J: Kuna mambo matatu ya kuzingatia wakati wa kujubu swali hili:

1. Mistari mingi inaonyesha kuwa hatupaswi kuwaonea wivu watu wengine kwa vitu walivyo navyo, au hata vitu ambavyo Mungu amewabariki navyo.

2. Mungu si kiumbe, na kwa amri zake, ni SAWASAWA kwake kuwa na wivu kwa ibada na kujitoa ambavyo ni vyake kwa haki. Jambo hili linafanana na mtu anayetegemea kujitoa na uaminifu toka kwa mwenzi wake, au mzazi anayetegemea heshima na utiifu toka kwa mtoto.

3. Hata zaidi ya jambo hili, 2 Kor 11:2 inaonyesha kuwa tunatakiwa kuwa na wivu wa kiungu kwa watu wengine kuendelea kujitoa kwa Yesu wa kweli badala ya Yesu wa uongo.

 

S: Kwenye Kut 20:5, kwa ufupi, kwa nini Mungu mwenye haki analipiza kwa watoto maovu ya baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne?

J: Ezekieli 18 na Kumb 24:16 zinaonyesha kuwa Mungu hamhesabii mwana uovu wa baba yake, lakini Kut 20:5 na mistari mingine inaonyesha kuwa watoto wanapata madhara mabaya ya dhambi za watu wengine. Watu wengi wanaamini kuwa hukumu ya Mungu inachukulia mahali walipo anzia na vitu walivyokuwa navyo, lakini watu wote hawaanzii mahali pamoja na hawawi na fursa sawa.

 

S: Kwenye Kut 20:5; 34:7; Hes 14:18 na Kumb 5:9, Mungu anawaadhibu vipi watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne, wakati Eze 18:4, 18-19 na Kumb 24:16 zinasema kila mtu atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, si za baba yake, na Eze 18:19 inasema mwana hatauchukua uovu wa baba yake?

J: Inavyoonekana Mungu aliifikiria dhana hii muhimu kwa sababu mistari minne kwenye Sheria inarudia kitu hichohicho kwa kutumia maneno hayohayo mawili ya Kiebrania.

Kutembelea ni paqad (Strong, namba 6485) ambalo ni neno lisilosimamia upande wowote linaloweza kumaanisha ama lengo la kirafiki ama la kiadui.

Uovu ni ‘avon (Strong, namba 5771) ambalo linamaanisha upotofu, uovu, makosa, udhalimu, fitina, hukumu (ya fitina), dhambi.

Kuna watu wanafikiri kuwa dhambi zao hazina madhara kwa watoto wao; watu wengine wanafikiri mtoto anaweza kuwa na hatia kwa sababu ya mzazi wake. Yer 31:29-30 na Eze 18:2 zinakaripia watu kwa kusema, "Baba wamekula zabibu mbichi, nao watoto wakatiwa ganzi la meno." Kwenye Ayu 21:19, Ayubu anasema maneno kama hayo. Ukweli haupo kwenye maoni haya yaliyovuka mipaka. Kwanza, tutaangalia mambo mawili yasiyokuwa jibu, kisha jibu.

Ufunuo wa awali dhidi ya ufunuo wa baadaye (siyo jibu): Torati (Sheria) ilitolewa karibu mwaka 1440 KK na Ezekieli baada ya mwaka 587 KK. Kwa kuwa njia ya Mungu ya kushughulika na watu ilikuwa tofauti kwa kiasi kikubwa wakati wa Nuhu, wakati wa Ibrahimu, chini ya sheria ya Musa, na baada ya Kristo, njia ya Mungu ya kushughulika na watu ilikuwa tofauti kwa kiasi kidogo kati Musa (walipokuwa na sheria tu) na Ezekieli (walipokuwa na vitabu vya manabii pia). Hata hivyo, nyakati zote hizo walikuwa chini ya Sheria ya Musa, na hapakuwa na mabadiliko yanayoonekana ya agano/dispensheni (mpango uliowekwa na Mungu unaotawala kipindi husika cha historia) kati ya hivi viwili. Isitoshe, Kumb 24:16 pia inasema kina baba na watoto hawasababishi yeyote kati yao kuuawa, na iliandikwa muda mmoja na sehemu zilizobaki za Kitabu cha Kumbukumbu ya Torati.

Kutembelea maovu dhidi ya kufa kwa ajili ya dhambi (siyo jibu): Aya za kwenye Torati hazisemi watoto watakufa kwa sababu ya dhambi za wazazi/wahenga wao, ila tu kuwa maovu yatatembelewa juu yao. Ezekieli 18 na Kum 24:16 zinasema tu kuwa mtoto hatakufa kwa ajili ya dhambi za baba yake. Hata hivyo, ingawa Kum 24:16 na Ezekieli 18 zinaonesha kuwa kifo [cha kimwili na kiroho] na madhara ya milele si jukumu la wazazi lakini la mtu mwenyewe, huwezi kuepuka ukweli kwamba aya nyingine zinathibitisha kuwa dhambi zina madhara katika vizazi vya watu. Kuna matokea angalau matatu.

Matokeo: Matokeo ya kimwili ni rahisi kuyaona: watoto waliozaliwa na wakina mama wanaotawaliwa na madawa wanazaliwa wakiwa wanatawaliwa na madawa. Kuna watoto wanaolaaniwa na dalili zenye kusababisha kifo za pombe kutokana na mama zao wanaotawaliwa na pombe. Endapo wataanza kunywa pombe, watakuwa na mazoa makubwa ya kunywa pombe. Lakini wakati mwingine Mungu huleta madhara mengine pia yasiyokuwa ya kimwili. Kanaani na uzao wake walilaaniwa kwa sababu ya dhambi ya Hamukwenye Mwa 9:25-27. Uzao wa Eli ulilaaniwa kwenye 1 Sam 2:31-33 kwa sababu ya dhambi kubwa ya watoto wa Eli. Uzao wa Yehoachini hawangetawala tena kwenye Yer 22:28-30. Lakini kuna matokeo mazuri pia, kama kwa wazao wa Warekabi kwenye Yer 35:18-19, na wazao wa Ibrahimu kwenye Mwa 12:2, n.k. Mwishoni, Rum 8:28 inaahidi kuwa mambo yote hutendeka vizuri kwa lengo jema la watu wanaompenda Mungu. Tunapokuwa tumebeba laana, Mungu ana nguvu sana kiasi cha kuzibadilisha ili ziwe baraka.

Kukua katika dhambi: Kut 20:5 na Kumb 5:9 zinasema Mungu anapatiliza uovu kwa watoto wa watu wanaomchukia. Mara nyingi watoto wanaokua wakiwa wanajifunza viwango vya maadili vya wazazi wao. Endapo wazazi walikuwa wanamchukia Mungu watoto wana uwezekano wa kukua kujifunza hivyo pia, ama kwa njia ya wazi kabisa ama kwa njia isiyokuwa ya wazi. Hata hivyo, kama Adamu wa Uri, Wagideoni wa Kanaani, Ruth Mmoabu, na wapagani waliohubiriwa na Wakristo wa awali pia, tunaweza kuufuata wito wa Mungu wa kuwa juu ya makuzo yote mabaya na kuishi maisha mapya yanayompendeza.

Lazima kuchagua kwenda kinyume na dhambi: Wazazi wa mtoto wanapojihusisha na dhambi, hususani endapo wazazi wanamchukia Mungu, mtoto atapatilizwa na fursa ya hiyo. Mtoto anapaswa kuchagua kwenda kinyume cha mifumo ya wazazi wake, au hata kinyume cha desturi ya jamii yao, na kumfuata Mungu. Kama vile Ibrahimu alivyoambiwa aiache familia yake na kwenda mahali ambako Mungu alimuongoza, nasi tunahitaji, kwa namna fulani, kuacha sehemu za jamii zetu na makuzi yetu na kumfuata Yesu.

Mfano rahisi wa mambo matatu: Mara nyingi Waisraeli walitenda dhambi ya kuabudu miungu mingine hadi wakati wa Uhamisho (wa Babeli). Watoto wa Kiisraeli waliozaliwa baada ya hapo walikabiliwa na madhara ya kuwa uhamishoni kwa sababu ya dhambi ya wazazi na wahenga wao. Wakati wa makuzi yao, walijaribiwa sana kuiabudu miungu ya Babeli iliyokuwa imewazunguka kama mtu mwingine yeyote alivyokuwa anafanya; wengi walifanya hivyo na walisimilishwa kwenye jamii hiyo. Lakini wengine walipambana na sanamu wakati wa laana ya kuwa kwao Babeli, walimchagua Mungu na kuwa kinyume na dhambi, na walirudi kwenye nchi ya Israeli. Baada ya muda huo, Waisraeli hawajawa na shida ya kuabudu sanamu tena.

Hitimisho: Ikiwa watu watapenda au la, Mungu ameonyesha kuwa kuna mambo yanayohusu dhambi yenye kwenda vizazi vingine. Mungu ni wa haki na tunaweza kutambua mambo ambayo Mungu ameyafunua kuhusu haki yake. Hat hivyo, haki ya Mungu imefafanuliwa na neno lake, hatuna uhuru wa kulipuuzia neno lake na kumtaka Mungu ajifananishe na fikra zetu wenyewe kuhusu dhambi. Kwenye jamii "huru" ya nchi za magharibi, tunaweza kutaka kuukwepa ukweli kuwa kuna mambo yahusuyo dhambi yenye kudhuru vizazi vyetu, lakini haki ya Mungu inafafanuliwa na maneno ambayo Mungu amesema, siyo namna tunvayopenda sisi.

 

S: Kwe kuwa Kut 20:8 inawma tunapaswa kuiheshimu siku ya Sabato (jumamosi), kwa nini Wakristo wa leo wanasema kuwa ni sawasawa kufanya kazi jumamosi?

J: Wakristo wa kweli wana maoni matatu:

Jumamosi: Kwenye Agano la Kale Sabato ilikuwa machweo ya ijumaa hadi machewo ya jumamosi. Moja ya sababu ya taifa la Yuda kupelekwa Uhamishoni Babeli kwa miaka ilikuwa miaka 70 x 7 = 490 ya kutokuitimiza Sabato. (Mwaka wao ulikuwa na siku 360). Tazama Law 26:31-36; Yer 25:11-12; 29:10,16 na Dan 9:2.

Jumapili: Baada ya Yesu kufufuka toka mauti, Jumapili imakuja kuwa Siku ya Bwana na iliadhimishwa na Wakristo wa awali. Paulo hakuwaelezea Wakristo sababy ya siku ya kwanza ya juma kwenye 1 Kor 16:2, Paulo alichukulia kuwa tayari wanafahamu.Ufu 1:10 pia inaongelea Jumapili, ama vinginevyo maono ya Siku ya Bwana. Justin's First Apology (karibu mwaka 138-165 BK), sura ya 57 pia inataja ibada ya jumapili. Irenaeus (akiandikwa waka 182-188 BK) kwenye Fragments 7 (uk.569) pia anasema kuwa kuhusu Pasaka na Siku ya Bwana.

Siku zote: Kwenye nyakati za Agano la Kale, waamini walitakiwa kuwepo pumziko la Mungu siku moja kwa juma. Hata hivyo, Ebr 4:11 inaonyesha kuwa tuna siku tofauti na nzuri zaidi ya kupumzika. Tunapaswa kutoa kila siku ya juma kuwepo kwenye pumziko la Mungu. Kwenye Kol 2:16, Paula anawaadabisha Wakolosai kuendelea kuitunza siku ya Sabato. Rum 14:5 inaongelea, bila kukataza, juu ya Wakristo kuzichukulia siku zote kuwa sawa. Kwenye 1 Kor 16:2 walitunza makusanyo siku ya jumapili.

Tazama swali kuhusu Rum 14:5 ili kujua jinsi kanisa la Agano Jipya lilivyofanya. Kanisa la kipindi kilichofuatia Agano Jipya lilikutana kwa ajili ya ibada siku ya jumapili kama ilivyoonyeshwa na First Apology of Justin Martyr (aliyeandika karibu mwaka 138-165 BK) sura ya 68.

