Wababi: Waazali na Makundi Mawili ya Wabaha'i

Uazali na Ubaha'i ni dini mbili zinazofanana zenye kujaribu kuunganisha dini kwa kukubali mafundisho ya Krishna, Zoroaster, Musa, Muhammad na Yesu. Dini hizi zina asili ya Uislam, zinadai kumfuata Muhammad, lakini hazijiiti kuwa ni Uislam. Kwanza tutaangalia usuli wa Uisalam, hususan Ushia kisha muhtasari wa Ubabi. Tutawaangalia Wazali kwa ufupi, kisha kumakinia Wabaha'i, ukinzani wao, na kwa nini wanahitaji kuondoka na kuja kumjua Yesu wa kweli.

Usuli wa Uislam

Uislam unamheshimu sana Yesu, lakini mbali ya vitu kadhaa vilivyomo kwenye Kurani, Muhammad alidai kwamba Yesu alisema kuwa Waislam hawawezi kuonyesha neno lolote la Yesu ambalo wanalifuata. Kwa nini mambo yako hivi? Sababu kubwa ni kwamba wanasema kuwa Biblia imepotoshwa na kwamba haiaminiki tena; nabii mpya alitakiwa.
 
Waislam wanakubaliana na Wakristo kuwa Yesu atarudi tena kutoka mbinguni, lakini wanakataa kuwa alikufa msalabani. Badala yake wanasema kuwa Mungu alimweka mtu mwingine kimiujiza, na Yesu alitoweka kisiri.

Usuli wa Uislam wa Kishia

Vita vya kikatili kati ya Khalifa 'Ali na Khalifa Mu'awiyah aliyemfuata, kifo cha kishahidi cha Husain kule Karbala na mwenendo uliojitokeza wa Khalifa Yezid, vinawakumbusha Washia maoni yao ya kuharibiwa kwa miliki ya Khalifa kulikofanywa na Wasuni. Si hivyo tu, bali pia hawaziamini simulizi za Wasuni za Nabii kwenye Hadithi na wengi hata wanaamini kuwa Wasuni waliondoa aya kuu toka kwenye Kurani. Wanamheshimu sana Muhammad, lakini wanaamini kuwa imamu anatakiwa kuonyesha ukweli na kutafsiri kiusahihi.
 
Washia wamegawanyikana kuhusu mrithi wa imamu wa sita. Je awe mdogo wa Musa al-Kazim, kwa kuwa kaka yake mkubwa, Isma'il (bila ubishi) alikuwa mnywaji pombe? Leo hii, wachache miongoni mwao, wanaoitwa 7'ers, (Waisimailia) walimtabua Isma'il, lakini wengi wao, wanaoitwa 12'ers (Waithna'ashariyya), wanamtambua al-Kazim na dhuria wake hadi imamu wa 12.
 
Hata hivyo, imamu wa 12 alitoweka kwa namna ya ajabu, bila ya kuwa na mrithi anayefahamika. Washia Waithna'ashariyya wanaamini kuwa hakufa bali alichukuliwa kimiujiza kwenda mbinguni, na kwamba siku za mwisho atarudi tena, kabla ya Yesu.
 
Neno bab, lenye kumaanisha 'lango', ni dhana ya kidini ya Washia wengi, na wengi wao wamejiita Wababi. "Mimi [Muhammad] ni Jiji la Ufahamu na 'Ali ni Lango (Bab)." Al-Hakim al-Mustadrak. Juzuu ya 3 uk.126-127 imenukuliwa kutoka Introduction to Shi'i Islam uk.14. Mshia mwingine wa zamani zaidi alikuwa Muhammad ibn Nusayr an-Namiri (karibu mwaka 850 BK), aliyejiita Lango (Bab) la kuuelekea Ukweli. Waislam Waalawiti ('Alawite Muslims) wanaamini kuwa kulikuwa na Wababi wengi, wa saba wao akiwa Saliman al-Farisi, mshiriki wa Muhammad.

Wababi, Watangulizi wa Wabaha'i na Wazali

Wababi walitokana na harakati ya Shayki ya Kishia wakati Ali Muhammad wa Shiraz, kusini mwa Irani, dhuria wa Muhammad aliyezaliwa mwaka 1819/1821, alipodai kwa Bab ul-Bab (Lango la Malango), au mtangulizi wa imamu (wa 12) aliyefichwa. Alidai hivi kwenye hija ya Maka mwaka 1844 BK. Babi aliandika kazi nyingi sana; lakini mafunuo yake yalinakiriwa kwenye Kitabu cha bayani (The Book of Bayan 12). Alifundisha upendo wa kindugu, usafi, elimu, uhuru zaidi kwa wanawake, na kuzuia kuombaomba na pombe.
 
Babi alifundisha kuwa mambo mengi yalikuwa ufananisho. Kwa mfano, kufufuka kulimaanisha kuamka kiroho kutoka kwenye ujinga, uzembe na tamaa. Siku ya hukumu ilikuwa ni muda ambao watasikia na kila mmoja atakubali au kukataa udhihirisho mpya. Paradiso ni furaha ya kumjua na kumpenda Mungu kupitia udhihirisho huu. Jehanamu ni kunyimwa ufahamu huo na kukosa fadhila ya milele. Alitangaza waziwazi kuwa maneno haya hayana maana yoyote halisi zaidi ya hii; na kwamba wazo kuu la kufufuka kwa mwili, uwepo wa mbingu na jehanamu, na vitu vingine kama hivyo ni ndoto za kubuniwa. Alifundisha kuwa binadamu anayo maisha baada ya kifo, na kwamba mchakato wa maisha hayo ya baadaye hauna kikomo.

Baadhi ya mafundisho ya kufurahisha zaidi ya Bayan 8:14 ni kwamba Bab anawataka wafuasi wake watongoe aya 700 za Bayan kila baada ya masaa ishirini na nne. (http://bahai-library.com/unpubl.articles/walbridge.panj.html)
Wabaha'i wanashindwa kuifuata amri hii leo.
 
Babi alikamatwa na Wababi wakaanza uasi huko Uajemi. Kwenye vita vya Shaykh Tabarsi, Nayriz, na ngome ya Zanjan wengi wa viongozi wa Wababi na Wababi 2,000 hadi 3,000 waliuawa. Wabaha'i wanadai watu 20,000, wasomi kama vile Dennis MacEoin wanapinga madai haya. Baada ya vita, serikali ya Uturuki ilimuua Babi kwa kikosi cha wapiga risasi tarehe 9 Julai, 1850 BK. Mwaka 1852 mbabi mmoja alitaka kumpiga Washah kwa bunduki, na Washah alilipiza kisasi kwa Wababi.
 
Wabaha'i wanasema kuwa Babi na Baha'u'llah walikuwa ni udhihirisho wa Mungu, na sherehe tatu kati ya kumi za Kibaha'i huadhimisha matukio kwenye maisha ya Babi.

Waazali
 

Baada ya Babi kuuawa mwaka 1850, angalau watu saba wamedai kuwa ni warithi wake kama "Mtu ambaye ni lazima adhihirishwe na Mungu." Karibu Wababi wote walimfuata Mirza Yahya Nuri Subh/Sobh al-Azal (karibu mwaka 1830-1912) mwanzoni kwa miaka 13. Alikuwa na usia toka kwa Babi unaomwenyesha kuwa mrithi aliyechaguliwa naye. (Subh al-Azal inamaanisha kuja kwa umilele.) Al-Azal aliunga mkono uongo (kudanganya watu kuhusu kitu walichoamini) badala ya migogoro. Kundi lake linaitwa Wazali.
 
Baada ya miaka 13, kikundi kingine cha Wabaha'i kilianzishwa na kaka mkubwa wa al-Azal aliyeitwa Husayn 'Ali Nuri Baha' (1817-1892), ambaye miaka 6 baadaye alijifanya kuwa Baha'u'llah. Baadhi ya Wabaha'i walisema kitendo cha Bab kumteua al-Azal kuwa mrithi wake kilikuwa ni mbinu ya kuifanya serikali iachane na Husayn. Hata hivyo serikali iliwatimua wote na kuwafanyia ukarimu.
 
http://www.h-net.org/~bahai/arabic/ vol4/niraqi/niraqi.html ina maelezo zaidi juu ya Babi alivyomteua Mirza Yahya awe mrithi wake mpendwa.
 
Mulla Rajab 'Ali, aliyepewa jina la utani Qahir, alikwa mwandishi mashuhuri wa Kiazali ambaye Waazali wanadai kuwa aliuawa na Wabahai'. Tazama www.h-net.org/ ~bahai/arabic/vol4/qahir/qahir.html. (11/13/2004)
 
Wakati Babi alifundisha kuwa Jihad ilikuwa sahihi, na Wabaha'u'llah waliikataa Jihad, Baha'u'llah aliwasihi wafuasi wake kuwa wakatili kwa adui zao. Serikali ilivitimua vikundi vyote na kuvipeleka sehemu tofauti tofauti. Wazali walipelekwa Cyprus wakati ambapo Wabaha'i walipelekwa Acre ya Palestina. Mara baada ya hapo, idadi kubwa ya viongozi wa Kiazali waliuawa.
http://www.geocities.com/Athens/Acropolis/5111/mirza.html 11/13/2004
 
Tazama Denis MacEoin, "Divisions and Authority Claims in Babism (1850-1866)." Studia Iranica 18, 1 (1989):93-129 kwa habari zaidi juu ya mauaji ambayo Wabaha'i wanadaiwa kufanya dhidi ya Waazali.

Baha'u'llah na Matatizo Yake

Wakati ambapo kuna Waazali elfu kidogo tu nchini Irani leo, New 20th Century Encyclopedia of Religious Knowledge inakadiria kuwa kulikuwa na Wabaha'i karibu milioni 1.3 hadi 2 mwaka 1991. Wayahudi wengi walibadili dini na kuwa Wabaha'i Irani wakati wa utawala wa Shah. Wengi wao waliuawa wakati wa utawala wa Khomeini. Kuna karibu Wabaha'i 100,000 Marekani walio kwenye shirika 1,000 hivi. Kuna Wabaha'i wengi India.
 
Wabaha'i wanamfuata na kumwabudu Baha'u'llah ambaye alizaliwa Uajemi (Irani ya sasa) mwaka 1817 na kufariki Palestina mwaka 1892. Mwaka 1863, miaka kumi na tisa baada ya Babi kujitangaza, Baha'u'llah alijitangaza kuwa imamu wa 12 aliyerudi na kwamba Kristo aliisharudi. Baha'u'llah aliandika Kibao cha Ishraqat, Kibao cha Tarazat, na Kitabu cha Aqdas (Lawb-i-Aqdas) - vilivyowalenga Wakristo.
 
Hata hivyo, Babi alidai kuwa yeye ni Mahdi, wakati ambapo Baha'ullah alidai kuwa yeye ni Mahdi.
Babi alimteua Subh-i Azal kuwa mrithi wake, si Baha'ullah. Pia Babi alisema kuwa udhihirisho mpya hautatokea katika kipindi cha miaka 1,000 ijayo, si miaka 19. Tazama http://www.geocities.com/Athens/ Acropolis/5111/mirza.html 11/13/2004 kwa maelezo zaidi.

Warithi wa Baha'u'llah

Baada ya Baha'u'llah kufariki, mtoto wake mkubwa wa kiume 'Abdu'l-Baha 'Abbas (=Abbas Effendi) (5/23/1844-1921) alichukua nafasi yake. Alizaliwa Tehran usiku uleule Babi alipijitangaza. Mjukuu wake mkubwa wa kiume, Shoghi Effendi Rabbani (1897-1957) alimbadili. Baada yake, Wabaha'i waliongozwa na baraza lililoitwa 'Nyumba ya Kimataifa ya Haki' (International House of Justice). Hata hivyo, kundi la watu ambalo linafahamika kwa sasa kama 'Imani Sahihi ya Kibaha'i' (the Orthodox Baha'i Faith) liligawanyika, likisema kuwa mrithi hakuwa baraza bali Mason Remey. Beckwith anasema kuwa imani nyingine za makundi hayo mawili ya Kibaha'i zipo karibu sawa.
 
Katika miaka elfu moja au zaidi Wabaha'u'llah wamedai kuwa Udhihirisho mwingine utatokea chini ya kivuli cha Baha'u'llah, ukiwa na vithibitisho vya wazi vya lengo lake, lakini kabla ya wakati huo kufika, maneno ya Baha'u'llah, Abdu'l-Baha na msimamizi na maamuzi ya Nyumba ya Kimataifa ya Haki ndio mamlaka ambazo waumini wote wanapaswa kuzifuata ili kupata muongozo. Mbahá'í yoyote haruhusiwi kuanzisha shule au dhehebu kwa kusimamia tafsiri yoyote maalum ya mafundisho ya au mafunuo yoyote yanadhaniwa kuwa ni ya kiungu. Mtu yoyote atakayevunja amri hizi atachukuliwa kuwa ni "Mvunja agano."
http://bahai-library.com/books/new.era/8.html

Umuhimu wa Kalenda

Wabaha'i wafundisha kuwa "muda si mrefu sana ujao watu wote duniani watapaswa kukubaliana na kalenda moja." Mwaka wa Kibaha'i una miezi 19 yenye siku 19 kila mmoja (= siku 361). Pia wanaongeza siku nne hadi tano za nyongeza kati ya miezi ya kumi na nane na kumi na tisa ili kuifanya kalenda ilingane na mzunguko wa jua wa mwaka. Mwaka mpya wa Kibahá'í huanza sawa na mwaka mpya wa Kiajemi kwenye ikwinoksi ya Machi.

Mafundisho ua Ubaha'i kuhusu Mungu

Imani ya Ubaha'i kuhusu Mungu
● Mungu hawezi kufahamika isipokuwa kwa kujidhihirisha kwake
● Dini kubwa za hapa duniani zinatoka kwa Mungu: Uyahudi, Ukristo, Uislam, Uhindu na Ubudha.
● Mheshimu Ibraham, Musa, Zoroaster, Muhammad, Yesu, Krishna, Buddha, Babi na Baha'u'llah
● Manabii hawakutenda dhambi, lakini mafundisho ya wote hao kasoro wawili wa mwisho yamepotea au kuharibiwa
● Nabii afuataye atakuja baada ya miaka 1,000
● Watu wote wanatakiwa kuabudu udhihirisho wa Mungu
● Baha'u'llah ni udhihirisho wa Mungu kwa sasa
● Mageuko ya polepole yasiyoingiliwa kati ni njia ambayo Mungu aliitumia kuumba kila kitu
● Uovo unakuwepo tu kwa sababu ya upungufu au kukosekana kwa wema Matendo ya Ubaha'i
● Dini zote za ulimwenguni zinatakiwa kuungana
● Jiepushe na Waazali, Wabaha'i wa kweli, na watu waliowahi kuwa Wabaaha'i
● Maombi ni kuzungumza na Mungu (kama katika Ukristo) ● Watu wote wanatakiwa kuzungumza lugha moja, kama vile vile Kiesperanto, lugha bandia iliyoundwa kutumiwa na watu wote duniani
● Jing'amue (Achieve self-realization)
● Watu waliokufa wanaweza kuongea nasi kwa njia ya telepathia
● Hairuhusiwi kupigana isipokuwa kati ya mataifa na wakandamizaji
● Vitu vyote vyenye kulevya au pombe haviruhusiwi, isipokuwa kwa ajili ya mahitaji ya kiafya
● Usafi na elimu ni muhimu
● Hairuhusiwi kucheza kamari, lakini michezo mingine ya kubahatisha inaruhusiwa
Mafundisho Yanaypoingana na Uhindu na Ubudha

● Mengi ya mafundisho ya Krishna na Buddha yamepotea
● Mungu ni mmoja; kuabudu sanamu siyo sahihi
● Imani ya kuwa roho ya marehemu huingia katika mwili wa kiumbe kingine (reincarnation) si sahihi. Kuabudu miungu wengi si sahihi
● Hakuna kufanya kazi ya uukuhani kama ajira (hakuna Wabrahmini)
● Binadamu wote ni sawa, na wanatakiwa wawe chini ya serikali moja (wazo hili linapingana na mfumo wa matabaka)
Mafundhisho Yanayopingana na Uislam

● Mengi ya mafundisho ya Muhammad yalipotea
● Mambo yote ambayo Kurani inasema kuhusu mbinguni, jehanamu, kufufuka, kurudi kwa Yesu ni ufananisho
● Mungu ni Baba. Kristo alijiita Mwana wa Mungu
● Muhammad hakuwa nabii wa mwisho
● Hija ya Maka haitakiwi
● Hakuna haja ya kufanya swala mara tano kwa siku
● Watu hawapaswi kuwa chini ya Sharia
● Utumwa si sahihi kwa siku za leo
● Wanawake hawahijati mitando. Hata hivyo, ni vema kuivaa kwenye nchi kali za Kiislam ili kuepuka matatizo. Ndoa ni ya mume mmoja na mke mmoja
● Usawa wa wanawake na wanaume (yaani wanawake si dhaifu kidini, kiakili, bali wanapaswa kupewa na usawa kwenye mahakama, talaka, n.k.)
● Hakuna vita takatifu au Jihad (hapa wanatofautiana na Wababi)
● Tengeneza wosia, lakini toa mirathi kwa kadri unavyopenda (Waislam wanazo sheria za namna ya kufanya hivi)
● Waumayyad (Makhalifa wa kwanza) walikuwa ni ni mnyama wa Ufunuo 11 aliyepinga dini ya Muhammad na 'Ali
● Babi na Baha'u'llah walizaliwa kwenye Ushia wa Uajemi, kwa sababu hapo palikuwa ni moja ya sehemu zilizokuwa nyuma zaidi kidini kwenye ulimwenguni wa wakati ule
Kwa ujumla Waislam husema kuwa mafundisho ya Ubaha'i si tu mapotofu bali mafundusho hayo kuhusu Muhammad hayauwakilishi Uislam. Tazama www.BahaiAwareness.com kwa masomo ya kina ya ukinzani wa imani za Kibabi na Kibaha'i - toka kwenye vyanzo vilivyotokana na vitabu vyao wenyewe
Mafundisho Yanayopingana na Uyahudi
● Mengi ya mafundisho ya Musa yalipotea
● Yesu alizaliwa na bikira na alikuwa nabii wa kweli wa Mungu
● Manabii kama Yesu wanaweza wakayatangua mafundisho yaliyowatangulia
Mafunndisho Yanayopingana na Ukristo

● Mengi ya mafundisho ya Yesu yalipotea
● Sehemu kubwa ya Biblia ni ya ufananisho, ikiwa ni pamoja na mbinguni, jehanamu, ufufuo, kurudi kwa Yesu, n.k.
● Yesu si Mungu aliyefanyika mwili; Utatu Mtakatifu si wa kweli
● Watu wote hawajatengwa na Mungu kutokana na dhambi
● Yesu si njia pekee ya kwendea kwa Mungu
● Yesu hakufa kwa ajili ya dhambi; hakufufuka
● Hakuna haja ya kumfuata Yesu kama Bwana na Mwokozi wako
● Kuongopa unapokuwa unateswa ili kuficha imani yako ni sahihi
● Ushikiliaji mno wa sheria: ni lazima kuifuata kalenda mpya ya Kibaha'ir
Mafundisho Yanayopingana na Ukatoliki

● Mapapa walimwaga damu na kukandamiza ufahamu

Ungependa Kuamini Nafsi Zipi za Mungu Leo?

Ni Mungu gani anayewaruhusu watu wake (Wahindu) wafikiri kuwa nabii wake alitaka wamwabudu nabii na sanamu nyingine, na wakati huo huo awaamuru watu wake (Waislam) kuua watu wanaoabudu sanamu!
 
Ni Mungu gani atakaye "funua" kuwa Allah aliamuru ngozi za watu zichomwe moto jehanamu kisha, na kisha awape ngozi mpya ili zichomwe moto tena, na kisha Baha'u'llah anasema kuwa mbinguni na jehanamu ni vifananishi tu vyenye manufaa ya kuelimisha watu kiroho au kudhoofisha kwa ujinga wa kiroho?
 
Ni Mungu gani atakayetuambia kuwa wokovu u ndani mwako wewe (Buddha), hakuna anayeweza kuja kwa Baba isopokuwa kupitia kwa Yesu (Yesu), Mungu si baba na wala hana mtoto (Muhammad kwenye Kurani).
 
Ni Mungu gani atakayemfanya Yesu aje tena kwa namna ileile aliyopaa kuelekea mawinguni (Mdo 1:9-11 and Ufu 1:7), ilhali Baha'u'llah ni Kristo aliyerudi?
 
Ni Mungu gani anayetuamuru "Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi" (Mt. 5:44-45; Luka 6:27-38), samehe "saba mara sabini (Mt. 18:21-22), dhidi ya "walaani Wakristo" (Muhammad karibu na mwisho wa maisha yake kwenye Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 8 na.427 uk.255) dhidi ya wafanya vita na Waislam wa Kiajemi (Wababi)?
 
Mifano zaidi inaweza kutolewa, lakini natumaini unalipata wazo langu. Watu wengine wanaweza kudhani kwamba Wabaha'i wanasumbuliwa na tatizo la kuchanganyikiwa liitwalo 'multiple personality disorder!'

Jibu la Kwanza la Wabaha'i: Mafunuo "Yanayoendelea" (au Mzunuko wa Ufunuo)

Wabaha'i wana jibu la swali hili, linaloitwa mafunuo yanayoendelea (progressive revelation). Sawa na Waislam, wanaamini kuwa nabii anaweza akazuia, ongeza, au hata kubadilisha amri ya nabii aliyemtangulia.
 
Hata hivyo, neno "yanayoendelea" si sahihi. Wanawake wa Kiyahudi na Kikristo hawakupaswa kuvaa mitando, wanawake wote huru wa Kiislam walivaa, na wanawake wa Kibaha'i hawavai. Huenda "mtiririko wa ufunuo" ni neno bora zaidi. Vilevile, Wayahudi walikuwa na miiko kadhaa ya vyakula ikiwa ni pamoja na nyama ya nguruwe na ngamia, Wakristo waliwekwa huru na miiko ya vyakula, na Waislam wana baadhi ya miiko ya vyakula (hakuna kula nyama ya nguruwe lakini ya ngamia ni sawasawa).
 
Vilevile mungu wa Wabaha'i alibadilisha mtazamo kuhusu talaka. Talaka ziliruhusiwa kwa sababu yoyote kwenye Agano la Kale kwa sababu mioyo ya watu ilikuwa migumu. Yesu alizuia talaka isipokuwa tu kwa sababu ya zinaa. Lakini wanaume wa Kiislam wanaweza kutoa talaka kwa kadri wapendavyo. Kwa hiyo kama Wabaha'i waangekuwa kweli, mafunuo yanazunguka sehemu moja tu (cyclical), hayaendelei mbele (not progressive).

Jibu la Pili wa Wabaha'i: Maneno Yaliyopotoshwa

Wabaha'i wanatoa jibu la pili ambalo ni la nyongeza: mengi ya maneno au manabii waliotangulia walikuwa wamepotea na kupotoka. Kwa hiyo, jambo lolote linalotofautiana na mafundisho ya Babi na Baha'u'llah sio tu kwamba lilitanguliwa, bali pia lilichukuliwa kuwa limepotoka.
 
Jambo hili lina matatizo mawili: Babi aliandika baada ya viwanda vya uchapishaji kugunduliwa na Baha'u'llah anatofautiana na kile alichokisema kwamba Imamu wa 12 hatatokea kwa miaka 1,000. Huku siyo tu kutengua amri: jambo hili linaufanya unabii wa Babi kuwa wa uongo.
 
Tatizo la pili ni hili: kutatokea nini endapo tutapata ushahidi wenye kuaminika zaidi wa usahihi wa Agano la Kale, Agano Jipya, na sehemu kubwa ya Kurani? Utetezi wa Ubaha'i nao pia utashindwa.
 
Hebu tuanze na Kurani na kurudi nyuma.
 
Wakati ambapo Kurani ilikusanywa baada ya kifo cha Muhammad, Sahih Muslim (juzuu ya 2:2286 uk.500, 501) inasema kuwa sura moja ilipotea, na Kurani ya Ibn Masu'd haikuwa na sura tatu, na Kurani ya 'Ubai bin Ka'b haikuwa na sura nyingi, tunaweza kujua kuwa nyingi za sura zilizopo zilitokana na dondoo na ufafanuzi wa Hadithi na wanahistoria wa mwanzo wa Kiislam. Hata kama sehemu za Kurani hazikuhifadhiwa kiusahihi, hakuna mashaka kuwa nyingi za sehemu hizo hazikufanyiwa hivyo. Kuna sehemu nyingi sana kwenye Kurani zinazoruhusu kufanya Jihad dhidi ya makafiri.
 
Hadith za Wasuni ziliandikwa miaka 200 baadaye, na wanahistoria wa mwanzo wa Kiislam wanathibitisha hivyo hivyo kuhusiana na mengi ya mafundihso ya Uislam (ingawa si kila kipengele cha Kurani). Hebu tuziangalie Injili.
 
Tuna nakala za Injili zilizoandikwa kwa mkono mwaka 150-200 BK, kipande cha maandiko cha John Rylands kiliandikwa karibu mwaka 117-138 BK. Pia tuna ushahidi unaothibitisha wa waandishi wa mwanzo wa kanisa kuanzia Clement wa Rumi mwaka 97/98 BK. Pia tuna hata mwandishi mwasi Tatian, ambaye karibu na mwaka 170 BK alidondoa neno kwa neno 73% ya Injili kwenye kazi yake, Diatessaron. (Diatessaron haina vitu vingine zaidi ya Injili).
 
Sura 5:46-48 ya Kurani inasema kwamba Yesu aliithibitisha Torati na Injili. Kwenye Injili Yesu pia alilithibitisha Agano la Kale la wakati ule aliokuwepo. Tuna nakala nyingi za Agano la Kale za wakati wa Yesu toka kwenye baadhi ya Hati toka Bahari ya Chumvi (Dead Sea Scrolls), nazo zinaonyehsa kuwa Agano la Kale tulilonalo limehifadhiwa kwa uaminifu kabisa.

Hitimisho

Kama ambavyo Washia wanavyodai kuwa maneno na simulizi vya Muhammad havitoshelezi, nabii wa kisasa zaidi anatakiwa, Wabaha'i wanasema kuwa mafunuo yote yaliyotangulia yanapaswa kubadilishwa ili kulingana na Baha'u'llah.
 
Kama ambavyo Waislam wanavyomheshim Yesu lakini wanasema kuwa maneno yote ya manabii waliotangulia yaliyopo sasa ni upotoshaji mtupu wa kile kilichosemwa nao hapo awali, Wbaha'i wanasema hivyo hivyo kuhusiana na manabii wote waliotangulia akiwamo Muhammad.
 
Lakini kama si mafundisho yote yaliyotangulia yaliyopotoshwa basi dini ya Ubaha'i inakuwa imeanguka.

Namna ya Kushirikisha Injili kwa Wabaha'i

Wabaha'i tayari wanaamini ukweli kuwa Mungu ni mmoja na kwamba kuabudu sanamu ni makosa. Lakini muulize Mbaha'i kama Mungu alikusudia kutuambia kwa uhalisi kuwa mbinguni na jehanamu ni sehemu halisi ambazo watu watakwenda, je wanajuaje hayo? Kukinzana kwa Baha'u'llah na manabii waliotangulia kumewabadilisha? Je ushuhuda wa maelfu ya wafia dini wa Kikristo waliokufa kwa ajili ya imani yao kuliko kudanganya unaweza kuwa ushuhuda kwao? Je wanawezaje kusikia?
 