Barua ya Barnabas (mwaka 100 BK)

Ignatius mwanafunzi wa Yohana Mtume (mwaka 110-117 BK)

Apostolic Constitutions (karne ya 2)

Dionysius wa Korinto (mwaka 175 BK)

Melitio wa Sardis (mwaka 175 BK)

Clement wa Alexandria (mwaka 183-217 BK)

Bardesanes (mwaka 180 BK)

Tertullian, Apologeticus (mwaka 200 BK)

Augustine aliamini kuwa kulikuwa na haja ya kuitunza Sabato kwenye nyakati za Agano Jipya.

Mabadiliko toka kwenye siku hii (jumamosi) yalitajwa na Justin Martyr, aliyeandika karibu mwaka 138-165 BK (Dialogue with Trypho, sura ya 47), anawaita watu wanaotunza Sabato "dhaifu wa imani", na Eusebius (mwaka 324 BK) anawataja wazushi wa Kiebioni (Wakristo wenye asili ya Kiyahudi wa karne za mwanzo za kanisa la awali waliochukuliwa kuwa waasi) kuwa waliitunza Sabato.

 

S: Kwa kuwa Kut 20:13 na Kumb 5:17 zinasema, "Usiue", kwa nini kuna watu na wanyama wengi sana waliokuwa wanauawa?

J: Hili ni swali zuri sana linalohuhu jambo ambalo linakosa kueleweka mara nyingi sana. Kama ni kweli kuwa Kut 20:13 ilimaanisha kutokuua mtu yeyote, jambo hili lingekuwa geni kwa Musa. Mara kadhaa Mungu amemwambia Musa kupigana vita na kuwaua wavunja sheria. Kama Kut 20:13 inamaanisha kutokuua kitu chochote jambo hili lingekuwa geni kwa Mungu aliyeamuru kafara ya wanyama.

Neno la Kiebrania, râtsach, linaweza kumaanisha kuua watu, lakini Hard Sayings of the Bible, uk.148-149 inasema kuwa katika ya maneno saba ya Kiewbrania yenye kumaanisha kuua, neno hili, linalotumiwa mara 47 kwenye Agano la Kale, ni lile lenye kumaanisha kuua kwa makusudi. Mandhari ya Kitabu cha Kutoka yanaonyesha kuwa baadhi ya vita na mauaji ya halali siyo tu viliruhusiwa bali pia viliamriwa.

Kama wazo la nyongeza lenye kufurahisha, gavana wa zamani wa jimbo la Pennsylvania alipinga sheria ya kurejesha adhabu ya kifo akinukuu na kuitafsiri aya hii.

 

S: Kut 20:13 na Kumb 5:17 zinasema usiue. Mungu aliagiza kuwa tuiue lakini alimtuma Mwanawe wa pekee kutolewa kafara (yaani kuuawa) na watu wake, Wayahudi wanaonichanganya . . . Naomba unieleze kwa nini Yesu alipaswa kufa kwa ajili ya dhambi zangu. Kwa nini niliishia kumuua Yesu? Kwa nini tuliishia kuvunja moja ya amri za Mungu kwa lengo la kuweka mambo sawa na Mungu wetu pia na nafsi zetu?

J: Tazama jibu la swali lililotangulia kuhusu kuua wanyama, mauaji yanafanywa kutekeleza sheria, na vita. Kuhusu upatanisho wa Mungu na wanadamu uliofanywa kifo cha Yesu, Mungu alimtuma `Yesu akijua kuwa atauawa na watenda maovu. Hata hivyo, hawa walikuwa katika hali ya kutokumtii Mungu walipofanya hivi. Lakini Mungu hutumia hata uasi na uovu wa kwa ajili ya makusudi yake. Rum 8:28 ni aya yenye kustaajabisha nasema ". . . katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema." HAISEMI kuwa Mungu hufaanya mambo mazuri tu. Badala yake, Mungu hafanya mambo yote (mazuri na mabaya) kwa kusudi jema kwa watu wanaompenda.

 

S: Kwa kuwa Kut 20:13 na Kumb zinasema usiue, kwa nini Mungu anaua watu wakati mwingine?

J: Amri kumi zilitolewa kwa watu; na Mungu, anayejua kila kitu, hafungwi na mambo aliyoyaagiza kwetu. Kwa mfano, Mungu huabudiwa lakini sisi hatuabudiwi.

 

S: Kwa kuwa Kut 20:14, 17 zinasema usizini, kwa nini kulikuwa na ndoa za mitala baada ya wakati huo?

J: Ndoa za wake wengi si uzinifu. Mitala iliruhusiwa lakini haikuhimizwa kwenye Agano la Kale, na kwenye Agano Jipya hairuhusiwi kwa viongozi wa kanisa.

Ingawa Kut 20:17 inasema usimtamani mke wa jirani yako (umoja), amri hii inaendelea kuwepo hata bila kujali kuwa jirani yako ana mke mmoja au zaidi. Kama Biblia ingekuwa haijazuia kutamani wake wa jirani yako (uwingi), watu wengine wangeweza kusema kuwa amri hii inamanisha kumtamani mmoja wa wake wa jirani yako ni SAWASAWA.

 

S: Kwenye Kut 20:20, kwa watu walitakiwa kutokuogopa, kwa kuwa walitakiwa kuongopa kwenye aya hiyohiyo?

J: Watu wa wakati na sisi pia hatutakiwa kumwogopa Mungu mwenye upendo mkubwa kiasi hiki kwetu. Lakini tunatakiwa kumwogopa Mungu kwa maana ya kumheshimu Yeye na nguvu na utakatifu wake. Leo hii, tunapaswa pia kuwaogopa watu waliopotea wanaogopa ghadhabu ya Mungu itakayowaangamiza endapo hawatatubu, kama Yuda 23 inavyosema.

Hata hivyo, kwa kuwa Kristo amefunuliwa, hatuna aina ileile ya hofu waliyokuwa nayo watu wa Agano la Kale, kama Ebr 12:18 inavyosema. Tazama pia maelezo ya Kut 9:30.

 

S: Kwenye Kut 20:24, je madhabahu ilitengenezwa kwa udongo, au mti wa mshita kama Kut 27:1; 30:1; 37:1 na 38:1 zinavyosema?

J: Kwenye Mlima Sinai, walitengeneza madhabahu ya udongo. Baadaye, kwa ajili ya hema la kukutania, walitengeneza madhabahu inayobebeka ya mti wa mshita, ingawa huenda ilikuwa na udongo ndani kwa ajili ya majivu.

Tazama When Critics Ask, uk.79 na Haley's Alleged Discrepancies of the Bible, uk.427-428 kwa jibu tofauti.

 

S: Kwenye Kut 20:25-26 na Yos 8:31, kwa nini haikuruhusiwa kutumia mawe yaliyochingea?

J: Biblia haisemi kwa nini Mungu aliamuru jambo hili, ila tu inasema kuwa aliamuru. Hata hivyo, mawe yaliyochingwa kwa kutumia patasi za chuma yalionyesha alama za kutu baada ya muda fulani. Alama za bluu-kijani zilionekana kwenye mawe yaliyochongwa na vifaa vya fedha au shaba.

 

S: Kwa nini Kut 21:2-21 na 32:1-6 zinaunga mkono utumwa?

J: Kwa kiasi kikubwa, utumwa wa kwenye Biblia haukufanana na utumwa uliokuweko kusini mwa Marekani, lakini unafanana na watumishi wa mkataba. Watumwa wote wa Kiebrania walitakiwa kuachwa huru baada ya miaka saba kwenye Kut 21:2-5. Wakati mtumwa anaachiwa huru, bwana wake alitakiwa kumpa kwa ukarimu vitu vyovyote alivyokuwa navyo kwa mujibu wa Kumb 15:13-15. Jambo pekee lisilofuata kawaida hii ya kumwachia huru mtumwa wa kiebrania lilikuwa kama mtumwa mwenyewe alimpenda bwana wake sana hata aamue kuwa mtumwa maisha yake yote kwenye Kut 21:5-6. Hata hivyo, Waebrania hawakuwa wanawaachia huru watumwa wao kila mara kama Yer 34:8-22 inavyoonyesha; Mungu aliwakaripia kwa ajili ya jambo hilo. Watu wafuatao waliweza kuwa watumwa:

Wezi ambao hawakuweza kuwalipa wadeni wao (Kut 22:3)

Wanawake waliouzwa na wazazi wao kuwa mahawara (Kut 21:7-11)

Watu waliojiuza wenyewe kuwa watumwa kwa sababu ya kukosa chakula

 

S: Kwenye Kut 21:13, je maneno "Mungu amemtia mkononi mwake" yanamaanisha nini hapa?

J: Maneno haya yanafanana na matumizi ya kisheria ya jamii za magharibi ya tendo la Mungu yenye kumaanisha kitu kilicho nje ya uwezo wa binadamu. The Expositor's Bible Commentary juzuu ya 2, uk. 432 inasema kuwa misemo kama hiyo inapatikana kwenye Sheria za Hammurabi 249:38-39; 266:77.

 

S: Kwenye Kut 21:17, je adhabu hii ilikuwa ya kikatili kwa watoto wasiokuwa watiifu?

J: Mambo manne ya kuzingatia katika kujibu swali hili.

1. Jambo hili lingeonekama kuwa ukatili kwetu leo hii, kwa kujua kuwa wazazi wana mamlaka hii kungewaepusha vijana kuyadharau kabisa mamlaka ya wazazi wao. Hata hivyo, adhabu hii ni ndogo ikilinganishwa na Wakanaani na Wafoeneke waliokuwa wanatoa kafara ya watoto. Hebu fikiria mtoto wa Kikanaani au Kifoenike akikosa utiifu, na mzazi akisema "tabia yako inanifanya nianze nijihisi mtu wa dini sana." Waisraeli pekee waliokuwa wanatoa kafara ya watoto walikuwa ni waabudu sanamu ambao Mungu aliwahukumu.

2. Kwa Waisraeli wacha Mungu, ukichukulia mwelekeo wao wa kifamilia, hakuna ushahidi kuwa watoto waliwahi kutokuwa watiifu kwa kiasi kikubwa sana hata kuwafanya wazazi watumie adhabu hii.

3. Hata kama palikuwa na watoto wasiokuwa watiifu, Kut 21:17 haisemi bayana kuwa wazazi wanatakiwa kufanya hivi; ilikuwa ni moja ya njia tu. Hakuna ushahidi kuwa mzazi yeyote alichagua kufanya hivi.

4. Katika jamii za Kirumi za miaka iliyofuata, wakina baba wa Kirumi walikuwa na "haki ya ukuu wa familia." Hii ilikuwa ni haki ya kisheria ambayo baba wa Kirumi alikuwa nayo kumuua mtoto wake aliyetoka kuzaliwa kwa sababu yeyote ile.

Hitimisho: Wakati mwingine katika kutengeneza sheria, kuweka namna mbalimbali za kuitimiza zenye adhabu kubwa, husaidia kutimiza malengo yake bila kuwa na matukio yanayoifanya itumike.

 

S: Kwenye Kut 21:20, kwa nini mtu "angeweza kuadhibiwa" tu kwa kumpiga mtumwa na kumuua?

J: Kut 21:12 inaweka adhabu bayana: kifo kwa kuua kwa makusudi, na kwenda mji wa kukimbilia kwa kuua bila kukusudia. Sheria hii inatumika kwa watu wote watumwa na walio huru.

Hakuna tofauti yeyote iliyoelezwa ya adhabu kati ya mtumwa, na hakuna haja ya kusema kuwa adhabu ilikuwa ni ileile, kama muuaji wa mtu huru au mtumwa ilivyokuwa ileile Misri walikoishi. Sheria hii ya Kimisri ilitajwa kwenye Life in Egypt in Ancient Times cha Bernard Romant, kilichotafsiriwa na J. Smith (Minerva 1978/81), uk.124.

 

S: Kwenye Kut 21:21, kwa nini Kitabu cha Kutoka kinaunga mkono kupiga watumwa?

J: Tabia nyingine kwenye Agano la Kale hazikuungwa mkono lakini ziliruhusiwa kwa sababu mioyo ya watu kwenye Agano la Kale ilikuwa migumu. Kwa mfano, kutoa talaka kuliruhusiwa kwenye Agano la Kale kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya watu (Mat 19:8) lakini kwenye Mal 2:16 Mungu alisema anachukia talaka. Kumpiga mtu mwingine bila kumwachia jeraha la kudumu kuliadhibiwa kwa faini ya fedha kwa ajili ya muda uliopotea kwenye Kut 21:18-19. Kut 21:21 inaonyesha tu kuwa mtu anaye miliki mtumwa hatozwi faini kwa ajili ya muda uliopotea kwa sababu alikuwa ni mmiliki (huenda kwa jambo la kijinga) aliyepoteza muda wa mtumwa. Hata hivyo, mtumwa au mtu asiye mtumwa, kama mtu amempiga mtu mwingine hadi akafa, mtu huyu atauawa kwenye Kut 21:12, 20. Vivyo hivy, kama mtu atasababisha jeraha la kudumu, patakuwa na faini ya hela, uhuru wa mtumwa, au jicho kwa jicho.

 

S: Je Kut 21:22-23 inaonyesha kuwa kutoa mimba si sahihi, au kuwa kijusi si mtoto?

J: Neno la Kiebrania (eats) linamaanisha kutoa (mtoto) wakati wa kuzaa lakini pia kutoa mimba. Kuna neno tofauti la Kiebrania la kutoa mimba ambalo halimaanishi kuzaa, lakini halikutumika hapa. Mwisho, neno "mtoto" ni neno linalotumika kwa watoto wadogo.

Kama maelezo ya ziada, utoaji mimba (kwa kutumia dawa/vidonge) ulifanyika nyakati za Biblia. Kwa mujibu wa Discover Magazine (Septemba 1998), mmea uliokuwa unalimwa Cyrenaica, ulioitwa Silphium, ulikuwa na uwezo wa kutoa mimba. Uliuzwa kwa uzito wake wa fedha. Wakristo wa kale walilijua jambo hili na walipinga utoaji mimba.

Tertullian's Apology, sura ya 9, uk.25 (mwaka 197-217 BK), "Kwa upande wetu, uuaji umezuiliwa kabisa, hatupaswi kuondosha maisha hata ya kijusi kilichopo tumbani, ingawa binadamu anapata damu kutoka sehemu nyingine za mwili ili kuweza kuishi. Kuzuia kuzaa ni njia ya kuharakisha kuua wa mtu; wala haijalishi endapo unatoa maisha ya kiumbe aliyekwisha zaliwa, au unaharibu uhai wa kiumbe anayekaribia kuzaliwa. Huyu ni binadamu anayekwenda kuzaliwa; tunda liko tayari kwenye mbegu yake."

Tertullian (mwaka 197-217 BK) alisema, "Sheria ya Musa inatoa adhabu kwa mtu anayesababisha kutoa mimba, maadamu kuna kiinitete cha binadamu ambacho kimeweka hata sasa hali ya maisha na kifo, kwa kuwa tayari kinahusishwa na mambo yahusuyo maisha na kifo, kwa kuendelea kuishi ndani ya mama, kinashiriki kwa sehemu kubwa hali yake yenyewe na mama." A Treatise on the Soul, sura ya 37, uk.218.

Tertullian pia alisema kuwa kutoa mimba kwa kutumia dawa/vidonge ni makosa kwenye On Exhortation to Chastity, sura ya 12, uk.57.

 

S: Kwenye Kut 21:29-30, kwa nini adhabu ya kifo haikutolewa kwa baadhi ya wauaji?

J: Kama ilivyo katika sheria za kisasa, hakuna adhabu haitolewi kwa mtu anayekuwa ameua bila kukukusudia. Ni jambo moja kuua mtu kwa makusudi na lingine kumuua mtu bila kufikiria.

 

S: Kwenye Kut 22:8-9 na 1 Sam 2:25, je watu walikwenda mbele ya waamuzi hapa au mbele ya Mungu?

J: Hakuna swali kuhusiana na neno la Kiebrania; ni elohim. Hata hivyo, elohim linaweza kumaanisha Mungu wa kweli, miungu wa uongo, au waamuzi. Hapa kuna maoni mawili.

Mungu: Septuajinti imelitafsiri neno hili kama watu kwenda kwa Mungu. Jay P. Greens kwenye Literal Translation pia anasema "Mungu." NRSV inasema "Mungu", lakini inaongeza maelezo chini ya ukurasa, "au mbele ya waamuzi."

Waamuzi: Elohim inaweza kumaanisha waamuzi wanadamu, kama kwenye Zab 82:6. Elohim inaongelea waamuzi kwenye Kut 21:6.

Hitimisho: Hivi ndivyo Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 3, uk.586 inavyosema kuhusu 1 Sam 2:25, "Kama pambizo la NIV linavyoonyesha, hatuwezi kuwa na uhakika wakati wote endapo (Elohim) inamaanisha "Mungu" au "waamuzi" kwenye mandhari kadhaa . . . Hapa kwenye mstari wa 25, na kwenye vifungu vya Kitabu cha Kutoka, inaweza kuwa vizuri kuliacha swali hili liendelee kujadiliwa, kwani kwa vyovyote vile "waamuzi" (kama ndio wao) wanaonekana kuwa wawakilishi wa Mungu wanaoonyesha mapenzi yake na kutimiza matakwa yake."

 

S: Kwenye Kut 22:18, kwa nini wanawake wachawi waliuawa [inavyodaiwa] lakini si wanaume?

J: Kuzuiliwa kwa uchawi, watu wanaowasiliana na mizimu, na kujihusisha na mizungu kuliwahusu watu wote wanawake na wanaume bila ubaguzi. Bila kujali jinsia, Mungu anakupa uzito mkubwa kujihusiha na uchawi. Wakristo hawapaswi kulidhalilisha jina wanalolibeba kwa kujihusisha na kuwasiliana na roho za watu waliokufa, mbao za Ouija (mchezo wa mbao unaomuwezesha mwenye kuucheza kuwasiliana na roho za watu waliokufa), ubashiri wa hali ya baadaye, au mambo mengine ya kichawi.

 

S: Kwenye Kut 22:18, mwalimu mmoja wa shule ya jumapili (darasa la watu wazima) aliwahi kusema kuwa anaweza kutibu magonjwa kwa kushikilia mnyororo wa metali kwa kutumia kipande cha metali kinachojitokeza kwenye mkufu unaovaliwa shingoni kikiwa kwenye kifundo cha mkono wake na kuuuliza mwili wake maswali. Kitazunguka kwa namna tofauti zenye kumaanisha ‘hapana' na ‘ndiyo.' Je unafikiri nini kuhusu jambo hili?

J: Jambo hili linahusu kuziomba roho [za namna fulani] zitoe majibu. Jambo hili linaonekana kufanana na mambo ya kishirikina (Kishetani) ya Ubao wa Ouija. Muulze kuwa anajuaje aina ya roho anayodhani inafanya hivi? 1 Yoh 4:1-2 inasema kuwa hatupaswi kuziamini tu roho zote. Kwenye 2 Kor 6:17 tunaambiwa kuwa hatutakiwo kugusa kitu chochote kilicho kichafu.

Nimewahi kusikia kuhusu mchungaji [kwa usahihi kabisa] aliyesema toka madhabahuni kuwa hatupaswi kuufuata unajimu. Lakini, katika kuthibitisha kuwa haukuwa na kitu chochote cha maana, aliagiza buruji (nyota) yake isomwe na angemwonyesha kila mtu jinsi ilivyokuwa uongo mtupu. Hata hivyo, ilionekana kuwa yale mambo yalianza kutimia. Aliogopa na kutubu mbele ya ushirika kwa jambo alilokuwa amelifanya. Ni baada ya kufanya hivyo ndio mambo mengine yaliyotabiriwa hayakutimia.

Shetani an nguvu kuliko sisi, na wakati mwingine anaweza kutabiri vitu kwa usahihi (au akahakikisha kuwa vinatokea). Anatumia jambo hili kuwafanya watu wakitumaini chanzo hiki cha ushauri, ili aweze kuwadanganya watu baadaye.

Hivi ndivyo ambavyo ningefanya kama ningekuwa mshiriki wa darasa hili la shule ya jumapili.

1. Nenda kwa mwalimu huyu na kumweleza kuwa umeweka tumaini lako kwa Yesu Kristo, siyo mapepo yanayowahudumia na kuwatii wachawi. Muonyeshe aya zinazozuia ushirikina, na huenda akaona na kutubu. Baadhi ya aya zenye kusema tusijihusishe kabisa na ushirikina, tusiwasiliane na watu waliokufa, n.k. ni:

Usijihusishe na uchawi na ushirikina, kama kuwasiliana na watu waliokufa, uchawi, safari za kinyota (kutafsiri mambo yanayotokea nje ya mwili, yaani Out-of-body-expereince - OBE, kunakoamini kuwepo kwa mwili wa kinyota ulio tofauti na mwili halisi na unaweza kusafiri nje ya mwili halisi), kuwatumia watu wenye kudai kuwasiliana na roho za watu waliokufa, wapiga ramli, unajimu, vibao vya oujia, Kutafakari kunakovuka mipaka ya kibinadamu (njia ya kujiondolea wasiwasi na kuongeza muafaka na kuufikia upeo wako kwa kutafakari, kurudiarudi mantra, na mambo mengi ya Kiyoga iliyoanzishwa na shirika la kimataifa lililoanzishwa na mwalimu wa kiroho wa Kihindi umia k mtu jifikisha kwenye kwenye Maharishi Mahesh Yogi), EST (Erhard Seminars Training) ambao ni mfumo wa kujiendeleza mwenyewe uliokusudia kuongeza uwezo wa mtu kupitia kujitambua kama kikundi na vipindi vya mafunzo, au Qi-gong (Law 19:26, 31; 20:6-8, 27; Mdo 19:19; Eze 13:18; 22:18; Kumb 18:9-14; Mik 5:12; Ufu 9:21).

Usijaribu kuwasiliana na watu waliokufa (Kumb 18:10-2; Isa 8:19; 1 Sam 28:3, 7-12 na Law 20:6-8).

Kwa habari ya maovu, tunatakiwa kuwa watoto wadogo (1 Kor 14:20; Mat 10:16) lakini tuwe macho (Mat 10:16-7).

2. Endapo hatakuwa ameshawishika kutubu, mwambie mchungaji na wazee wa kanisa kuwa jambo hili halipaswi kufanyika kwenye kanisa linalomwamini Kristo, na pendekeza kuwa wamuondoe kufundisha darasa la shule ya jumapili.

3. Endapo njia hii haitafanikiwa, mshirika anao wajibu wa kulihama kanisa, na kumwambia kila mtu anayetaka akujue kwa nini unaondoka. Kuondoka kwako kutakuwa ushuhuda mzuri zaidi kuliko kuendelea kuwepo na kuendelea kuwashawishi. Kwa kadri uatakavyoendelea kuwepo, utakuwa unasema kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja kuwa jambo hili si baya.

Kwa taarifa yako, sitatoa ushauri huu kwa mwalimu wa shule ya jumapili anayeamini na kufundisha kitu kisicho sahihi kinachohusu jambo lisilokuwa la msingi katika imani ya Kikristo. Lakini hatupaswi kujihusisha na utumiaji wa "chombo" chochote kile kutafuta ushauri toka katika ulimwengu wa kiroho.

 

S: Kwenye Kut 23:19 na Kumb 14:23, kwa nini hairuhusiwi kuchemsha mwana-mbuzi kwenye maziwa na mama yake?

J: Ni kwa sababu Mungu ameagiza kutokufanya hivyo. Endapo kitendo hicho ni cha ibada ya sanamu, kishirikina, chenye kukufuru, cha kikatili au kina dharau, silo jambo la msingi; sababu ya msingi ni kuwa Mungu hakipendi na ameagiza kisifanyike.