Munngu ni Mungu wa kweli, na Mungu haongei uongo (Hesabu 23:19; 1 Samweli 15:29). Lakini watu ni wenye dhambi na wanasema uongo, ikiwa ni pamoja wengi waliosema unogo kuhusu Mungu. Wengi wamedai kuwa warithi wa kweli wa Babi, na Washia wanasema kuwa kudai kwamba Babi na Baha'u'llah ni maimam wa 12 ni uongo. Unaweza kupima ukweli wa madai, na kigezo chako cha kupima ukweli wa hayo madai kinatumikaje kwa Baha'u'llah?
 
Kwenye Mathayo 24:4-5, Yesu alisema "Angalieni mtu asiwadanganye. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema mimi ni Kristo; nao watawadanganya wengi." Ufunuo 1:7 inasema, "Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina." Je kuna yoyote ambaye amemwona Baha'u'llah? Watu wasioamini kuwa Mungu yuko wamekuwa wakikejeli mstari huu wakisema kuwa haikuwezekana watu wote kumwona Yesu kwa sababu dunia ni ya duara. Ni kweli wakati huo ulikuwa kabla ya luninga kugunduliwa. Ni asilimia kidogo sana ya watu wa hapa duniani waliomwona Baha'u'llah.
 
"Akiisha kusema hayo [Yesu], walipokuwa wakitazamana, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. Walipokuwa wakitazama macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mnasimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni" (Mdo 1:9-11).
 
Unapaswa kufanya uamuzi wa kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wako. Kwa sababu kama ambavyo Wafilipi 2:9-11 inavyosema, "Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba."

Mrithi wa Babi ni Nani?

"Bab" ni neno la moja ya makundi ya Kishia na Kialawiti ('Alawite) lenye kumaanisha mtu ambaye ni "lango" la kuelekea kwenye kweli, mbinguni, au Mahdi. Ali Muhammad wa Shiraz, mzao wa Muhammad aliyezaliwa mwaka 1819/1821, alidai kuwa Babi, mtangulizi wa imamu wa 12 aliyefichwa. Alidai hivyo alipokuwa Maka mwaka 1844 BK.

Mifano ya Maandiko ya Babi

Babi aliandika vitabu kadhaa, kikiwemo Kitabu'l-Asma', huenda hata kazi yake muhimu zaidi, Bayan. Kikundi kidogo cha Waazali ambacho pia kinajiita Wabayani', kwa sababu wanamfuata Bayan wa Babi, wakati ambapo Wabaha'i wanadaiwa kutokumfuata. Ukweli ni kwamba Baha'u'llah kwenye Waraka wa Mbwa Mwitu alisema kuwa hakuwahi kuwa na muda wa kusoma maandiko ya Babi. Baha'u'llah and the New Era uk.60.
 
Yafuatayo yanatoka kwenye kazi ya Babi iitwayo Panj Sha'n (Hatua Tano), iliyotafsiriwa na http://bahai-library.com/unpubl.articles/walbridge.panj.html (11/23/2004)
 
Kwa jina la Mungu, Mungu Halisi, Mungu Halisi!
Mimi, naam, ni Mungu—Hakuna Mungu mwingine ispokuwa Mimi—Mungu Halisi, Mungu Halisi.
Kwa jina la Mungu, Mungu Halisi, Mungu Halisi.
Mungu kwa Mungu, Mungu Halisi, Mungu Halisi.
Kwa jina la Mungu, Mungu aliye kama Mungu, Mungu aliye kama Mungu.
Mungu, hakuna Mungu mwingine isipokuwa Yeye, Mungu Halisi, Mungu Halisi.
Mungu, hakuna Mungu mwingine isipokuwa Yeye, Mungu aliye kama Mungu, Mungu aliye kama Mungu.
Mungu, hakuna Mungu mwingine isipokuwa Mungu, Mungu kama Mungu wa Utatu (Godhead).
Mungu, hakuna Mungu isipokuwa Yeye, Mungu alifikia Uungu.
...
 
Sema, Ee Mungu, unainuka kama Mungu
Wa mbingu na nchi na uwazi uliopo kati yao
Kisha unapanda mti wa uthibitisho
katika vitu vyote ulivyoviumba
au utakavyoviumba kwa amri yako
mpaka siku utakapodhihirisha
Udhihirisho wa Nafsi yako
ili kwamba watu wote wamwamini Yeye
na waweze kuwa na haakika na Yeye
kisha wainame mbele ya uso wake.
 
Tambua kuwa watu wote walitakiwa kuinana mbele ya Udhihirisho wa Mungu, na huu ndio Babi alidai kuwa ndie.

Wanaodaiwa Kuwa Warithi

Wakati Washia wa Uajemi walipomtia nguvuni, palikuwa na Wababi wa kutosha kuanzisha maasi. Lakini baada ya kupigana mara tatu maelfu ya Wababi waliuawa. Waajemi waliwaua Wababi tarehe 9 Julai, 1850 BK. Mwaka 1852 Mbabi mmoja alijaribu kumpiga bunduki Mshaha, na Mshaha Washah walilipiza kisasi zaidi dhidi ya Wababi.
 
Lakini ni nani aliyepaswa kumrithi Babi?
Watu wengi walisema kuwa walipaswa kuwa

Mirza Yahya Nuri Subh-i Azal (kikundi kidogo cha Azali = Wabayani')
Husayn 'Ali Nuri Baha' (kaka mkubwa wa kambo wa Azal, kikundi kidogo cha Wabaha'i)
Mirza Asadullah
Mirza Abdullah Ghaugha
Husayn Maylani (aliyefahamika kama Husayn Jan)
Syed Husayn Hindiyani
Mirza Muhammed Zarandi

Kwa miaka kumi na mitatu ya kwanza, wengi wa Wababi walimfuata Azal. Baadaye Wabaha'u'llah walianzisha kundi lake, na miaka sita baadaye, Wabaha'u'llah walidai kuwa yeye ndiye aliyekuwa ameahidiwa.

Uhasama na Mauaji kwa Ajili ya Urithi

Baada ya Babi kuuawa, Wababi walikuwa na uhasama wa kiuuaji miongoni mwao. www.geocities.com/ Athens/Acropolis/5111/mirza.html inasema:
 
"Baada ya kufika Edirne mwezi Desemba mwaka 1863, mivutano miongoni mwa jamii ya Wababi iliongezeka. Mapema mwaka 1866 Bahaullah alirasimisha mgawanyo kwenye jamii, na Wababi waliahidi kuwaunga mkono ama Sobh-e Azal au Bahaullah, kundi la pili ndilo lilipendwa zaidi na watu. Licha ya Bahaullah kupinga vita takatifu ambayo Wababi waliifanya kwa juhudi kubwa, Bahaullah aliwashawishi wafuasi wake kufanya ukatili, na uhasama wa kiuuaji ukaanza. Viongozi wa serikali na wa jamii wa Edirne waliendelea kurafikiana na Wababi lakini baadaya ya mambo kuendelea namna hii baadaye, hawakupendezwa kabisa. Mwaka 1868 viongozi wa Ottoman waliingilia kati. Sobh-e Azal na wafuasi wake, Waazali, walitumwa Famagusta, Cyprus huku Bahahullah na Wabahai waliondolewa na kupelekwa Acre, Palestine. Mapatano yakawa yamewekwa kuwaweka waangalizi kwenye pande za mapigano zinazopingana kwa ajili ya kusimamia. Mauaji yaliendelea, hata hivyo, na waangalizi watatu wa Kiazali waliuawa katika usiku mmoja. Mauaji ya viongozi wa Kiazali yaliripotiwa huko Karbala, Baghdad, Tabriz, Acre na Irani yote. Watu mashuhuri kama Aqa Syed Ali Arab na Mulla Rajab Ali, ambao walikuwa ni miongoni wa Wababi 19 wa kwanza, Nyaraka za Walio hai, na Haji Mirza Jani Kashani, mtunzi wa Nuqtat ul-Qaf, waliingizwa kwenye safu ya Waazali waliouawa.
 
... Ingawa alishutumiwa na Wabahai wengi, Sobh-e Azal anafikiriwa na Wababi wengi kuwa ndie mrithi wa kweli wa, hasa nchini Irani. Waazali wanafuata kitabu cha awali cha mafundisho ya Babi, Bayan, na wamebakia kuwa kukundi kidogo."

Wosia na Agano vya Babi

Waazali wanadai kuwa na Wosia wa Mwisho wa Babi, uliondikwa muda mfupi kabla ya kuuawa kwake mwaka 1850 na kupelekwa kwa Azim Turshizi, ambaye aliutuma kwa Sub-i Azal. Wosia huu unamteua Subh-i Azal (siyo Baha'u'llah) kuwa mrithi. Vifuatavyo ni matini na tafsiri vilivyopo http://www.beliefnet.com/boards/message_list.asp?discussionID=178496 (11/23/2004).
 
Allahu Akbar Takbir'an Kabir'an
hadha kitab min `ind Allah al-muhayyamin al-qayyum ila Allah muhayyamin al-qayyum. qul: kullu min Allah mabda'un, qul, kullu ila Allah ya`udun.
hadha kitab min `Ali qabla Nabil dhikr Allah al-`alamin ila man ba`d li-ismih ism al-waheed dhikr Allah al-`alamin.
qul: kullu min nuqtatu'l-Bayan la-yubda'un, inna ya ism al-waheed fa-ahfaza ma nazala fi al-Bayan wa amr bihi fa-innaka li-sirat haqq al-`azeem.

Mungu ni Mkubwa zaidi, [Mkubwa mwenye] Ukubwa usio na Kikomo. Hiki ni kitabu cha Mungu, Mwenye kutunza, Mwenye kujitosheleza, kwa Mungu Mwenye kutunza, Anayejitosheleza. Sema: Watu wote hurudi kwa Mungu. Hiki ni Kitabu kutoka kwa `Ali kabla ya Nabil* ambaye ni Ukumbusho kwa Ulimwengu kwake ambaye jina lake ni Umoja/wa Kwanza, Ukumbusho wa Ulimwengu. Sema: [Vitu] vyote vimetengenezwa tokana na Mawazo ya Ufafanuzi/Bayan. Hakika, Ee jina la Umoja/Mmoja, tunza [na kulinda] kile ambacho kimeshushwa [au, kilichofunuliwa] kwenye Ufafanuzi/Bayan na kile kilichoamriwa nacho, na hakika wewe u Njia ya Kweli na Iliyonyooka zaidi. Muhuri (Inni ana hujjat Allah wa nurihi/Hakika, Mimi ni uthibitisho na mwanga wa Mungu).

*'Nabil' kwenye abjad/mfumo wa namba za ufahamu wa Uislam unalingana kitarakimu na wa Muhammad ambayo yote inathamini namba '92'. Hii ni njia nyingine ya Babi ya kusema jina lake, `Ali Muhammad.

# Waheed, umoja au mmoja, ni ya kumuonyesha Azal ambayo hapa pia ni sawa na 'Yahya' (yaani 28), jina la kwanza la Azali.
 
Notisi za kwenye tovuti ambazo mtu anaweza kusoma haya (zikiwa na tafsiri ya zamani ya Kiingereza) kwenye tafsiri ya E.G. Browne ya NEW HISTORY OF MIRZA `ALI MUHAMMAD, THE BAB (Amsterdam: 1975) ya Mirza Muhammad Hamadani.

Mtazamo wa Kibaha'i

Mtazamo mmoja wa Kibaha'i ni kwamba Babi hakuwa amependa Azal awe mrithi wake, lakini aliandika wosia huo ili kwamba Waajemi wasimjue mrithi wa kweli, Baha'ullah. Ni kweli, Waazali hawakubaliani na mtazamo huu.

Maoni ya Babi

Ingawa hatuwezi kumuuliza Babi leo, Wababi waliandika kitu kimoja: alisema kuwa udhihirisho mpya hautafika kwa miaka 1,000, wala miaka 19. Tazama
http://www.geocities.com/Athens/Acropolis/5111/mirza.html 11/13/2004 kwa habari zaidi.
 
Sasa Azal hakudai kuwa yeye ni udhihirisho lakini Baha'u'llah alifanya hivyo.

Maoni ya Waislam Washia wa Ithna'Ashariyya

Washia wa Irani wanaamini kuwa Imamu wa 12 atarudi, lakini si Babi wala Baha'u'llah.
Mahdi atatokana na Fatima, na ataitwa Muhammad. Wakati ambapo Babi alidai kuwa alitokana na Muhammad, Baha'u'llah wa Kiajemi (kwa ufahamu wangu) hakutona naye.
Mahdi atainua kiwango cha watu weusi huko Khurasan (Baha'u'llah hakuwahi kufanya hivyo).
Atakuja Maka na kisha atasafiri kuelekea Kufa. (Baha'u'llah hakuwahi kwenda Kufa)
Dajjil mwenye jicho moja (mpinga Kristo) atakuja upande wa mashariki
Jua litachomoza tokea upande wa magharibi, na nyota moja ya mashariki itatoa mwanga mwingi kama mwezi.
Kama Muhammad, Mahdi atakuwa na kusudi jipya na kitabu kipya na sheria mpya ya kidini. Hili litakuwa ni jaribu kubwa sana kwa Waarabu. Upanga utakuwa kati ya Mahdi na Waarabu. (Waarabu hawakumtesa Baha'u'llah; Waajemi na Waturuki walimtesa).
Yesu naye atarudi. (Yesu ni tofauti na Mahdi kwenye theolojia ya Kishia).
Wapiganaji 313 toka kwenye vita ya Badr pia watarudi. (Jambo hili halikutokea).
Maimamu na manabii waliotangulia nao wote pia watarudi.

Maoni ya Waislam wa Kisuni Kuhusu Wabaha'i

Wasuni wanaamini kuwa utambuzi wa mtu anayedaiwa kuwa ni Imamu wa 12 ni jambo lisilokuwa na maana kwa sababu hakuna Imamu halali wa 12. Muhammad alikuwa ni hitimisho la manabii, na mbali ya makhalifa hakuna imamu halali, Mshia au mwingineyo yote wa kumrithi Muhammad.
 