Kulikuwepo pia na desturi hii ya Kikanaani na Kiashuru ya zamani zile iliyokuwepo kuanzia karne ya 15 KK.

Baadaye, Wayahudi waliongeza wigo wa amri hii na kuhusisha kutokuwapa watu nyama na maziwa kwenye mlo mmoja, au hata kuviandaa kwa kutumia chombo hivyo hivyo.

 

S: Kwenye Kut 23:28, "manyigu" yaliwaondoaje Wakanaani?

J: Wadudu wanaoitwa manyigu hawakuwaondoa Wakanaani. "Manyigu" ambayo Mungu anayongelea hapa walikuwa ni Waisraeli wenyewe. Biblia ni kweli tupu' lakini jambo hili halimaanishi kuwa Mungu amezuiliwa kuwasiliana nasi kupitia lugha za picha.

 

S: Kwenye Kut 23:31, Wafilisti waliwezaje kuwepo Kanaani wakati wa Musa?

J: Tazama maelezo kwenye Mwanzo 20 kwa ajili ya jibu la swali hili.

 

S: Kwenye Kut 24:1, tunaweza kujifunza nini kutoka kwa Nadabu na Abihu?

J: Kama watoto wa Haruni, walikuwa kwenye mlolongo wa kuja kuwa kuhani mkuu atakayefuata. Lakini kuwa mtoto wa mtu anayemcha Mungu hakumwepushi mtu na hatari; ukweli ni kwamba inakuwa hatari zaidi endapo mtu anakuwa hataki kumfuata Mungu. Kwa jinsi unavyojua vitu vingi zaidi ndivyo utakavyo adhibiwa zaidi kwa kutokutii kama 2 Pet 2:21 inavyosema.

 

S: Kwenye Kut 24:4, Musa aliwezaje kuandika "Basi Musa akayaandika maneno yote ya BWANA"?

J: Kwa njia ileile aliyoandika Kut 6:26-27. Tazama maelezo kuhusu jambo hili. Kwa upande mwingine, mtu aliyekuwa anamwandikia Musa aliandika maneno haya.

 

S: Kwenye Kut 24:9-11, wazee waliwezaje kukwea Mlima Sinai, kwa kuwa kila mtu atakayeupanda atauawa kwenye 19:12-13?

J: Watu waliweza kupanda Mlina Sinai pale tu walipokuwa wameitwa. Vivyo hivyo, walitakiwa kwenda kwenye nchi ya ahadi, lakini baada ya taarifa ya kuvunja moyo ya wapelelezi walikataa kwenda. Baada ya Mungu kuwaadhibu na kuwaambia kuwa watakufa jangwani, waliamua kwenda nchi ya ahadi kwa hiari yao. Walirudishwa nyuma na maadui wao. Kufanya kitu sahihi si kitu cha muhimu zaidi. Kitu cha muhimu zaidi ni kumpenda Mungu na kumtii ambako kunahusisha kufanya vitu sahihi katika njia sahihi na kwa wakati sahihi.

 

S: Kwenye Kut 24:10, je waliwezaje kuona umbo la Mungu kwani Mungu hana mwili?

J: Mungu anaweza kutwaa umbo lolote la kimwili analopenda kuwa nalo.

 

S: Kwenye Kut 25:18, kwa nini Mungu alimwamuru Musa kutengeneza sanamu za kuchonga za makerubi?

J: Hizi ni sanamu zilizolipamba hema la kukutania, lakini sanamu hizi hazikuabudiwa, kuombwa, au kutukuzwa. Makerubi yalikuwa kwa ajili ya mapambo tu, hayakuwa sanamu za Mungu, na hayakuwa kwa ajili ya kuabudiwa au kutukuzwa.

 

S: Kwenye Kut 27:1 na Kumb 10:3, mti wa mshita ni nini?

J: Shitimu ni sehemu mashariki ya Mlima Sinai iliyotajwa kwenye Hes 25:1. Mti huu unaweza kuwa ulitokea hapo, ulipewa jina la mahali hapo, au mahali hapo ndipo palipopewa jina la mti huo.

 

S: Kwenye Kut 28:30, je "Urimu" na "Thumimu" ni nini?

J: Vilikuwa ni vitu ambavyo Mungu aliwapa makuhani kupiga kura kutambua mapenzi ya Mungu. Maelezo ya sura yake halisi hayapo ila Josephus anadai kuwa yalikuwa mawe yaliyo kwenye deraya ya kifua. Msemo "Urimu na Thumimu" unaweza kumaanisha "mianga na ukamilifu."

 

S: Kwenye Kut 28:34-35, je njuga ziliwasaidiaje Haruni na uzao wake wasife?

J: Njuga kama njuga hazikuwasaidia. Lakini namna ya kuabudu katika hema hili la kukutania lilikuwa ni jambo la muhimu sana kwa Mungu, na kuipuuzia amri hii kungeleta kifo. Tazama pia swali linalifuata.

 

S: Kwenye Kut 28:34-45 na 39:22-26, njuga zilikuwa na kazi gani kwenye joho la kuhani?

J: Maandiko hayasemi, lakini tunaweza kukisia sababu mbili.

1. Wakati watu waliokuwa nje waliposikiliza, wangeweza kumsikia kuhani, ambaye hawakuweza kumuona, akitoa kafara kama malipo ya dhambi zao.

2. Kama njuga zilinyamaza ingeonyesha kuwa Mungu hakuwa amefurahishwa na kuhani na hivyo alimuua. Kisha watu walimtoa kuhani nje kwa kumvuta na kamba aliyojifunga.

 

S: Kwenye Kut 29:20 na Law 8:23-24, kwa nini Musa aliambiwa kutia damu katika ncha ya sikio la kulia, kidole gumba cha kulia na kidole kikubwa cha mguuni cha kulia cha Haruni?

J: Ingawa Maandiko hayasemi kiwazi kwa nini Mungu alipenda hivi, ishara ya jambo hili si nguvu kuiona. Inaonyesha kufunganishwa na kafara. Kama mfano mwingine, jambo hili lilifanywa kwa mtu aliyekuwa ametakaswa tokana na ugonjwa wa ngozi, wakati walipoleta kafara ya utakaso kwa kuhani (Law 14:1-2, 14-17).

 

S: Kwenye Kutoka 30, je vyombo hivi vinamaanisha nini na vinawakilisha nini?

J: Kwanza kabisa, huenda pakawa na mafumbo mengine ambayo bado hatuyajui; Mungu anaweza kuwa hajafunua kila sababu ya vitu kuwa namna hii. Ebr 8:5 inasema, "Watumikao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kufanya ile hema; maana nasema Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule uiloonyeshwa katika mlima" (NIV). Tazama Waebrania sura ya 9 na 10 kwa maelezo zaidi juu ya umuhimu wa hema la kukutania na vyombo vilivyokuwa ndani yake.

Yafuatayo ni maelezo ya kina ya Kutoka 30.

Kut 30:1-9 Madhabahu ya mti wa mshita ilikuwa ndogo, karibu urefu wa karibu mita 1 (futi 3) na karibu sentimita 118 (inchi 18) za mraba, lakini nzito sana kwa sababu ilikuwa imefunikiziwa dhahabu juu yake. Dhahabu inaweza kuwakilisha utakatifu na Mungu, na dhahabu ilikuwa moja ya zawadi tatu ambazo mamajusi walileta kwa Yesu. Madhabahu hii ni taipolojia ya kafara ya Kristo kwa ajili yetu. Kitu cha kustaajabisha ni kuwa hakuna mapambo ya hekalu yaliyotajwa kuwa "matakatifu zaidi" isipokuwa madhabahu.

Jambo la pili la kufanyia kazi katika maisha yetu ni kuwa kama ambavyo kuhani alipaswa kuchoma uvumba madhabahuni kila asubuhi na jioni, tunapaswa kuongea na Mungu angalau kila asubuhi na jioni. Kama ambavyo Kristo alivyotoa maisha yake kafara kwa ajili yetu, kwa namna ndogo, tunapaswa kuwa tayari kuumia kwa ajili ya watu wengine, kama Paulo kwenye Kol 1:24.

Kut 30:10 mara moja kwa mwaka Haruni, kuhani mkuu wa Waisraeli, alipaswa kufanya malipo ya dhambi kwenye pembe za madhabahu.

Kama ambavyo Waisraeli walikuwa na kuhani mkuu kwenye Kutoka 30, tunaye kuhani mkuu aliyetoa kafara kwa ajili yetu kwenye Ebr 4:14: Yesu.

Kut 30:17-21 Birika la shaba la kuogea. Haruni na watoto [wazao] wake walitakiwa kuosha mikono na miguu yao kabla ya kuingia kwenye hema la kukutania, na kabla ya kuikaribia madhabahu.

Kimsingi, hatupaswi kwenda mbele ya Mungu huku tunafikiri kuwa hatutakiwa kuwa safi. Tunatakiwa kuoshwa. Isitoshe, Wakristo ni makuhani na wafalme, na tumeoshwa kwa damu ya Yesu, kwa hiyo alitimiza hili kwa ajili yetu. Lakini tunatakiwa kuishi maisha safi yaliyotakaswa. Tazama 1 Pet 1:15-16; 2:11-12.

Kama nyongeza, shaba ilitoka kwenye vioo vya shaba vilivyotolewa na wanawake kwenye Kut 38:8. Jambo la pili la kufanya katika maisha yetu tokana na ujumbe huu kuwa vitu vilivyokuwa vinatumika kwa ajili ya majivuno na mapambo sasa viliyeyushwa upya na kutumika kwa ajili ya utakaso. Litakuwa jambo la kumpendeza Mungu endapo baadhi ya desturi na mazoea yetu tunayoyajua "yangeyeyushwa" na kubadilishwa kwa ajili ya kazi yaake. Tazama Rum 12:1-2 na Yak 1:23-25.

Kut 30:22-33 Kupaka mafuta kwenye vyombo vitakatifu. Nafikiri kiambato hiki kilifanywa kwa sababu kilikuwa kinaleta harufu nzuri. Mafuta ya kupata yalikuwa ni aina ya Roho Mtakatifu na yanawakilisha kutakaswa na Mungu. Yaliwekwa chumvi kwenye Kut 30:35, huenda ni kwa ajili ya kuyatunza. Manemane iliyokuwa ghali sana ni moja ya zawadi ambazo mamajusi walimpelekea Yesu.

Kimsingi, kama harufu ya mafuta ya kupaka "iliyoweka mazingira" ya kila kitu, kuoshwa na kutakaswa kwetu kupitia Roho Mtakatifu hutupa harufu ya Kristo. Tazama 2 Kor 2:14-16 kwa maelezo zaidi juu ya sisi kuwa manukato ya Kristo.

Jambo la pili la kulifanya tokana na ujumbe huu ni kuwa mafuta haya ya kupaka hayakupaswa kuchukuliwa kirahisi tu na "yalifanywa kuwa ya kawaida" kwa kutumika kwa ajili ya kitu kingine chochote. Miili yetu (hekalu la Mungu kwenye 1 Kor 6:19-20), umoja wetu wa roho (Efe 4:3), na maisha yetu hayapaswi kufanywa kuwa ya kawaida kwa matumizi yasiyokuwa matakatifu. Hatupaswi kuwatupia nguruwe lulu zetu, kufungwa nira pamoja na wasioamini (2 Kor 6:14-18), kuvichukulia kwa vitakatifu vitu ambavyo si vitakatifu, au kupotoshwa kutoka katika upendo wetu wa kweli kwa Yesu (2 Kor 11:3-4).

Kut 30:34-38 Uvumba unawakilisha maombi na maombezi. Lakini uvumba haukutakiwa kutumika kwa kitu chochote kingine. Uvumba, isitoshe, ulikuwa ghali sana, na ulikuwa ni moja ya zawadi tatu ambazo mamajusi walimletea Yesu. Tazama Ufu 8:3-4 juu ya uvumba kuhusiana na maombi.