Wasuni wanawaona Wabaha'i kuwa ni wazushi wasiokuwa Waislam. Wabaha'i wako chini ya maagizo haya:
 
Hapo baadaye utapaswa kujihadhari na watu wanaoikubali Kurani tu lakini wanaikana Sunnah. Abu Dawud juzuu ya 3:4587-4589 uk.1293-1294.
 
Kila kitu kpya ni uvumbuzi, na kila uvumbuzi ni makosa. Abu Dawud juzuu ya 3:4590 uk.1294.
 
Hakuna uvumbuzi baada ya kuanzishwa kwa Sunnah. Abu Dawud juzuu ya 3:4595 uk.1296.
 
Waislam wa Kisuni wanaamini kuwa Yesu atarudi tena. Lakini wanadai kuwa ataivunja misalaba, atakomesha kodi ya jizya ambayo iliwalinda Wakristo na Wayahudi kwa maneno tu, na kumchinja mpinga Kristo kwa mikono yake mwenyewe (dajjal). Kabla ya kufa, Baha'u'llah hakufanya lolote kati ya mambo haya.

Mtazamo wa Kikristo kuhusu Wabaha'i

Ingawa Baha'ullah alidai kuwa yeye ni Kristo aliyerudi, Wakristo wanaamini kuwa Baha'u'llah ni sehemu ya utimilifu wa Mathayo 24:1,44.
 
*"Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi (4-5). Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana. Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi" (10-11).
 
Mdo 1:9-11 inasema, "Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimaama karibu nao, wenye nguo nyeupe, wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mnasimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni."
 
Tazama: Biblia inasema "Huyu Yesu" na "atakuja jinsi iyo hiyo."

Mtazamo wa Wayahudi Kuhusu Wabaha'i

Kwa Wayahudi wa kweli, jambo lote hili halina maana; Baha'u'llah si mrithi wa Muhammad kwa sababu Muhammad hakutoka kwa Mungu. Wanafikiri kuwa Baha'u'llah hakuwa Kristo aliyerudi, kwa sababu wanaamini kuwa Yesu hakuwa Masihi aliyetoka kwa Mungu.
 
Lakini wakati Masihi atakapokuja, ataikomboa Israel kutoka kwa maadui wake. Baha'u'llah hakufanya jambo lolote la aina hii.

Je Kuna Nabii wa Kweli Hebu na Asimame?

Kama hatujajifunza kitu chochote zaidi chenye umuhimu, tunaweza kuona kuwa ni rahisi kwa mtu kudai kuwa ni nabii wa Mungu, au mrithi wa mtu mwingine. Kuthibitisha madai hayo linakuwa ni jambo tofauti kabisa.
 
Kila mtu anaweza kukubali kuwa watu wengi waliowahi kudai kuwa wametoka kwa Mungu ni waongo na walikuwa hawakuwa wanamtumikia Mungu wa kweli bali Shetani. Hivyo basi twawezaje kujua wapi kati yao walitoka kwa Mungu kweli?

Maisha na Mafundisho

Ingawa Baha'u'llah naye alifungwa, alikufa kifo cha kawaida (tokana na homa) na aliishi kitajiri sana mwishoni mwa maisha yake. Waazali wanadai kuwa aliwaamuru wafuasi wake kuwashambulia Waazali.
 
Muhammad
pia aliteswa, lakini aliwatesa watu wengine kwa kiasi kikubwa zaidi. Alikufa kifo cha kawaida, lakini ilikuwa mwaka mmoja baada ya kula nyama ya kondoo iliyotiwa sumu ambayo alipewa na mwanamke ambaye mume wake aliuawa na Muhammad. Hadithi zinarekodi kuwa Muhammad aliamuru mauaji, mateso, na mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya watu aliokuwa anawashuku. Muhammad aliomba msamaha wa dhambi zake mara nyingi sana.
 
Yesu
aliteseka na kufa kama shahidi wa mafundisho yake. Alikuwa maskini wa mali maisha yake yote. Yesu hakumtesa mtu yoyote. Aliagiza kuwapenda maadui na kuwaombea wale wanaowaudhi. Hata Waislam wanakubaliana na Biblia kuwa Yesu aliishi maisha yasiyokuwa na dhambi.

Miujiza

Baha'u'llah hakutenda muujiza wowote ambao umeandikwa.
 
Ingawa hadithi zinadai kwamba Muhammad alitenda miujiza mingi sana, ikiwamo kuugawa mwezi vipande viwili, mafundisho ya Kurani yanasema kwamba Muhammad hakutenda miujiza, zaidi ya kuileta Kurani.
 
Yesu
alitenda miujiza mingi, iliyothibitishwa na watu wengi kama Mathayo, Yohana, na Petro. Yesu alifufua wafu, na Yeye mwenyewe alifufuliwa kutoka kifoni.
 

Unabii Unaomhusu

Baha'u'llah alidai kuwa alitabiriwa na Wazoroastria (Shah Bahram), Biblia (Kristo aliyerudi) na Waislam wa Kishia (Imamu wa 12 aliyerudi). Hata hivyo, Baha'u'llah hakuweza kumng'oa mwovu Ahiram kwa uhakika kwenye Uzoroastria. Kwa hakika, Baha'u'llah hakuweza kumng'oa mtu yoyote yule. Babi alitabiri kuwa Mahdi angakuja baada ya miaka 1,000, na Baha'u'llah alidai kuwa yeye ndiye miaka 19 tu baada ya kifo cha Babi. Kama ilivyoonyeshwa hapo awali, Baha'u'llah hakufuata nabii za Kishia zinazomhusu Mahdi, ndogo kati ya hizo ikiwa kwamba Mahdi na Kristo ni watu wawili tofauti ambao wote watarudi. Matendo 1 and Ufunuo 1 vinaonyesha kuwa wakati Kristo atakaporudi, atakuwa ni Kristo yule yule, kwenye mawingu, na kila jicho litamwona. Na hata kama angedaiwa kuwa wazi kabisa, watu wengi duniani hawajawahi kusikia kuhusu Baha'u'llah.
 
Waislam wanadai kuwa Muhammad alitabiriwa kweney Biblia katika Kumbukumbu 18:15-18, Yohana 14:16-26; 15:26; 16:5-15, na sehemu nyingine. Hata hivyo, Kumbukumbu 18:15-18 inaendana zaidi na Yesu kuliko Muhammad, kwa sababu nabii anayesemwa atakuwa atatoka "miongoni mwa ndugu zako", Yesu alikuwa Myahudi, na Muhammad hakuwa Myahudi. Mistari ya kwenye Injili ya Yohana inamwongelea mfariji, ambaye "atamtukuza Yesu", na alikuwa "ndani ya mitume wa Yesu" (Yohana 16:17). Hivyo basi kwa nini Waislam hawakubali kwamba wao na Muhammad wanatakiwa kumtukuza Yesu?
 
Kuna nabii nyingi sana zinazomhusu Kristo kwenye Agano la Kale. Zifuatazo ni baadhi tu ya nabii hizo:
Anatokana na Daudi: Yer 42; Mdo 13:22-23; Ufu 22:16.
Mwana wa Mungu: Zab 2:7 Mat 3:17; 16:16-17; 27:54; 9:7; Lk 9:35; Yoh 1:34; Mdo 13:33; Ebr 5:5.
Mtoto anayeitwa Mungu mwenye Nguvu, Mfalme wa Amani, n.k. Isa 9:6. Mwenye umasihi kwa mujibu wa Yemenite Midrash 349-350 na Pereq Shalom uk.101.
 
Je Masihi Atakuja Lini?

Fimbo ya enzi haitatoka: Mwa 49:10; Lk 3:23,33 Mwenye umasihi kwa mujibu wa Talmudi za Babeli na Yerusalem, Targum ya Yonathani, Targum ya Yonathani wa Bandia, Targum ya Waonkelo, Maoni ya Hati za Bahari ya Chumvi, na Targum ya Kiaramiki. Wayahudi walipoteza haki yao ya kutekeleza adhabu ya kifo mwaka 11 KK kwa mujibu wa Talmudi ya Babeli, Sanhedrin sura ya 4.
Kabla ya hekalu kubomolewa (mwaka 70 BK) Mal 3:1
Aliuawa mwaka 32/33 BK. Dan 9:20-27 na Neh 2:1-10 (445/4 KK) Mwenye umasihi kwa mujibu wa Wamaimonidi kwenye Igeret Teiman, Rabbi Musa Abraham Lawi kwenye The Messiah of the Targums, Talmuds and Rabbinical Writers
 
Je Masihi Atafanya Nini?

Huduma ya Miujiza. Isa 35:5,6a; Mt 9:6-7,22, 32-35; 11:4-6; 12:13; Yoh 5:5-9; 9:6-11, n.k.
Ataingia kama mfalme akiwa amepanda punda. Zak 9:9; Luk 19:35-37; Mt 21:5-9; Yoh 12:15
Hatatelekezwa kwenye kifo. Zab 16:8-11; 30:3; Mdo 2:31; 13:33; Mk 16:6; Mt 28:6; Lk 24:46
Roho wa Bwana atakuwa juu yake. Isa 11:2; Mt 3:16; Mk 1:10-11; Lk 4:15-21,32; Yoh 1:32 Masihi kwa mujibu wa Targum ya Isaiah na Talmudu ya Babeli.
 
Maitikio ya Watu

Alisalitiwa na rafiki yake . Zab 41:9; Mt 10:4; 26:48-50; Mk 14:43-44; Lk 22:47-48; Yoh 18:3, 5.
Alikataliwa na watu wake mwenyewe. Isa 53:3-4; Zab 69:8; Yoh 1:11; 7:5; Mt 21:42-44.
Walimpa siki kunywa. Zab 69:21; Mt 27:48
Aliuawa pamoja na wahalifu. Isa 53:12; Mt 27:38; Mk 15:27.
Alizikwa kwenye kaburi la tajiri. Isa 53:9; Mt 27:57-60.
Wayahudi wengi walishindwa kumuona Masihi kwa sababu walikuwa na shauku ya mkombozi wa kisiasa, na hawakutofautisha kati ya kuja kwake kwa mara ya kwanza na mara ya pili.

Nabii Alizofanya

Baha'u'llah alimwandikia barua Napoleon III akimwonya aache kuwa mtu wa vita. Baadaye Napoleon III alishindwa na Ujerumani. Kwa upande mwingine, toleo la mwana 1923 la Baha'u'llah and the New Era uk. 278, 288-289 linasema kuwa Baha'u'llah na 'Abu'l-Baha' walitabiri amani kubwa zaidi na waliahidi umoja wa watu vitatokea kwenye karne ya 20. Jambo hili liliondolewa kwenye matoleo yaliyofuata kwa mujibu wa Beckwith uk.37.
 
Muhammad
kwenye hadithi alitabiri kuwa wangewavamia Warumi (wa Mashariki-Byzantines) na Waajemi, na kuwapiga watu wenye nyuso bapa (Waturuki).
 
Yesu
alitabiri kuwa angeuawa, angefufuka toka kwa wafu, kwamba Yerusalemu ingeangamizwa. Kitabu chote cha Ufunuo kilikuwa ni unabii uliotolewa na Yesu.

Ushuhuda na Maisha ya Mashahidi

Wafuasi wa Baha'u'llah waliteswa, na wengi wao waliuawa kwa ajili ya imani yao Irani. Hata hivyo, viongozi wengi wa Kiazali waliuawa kimaajabu, na ni nani aliyetaka kuwaua viongozi wa Kiazali kama si viongozi wa Kibaha'i?
 
Wafuasi wa Muhammad waliwapiga watu wengi kwa uaminifu ili kueneza Uislam na kupata sehemu 4/5 ya nyara. Baada ya Muhammad kufa, Waarabu wengi waliacha kuwa Waislam. Waislam waliwapiga sana hadi ama wakarudi kuwa Waislam ama wakafa. Baada ya Waislam kuiteka Mashariki ya kati na Uajemi, walikuwa na vita vya wao kwa wao kati ya mkwe wa Muhammad 'Ali bin Abi Talib upande mmoja, na mke wa Muhammad 'Aisha na majenerali wawili, Talhah na al-Zubayr, upande mwingine. Katika mapigano ya Ngamia, Talhah na al-Zubayr waliuawa na Waislam kwa upande wa 'Ali. Talhah aliwahi kuokoa maisha ya Muhammad katika mapigano ya Uhud. Talhah na al-Zubayr walikuwa Waislam wawili tu kati ya kumi waliohakikishiwa kuwa wataenda peponi. Baada ya hapo, kulitokea vita mbaya sana ya wenyewe kwa wenyewe kati ya 'Ali na Mu'awiyah iliyosababisha mapigano ya Siffin. Baada ya hapo, tawi la Kharijite la Uislam lilikaribia kung'olewa na 'Ali na Mu'awiyah.
 
Wafuasi wa mwanzo wa Yesu hawakumuua au kumtesa mtu yoyote. Kati ya wanafunzi kumi na mmoja, kumi waliuawa kwa ajili ya imani yao: Yohana alikufa kifo cha kawaida.

Hitimisho

Watu wengi wamewahi kudai kuwa wametoka kwa Mungu, na baadhi yao walikuja kuwa matajiri kwa kufanya hivyo. Hata hivyo, Yesu alikuwa na miujiza, unabii kuhusu Yeye, na maisha yasiyokuwa na dhambi vilivyothibitisha madai yake. Wafuasi wa mwanzo wa Yesu walieneza injili kwa njia ya amani, wakati ambapo wafuasi wa Muhammad walishambulia watu kwa mapanga. Hata kama Wabaha'i hawakueneza dini yao kwa mapanga, bado walidai kuwa wanamfuata Muhammad ambaye alieneza dini yake kwa upanga.
 
Kwa hiyo achana na wazushi na mgeukie yeye ambaye Mungu amemwonyesha kuwa ametoka kwake: Yesu Kristo.