Kimsingi, kama ambavyo harufu ilikuwemo kwenye kila kitu wakati makuhani walipokuwa wanachoma uvumba, Roho Mtakatifu, aliyetumwa na Baba na Yesu (Yoh 16:7) anapaswa kuwemo katika kila sehemu ya maisha yetu. Kristo, na Kristo tu, ndiye mpatanishi wetu (Efe 2:13-17; Kol 1:20; Ebr 8:6) na Roho Mtakatifu hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkika (Rum 8:26-27).

Jambo la pili la kulifanyia kazi katika maisha yetu ni kuwa katika kumfuata Yesu, tunatakiwa tudumu tukiomba, kumsifu Mungu na kuwaombea watu wengine (1 Thes 5:17; Fil 4:6).

 

S: Kwenye Kut 30:11, 15, kwa nini watu maskini wanatakiwa kulipa kiasi sawa na matajiri ambao walikuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kulipa?

J: Sadaka ya nusu shekeli kama fidia ya maisha yao, na kuna jambo muhimu hapa. Maisha ya tajiri si muhimu zaidi au kidogo kuliko maisha ya maskini. Katika sheria zote za Agano la Kale, hakukuwa na adhabu ndogo ya kumuua au kumdhuru maskini kuliko tajiri.

Sadaka hii ilikuwa kwa watu wenye miaka ishirini na zaidi tu, na huenda ilikuwa kwa wanaume tu, jambo ambalo lingemaanisha kuwa sadaka hii ilikuwa kwa familia nzima. Familia haikuadhibiwa kwa kuwa na watoto zaidi.

 

S: Kwenye Kut 30:12 na Law 9:7, ng'ombe dume au mwanakondoo anawezaje kulipia dhambi za mtu?

J: Wanyama hawawezi kulipia dhambi za mtu, kwa mujibu wa Ebr 9:9 na 10:4. Hata hivyo, Waebrania 9-11 inaonyesha kuwa kafara za Agano la Kale zilikuwa taipolojia, au kifananisho cha kafara ya Yesu.

Kwa kuelezea jambo hili katika msemo wa kila siku, chukulia mtu ana deni kubwa sana (au dhambi) sana kiasi kwamba hawezi kumlilipa mdai wao (matakwa yasiyobagua ya haki ya Mungu). Uwezo wao wa kulipa hauwezi kuaminiwa. Lakini mfalme tajiri (Mungu) anaingilia kati, na anaandika jina lake kuafiki kulipa deni lote. Kisha mtoto wake analipa deni lote. Wakati mdai anakuja kuchukua hela zake, kwa kumtii mfalme, watu wanaonyesha alama halisi kuwa deni lao limelipwa na mfalme.

 

S: Kwenye Kut 31:12, kwa nini maadhimisho ya siku ya Sabato yalikuwa muhimu sana?

J: Wakristo wengi wa kweli wanaamini kuwa siku zote ni pumziko ndani ya Yesu (Ebr 4:8-11), wakati Wakristo wengine wa kweli wanaamini kuwa tunapaswa kuiadhimisha siku ya Sabato leo hii. Paulo anazitambua desturi zote kwenye Rum 14:5-7, na anasema kuwa jambo la muhimu ni kumuishia Bwana.

Hata hivyo, Wakristo wote wanapaswa kukubali kuwa kuiadhimisha siku ya Sabato ilikuwa ni amri muhimu wakati wa sheria ya Musa, na kama tungekuwa tunaishi wakati ule, tungepaswa kufanya bidii kuiadhimisha.

Kuna amri tatu zilizo wazi kabisa, na sababu nne wazi kuhusu Sabato, lakini tunaweza kuona sababu zaidi pia.

Amri zinazohusu Sabato:

1. Ikumbuke siku ya Sabato uitakase (Kut 20:8; Kumb 6:12)

2. Usifanye kazi yeyote (Kut 20:10; Kumb 6:13-14)

3. Watu walio chini yako: mwana wa kiume, binti, watumwa, na hata wageni (wasiokuwa Wayahudi) walio ndani ya malango yako, hata wanyama, watakuwa na siku ya kupumzika (Kut 20:10; Kumb 6:14)

Sababu za wazi za kuadhimisha Sabato:

1. Utii: Inatupasa kuzitii amri za Mungu

2. Kumkumbuka Muumba wetu: Kama Mungu alivyoiumba dunia kwa siku sita kisha akapumzika, ndivyo hivyo wanavyotakiwa kumheshimu kwa kupumzika siku ya Sabato (Kut 20:11)

3. Kukumbuka utumwa na ukombozi wetu: Kama Waisraeli walivyokuwa watumwa Misri (inadhiniwa bila kupumzika), na Mungu aliwatoa, wanatakiwa kuikumbuka na kuiadhimisha Sabato (Kumb 16:15b)

4. Kama ishara ya watu wa Mungu wa Agano la Kale, kuwa wajue kuwa Mungu anatutakasa (Kut 31:13)

5. Mungu aliibariki Sabato na kuitakasa, hivyo tunapaswa kulitambu jambo hilo (Kut20:11b)

Sababu za ziada zenye kuwezekana:

1. Sabato ilikuwa chukizo kwa hekima na jitihada za watu. Inaweza kuwa dhahiri kwa mtu mwenye hekima hapa duniani kuwa ukifanya kazi zaidi utapata manufaa zaidi. Na hata unapotaka kupumzika, unaweza kuwafanya waajiriwa, watumwa na wanyama wako wafanye kazi zaidi. Mungu hakupingana na wazo hili, au hata kusema endapo lilikuwa sahihi au la. Bila kujali ukweli uliotambulika wa fikra hii, Mungu aliagiza kumtii Yeye kwanza.

2. Sabato ilikuwa chukizo kwa uhuru na kujitegemea kwao. Mfanya biashara, mkulima, fundi, au mfanya kazi mwingine yeyote yule angependa kufanya kazi siku ya Sabato endapo walifikiria ustawi au hata kuendelea kuishi kwao na kwa familia vilitegemea kazi hizo. Lakini jambo hili linaishia kuwa tumaini: je ustawi wako na kuendelea kwako kuishi kunakutegemea wewe, au unaamini kuwa kunamtegemea Mungu?

3. Kuwa na siku ya kupumzika kungewafanya Waisraeli, watu walio chini yao, na hata wanyama wao kuwa na afya zaidi, kimwili, kiakili, na kihisia, kwa kupata muda wa kuburudisha na kupata nguvu mpya kutoka kazi za juma zima. Watu leo hii, bila kujali imani zao wanahitaji muda wa kupumzika na kuburudisha miili yao.

4. Kuwa na siku ya kupumzika kunasaidia kuepusha kuchoka sana kunakosababishwa na kufanya kazi kwa muda mrefu sana, kutoka kufanya kitu hichohicho bila kubadilisha kwa miaka na miaka. Hata Wakristo wanaochukulia siku zote kuwa sawa bado wanahitaji muda wa kupumzika na kurejesha nguvu upya.

Ingawa Wakristo wa kweli hawakubaliani juu ya kufanya kazi siku ya Sabato (jumamosi) au la, au jumapili, au siku zote kuwa sawa, Wakristo wote wanatakiwa kukubaliana juu ya vitu viwili hapa.

a) Kama tunaamini kuwa Mungu anataka tuwe na siku moja ambayo hatufanyi kazi leo hii, natufanye hivyo.

b) Siku zetu zote, siyo siku moja kwa saba, tunatakiwa kujitoa kumtumikia Mungu.

 

S: Kwenye Kut 31:17, je Mungu anaweza kuchoka?

J: Mungu hachoki (Isa 40:28). Hata hivyo, kama ambavyo watu wanaweza kusema kuwa wamechoka kulalamika na upendo usio wa kweli, huu ni msemo unaoonyesha kuchoshwa kwa Mungu na kumwabudu kusiki kweli. Isa 43:24 inasema kuwa dhambi za Waisraeli zilimchosha Mungu. Isa 1:14 inasema sikukuu zao zilimchosha Mungu walipokuwa waovu. Kutokuamini kwa Ahazi kulimchosha Mungu kwenye Isa 7:14. Mal2:17 inasema kuwa maneno yao yamemchosha Mungu waliposema wanaotenda maovu ni wazuri, na yuko wapi Mungu wa haki. Tazama Bible Difficulties and Seeming Contradictions, uk.212-213 kwa maelezo zaidi.

 

S: Kwenye Kut 31:30, je si kosa kubwa sana kumuua mtu kwa lengo la kutengeneza kiambato cha aina fulani cha manukato?

J: Ndiyo, ni yenye kutiisha. Ingawa si dhuruma endapo kila mtu atazifahamu kanuni. Hakuna ushahidi kuwa kuna mtu yeyote aliyewahi kuivunja amri hii au aliadhibiwa kwa ajili yake.

 

S: Kwenye Kut 32:2-5, je kuunga mkono ibada ya sanamu?

J: Haruni alifanya dhambi mbaya sana. Hakuna kitu cha kujitetea kwa jambo alilolifanya, lakini yafuatayo ni maelezo yanayoweza kutolewa kuhusu vitendo vyake. Musa alipokawia kurudi, watu wengi walianza kutia shaka endapo atarudi. Shinikizo la watu wengi hawana kiongozi na waliokuwa wamefadhahishwa na shida waliomwomba Haruni awatengenezee sanamu, Haruni alisalimu amri na alithamini kuwaongoza watu kama kuhani ili kurejesha upya muundo na utulivu kuliko kumsubiri Bwana kwa muda usiofahamika.

 

S: Kwenye Kut 32:1-10, kwa nini Mungu aliwaua Waisraeli walioiabudu ndama ya dhahabu na si Haruni aliyeitengeneza?

J: Mungu angekuwa mwenye haki endapo angewaua watu wote. Hata hivyo, Mungu anayo haki ya kuchelewesha haki. Pia anayo haki ya kutoa rehema kwa kadri anavyopenda kama Rum 9:15 inavyoonyesha.

Mazingira: Watu walipendekeza ndama wa dhahabu na walitoa vifaa vya kumtengenezea. Maandiko hayasemi endapo haruni aliitikia ombi hilo kwa furaha au alijihisi kuwa amelazimishwa na watu waliokuwa naye. Ndama wa dhahabu alikuwa anatumia sanamu kumwabudu Mungu kwenye Kut 32:5, si Mungu mwingine. Ingawa mazingira yanaweza kutusaidia kufahamu kwa nini Haruni alifanya jambo hili, mazingira hayawezi kumwepushia Haruni lawama.

Mungu ni mwenye rehema kwa baadhi ya watu na anaweza kuchelewesha haki: Mungu alikuwa na hasira sana kwenye aya ya 10 na alifikiria kuwaangamiza wote kabisa. Mungu angekuwa na haki kumwangamiza Haruni na watu wengine wote. Mungu alikuwa na rehema kwa kutokuwaangamiza Waisraeli wote siyo Haruni tu, na mwenye rehema kwa kutokuwaua Waisraeli wote pia.

 

S: Kwenye Kut 32:14 je Mungu hubadilisha mawazo yake, tofauti na Hes 23:19 na 1 Sam 15:29?

J: Tazama jibu la Kut 33:3, When Critics Ask p.85, and Hard Sayings of the Bible, uk.209-210 kwa habari zaidi.

 

S: Kwenye Kut 32:30, Musa aliwezaje kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi za watu?

J: Watu wanaweza kujaribu kufanya mambo yasiyowezekana, lakini hata Musa hakuweza kuchukua nafasi ya mtu mwingine yeyote yule, kama Yer 15:1 inavyoonyehsa. Musa alimwomba Mungu awasamehe watu dhambi yao kuu, la kama si hivyo, amfute katika kitabu chake. Maneno haya yanafanana na hisia za Paulo kwenye Rum 9:1-4.

 

S: Je Kut 32:30-32 inaonyehsa kuwa Musa angeweza kuchukua nafasi ya watu kama na imani ya Kikatoliki ya "Msamaha wa Pagatori"?

J: Hapana. Kama kuna kitu chochote, kinamaanisha kinyume cha hivi kwa sababu mbili.

1. Kwenye Kut 32:33-34, Mungu alisema kuwa ombi la Musa halikukubaliwa. Kama wazo la ziada, Paulo alikuwa na fikra hizohizo za upendo wa kujitoa kafara kwa ajili ya Wayahudi kwenye Rum 9:3, lakini nazo hazikuwasaidia Wayahudi.

2. Musa hakuwa amejitoa kuumia kwa ajili ya watu aliokuwa anawaombea. Ombi la Musa la kufutwa kabisa kwenye kitabu lilimaanisha kuwa aende jehanamu. Wakatoliki, Waorthodox, na Waprotestanti wanakubaliana kuwa hakuna Mkristo anayekwenda jehanamu kwa ajili ya Wakristo wengine.

Kama wazo la ziada, katika mapokeo ya kanisa, dhana ya "msamaha wa adhabu ya Pagatori" haipo kabisa kwenye kazi za waandishi wa Kikristo walioandika kabla ya Baraza la Nikea.

Tazama When Cultists Ask, uk.37-38 kwa habari zaidi.

 

S: Kwenye Kut 32:12, kwa nini Musa alimwomba Mungu "Geuka katika hasira yako kali"?

J: Neno "ovu" hapa linaweza pia kumaanisha maafa. Musa alimwomba Mungu kugeuka toka kuleta maafa aliyotishia kwa sababu Kumb 9:8 inasema ghadhabu ya Mungu ilipanda sana kiasi cha kuangamiza watu.

 

S: Kwenye Kut 33:3 na Yoshua 1, je Mungu alikwenda na Waisraeli kwenye nchi ya ahadi au la?

J: Mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa mara nyingi huja kwa wakati unaofaa na unakuwa ma masharti yake, na mara nyingine huelezwa kwa kutumia msemo wa anthropomofisimu.

Kwa wakati unaofaa: Mungu alikiambia kizazi chenye kuasi kuwa hatakwenda nao. Wote walikufa, na Mungu alikwenda na kizazi kilichofuatia.

Yenye masharti: Vingi vya vitisho au ahadi za Mungu vilikuwa na masharti ambayo yalidokezwa ndani yake. Tazama Yona 3 na Mwa 20:3 kupata baadhi ya mifano iliyodokezwa ya vitisho vyenye masharti.

Anthropomofisimu: Mungu ambaye hafungwi na muda, alikwishajua jambo ambalo wangefanya. Hata hivyo, mara nyingine huwa vigumu kwa watu kuliona na wakati huohuo kuona kuwa watu bado wanayo nafasi ya kweli ya kuchagua. Ni kweli kuwa kama Mungu angewaambia jambo la kufanya kwa uhaakika na jambo ambalo angelifanya kwa uhakika, kitu hicho kingewapunguzia uwezo wao wa kuchagua.

Binadamu hawana haja ya kuafiki au hata kuelewa dhana ya kuwa Mungu hafungwi na muda. Hawahitaji kufikiria hali ya kutofungwa na muda kabla hata Mungu hajawasiliana nao kwa njia inayoeleweka sana. Mungu huwasiliana na watu wake kwa njia ambayo inaeleweka na watu wote. Tazama Now That's A Good Question, uk.202-205 kwa maelezo zaidi kuhusu anthropomofisimu.

 

S: Kwenye Kut 33:5-6, kwa nini Waisraeli walitakiwa kutoa mapambo yao ili ajue kitu cha kufanya nayo?

J: Walitakiwa kutoa mapambo waliyokuwa nayo wakati wanafanya dhambi, kama ishara ya kuomboleza, na (inategemewa) toba. Kuna kanuni kubwa iliyogusiwa hapa. Mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa yanaweza kubadilika wakati mioyo yetu inabadilika. Waisraeli hawa walikuwa na uhuru wa kumtii na kuomboleza kwa ajili ya dhambi zao au la.

Tazama maelezo kuhusu Mwa 20:3-6; Kumb 20:17; Yer 15:6; Yoh 3-4; Yoh 3:10 na Yoh 4:1-2 kwa habari zaidi.

 

S: Kwenye Kut 33:19-20, Musa aliwezaje kuona nyuma yake kwani Mungu ni roho?

J: Ni vigumu kuongelea sehemu mbalimbali za roho bila kutumia misemo ya kianthropomofisimu. "Nyuma" haimaanishi "sehemu ya mgongo" bali "nyuma' inaweza kumaanisha "nyuma" tofauti na "mbele."

Jambo hili linaongelea kuonekana kwa baadhi ya sifa za Mungu. Si utukufu wote wa Mungu, kwani Mungu hakumtimizia Musa ombi lake la kuuona utukufe wa Mungu (huenda ilikuwa ni kwa usalama wa Musa mwenyewe).

 

S: Kwenye Kut 33:11, je Musa angeweza kuongea na uso kwa uso?

J: Kama Norman Geisler na Thomas Howe walivyoandika, kipofu hawezi kuongea uso kwa uso na mtu bila ya wawili hao kuangaliana nyuso zao. Msemo huu unaonyesha kuwa Musa na Mungu waliongea kwa ukaribu sana, lakini hausemi kuwa Musa aliuona uso wa Mungu kama Kut 33:20 inavyoonyesha.

 

S: Kwenye Kut 34:20; 13:2 na Hes 18:15-16, je watu wanatakiwa kuwaua wanyama wasiokuwa safi au wawakomboe kwa fedha?

J: Kut 34:20 inasema mmiliki anatakiwa ama kumuua mzaliwa wa kwanza wa mnyama au kumkomboa kwa fedha, isipokuwa tu anaweza kumkomboa punda kwa mwana kondoo. Hakuna tofauti nyingine iliyofanywa kati ya wanyama sasi na wasio safi. Baadaye kwenye Hes 18:15-16 sheria ilipunguzwa upana wake ili kuruhusu kukomboa kwa fedha tu wazaliwa wa kwanza wa wanyama wasio safi.

Kuna watu wanaoweza kuwa na shida na kubadilika kokote kwa sheria ya Mungu, kwa sababu sura tatu tofauti za sheria: kanuni za mema na mabaya, mahusiano ya kijamii zisizo za jinai na na sheria za sherehe/ibada (ceremonial law). Sheria za sherehe/ibada zilibadilika kwa njia nyingine pia, kwa kadri ambavyo mazingira yalivyobadilika. Kwa mfano, kafara hazikuwepo hekaluni kabla ya hekalu kujengwa.

 

S: Kwenye Kut 34:23, kwa nini wanaume wote walitaiwa kuhudhuria na si wanawake na watoto? (Kuna Muislamu aliyeuliza hivi).

J: Tunaweza kuona jibu la swali hili kwa kusoma Kut 34:23 na 24 kwa uangalifu. Inasema, "Mara tatu kila mwaka watu waume wako wote watahudhuria mbele za Bwana na MUNGU, Mungu wa Israeli. Kwa kuwa mimi nitazitupa nje taifa za watu mbele yako, na kuipanua mipaka yako; wala hapana mtu yeyote atakayeitamani nchi yako, hapo utakapokwea kwenda kuhudhuria mbele za BWANA Mungu wako mara tatu kila mwaka." Wanawake hawakupigana vitani, ni wanaume tu. Hakuna mwanaume aliyeruhusiwa "kujificha" kwa kutokuhudhuria.

 

S: Kwenye Kutoka 35-40, samani zilizokuwa ndani ya hema ya kukutania ziliashiria nini?

J: Kuna watu wanaona mambo yafuatayo:

Madhabahu ya shaba iliashiria kuwa hata mlango ulihitaji kafra

Birika la shaba lilionyesha kuwa watu waliomo ndani yake walihitaji utakaso

Mkate wa wonyesho ulionyesha kuwa Kristo ni mkate wetu, anatupa vitu vyote tunavyohitaji ili tuweze kuishi

Taa ya dhahabu iliwakilisha sifa na maombi

Sanduku liliwakilisha uwepo wa Mungu

Utaji/pazia ulionyesha kuwa njia ya kuelekea kwenye uwepo wa Mungu haikuwa wazi kwa kila mtu (isipokuwa kuhani mara moja kwa mwaka). (Pazia lilipasuliwa vipande viwili wakati Yesu alipokuwa anakufa msalabani).

 

S: Kwenye Kut 36:8-14, niliambiwa kuwa vipimo ambavyo Musa alipokea toka kwa Mungu kuijenga hema ya kukutania vilikuwa karibu sawa kabisa na vipimo ambavyo watu wengine wa kale (si Waebrania) walivitumia kujenga majengo yao ya ibada. Je jambo hili linaathiri urahisi wa kuamini ukweli wa vipimo vya Mungu vya hema la kukutania?

J: Kwanza, hebu tuchukulie kuwa mawazo hayo ni sahihi. (Nitayatathmini mawazo hayo baadaye). Kama ilikuwa ni vipimo sawa na vipimo vya watu wengine wa kale vilivyotumika kujengea mahekalu yao, jambo hilo halitathiri usahihi wa Biblia. Endapo kulikuwa na kitu maalumu kuhusu vipimo hivi, shetani angetumia habari hiyo kutengeneza hema la bandia.

Kwa upande mwingine, nina mashaka sana na madai kuwa vipimo hivi ndivyo vilivyotumiwa na watu wa kale kujengea mahekalu yao, kwa sababu zifuatazo.

a) Majengo tofauti ya ibada yalikuwa na vipimo tofauti miongoni mwao. Mfano rahisi ni huu, fikiria kuwa kuna mahekalu 10 ya kale yenye vipimo vya 100, 105, 110, 120, 125, 130, 135, 140, 145, 150, na hema la kukutania lilikuwa na vipimo kati ya 100 na 150. Bila kujali vipimo vya hema hilo la kukutania, inawezekana kudaiwa kuwa lilifanana na moja ya mahekalu 8 - lakini jambo hili halithibitishi kitu chochote kile.

b) Mahekalu ya kale hayakuwa na patakatifu pa patakatifu, nay ale tunayoyajua yalikuwa hayatembesheki, siyo mahema.

c) Mwisho, kumbuka kuwa hema la kukutania lilijengwa karibu mwaka 1400 KK, lilikuwa la zamani kuliko mahekalu yote ya Kirumi na mahekalu yote ya Kigiriki, isipokuwa Myceneans. Hivyo endapo vipimo vilikuwa sawa na vile vya hekalu lililokuja kujengwa baadaye, basi huenda hapakuwa na kufuatisha, au hekalu lilijongwa baadaye lililifuatisha hekalu lililojengwa kabla, siyo kinyume na hapo. Kwa ujumla, si busara kuyakubali mambo ya jinsi hii kuwa ya kweli, isipokuwa pale tu panapotolewa mifano.

 

S: Kwenye Kut 37:14, je kinara cha taa chenye sehemu saba kinaonyesha kuwa Kitabu cha Kutokwa kiliandikwa baadaye, kwani vinara saba vya taa [inadaiwa] havikuwepo hadi mwaka 600 KK?

J: Kuna watu waliowahi kufikiri hivi, lakini Can Archaeology Prove the Old Testament?, uk.31-32 inaonyesha kuwa wataalamu wa elimukale wamevumbua vinara saba vya taa kule Tell Beit Mirsim na makaburi kadhaa huko Dothan yaliyojengwa wakati wa Musa yenye kuonyesha vinara saba vya taa. Wycliffe Bible Dictionary, uk.1006 inasema kuwa taa zenye midomo saba zimeonekana kwenye makaburi na mahekalu ya Wakanaani "Hivyo, dhana ya taa zenye sehemu saba zilizotumiwa kwa ajili ya ibada kenye hema la kukutania alilolijenga Musa halipingani na muda, kama wanazuoni wamakinifu (walio tayari kutafsiri maandishi kinyume cha mapokeo yao na jinsi wanavyopendelea ili kuacha ushahidi uongoze fikra zao hata kufikia uamuzi) wa Agano la Kale walivyokuwa wakidai."

 

S: Je Kut 38:8 ni ushahidi wa Kitabu cha Kutoka kuandikwa baadaye, kama inavyodaiwa kuwa hapakuwa na vioo vya shaba (nyeusi) wakati ule?