Jinsi Gani Wabaha'i Wanaweza Kukubaliana na Ukristo, kwa Kutoa Maana Mpya ya Maneno

Ubah'i unaweza kuelezwa kwa njia ambayo inafanana sana na Ukristo, lakini wanafanya hivyo bila kukuambia kuwa wametoa maana mpya ya maneno. Wakati Wabaha'i wanasema kuwa wanaamini kile ambacho Wakristo wanaamini, na kasha wanatoa maana mpya ya maneno, ni muhimu kuweka mambo sawa na kuonyesha vitu tofauti ambavyo wao na Wakristo wanaamini. Wafuasi wa dini yoyote ile wanatakiwa kutumia vitu ambavyo vinaiwakilisha dini yao kwa usahihi; si vile ambavyo vinaifanya ionekane sawa na nyingine. Ifuatayo ni baadhi ya mifano, kila mmoja unafuatiwa na kitu ambacho Wabaha'i wanafundisha.

Yesu ni Njia Pekee ya Kwenda kwa Mungu

Kijitabu cha Kibaha'i kiitwacho "Kristo Asiye Mfano" (The Incomparable Christ) kilichoandikwa na Stonehaven Press (1997) kinaanza hivi:
 
"Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi" - Yesu Kristo (Yohana 14:6).
 
Baadaye kijitabu hicho kinasema: "Tokana na mtazamo huu, kuna Kristo mmoja tu. Haiwezekani kuwa na Kristo wawili, au kumi; Kristo hawezi kuwa na mtangulizi, mrithi, mbadala au mtu mwingine anayechukua mahali pake. Yeye ni njia pekee kupitia hiyo tunaweza kumjua Mungu: 'Hakuna mtu atakayeweza kuja kwa Baba bila kupitia kwangu' (Yohana 14:6).
 
"Wabaha'i wanaamni kuwa uwepo huu huu wa Mungu [Kristo] umetokea tena katika nyakati zetu kama Baha'u'llah, mwanzilishi na mtu muhimu sana kwenye imani ya Kibaha'i, anayetimiza ahadi za Biblia zinazohusu 'kurudi' kwa Kristo. (Kabrasha la Utukufu wa Kristo).
 
'Yesu, Roho wa Mungu ... amejidhihirisha kwako, mara nyingine tena, kupitia kwangu (Gleanings from the Writings of Baha'u'llah 101).

Kristo Asiye na Mfano - Kusema Ukweli ni Mdogo kwa Baha'u'llah

Mara baada ya hapo, kabrasha hilo hilo linaendelea:
"Kuna Kristo mmoja tu. Huu ni ukweli uliopo, na utaendelea kuwa hivyo. Kristo ni wa pekee, asiyebadilika, asiyegawanyika, asiye na mwenzi, na asiyefananishwa - 'Alfa na Omega (Ufu 1:8). Hatuwezi kueleza kikamilifu utukufu wake, wala kutia chumvi umuhimu wake. Ni kwa kupitia kwake tu tunaweza kumfikia Mungu."
 
Jambo hili linaonekana kuwa la Kikristo, na hakuna jambo lingine kwenye kabrasha linalosema kuwa hili si sahihi. Hata hivyo, kabrasha hili linatoa sura isiyokuwa ya kweli kama wanawaambia watu kuwa Yesu "hana mwenzi" na "hafananishwi" na "hatuwezi kuutilia chumvi umuhimu wake" wakati kitu wanachomaanisha hasa ni kuwa Baha'u'llah si mwenzi wake, kwa sababu kitu wanachokifikiri hasa ni kuwa Baha'u'llah ni mkubwa kuliko Kristo. Wanasema kuwa Baha'ullah ni Kristo aliyerudi kwa upande mmoja, kasha wanasema kuwa ni mkubwa kuliko Kristo kwa upande wa pili.
 
'Abdul-Baha' kwenye Some Answered Questions uk.65 anasema "lile Tawi Lisilolinganishwa" ni Baha'u'llah, si Kristo.
 
'Abdul-Baha' kwenye Some Answered Questions uk.57-58 anasema, "Kwenye kila mzunguko wa walinzi na roho takatifu wamekuwa kumi na mbili. Kwa hiyo Yakobo alikuwa na watoto wa kiume kumi na mbili; wakati wa Musa palikuwa na viongozi au machifu kumi na mbili wa makabila; wakati wa Kristo palikuwa na mitume kumi na mbili; na wakati wa Muhammad palikuwa na maimamu kumin na mbili. Lakini kwenye udhihirisho huu wa utukufu kuna ishirini na nne, mara mbili ya idadi ya nyingine zote, kwa sababu ukubwa wa udhihirisho huu unahitaji hivyo. ... Watu hawa wakubwa ishirini na nne, ingawa wamekaa kwenye viti vya enzi vya utawala usio na mwisho, wao ni waabudu wa kuonekana kwa udhihirisho wa wakati wote [yaani Baha'u'llah].
 
Wanaandika "kupitia kwake tu tunaweza kumfikia Mungu" lakini Wabaha'i hawamfikii Mungu kupitia kwa Kristo kwa namna yoyote ile zaidi ya kupitia Krishna, Muhammad, au watu wengine, au pungufu ya Baha'u'llah.
 
Kijitabu kiitwacho "Christianity and the Baha'i Faith" kilichoandikwa na Stonehaven Press 1997 kinasema "Kutokana na mtazamo huu, Baha'u'llah ni Yesu kwa kila namna muhimu."

Ufufuko wa Yesu - Sio Ufufuko wa Mwili

Mara baada ya hili wanaandika "Mtazamo binafsi umejengwa kwenye maisha yake ya hapa duniani, kuzaliwa kwake kwa ajabu, maisha yake yasiyokuwa na dhambi, huduma yake ya kufundusha na kuponya, kushindana kwake na uovu, kusalitiwa kwake na mmoja wa wanafunzi wake, na kufa kwake kama kafara ya dhambi kulikofuatiwa na kufufuka na ushindi wake mkamilifu."
 
Hakuna jambo lolote kwenye kabrasha linalosema kuwa mambo haya si sahihi, na mtu anaweza kudhani kuwa Wabaha'i wanaamini mambo haya. Ukweli ni kwamba Wabaha'i wanaamini mambo haya yote: isipokuwa kufa kama kafara ya dhambi na kufufuka.
 
'Abdu'l-Baha kwenye Some Answered Questions uk.103 katika sura inayohusu "Kufufuka kwa Kristo" anasema, "Swali. - Ni maana ya kufufuka kwa Kristo baada ya siku tatu?
Jibu. - Kufufuka kwa Madhihirisho ya Uungu hayauhusu mwili. Hali zao, . . . zina umuhimu wa kiroho na kiungu, na hazina uhusiano wowote na vitu vya kimwili."
 
Kwa kurudia, kwenye uk.104 anasema, "Kwa hiyo, tunasema kuwa maana ya kufufuka kwa Kristo ni kama ifuatavyo: wanafunzi walitiwa wasiwasi na kuhangaishwa baada ya kuuawa kwa Yesu. Uhalisi wa Yesu, unaoonyesha mafundisho yake, . . . ulifichwa na kufunikwa kwa siku mbili au tatu baada ya kuuawa kwake, na haukuwa mzuri na uliodhihirishwa. Hapana, badala yake ulipotea, kwa sababu waamini walikuwa wachache kiidadi na walitiwa wasiwasi na kuhangaishwa. Kusudi la Kristo lilikuwa kama mwili usiokuwa na uhai; na baada ya siku tatu wanafunzi walipopata uhakika na uthabiti, na walipoanza kutumikia kusudi la Kristo, na walipoamua kueneza mafundisho ya kiungu, . . . uhalisi wa Kristo ulikuwa mzuri na zawadi yake ilitokea; Dini yake ikawa hai . . . Kwa maneno mengine, kusudi la Kristo lilikuwa kama mwili usiokuwa na maisha mpaka wakati maisha na neema vya Roho Mtakatifu vilipouzunguka. Hii ndio maana ya kufufuka kwa Kristo, na huku kulikuwa ni kufufuka kwa kweli."
 
Kufufuka hakuhusiani kwa namna yoyote ile na kufufuka kwa mwili halisi. Baha'u'llah and the New Era uk.271, 272.

Wanaamini Utatu Mtakatifu - Hapana Wanaukana Utatu Mtakatifu wa Kikristo

Kabrasha la Utukufu wa Kristo linasistiza kuwa Wabaha'i wanaukubali Utatu Mtakatifu ambao Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni nafsi au sura tatu za Mungu mmoja. Hata hivyo, wanajichanganya wanaposema kuwa "Kufanyika mwili kunaongelea ukamilifu wa asili ya Mungu siyo uhalisi wake."
 
Wabaha'i hawamwabudu Yesu au Roho Mtakatifu.

Wanaiamini Biblia - Lakini Sio Vitu Inavyosema

Kufufuka si kwa mwili; wanautambua umuhimu wake wa kiungu lakini hawaoni kama kunahusiana na ufufuko wa kimwili. Some Answered Questions uk.103.
 
Mapigo ya Misri na siku ndefu ya Yoshua si matukio ya ukwei halisia. Baha'u'llah and the New Era uk.243.
 
Hawaamini uumbaji wa siku sita uliondikwa kwenye Kitabu cha Mwanzo. Hawaamini kuwa Kutoka kwa Waisraeli na mapigo kumi ya Misri yalikuwa ni matukio ya kweli.
http://bahai-library.com/books/new.era/12.html
 
Uumbaji hauanzi na mwanzo wa muda kwa mujibu wa Baha'u'llah. Baha'u'llah and the New Era uk.249.
 
Uumbaji wa mbingu na jehanamu ni kwa ishara tu na si mambo ya ukweli halisi. Baha'u'llah and the New Era uk.231.
 
". . . taarifa iliyo wazi na ambayo haijabadilishwa iliyotolewa kwenye Maandiko ya Kiebrania." Hata hivyo, taarifa hiyo ilikuwa na malengo yake hapo awali. Baha'u'llah and the New Era uk.249-250.
 
Adam na Eva na tunda ni ishara tu. Baha'u'llah and the New Era uk.252.
 
Baha'u'llah na Abdu'l-Baha wanayaona maelezo ya mbingu na jehanamu kwenye maandiko ya kale ya kidini, kama hadithi ya Kibiblia ya uumbaji, kuwa ni ishara tu, kamwe si ukweli halisi. Kwa mujibu wa maelezo hayo, mbingu ni hali ya ukamilifu, na jehanamu ni hali ya kutokukamilika; Mbingu ni kupatana na mapenzi ya Mungu na watu wengine, na jehanamu ni upungufu wa kupatana huko; Mbingu ni hali ya maisha ya kiroho, na jehanamu ni hali ya kufa kiroho. Mwanadamu anaweza kuwa mbinguni au jehanamu akiwa bado yupo katika mwili. Furaha za mbinguni ni furaha za kiroho; na maumivu ya jehanamu yanahusika na ukosefu wa furaha hizi.
http://bahai-library.com/books/new.era/11.html

Wanaamini Uwepo wa Uovu na Shetani - Lakini Sio Kiumbe Aitwaye Shetani

Uovu haupo, ila ni kukosekana au kupungua kwa wema. Baha'u'llah and the New Era uk.237.
 
Kijitabu cha Kibaha'i kiitwacho Christianity and the Baha'i Faith, Stonehaven Press 1997, kinasema, "Je Wabaha'i wanaamini kuwa shetani yupo? . . . Maandiko matakatifu ya Kibaaha'i yamejaa vifungu vinavyomwongelea shetani sawa kabisa na Biblia inavyofanya. Ukweli kuhusu shetani ni jambo moja; asili yake ni jambo linguine. Wabaha'i wanaamini kuwa shetani ni udhihirisho wa asili duni na yenye kuasi ya ubinafsi wa binadamu. Shetani anawakilisha mnyama aliyefungwa ndani ya kila mwanadamu, ikitafuta kutujaribu tuende mbali na njia ya Mungu. Kwa sababu shetani anaishi ndani ya kila mmoja wetu amekuwa ni hatari kubwa zaidi kuliko adui yoyote anayeweza kuwepo atokeaye nje."
 
Lakini kama shetani haishi nje yetu, angewezaje basi kuanguka kutoka mbinguni?
 
 

Mistari ya Kuwashirikisha Wabaha'i


Hes 23:19; Ebr 6:18 - Mungu hadanganyi
Yoh 14:6; Mdo 4:12 - Yesu ni njia pekee
Mdo 1:11; Ufu 1:7 - Yesu Yuley yule, njia ile ile
1 Pet 2:4-8; Yoh 5:21-23 - Yesu ni jiwe kuu la pembeni
Fil 2:9-11; 2 Kor 11:3-6 - Kila goti litapigwa
1 Kor 15:1-6; Yoh 20:27-28 - Kufufuka kwa mwili
Ufu 5:9-14; Mt 14:33 - Kumwabudu Kristo
Mt 24:4, 26-27; Lk 17:23-24 - Msiwafuate hao wanaodai kuwa ni Kristo. Kurudi kwake kutakuwa dhahiri kama kumulika kwa umeme

Jinsi Gani Wabaha'i Wanaipindisha Biblia?

Baha'u'llah na mrithi wake Babi walijaribu kutumia mistari kadhaa ya Biblia kuthibitisha madai yao kuwa ni Kristo aliyerudi. Ifuatayo ni baadhi ya mistari ambayo Wabaha'i wanaitumia siku hizi, na majibu ya kuwapa Wabaha'i. Orodha hii ina vifungu 10 vya Agano la Kale, 7 kutoka Ufuno, na 9 kutoka sehemu nyingine za Agano Jipya.
 
Swala la 1: Je Mwa 1:26 inamaanisha kuwa tunapaswa kujifunza ili tupate ukamilifu wa kiungu na kusistiza Baraka za kiungu, kama Wabahai' wanavyofundisha kwenye Some Answered Questions uk.8, 9?