J: Hapana, kwa sababu hawakuwa na vioo vya shaba (nyeusi). Shaba nyeusi ni mchanganyiko wa shaba na asilimia 2-18 ya bati. Vyombo vya shaba nyeusi vilivyotengenezwa karibu mwaka 2500 KK vimepatikana huko Uri.

Kwenye uk.1139 inasema kuwa vioo vya shaba (nyeusi) vilikuwa vichache, isipokuwa Misri. Hata hivyo vilikuwa vya thamani sana, kwani vioo vya shaba havienea na kutumika na watu wa kawaida hadi nyakati za Wagiriki. Pia inasema kuwa katika wakati wa Yoshua, barua za Amarna zinamtaja mtwana akiwasilisha vioo vya shaba 32 vilivyong'arishwa kwa Farao. Mfale wa Wahiti alimpa kioo kimoja cha fedha.

Kama maelezo ya ziada, maandishi ya zamani zaidi ya Agano la Kale yanayofahamika yaliyopo leo hii ni 4Q17 ya hati za kale kutoka Bahari ya Chumvi (Dead Sea Scrolls). Maandishi haya yaliandikwa mwaka 250 BK na yana maneno kuanzia Kutoka 38 had Walawi 2. The Dead Sea Scrolls Translated, uk.474 inasema maneno haya yanafanana kabisa na maandishi ya Kimasoretiki (Agano la Kale kwa lugha ya Kiebrania).

 

S: Kwenye Kutoka 40, je waliwezaje kujenga hema la kukutania wakati hema lilikuwa tayari lipo kwenye Kut 33:7-8?

J: Kwanza kabisa, mambo mawili ambayo huenda hayahusiki kisha jibu la swali.

1. Si lazima kuwa Kut 33:7-8 na Kutoka 40 viwe viliandikwa kwa kufuata mfululizo wa matukio, ingawa kuna uwezekano kuwa ndivyo zilivyokuwa hapa.

2. Baada ya kutumiwa kwa muda mrefu juani, hema linaweza kuwa lilichakaa.

Jibu: Kut 33:7-8 inasema Musa alichukua hema lililokuwepo na kuliita hema la kukutania. Baada ya Mungu kuwapaka mafuta Bezaleli na Aholiabu kwenye Kut 31:2-7; 35:30; 36:1, walitengeneza vifaa vitakatifu likiwemo hema la kukutania kwa kufuata maelekezo ya Mungu.

 

S: Kwenye Kutoka, tunajuaje kuwa maandiko tulicyonayo ndiyo yaliyokuwepo mwanzoni kwa mujibu mwandishi wa Kiyahudi aitwaye Philo?

J: Kama Wakristo tunaamini kuwa Agano la Kale ambalo Kristo alilithibitisha ndilo Agano la Kale tulilo nalo. Kwa ajili hiyo, kwa Waislamu Kurani yao inasema kuwa Yesu alipewa Toraati kwenye Sura 5:46. Tunayo maandishi ya awali tokea wakati wa Yesu, ambayo swali linalofuata linayaongelea. Hata hivyo, una ushahidi mwingine zaidi. Philo wa Alexandria alikuwa ni mwanazuoni wa Kiyahudi aliyeishi kutoka mwaka 15/20 KK hadi mwaka 50 BK. Aliandika kwa Kigiriki, lakini inashangaza kuwa nukuu zake za Kigiriki za Agano la Kale zinakubaliana zaidi na maandishi ya Kiebrania ya Kimasoreti badala ya Septuajinti ya Kigiriki. Alielezea kwa undani sana maana ya aya mbalimbali. Zifuatazo ni aya za Kitabu cha Kutoka alizoziongelea.

1:8, 9, 11, 15, 18, 20, 21

2:1, 3, 6, 12, 15-16, 18, 21, 23, 25

3:1-2, 4-6, 9, 14-15, 17

4:3, 10, 12, 14, 22

5:2

6:3, 12, 16, 23, 26, 29

7:1, 12, 15, 17, 23

8:1, 9, 19, 26, 29

10:20-23

11:7

12:2-4, 8, 11-12, 16, 23, 34, 38

13:2, 11-13, 15, 19

14:4, 7, 13-14, 19, 27, 30

15:1, 4, 9, 17, 20, 23, 25, 27

16:4, 6, 13, 15, 18, 36

17:6, 11-12

18:4, 7, 11, 14, 16, 25

19:6, 17-20

20:2, 5, 9, 12-13, 16, 18-22

21:5-6, 10, 12-16, 22, 26, 28, 31, 33

22:1, 6-7, 26

23:1-5, 8, 10, 13, 18-20, 28

24:1, 6, 10-11, 18

25:1, 22, 30, 31, 33, 40

26:1

27:9

28:17, 30, 34, 36

30:8, 13, 15, 34

31:1-2, 39

32:1, 7, 16-17, 20, 26, 27, 32

33:5, 7, 12-13, 17-18, 23

34:12, 28

35:22, 30

38:8

39:3, 26

 

S: Kwenye Kutoka, je ni maandishi gani ya zamani zaidi ambayo bado yapo leo?

J: Hati za Kale toka Bahari ya Chumvi: (mwaka 250 KK na kuendelea) nakala 17 tofauti (The Dead Sea Scrolls Today, uk.30 na The Dead Sea Scrolls Translated: The Qumran Texts in English 2nd ed.), kutoka kwenye nakala za asili zisizopungua 23 (The Dead Sea Scrolls in English 4th ed.). Wycliffe Bible Dictionary, uk.436-438 insema kuna nakala 15. Hati ya maandiko ya kazi ya kale ambayo nakala zake ya awali haipo kutoka kwenye pango la 4 ni ya kundi la Samaria. Kwa mujibu wa The Dead Sea Scrolls Translated: The Qumran Texts in English 2nd ed., uk.474, kipande 4Q17 kwenye pango la 4 (chenye Kutoka 38 hadi Walawi 2) ni moja ya hati zenye maandiko ya kazi za kale iliyo ya zamani zaidi, ilinakiriwa karibu mwaka 250 KK inafanana sana na maandishi ya Kimasoretiki. Hati hizi zinaitwa

1Q2 Kutoka

2Q2 Kutoka

2Q3 (=2Q Kutokab) Kiebrania cha zamani cha Kut 19:9 ikifuatiwa mara na mstari ukio wazi unaofuatiwa mara na Kut 34:10

2Q4

4Q1 Mwanzo na Kutoka

4Q11 Kiebrania cha zamani cha Mwa 50:26 na Kutoka 1-36

4Q13 ina vipande 6 vya Kutoka 1-5

4Q14 ina vipande 36 vya Kutoka 7-18

4Q15 Kut 13:15-17 ikifuatiwa mara na Kut 15:1

4Q16 Kut 13:3-5

4Q17 Kutoka 38 – Walawi 2 (mwaka 250 KK)

4Q18 Kut 14:21-27

4Q19 Kut 6:3-6

4Q20 Kutoka 7-8

4Q21 Kut 36:9-10

4Q22 Kutoka maandiko ya Kiebrania ya kale ya aina ya Samaria. Muda wake wa kuandikwa ni mwaka 100-25 KK. The accelerated mass. Spec. yenye kutambua umri ya kitu cha kale kwenye maabara ya Tucson imeiona kuwa iliandikwa mwaka 116 KK – 48 BK.

4Q37 (ikiwemo Kumb 11:21 ikifuatiwa na Kut 12:43-13:5)

7Q1 (= 7QLXXExod) ni nakala ya Septujuanti ya Kigiriki ya Kut 28:4-6 (mwaka 100 KK).

Hirizi na mezuzot (zenye kuvaliwa kwenye kipaji cha uso na mikononi kwa mfuatano) vimeonekana vya Kutoka na Kumbukumbu la Torati miongoni mwa hati za kale kutoka Bahari ya Chumvi kwa mujibu wa The Dead Sea Scrolls Today, uk.33.

8Q3 ni hirizi (kisanduku kidogo cha ngozi chenye maandishi ya Kiebrania kwnye kipande cha ngozi kinachovaliwa na wanaume wa Kiyahudi wakati wa sala ya asubuhi kama kitu cha kuwakumbusha kutunza sheria ya Mungu) yenye Kut 13:1-10; 13:11-16; 12:43-51; 20:11; Kumb 6:5-9; 11:13; 6:1-3; 10:20-22; 10:12-19; 5:1-14; 10:13(?); 11:2; 10:21-22; 11:1,6-12.

8Q4 ni Mezuza (Kipande cha ngozi kilichoandikwa maandishi ya kidini na kuwekwa kwenye kimfuko katika nguzo ya mlango wa nyumba za Wayahudi kama ishara ya imani) ya Kumb 10:12-11:21.

Pentatiuki sanjari ilipatikana miongoni mwa hati za kale kutoka Bahari ya Chumvi. Kama ambavyo baadhi ya watu walivyoitengeneza masimulizi ya injili kwa kuweka vifungu mbalimbali vya Injili kimoja baada ya kingine, jamii ya Qumran ilifanya hivyo hivyo na Pentatiuki, ambayo iliitwa hati 4Q158.

Hati za kale kutoka Bahari ya Chumvi zina aya zifuatazo za Kitabu cha Kutoka: 1:1-22; 2:1-18, 22-25; 3:1-4, 8-21; 4:1-9, 26-31; 5:1, 3-17; 6:3-21, 30; 7:1-13, 26-29; 8:1, 5-22; 9:5b-35; 10:1-28; 11:3-10; 12:1-2, 6-8, 12-22, 31-51; 13:1-7, 12-13, 15-16, 18-22; 14:1-1, 25-27; 15:1, 9-21, 23-27; 16:1-8, 13-14, 1-20, 23-36; 17:1-16; 18:1-27; 19:1, 7-17, 23-25; 20:1-2, 18-19a; 21:1, 4-6, 13-14, 18-20?, 22-32, 37; 22:1-4, 6-7, 11-13, 15-30; 23:5-16, 29-31; 24:1-4, 6-11; 25:7-29, 31-34; 26:8-15, 21-37; 27:1-3, 4?, 6-14, 18-19; 28:3-12, 22-24, 26-28, 30-43; 29:1-5, 20, 22-25, 31-41; 30:10, 12-18, 21?, 23-25, 29-31, 34-38; 31:1-8, 13-17; 32:2-19, 25-30, 32-34; 33:12-23; 34:1-3, 10-13, 15-18, 20-24, 27-28; 34:10; 35:1; 36:9-10, 21-24, 34-36; 27:9-16; 38:18-22; 39:3-24; 40:8-27; 40:15?. Kut 34:23-24, 27-28 zimekatika vipande vidogo vidogo sana.

Mafunjo ya Nashi, yaliyoandikwa mwaka 150 KK, yana amri kumi zikiwa pamoja vifungu vya Kut 20:2-17 na Kumb 5:6-6:4 na kuendelea. Mafunjo haya yalikuwa miongoni mwa maandishi ya zamani zaidi Biblia yaliyokuwa yanafahamika mapaka hati za kale kutoka Bahari ya Chumvi zilipogunduliwa.

Mafunji ya Oxyrhynchus (mwaka 1074 BK) ya Kitabu cha Kutoka iliyoandikwa karibu karne ya pili

Vaticanus (mwaka 325-350 BK) ina kitabu chote cha Kutoka.

Hatuna kurasa zozote za Sinaiticus (mwaka 340-350 BK) yenye Kitabu cha Kutoka.

Alexandrinus (karibu mwaka 450 BK) ina kitabu chote cha Kutoka

Septuajinti ni tafsiri ya Kigiriki ya Agano la Kale na Apokrifa (vitabu vya kubuniwa vya dini ya Kiyahudi).

Wasamaria walitengeneza toleo lao wenyewe la Pentatiuki kwenye karne ya pili KK, ingawa nakala za kale zaidi zilizopo ziliandikwa katika Enzi za Kati. The Encyclopedia of the Dead Sea Scrolls juzuu ya 1, uk.277 inasema "Pentatiuki ya Wasamaria ina kawaida ya kuongeza maandiko kwa kuweka habari zinazofanana kutoka sehemu nyingine za Pentatiuki."