Jibu: Hapana, kwa sababu Mwanzo 1:27 inasema kuwa Mungu alifanya kile alichosema kwenye Mwanzo 1:26. Adam na Hawa walipoumbwa, walikuwa wakamilifu bila kuwa na dhambi kabla ya kuanguka, na hawakuhitaji elimu. Ingawa bado tuna sura ya Mungu, Mwanzo 1:26-28 inaongelea mambo ambayo Mungu tayari ameyafanya.
 
Swali la 2: Kwenye Mwa 3:5-22, je Adam anawakilisha roho ya kimbinguni, Hawa anawakilisha nafsi ya kiduniani, na nyoka anawakilisha kushikamana na ulimwengu wa wanadamu kama ambavyo Wabahai' wanafundisha kwenye Some Answered Questions uk.123?

Jibu: Hapana. Watu wamekuwa wakijaribu kupata maana za kiroho kinyume cha maana za wazi kwenye kitabu cha Mwanzo kwa karne nyingi sana. Ni dhahiri, Adam ni mwanaume na Hawa ni mwanamke, na kuongezea tafsiri nyingine zisizotakiwa huwafanya wanaume wawe "roho za kimbingu" zilizo juu na wanawake ni "nafsi za kidunia." Badala yake, wanawaume na wanawake wako sawa na wana thamani sawa machoni pa Mungu (Wagalatia 3:28).
 
Swali la 3: Je Isa 9:1, 6, 7 inaweza kuwa inaongea kuhusu Baha'u'llah wa Wabaha'i, kwani Yesu hakuwa na uweza wa kifalme kwenye mabega yake (Baha'u'llah and the New Era uk.261-262)?

Jibu: Hapana, uweza wa kifalme utakuwa kwenye mabega ya Yesu wakati Yesu atakapokuja tena. Jambo hili haliwezi kuwa linamwongelea Baha'u'llah kwa kuwa:
a)
Baha'u'llah hakuwa anaitwa Mungu mwenye nguvu (Isaya 9:6).
b)
Baha'u'llah hakuiondoa mizigo iliyokuwa inawalemea watu wa Galilaya kama ilivyokuwa wakati wa kuanguka kwa Midia (Isaya 9:4).
c)
Baha'u'llah alikufa kabla hajatawala nchi yoyote, na Wabaha'i hawadai kuwa Baha'u'llah atakuja tena.
d)
Ingawa Wabaha'i wanaweza kupenda kuutawala ulimwengu, Nyumba ya Haki ya Kimataifa (International House of Justice) wanayoimiliki haina umuhimu mkubwa katika siasa ya na utawala vya karne za 20 na 21.
 
Swali la 4: Je Isa 11:1-10 yawezakuwa inamwongelea Baha'u'llah wa Wabaha'i, kwa sababu sehemu ya maandiko hayo bado haijatimia? Kwa mfano, kuwachinja waovu, simba na maksai watakaa pamoja, n.k. (Some Answered Questions uk.62-66 na Baha'u'llah and the New Era uk.266-267).

Jibu: Hapana. Wakati ambapo Kristo alitimiza sehemu ya maandiko haya katika ujio wake wa kwanza, sehemu nyinine itatimizwa kwenye ujio wake wa pili. Sababu ya Wabaha'i kukigeuza kifungu hiki, na kuwa hakimwongelei Baha'u'llah, ni kwamba
Yesu, sio Baha'u'llah, alikuwa wa ukoo wa Yese (Isaya 11:1,10).
Yesu, sio Baha'u'llah, "kwa pumzi ya modomo yake atawaua wabaya" (Isaya 11:4b). Kupitia Baha'u'llah, jambo lililo kinyume lilitokea, Wabaha'i wengi waliuawa, haikuwa Baha'u'llah aliyekuwa akifanya mauaji.
Simba na maksai na wanyama wengine hawakukaa pamoja pia wakati Baha'u'llah alipokuja (Isaya 11:6-8).
Injili ya Yesu inatimiza unabii kuwa "dunia itajawa na kumjua Bwana" (Isaya 11:9). Kama ilivyo leo, watu wengi zaidi ulimwenguni hawafahamu kitu chochote kuhusu madai ya Baha'u'llah.
 
Swali la 5: Je Isa 35:1, 2 inaweza kuwa inamwongelea Baha'u'llah wa Wabahai', kwani inasema kuhusu mahali palipo ukiwa patafurahi, na Lebanon na Ngamia, ndipo Baha'u'llah alipoishi miaka ya mwisho ya maisha yake?

Jibu: Yesu naye aliwahi kuishi kwenye eneo hilo, kwa hiyo kusemwa tu kwa maeneo hayo hakumpi Baha'u'llah nafasi kubwa zaidi ya kuwa ndie aliyeongelea kuliko Yesu. Tofauti na unabii wa Isaya 35:1, 2 watu wachache wa Lebanoni au Israel "walifurahi sana" kwa ajili ya Baha'u'llah kuwepo huko. Wakati Waingereza walipolichukua eneo hilo baada ya Vita Kuu ya I, Waislam waliendelea kufanya mambo yao, Wadruze walikuwa wakiendelea kufanya mambo yao, Wayahudi baadaye waliingia Israel na huko walikuwa na vita kali (sio furaha) kati ya hao wawili, na hapakuwa na furaha kubwa katika eneo hilo toka wakati Baha'u'llah alipokwenda hapo. Kwa kusema hivi haimaanishi kuwa Baha'u'llah alisababisha ugomvi na mateso yote haya pale; badala yake Baha'u'llah hahusiki na furaha au mateso vya mlima wa Ngamia.
 
Swali la 6: Je Isa 40:1-5a inaweza kuwa inamwongelea Yohana Mbatizaji, na kwa kiasi Babi na Baha'u'llah, kama ambavyo Wabaha'i wanafundisha kwenye Baha'u'llah and the New Era uk.263-264?

Jibu: Hapana. Maelezo yao yanafurahisha sana. Wanasema kuwa kifungu hiki hakiwezi kuwa kinamwongelea Yohana Mbatizaji na Kristo tu, kwa sababu vita vya Yerusalem havijatimia "huduma yake ngumu haijatimia" Isa 40:2b. Hata hivyo, vita vyake havikutimia wakati wa Baha'u'llah pia. Bila hilo, hakuna kitu chochote kwenye kifungu hiki kinachomaanisha kuwa ni Babi na Baha'u'llah. Zaidi ya hayo, ni wapi ambapo Babi alisema "Itengenezeni njia ya Bwana?" Yeye alifundisha kuwa alikuwa ni udhihirisho wa Mungu, na kwamba udhihirisho mwingine utatokea kwa miaka mingine 1,000.
Wabaha'i wanasema Baha'u'llah inamaanisha "utukufu wa Mungu" kwa Kiarabu, na Isaya 40:5 inatumia msemo "utukufu wa Bwana", lakini inasema kwamba watu wote watauona/watamwona. Sasa Wabaha'i wanasema cheo hiki kinamwongelea mtu, wala si sheria zake au taasisi yake. Lakini wakati Baha'u'llah alipokufa, asilimia ndogo ndogo sana ya watu wa duniani walikuwa wamesikia habari zake. Ama sivyo wawe wanafikiria kuionyesha maiti yake kwa kila mtu, ulimwengu wote hautaweza kumwona yeye wanayemwita "utukufu wa Mungu."
 
Swali la 7: Je jioni na asubuhi 2,300 kwenye Dan 8:13-17 zinaweza kuwa ni unabii wa miaka 2,300 kutoka wakati wa agizo la Artashasta [linalodaiwa kutolewa mwaka 457 KK] hadi udhihirisho wa Babi mwaka 1844 BK kwa mujibu wa madai ya Wabaha'i? (Some Answered Questions uk.40-42)

Jibu: Hapana, kuna matatizo manne katika hili.
Miaka isiyo sahihi:
1844 (BK) + 457 (KK) -1 (hakuna mwaka 0 BK) = 2300 (miaka yenye siku 365.25). Hata hivyo miaka ya kinabii ya kwenye Biblia ni miaka ya kidini yenye siku 360, si miaka yenye siku 365.25.
Urefu wa muda usiokuwa sahihi:
Hizi 2,300 ni jioni na asubuhi, na hakuna sehemu kwenye Daniel inayosema kuwa "jioni na asubuhi" ni miaka.
Muda usiokuwa sahihi wa kuanzia:
Amri ilitolewa katika mwaka wa 20 wa utawala wa Artashasta kwa mujibu wa Nehemiah 2, kwa hiyo muda wa kuanza kuhesabia ulikuwa ni mwaka 445/444 KK, si 457 KK. Mwaka 457 KK ulikuwa ni amri tu toka kwa Artashasta ikithibitisha amri ya awali ya Mfalme Koreshi kuwa Wayahudi wanaweza kurudi Yerusalemu.
Muda usiokuwa sahihi wa kumalizia:
Kama ukiangalia maneno yaliyosalia, si namba peke yake, jioni na asubuhi 2,300 ni muda madhabahu ilipobomolewa hadi ilipowekwa wakfu tena. Wabaha'i wanasema kuwa hii inamaanisha kuwa madhabahu ya Mungu ilikanyagwa na kubomolewa wakati Mwajemi aitwaye Artashasta alipopata ufalme; ilibaki hivyo hivyo hadi wakati wa Yesu hata Babi.
Hitimisho:
Vitu pekee ambavyo Baha'u'llah alivikosea ni urefu wa muda, muda wa kuanzia na muda wa kumalizia. Kwa maneno mengine, alikosea kila kitu!
 
Swali la 8: Je Dan 12:6 inawezakuwa inamwongelea Babi kama Wabaha'i wanavyodai, kwa sababu alitokea miaka 1,260 baada ya Hijra ya Muhammad? (Some Answered Questions uk.43).

Jibu: Hapana. Wanadai hivi kwa sababu mara 3 1/2 au miaka 3 1/2 ya mwaka wenye siku 360 zinazohesabiwa kwa kufuata mwandamo wa mwezi ni 360 x 3 1/2 = siku 1,260. Wanasema siku moja ni mwaka, na Babi alitokea miaka 1,260 yenye miezi inayofuata mwandamo wa mwezi toka Hijra ya Muhammad.
Kwanza kabisa siku hazimaanishi miaka hapa. Pili, muda wa kuanzia kuhesabu si ule ambao Biblia inasema. Licha ya kutumia mbinu za kimahesabu zisizokuwa halali ili kufikia kwenye namba hii, unatakiwa pia usome wazo la mwisho kwenye Daniel 12:1-4. Wakati huu umati wa watu utafufuliwa kutoka usingizi wa kwenye mavumbi, na Mikaeli, ambaye anawalinda Wayahudi atainuka. Kwa hakika jambo hili halikutokea; hasa kwa sababu mauaji ya kimbari ya Wayahudi yalitokea baada ya jambo hili.
Kimsingi Wabaha'i wanachukua karibu kila unabii unaoongelea ufahamu au ukombozi wa siku zijazo na kukwepa jambo halisi linaliongelewa kwa kusema kuwa linamwongelea Baha'u'llah. Kisha wanaweza kusema, "Tazama, unabii huu ulitimia, kwa hiyo Baha'u'llah ni anasema kweli."
 
Swali la 9: Je siku 1,290 kwenye Dan 12:11-12 zinamaanisha kuwepo kwa Baha'ullah miaka 1,290 baada ya Muhammad kutangaza mpango wake kwa mujibu wa madai ya Wabaha'i kwenye Some Answered Questions uk.43-44?

Jibu: Baha'u'llah alitoa madai haya miaka 19 baada ya Babi, kwa hiyo mtu anaweza kufikiri kuwa watasema ilikuwa miaka 1279. Lakini kwa kuwa muda huo haufiki miaka 1,290, muda wa kuanzia hadi karibu na wakati Muhammad aliposema kuwa alikuwa ni nabii.
 
Swali la 10: Je Yoeli 2:30-32 na Mt 24:29-30 inawaongelea Musa, Kristo, na Muhammad, mafundhisho ya awali yakiwa jua, lakini yakatiwa giza na uharibifu uliotokea baadaye? Hivi ndivyo Wabaha'i wanavyofundisha kwenye Baha'u'llah and the New Era uk.277-278.

Jibu: Hapana. Kristo si tu kwamba atakuja kwenye mawingu halisi, kama Matendo 1:9-11 inavyoonyesha, lakini Mwenyezi Mungu anaweza kuvitia giza jua na mwezi na atafanya hivyo. Huna uhuru wa kukiita kifananishi kitu chochote tu unachopenda kisiwe kweli.
 
Swali la 11: Je giza, tetemeko la ardhi na kupasuka kwa pazia wakati Yesu aliposulubiwa ni maelezo fananishi kwenye Injili na kwamba vitu hivi havikutokea hasa kwa sababu havikuandikwa sehemu nyingine yoyote ile, kama Some Answered Questions uk.37-38 inavyosema?

Jibu: Waandishi watano wanaelezea giza lililotokea Yesu aliposulubiwa.
Thales
(ambaye jina lake huandikwa Thallus pia), alikuwa mwana historia wa Kipalestina asiyekuwa Mkristo ambaye aliandika mwaka 52 BK, chini ya miaka ishirini baada ya kusulubiwa kwa Yesu. Alisema kuwa giza liliandamana na kusulubiwa kwa Yesu.
Phlegon
alikuwa mwandishi wa Ugiriki ya Karia aliyeandika muda mfupi baada ya mwaka 137 BK. Aliandika kuwa katika mwaka wa nne wa Olympiad ya 202 [33 BK] kuwa palikuwa na "kupatwa kwa jua kukubwa zaidi" na kwamba "giza lilishuka saa sita mchana hata nyota zilionekana mbinguni. Kulikuwa na tetemeko kubwa sana Bithynia na vitu vingi sana vilipinduliwa Nikea." (imenukuliwa kutoka The Case for Christ uk.111).
Mwandishi wa kikristo Tertullian, akiandika karibu mwaka 200 BK kwenye On Fasting sura ya 10, pia anasimulia giza lililoambatana na kusulubiwa kwa Yesu.
Mwandishi wa kale Origen (akiandika mwaka 230-254 BK) anasimulia giza lililoifunuka nchi, na makaaburi yaliyofunguka kwenye Against Celsus kitabu cha 2 sura ya 33.
Arnobius
(aliandika mwaka 297-303 BK) kwenye Against the Heathen 54 anasimulia giza wakati wa kifo cha Yesu.
Wengine wanaweza kudai kuwa watu wa sehemu nyingine wangeweza kuandika pia. Jambo hili si la kweli kama giza hili lilikuwepo kwenye sehemu ndogo tu. Pia, giza lisilokuwa la kawaida halikuwa linarekodiwa mara nyingi. Kwa mfano, hesabu zilizofanywa zinaonyesha kuwa jua lilipatwa Desemba 12, 504 KK huko Misri, lakini hakuna kumbukumbu za kihistoria, miongoni mwa Wamisri waliostaarabika sana, au mtu mwingine yoyote kuhusiana na hili. Tazama www.informationblast.com/500s_BC.html kwa habari zaidi.
 
Swali la 12: Je kumkufuru Roho Mtakatifu (Mt 12:31-32) kunamaanisha kukana udhihirisho wa Mungu kama Baha'u'llah na Wabaha'i wanavyofundisha kwenye Some Answered Questions uk.127-128?

Jibu: Hapana, kufanya hivi ni kukwepa swali kwa kudhania kuwa kwa vile Baha'u'llah ni nuru, mstari huu unathibitisha kuwa Baha'u'llah alikuwa nuru. Lakini, hata kwa Yesu, tazama Mathayo 12:31 alisema kuwa wale wanaompinga Yesu watasamehewa, kwa hiyo kumpinga nabii wa Mungu SI kumkufuru Roho Mtakatifu.
 
Swali la 13: Je Mt 16:27 inaongelea juu ya udhihirisho mkubwa wa Baha'u'llah wala si mwisho wa dunia kama ambavyo Wabaha'i wanafundisha kwenye Baha'u'llah and the New Era uk.268-269?

Jibu: Hapana, soma mstari huu kwa makini zaidi. Unasema kuwa Mwana wa Adam atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika wake, na atamlipa kila mtu kwa kadri ya matendo yake. Baha'u'llah hakuwa na malaika ambao mtu yeyote aliweza kuwaona pamoja naye, na Baha'u'llah hakuwalipa ama Baha'i waaminifu waliokimbia au kufa ama Waislam waliowatesa.
 
Swali la 14: Je maneno haya "waitwao ni wengi bali wateule ni wachache" (Mt 22:14) yanaongelea kuhusu viwango vya imani na uhakika kama Wabaha'i wanavyofundusha kwenye Some Answered Questions uk.129-131?

Jibu: Hapana. Kama ukisoma mfano wote kwenye Mathayo 22:1-14, unawagawa watu kwenye makundi mawili: wale wanaoingia kwenye karamu ya harusi na wale wasioingia. Waitwao ni wengi bali wateule ni wachache inaongelea wale walioalikwa kuingia lakini walikataa, na mtu aliyependa kuingia na mavazi yasiyotakiwa.
Kuna somo kwa kila mtu hapa. Huwezi kusoma mstari mmoja tu kwenye Biblia na kupuuzia mambo yaliyoandikwa kabla au baada, na kutegemea kupata tafsiri sahihi.
 
Swali la 15: Je mawingu kwenye Mt 24:30 yanamaanisha kuwa ni vitu vinavyopingana na njia na matakwa ya watu kama Wabaha'i wanavyofundisha kwenye Baha'u'llah and the New Era uk.280-281?

Jibu: Hapana. Si tu kwamba kila mtu atamwona Yesu atakaporudi mawinguni, na watu wa dunia yote wataomboleza kwa ajili yake (Ufunuo 1:7), bali Yesu huyohuyo atarudi kwenye mawingu namna hiyohiyo kabisa kama alivyoondoka kwa mujibu wa Matendo 1:9-11.
 
Swali la 16: Je kurudi kwa Yesu kutoka mbinguni (Yoh 3:13 na Yoh 6:38, 42) ni kifananisho cha kiroho tu na si kitu halisi kama Wabaha'i wanavyofundisha kwenye Some Answered Questions uk.103-105?

Jibu: Hapana. 'Abdu'l-Baha anadai hivi kwa sababu Yohana 3:13f inasema, "...ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani Mwana wa Adamu, aliye mbinguni" wakati Yesu alipokuwepo duniani (uk.103).
Kwanza kabisa, maneno mawili ya mwisho yanatofautiana na maandiko mengine na hayapo kwenye nakala za awali za maandiko ingawa yamo kwenye toleo la baadaye la kitabu cha vifungu vya maandiko ya kusoma kanisani cha Kibyzantine (Byzantine Lectionary). Ni ajabu kujenga mafundisho kwa kutumia andiko moja tu na lisilo na uhakika.
Pili, uungu wake unaweza kuchukuliwa kuwepo mbinguni pia duniani kwa mujibu wa New Geneva Study Bible uk.1665.
Mwisho, na muhimu zaidi, hata kama hukubaliani na tofauti ya maandiko, kwenye mstari huohuo inasema kwamba Yesu alikuja toka mbinguni. Hakuna umuhimu wa kuonyesha kuwa Yesu alikuwa mbinguni kabla ya kufanyika mwili, na kwamba Yesu huyohuyo "alishuka" ni jambo la kweli.
 
Swali la 17: Je Roho wa Kweli kwenye Yoh 16:12-13 ni Baha'u'llah?

Jibu: Hapana, Roho wa Kweli hapa ni roho, si mtu. Ni Roho Mtakatifu yuleyule ambaye Yesu alikuwa anamwongelea kwenye Yohana 14-16. Huwezi kusema kuwa kwenye Yoh 16:12-13 "roho" inamaanisha mtu mmoja, na roho inamaanisha Roho Mtakatifu au kitu kingine kwenye Yohana 14:16-18,25-26; 15:26; 16:5-11; 16:14-15.
 
Swali la 18: je 1 Kor 15:22 si sahihi kwa sababu manabii wote hawakuwahi kufanya dhambi, kama ambavyo Wabaha'i wanafundisha kwenye Some Answered Questions uk.118-121?

Jibu: 1 Korinthians 15:22 inasema kwamba watu wote waliotokana na Adamu wamefanya dhambi, na hii ni pamoja na manabii isipokuwa Yesu. Ni kuelewa vibaya kwa Waislam walio wengi, ambako Wabaha'i wamekurithi kwamba manabii wote hawakuwahi kutenda dhambi. Lakini jambo hili linapelekea kwenye ukinzani wa ajabu. Yona (nabii mwenye kumcha Mungu ambaye Waislam wanamwita 'Yunus') alikimbilia Tarshish na alimezwa na samaki mkubwa. Je hapakuwa na dhambi katika kukimbia? Adam anahesabiwa kuwa nabii na Waislam, na kama hakufanya dhambi kwenye bustani ya Edeni, je maana yako ya dhambi haiishii kuwa msemo usiokuwa na maana? Musa alizuiliwa kuingia kwenye nchi ya ahadi kwa ajili ya kukasirika kwake pale Meriba. Kwa kuwa Mungu alikasirishwa na Musa kwenye Kumbukumbu 3:26, je Mungu anaweza kukasirishwa na mtu ambaye hajafanya dhambi?
Kuna sababu kwa kila mmoja hapa. Wakati mwingine mitazamo ya watu iliyopotoshwa huwalazimisha kuigeuza Biblia ili ilingane na maoni yao.
 
Swali la 19: Je uzima na mauti vilivyoongelewa kwenye 1 Kor 15:51-52 vinamaanisha imani na kutokuamini tu, kama Wabaha'i wanavyofundisha kwenye Baha'u'llah and the New Era uk.270?

Jibu: Hapana, Maandiko yanasema bila kubadilika badilika kuwa kutakuwa na ufufuko wa mwili.
Pamoja na 1 Korinto 15:51-52, tazama:
Dan 12:2
"Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele."
Ufu 20:5
"Hao wafu waliosalia watakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu "
1 Sam 2:6
"Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu."
Zab 49:15
"Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu, atanitoa mkononi mwa kuzimu, maana atanikaribisha."
Zab 22:29
". . . humwinamia wote washukao mavumbini; Naam, yeye asiyeweza kujihuisha nafsi yake . . ."
Zab 23:6
Baada ya ya kusema kuhusu bonde la uvuli wa mauti kwenye Zab 23:4, Daudi anasema, "Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele."
Zab 49:8-9
"(Maana fidia ya nafsi zao ina gharama, wala hana budi kuiacha hata milele;) Ili aishi siku zote asilione kaburi."
Psalm 52:8-9
"Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.Nitakushukuru milele . . . Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako."
Isaya 25:7-8
"Naye katika mlima huu [Mungu] atauharibu uso wa sitara iliyowekwa juu ya watu wote, na utaji ule uliotandwa juu ya mataifa yote. Amemeza mauti hata milele . . ."
Isaya 53:8-10
Baada ya kusema kuwa yeye anayeteseka kwa ajili yetu atauawa na kuzikwa kwenye kaburi la tajiri kwenye mistari ya 8-9, lakini ataona uzao wake kwenye mstari wa 10.
 
Mistari hii imenukuliwa kutoka kwenye Biblia ya Kiswahili, Union Version, 1952.
 
Swali la 20: Je mashahidi wawili kwenye Ufunuo 11, wanaweza kuwa ni Muhammad na 'Ali kama Wabahai's wanavyosema kwenye Some Answered Questions uk.43-61?

Jibu: Hapana kwa sababu kumi na moja zifuatazo:
1.
Ufu 11:3 inasema watatoa unabii kwa siku 1,260. Muhammad alitoa nabii kidogo sana, na 'Ali hakuwahi kufikiriwa kuwa nabii.
2.
Ufu 11:5 inasema kuwa endapo mtu yoyote atajaribu kuwadhuru moto utawaangamiza maadui wao. Muhammad alilishwa sumu (lakini alinusurika kidogo sana), na 'Ali aliuawa na Muislam. Kusudi la 'Ali lilizimwa na Mu'awiyah, na mwanae Husain aliuawa. Hakuwaangamiza maadui, aliuawa nao.
3.
Ufu 11:6 Manabii hawa wawili wanaweza kuzifunga mbingu na kuzuia mvua kunyesha. Muhammad hakuwahi kudai kufanya hivyo, 'Ali naye vivyo hivyo.
4.
Ufu 11:6 Muhammad na 'Ali hawakugeuza maji yawe damu, kama ambavyo wengi wa watu waliowaua, wachoma moto au vinginevyo kuwachinja haikuwa karibu na mito. Kama Salafi Muslim anadai kuwa walifanya mito ya damu hii haina umuhimu kwa sababu Ufu 11:6 inasema waligeuza maji kuwa damu.
5.
Ufu 11:7-8 Muhammad hakuuawa kikatili, na kwa hawa wawili miili yao haikudhalilishwa hadharani.
6.
Ufu 11:8 miili yao haikuwekwa kwenye barabara za mji mkubwa. Ukweli ni kwamba ni watu wachache tu ndio walioweza kumwona 'Ali akifa.
7.
Ufu 11:9 Si kila mtu aliyeikazia macho miili yao iliyokufa wala kuizuilia isizikwe. Kiupekee, Muhammad alizikwa haraka zaidi na wafuasi wake.
8.
Ufu 11:10 Ni nani aliyetuma zawadi nyingi sana baada ya Muhammad na 'Ali kuuawa?
9.
Ufu 11:11 Kuna dhehebu dogo la Waislam linaloitwa Muhammadiyya linalodai kuwa Muhammad hakufa. Wasaba'iyya ni dhehebu dogo la Waislam linalodai kuwa 'Ali hakufa. Ukiachia vikundi vidogo, Waislam hawana sababu ya kusema kuwa ama Muhammad ama 'Ali walifufuliwa.
10.
Ufu 11:12 Waislam hawasemi kuwa Muhammad na 'Ali hawakupaa mawinguni kwenda mbinguni. (Ingawa Wamuhammadiyya na Wasaba'iyya wanaweza wasikubali.)
11.
Ufu 11:13 Hapakuwa na tetemeko kuu la ardhi wakati Muhammad au 'Ali walipoondoka duniani kupitia kwenye mawingu ambayo hayapo.
Wazo kuu si kuona kama inawezekana kutoa maana ya ufananisho ili kuzipinga sababu hizi. Wazo kuu ni kwamba hata kama moja ya sababu hizi haiwezi kupingwa kwa kupewa maana ya ufananisho, unabii huu hauwaongelei wao.
 
Swali la 21: Je maelezo ya Ufu 11:2 kuwa Yerusalem itakanyagwa kwa miezi 42 yanaweza kuwa yanamaanisha muda kati ya Hijra ya Muhammad na kufunuliwa kwa Babi mwaka 1260 BK kama Wabaha'i wanavyofundisha kwenye Some Answered Questions uk.46-47?

Jibu: Hapana. Abdu'l-Baha anasema kuwa kwa vile siku huwa [inadaiwa] kuwa ni mwaka, hii itakuwa miaka 1,260. Lakini fikiria jambo hili: kama siku ilimaanisha siku, je Mungu angeweza kueleza hili kwa njia ambayo wangeikubali? Hapana, hakuna sababu ya kutilia shaka kwamba siku inamaanisha siku hapa.
Zaidi ya hayo, kama miezi 42 ilikuwa ni muda wa mataifa kuukangaga mji mtakatifu, basi tafsiri hii ingemaanisha kuwa Muhammad akiwa Madina na baadaye Muhammad akiwa Maka alikuwemo kwenye muda ambao mji ulikuwa unakanyagwa.
Ukweli ni kwamba Ufu 11:2 inaongelea somo lilelile sawa na Daniel 12:6.
 
Swali la 22: Je Ufu 11:12-13 ilitimizwa na tetemeko la ardhi la Shiraz wakati Babi alipouawa kama Wabaha'i wanavyosema kwenye Some Answered Questions uk.55-56?