Tafsiri ya Kishamu ya Septuajinti ilitengenezwa na Askofu Paulo wa Tella (mwaka 616-617 BK), ambayo bado tunayo hata leo.

Waandishi toka kanisa la awali walikitambua Kitabu cha Kutoka kuwa sehemu ya Biblia. Mfano mmojawapo ni Cyprian, aliyekuwa askofu wa Carthage tokea mwaka 248 K hadi kifo chake cha ufiadini mwaka 258 BK. Alinukuu Kitabu cha Kutoka akisema kuwa maneno hayo yanatoka kwenye Kutoka katika Treatise 12 The Third Book 11, 13, 113 pamoja na sehemu nyingine.

 

S: Ni waandishi gani wa kale walionukuu Kitabu cha Kutoka?

Philo Myahudi (mwaka 15/20 KK hadi 50 BK) alinukuu kwa kiasi kikubwa kwenye Kitabu cha Kutoka kwenye On the Confusion of Tongues, Who is the Heir of Divine Things, Preliminary Studies, na kazi nyingine.

Waandishi Wakristo wa zamani za miaka iliyotangulia baraza la kanisa la Nikea walikitambua Kitabu cha Kutoka kama sehemu ya Bilia. Clement ya Kwanza (mwaka 96-98 BK), Didache, Barnabas, Justin Martyr, Melito wa Sardis, Theophilus wa Antioch, Irenaeus, Tertullian, Clement wa Alexandrian, Hippolytus, Origen, Novatian, Anonymous Against Novatian, Anonymous Treatise on Rebaptism, Cyprian, Dionysius wa Alexandria, Anatolius wa Alexandria, Archelaeus, Diodorus, Arnobius, Victorinus wa Petau, na Methodius.

 

S: Kwenye Kitabu cha Kutoka, "Pentatiuki sanjari", (Hati ya kale toka Bahari ya Chumvi 4Q158) inasema nini?

J: Hii hapa ni sehemu yake ndogo. Maandiko inayoyaongelea yameandikwa kwa mlazo. Tafsiri imechukuliwa kutoka The Dead Sea Scrolls Study Edition, juzuu ya 2, uk.307.

"Kut 20:12-17 [baba] yako na mama yako [siku zako katika nchi ambayo BWANA Mungu wako amekupa zitaongezwa. Usiue. Usizini. Usinyang'anye. Usishuhudie uongo [dhidi] ya [jira]ni yako. Usitamani mke wa jira[ni yako, wala nyumba yake, wala mtumwa wake, wala kijakazi wake, wala punda wake, wala kitu chochote alicho nacho jirani yako.] Na BWANA alimwambia Musa: Kumb 5:30-31, Nenda ukawaambie: Rudini katika [mahema yenu! Lakini wewe, baki nami, kwani nitakuelezea amri zote, sheria] na hukumu utakazo wafundisha, ili kwamba wazifanye kwenye nchi ambayo [nitakayowapa kuimiliki . . . ] Na watu walirudi, kila mtu kwenye hema lake. Lakini Musa alibaki kwenye uwepo [wa BWANA . . .]."

 

S: Kwenye Kitabu cha Kutoka, kuna tofauti gani za tafsiri kati ya Kiebrania na Kigiriki?

J: Zifuatazo ni baadhi yake kwenye aya 1,213 za Kitabu cha Kutoka. Ili kupata sampuli ya tofauti za matoleo ya Kimasoretiki (Kiebrania) na Septuajinti (Kigiriki), ifuatayo inaangalia zaidi sura ya 30.

Kut 1:5 "Na nafsi zile zote zilizotoka viunoni mwa Yakobo zilikuwa ni nafsi sabini; na huyo Yusufu alikuwako huko ndani ya Misri tangu hapo" (Kimasoretiki) na "Lakini Yusufu alikuwa Misri. Na nafsi zote za Yakobo zilikuwa sabini na tano" (Septuajinti). Hati za kale toka Bahari ya Chumvi pia zinasema wazao 75. Kwenye Mdo 7:14, Stefano alisema wazao 75.

Kut 1:22 "atakayezaliwa" na "atakayezaliwa na Mwebrania" (Pentatiuki la Kisamaria, Septuajinti, na Targumu).

Kut 2:25 "[Mungu] akawaangalia" na "[Mungu] alijitambulisha kwao" (The Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 2 inasema Septuajinti imekosea hapa).

Kut 3:19 "hatawapa ruhusa mwende zenu, la, hata kwa mkono wa nguvu" na "nenda, si kwa mkono wenye nguvu" (Septuajinti, Vulgate –toleo kubwa la Biblia la Kilatini lililotayarishwa na Jerome mwishoni mwa karne ya 4 BK)

Kut 4:22 "mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu" na "watu wangu mimi" (Pentatiuki ya Kisamaria) (The Anchor Bible Dictionary, juzuu ya 5).

Kut 8:22 "nitatenga" vs. "nitatofautisha kwa namna ya ajabu" (The Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 2, uk.356 inasema watafsiri wa Septuajinti walilielewa vibaya neno la Kiebrani hapa)

Kut 8:32 "hao watu" na "watu wako" (Septuajinti)

Kut 8:23 "nitatia mpaka" na "leta ukombozi/wokuvu" kwenye Septuajinti na Vulgate.

Kut 9:32 Neno la Kiebrania kwa nafaka ya pili, huenda ikawa ni "emmer (aina ya ngano ya zamani huko Asia)" na "shayiri" kwenye Septuajinti, na "mmea wa msimu" kwenye toleo la Kikhufti (Misri ya kale). (The Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 2 inasema nafaka ya ‘emmer' inapatikana kwenye makaburi ya Kimisri, lakini aina ya ngano ya zamani (spelt) haipatikani).

Kut 12:22 "bakuli" na "kizingiti cha mlango"

Kut 12:40 "Wana wa Israeli kukaa kwao, maana muda waliokaa Misri" (Kimasoretiki) na "Wana wa Israeli walikaa Misri na Kanaani" (kwenye Septuajinti) na "wana wa Israeli na baba zao waliishi Misri na Kanaani" (Pentatiuki ya Kisamaria). Josephus akiandika karibu mwaka 93-94 BK kwenye Antiquities of the Jews 2.15.2 pia anasema walikuwa Misri miaka 215 kitu ambacho kinafanana na Pentatiuki ya Kisamaria. Josephus alisema ilikuwa miaka 430 baada ya Abrahamu kwenda Kanaani.

Kut 14:25 "Akayaondoa" na "akayazuia" (Pentatiuki ya Kisamaria, Septuajinti, toleo la Kishamu)

Kut 15:8 "Upepo wa mianzi ya pua yako" na "pumzi toka kwako" (Pentatiuki ya Kisamaria)

Kut 18:5 "Kula mkate" (Kimasoretiki, Septuajinti) na "toa mkata" (Kishamu, Targumu, Vulgate)

Kut 18:12 "Akamletea" (Kimasoretiki, Septuajinti) na "alitoa" (Kishamu, Targumu, na Vulgate) The Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 2, uk.413-414 inasema kuwa ‘akamletea' ndilo neno sahihi, na ‘alitoa' ilikuwa ni tafsiri tu.

Kut 19:18 "Mlima wa Sayuni wote" na "watu wote" kwenye hati zenye maandiko ya kale za Kiebrania na Septuajinti.

Kut 20:17 inafuatiwa mara moja na Kumb 11:29-30 na 27:2b-3a, 407, ikitueleza kuwa Waisraeli walijenga hekal kwenye Mlima Gerizim kwenye Septuajinti ya Kisamaria (The Anchor Bible Dictionary, juzuu ya 5, uk.937).

Kut 20:18 Kwenye Mafunjo ya Nashi amri ya sita na saba zimegeuzwa mfuatano wake kwa mujibu wa The Journey from Texts to Translations, uk.188.

Kut 20:24 "kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu" na "kila mahali nitakapofanya jina langu" (Pentatiuki ya Kisamaria) kwenye The Anchor Bible Dictionary, juzuu ya 5.

Kut 22:8 "BWANA" kuwa "Mungu" (Pentatiuki ya Kisamaria) kwenye The Anchor Bible Dictionary, juzuu ya 5.

Kut 23:20 "Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani, na kukupeleka mpaka mahali pale nilipopatengeneza" na "Na tazama, namtuma malaika wangu mbele ya uso wako, ili akupeleke kwenye nchi niliyoitengeneza kwa ajili yako."

Kut 23:21 "Jitunzeni mbele yake, mwisikilize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake" na "Jihadhari na msikilize, na msiache kumtii; kwa kuwa hatawaruhu kwenda, kwa maana jina langu lipo juu yake."

Kut 23:25 "Naye [Mungu] atakibarikia chakula chako" na "Nitakubariki (Septuajinti, Vulgate)

Kut 24:10 "Wakamwona Mungu wa Israeli . . . kwa usafi wake" na "Wakapaona mahali ambapo Mungu wa Israeli alisimama . . . usafi."

Kut 24:11 "Naye hakuweka mkono wake juu ya hao wakuu wa wana wa Israeli; nao wakamwona Mungu" na "hapakuwa na hata mmoja wao aliyekosekana, na walitokea mahali pa Mungu."

Kut 28:23-28 ipo kwenye maandishi ya Kimasoretiki ya Kiebrania na Septuajinti ya Comlutensia (Toleo la Biblia nzima la Complutensia, lenye lugha nyingi lililofadhiliwa na Kadinali Francisco Jimenez de Cisneros [1436-1517] na kuchapishwa na Chuo Kikuu cha Complutense cha Madrid Hispania. Complutensia ina toleo la kwanza kuchapishwa la Agano Jipya ya Kigiriki, Septuajinti yote na Targumu Onkelosi). Haipo kwenye matoleo ya Vatican na Alexandrine ya Septuajinti.

Kut 29:9 "Uwakaze mshipi, Haruni na wanawe" na "kwao" kwenye Septuajinti.

Kut 30:1 "Madhabahu ya kufukizia uvumba" na "madhabahu ya uvumba" kwenye Septuajinti.

Kut 30:1 "Mti wa mshita" na "mtu usioharibika" kwenye Septuajinti.

Kut 30:12 "Uharibifu" na "pigo" kwenye Septuajinti.

Kut 30:21 "Wataosha mikono na miguu yao ili kwamba wasife" na "miguu kwa maji, wakati wowote wanapokwenda kwenye hema la kukutania la uashahidi; watajiosha kwa maji ili kwamba wasife." (Huenda mtafsiri wa Septuajinti alirudia sehemu ya mstari huu kwa makosa).

Kut 30:27, 28 Septuajinti imeongeza "na samani zake zote" mara nne.

Kut 30:35 "yamekolea, safi, matakatifu" na "kazi safi na takatifu" kwenye Septuajinti.

Kut 31:4-5 "kuwa fundi wa . . . shaba na kukata vito kwa kutiwa mahali" na "shaba nyeupe na bluu, na zambarau na nyekundu iliyosokotwa, na kazi za mawe."

Kut 32:29 "Jiwekwni wakfu kwa BWANA leo" na "Leo mmejiweka wakfu wenyewe" (Septuajinti, Vulgate).

Kut 33:16 "Tutengwe na watu wote" na "tutatukuzwa" (The Expositor's Bible Commentary, juzuu ya 2, uk.356 inasema watafsiri wa Septuajinti walilielewa vibaya neno la Kiebrania hapa).

Bibliografia ya swali hili: tafsiri ya Kiebrania inatoka kwenye Literal Translation ya Jay P. Green na maana za Septuajinti zinatoka kwenye tafsiri za Sir Lancelot C.L. Brenton za The Septuagint: Greek and English. The Expositor's Bible Commentary, The Anchor Bible Dictionary, juzuu ya 5, na maelezo chini ya ukurasa kwenye matoleo ya Kiingereza ya Biblia ya NASB, NIV, NKJV, na NRSV yalitumika pia.