Jibu: Hapana. Kwanza kabisa, hakuna ushahdi wowote wa tetemeko la ardhi Shiraz kwa wakati huu. Pili, kama Wabaha'i wanataka kuifanya Ufunuo 11 ionge kuhusu Muhammad na 'Ali, na kisha wanabadilisha somo kuelekea kwa Babi kwenya Ufu 11:12-13, hawawezi kufanikiwa kufanya mambo yote mawili. Ama Babi alikuwa mmoja wa mashahidi wawili au hakuwa mmoja wao. Kama hakuwa, basi kuuchukua mstari huu bila kuangalia muktadha wake ni kuitumia Biblia tofauti na inavyofundisha na kusema kuwa unamwongelea Babi.
 
Swali la 23: Je Muhammad ndie ole wa kwanza kwenye Ufu 11:14-15, na Babi ni wa pili kama Some Answered Questions uk.56-57 inavyosema?

Jibu: Wabaha'i wanaweza kusema kuwa Muhammad ndie ole wa kwanza kama wanataka, lakini sidhani kama wanaweza kusema hivyo kama kwanza watasoma ole wa kwanza ni upi hasa. Ole wa kwanza, baragumu la tano, unaelezewa kiundani sana kwenye Ufunuo 9-12. Nzige wa kuzimu waliotoka kwenye shimo waliwauma watu wasioamini duniani. Waliwatesa kwa miezi 42. Itakuwa ni uchungu mkubwa kwamba watu watataka kufa lakini kifo kitawakimbia.
Ole wa sita, baragumu la sita, ni wakati malaika wanne waliokuwa mto Frati watakapoachilia vikosi vya askari 200,000,000 walioandaliwa kuwaua theluthi ya watu wote ulimwenguni. Je Wabaha'i wanataka kusema kuwa Babi aliwaachilia askari walioua theluthi ya watu wote ulimwenguni?
 
Swali la 24: Je Ufu 12:1 inaongelea mwanamke wa sheria ya Mungu chini ya Muhammad, na mtoto wa kiume ni sheria mpya ya Mungu chini ya Baha'u'llah kama Wabaha'i wanavyofundisha kwenye Some Answered Questions uk.67-72?

Jibu: Hapana. Wabaha'i pamoja na Waislam hawakubali mamlaka ya sasa ya Yesu kwenye Ufunuo 12:10 kwa sababu wanafikiri kuwa maneno yake yaliharibiwa. Hawamshindi mnyama kwa damu ya Mwana Kondoo kwenye Ufunuo 12:11. Endapo tu wangeufahamu umuhimu wa damu ya Mwana Kondoo!
 
Swali la 25: Je nyoka mkubwa sana mwekundu kwenye Ufu 12:3 ulikuwa ni himaya ya uovu ya Umayyad (Abu Bakr, 'Umar, 'Uthman, Mu'awiyah, n.k.) aliyekuwa na milki saba: Rumi kuzunguka Dameski, Uajemi, Arabuni, Misri, Afrika, Uhispania na Uturuki ya Transoxania kama Wabaha'i wanavyofundhisha kwenye Some Answered Questions uk.69-70?

Jibu: Hapana. Wanasema vichwa kumi vilikuwa ni makamanda kumi: kuanzia Abu Sufyan na kuishia na Marwan. Pia wanakiri kuwa kuna zaidi ya watu kumi, lakini kwa vile kuna Mu'awiyah wawili, Yazid watatu, Walid wawili na Marwan wawili, kama unaweza kuhesabu majina bila kurudia, yanafika kumi!
Katika hali halisi, mnyama ni Shetani, kwa sababu Ufunuo 12:10 inamwita mnyama huyo kuwa ni mshtaki wa ndugu zetu. Mnyama anamtafuta Kristo na Wakristo kwa sababu Ufu 12:10 inazungumzia mamlaka ya Kristo wa Mungu. Angalia kuwa mwanamke alitunzwa na Mungu kwa siku 1,260. Sasa angewezaje kutunzwa kama Waumayyad walilikanyaga hekalu kwa siku 1,260?
 
Swali la 26: Je mbingu za kwanza na nchi za kwanza kwenye Ufu 21:1-3 zinamaanisha sheria ya kale na mbingu na nchi mpya sheria mpya chini ya Baha'u'llah, na kutokuwepo kwa bahari kunamaanisha watu wote watamfuata Baha'u'llah kama Wabaha'i wanavyofundisha kwenye Some Answered Questions uk.67-68?

Jibu: Hapana. Ufunuo 21:2 inasema Yerusalem mpya ni bibi harusi wa mumewe (Mungu). Sisi Wakristo ni bibi harusi wa Kristo kwa ufananisho, si kwa baadhi ya sheria. Ufunuo 21:4-5 inasema kwamba Mungu atafuta kila chozi toka kwenye macho yao. Hapakuwa na kifo tena, maombolezo au kilio au maumivu. Unabii huu haukutimia wakati wa uhai wa Baha'u'llah. Unabii huu hautatimia hadi baada ya kurudi kwa Yesu.

Orodha ya Marejeo ya Wabaha'i

America's Challenge : World Peace Through Racial Unity. (kabrasha toka "the Baha'i Faith") (tarehe haijaonyeshwa)
A New Vision of Race Unity : An Abridged Summary of the Baha'i statement on the Oneness of Humanity
. Baha'i National Center. 1997. (Kabrasha)
Baha'is and the Bible
. Stonehaven Press (kabrasha) (tarehe haijaonyeshwa)
Baha'u'llah : God's Messenger to Humanity
. National Spiritual Assembly of the Baha'is of the United States. 1994 (kabrasha)
Barney, Laura Clifford (mtafsiri) 'Abdu'l-Baha Some Answered Questions. Baha'i Publishing Trust. 1981
Beckwith, Francis. Baha'i : Bethany House Publishers. 1985.
Browne, E.G. (translator) New History of the Bab
Browne, E.G. Babis of Persia II
Browne, Edward G. (mtafsiri) A Traveller's Narrative Written to Illustrate the Episode of the Bab, The University Press, 1918 uk.175-243.
Christianity and the Baha'i Faith : Frequently Asked Questions
. Stonehaven Press (kabrasha) (tarehe haijaonyeshwa)
Baha'u'llah : A Brief Introduction to His Life and Work. Baha'i International Community. 1991.
Douglas, J.D. New 20th-Century Encyclopedia of Religious Knowledge 2nd edition. Baker Book House 1991.
Esslemont, J.E. Baha'u'llah and the New Era. Revised Edition. The Baha'i Publishing Committee 1940.
http://bahai-library.com/books/new.era/...
... is 1-12.html
Sobjani, Mouhebat (mkusanyaji) Baha'i : Teachings for the New World Order. Waldorf Enterprises. 1992-2003 (kijitabu cha kurasa 80)
The Baha'i' Faith : Its Principles and History
. Baha'i Publishing Trust. 1996,1997.(kijitabu cha kurasa 29)
The Glory of Christ : A Baha'i Testimony.
Stonehaven Press (kabrasha) (tarehe haijaonyeshwa)
The Light of Unity : The Power of Prayer
. Baha'i Publishing Trust. 1999.
The Promise of World Peace to the Peoples of the World
. A Statement by the Universal House of Justice. (kurasa 12) (tarehe haijaonyeshwa)
The Vision of Race Unity : America's Most Challenging Issue
. A Statement by the National Spiritual Assembly of the Baha'is of the United States. 1991. (kurasa 13)
Tangler, Howard. Who are the Baha'is? (kabrasha) 1993.

Orodha ya Baadhi ya Marejeo ya Uislam

www.AnsweringIslam.org ni tovuti pan asana inayowakilisha na kujadiliana mambo mengi yahusuyo Uislam.
Hasan, Prof. Ahmad. Sunan Abu Dawud : English Translation with Explanatory Notes. Sh. Muhammad Ashraf Publishers, Booksellers & Exporters 1984 (juzuu tatu)
The Holy Qur-an : English translation of the meanings and Commentary
. Imetafsiriwa na 'Abdullah Yusuf 'Ali. Revised and edited by The Presidency of Islamic Researches, IFTA, Call and Guidance. King Fahd Holy Qur-an Printing Complex. (tarehe haijaonyeshwa).
Khan, Dr. Muhammad Muhsin (mtafsiri) The Translation of the Meanings of Sahih Al-Bukhari Arabic-English. Islamic University, Al-Medina Al-Munawwara AL MAKTABAT AL SALAFIAT AL MADINATO AL MONAWART. Tarehe haijaonyeshwa na haina haki miliki.
Sahih Muslim
by Imam Muslim. Imetafsiriwa kuwa Kiingereza na 'Abdul Hamid Siddiqi. International Islamic Publishing House. (tarehe haijaonyeshwa).
 
 

Faharasa ya Vitabu vya Ubaha'i

Baha'u'llah and the New Era

(Maingizo 122)

Baha'u'llah and the New Era - Revised Edition by J.E. Esslemont. Baha'i Publishing Committee 1930, 1940.
 
Baha'u'llah alikuwa akivuta kiko kikubwa cha mashariki (Narguileh au hubble-bubble pipe). Baha'u'llah and the New Era uk.47.
Watu waliokuwa wachache chini ya utawala wa Mirza Yahya walimpinga Baha'u'llah kikatili. Baha'u'llah and the New Era uk.40.
Baha'u'llah alikufa kwa homa 5/29/1892 alipokuwa na umri wa miaka 74. Baha'u'llah and the New Era uk.50.
Baha'u'llah aliacha wosia na agano la mwisho akimtaja Abd'ul Baha kuwa mrithi wake. Baha'u'llah and the New Era uk.50-51.
Baha'u'llah aliongea kama mtu, Baha'u'llah and the New Era uk.54, lakini pia aliongea toka kwenye hali ya uungu." Baha'u'llah and the New Era uk.56.
Wabaha'i wanatumia dhana za Wasufi za kuangamizwa kwenye God and abnegation. Baha'u'llah and the New Era uk.54.
Baha'u'llah alidai kuwa mwokozi wa Kizoroastria aitwaye Shah Bahram, ambaye anaishinda roho ya Ahriman. Baha'u'llah and the New Era uk.57-58.
Kwenye Waraka wa Mbwa mwitu, Baha'u'llah alisema hajawahi kupata muda au nafasi ya kusoma maandiko ya Babi. Baha'u'llah and the New Era uk.60.
'Abdu'l-Baha ('Abbas Effendi) alizaliwa Tihran/Tehran tarehe 23/5/1844, saa ileile Babi alipotangaza misheni yake. Baha'u'llah and the New Era uk.64.
'Abdu'l-Baha alikariri vibao vya Babi. [Jambo hili ni la ajabu kwa sababu baba yake, Baha'u'llah hakuwahi kuvisoma.] Baha'u'llah and the New Era uk.66.
Wasufi kama 'Ali Shawkat Pasha walimtembelea Baha'u'llah. Baha'u'llah and the New Era uk.66.
Wakati Abdu'l Baha alipomrithi Baha'u'llah, baadhi ya Wabaha'i walipinga na kuanzisha vurugu na serikali ya Uturuki. Baha'u'llah and the New Era uk.69.
Mfumo wa matabaka wa India utokanao na kazi, vyeo, weledi n.k. haukuwa sahihi. Baha'u'llah and the New Era uk.70.
Abdu'l Baha pia alikishabikia Kiesperanto. Baha'u'llah and the New Era uk.76. Ingawa hakuna uhakika mkamilifu kuwa hiki ni Kiesperanto. Ibid., uk.202.
23/9/1918, vikosi vinavyopigana kwa kutumia farasi vya Uingereza na India viliiteka Haifa toka kwa Watutuki. Baha'u'llah and the New Era uk.80.
Abdu'l Baha alikuwa akienda kwenye msikiti. Baha'u'llah and the New Era uk.82.
Abdu'l Baha alikufa tarehe 28/11/1921. Baha'u'llah and the New Era uk.82.
Ufafanuzi wenye kuusifia Ubaha'i kupita kiasi ungeweza [kudhaniwa] kuhusisha Waazali na Wabaha'i wa kweli pia. Baha'u'llah and the New Era p.90.
Wabaha'i hawamwabudu Baha'u'llah kama mwanadamu bali utukufu wa Mungu ulijidhihirisha kupitia uanadamu wake. Baha'u'llah and the New Era uk.91.
Wanakubali kwamba Yesu alisema, "Jitwike msalaba wako na unifuate." Baha'u'llah and the New Era uk.92.
Ni muhimu kwa kila mtu kumkubali Baha'u'llah. Baha'u'llah and the New Era uk.93.
Kibao chenye maandishi cha Baha'u'llah kilichoko Tarazat. Baha'u'llah and the New Era uk.94.
Wabaha'i wanataka kuwa marafiki na wapenzi wa Mungu. Baha'u'llah and the New Era uk.95.
Kibao chenye maandishi cha Tajalliyat kimeelezwa. Baha'u'llah and the New Era uk.99.
Wabaha'i hawalazimishi imani yao kwa watu wengine. Baha'u'llah and the New Era uk.101.
[Tofauti na Waislam] Wabaha'i hawaruhusiwi kuwalaani watu wengine. Baha'u'llah and the New Era uk.102.
Wachukulie watu wengine kuwa kama mimea adimu na mizuri. Baha'u'llah and the New Era uk.103.
Usitafutize makosa. Tofauti na hotuba isiyotekelezeka ya Mlimani, Wabaha'i wanatakiwa kutii kila neno la Baha'u'llah na 'Abdu'l Baha. Baha'u'llah and the New Era uk.104.
Angalia makosa yako mwenyewe siyo ya wengine. Baha'u'llah and the New Era uk.105-106.
Wabaha'i wamezuiliwa kutubu dhambi zao kwa mapadri. Baha'u'llah and the New Era uk.106.
Wabaha'i wanatakiwa kuwa waaminifu. Baha'u'llah and the New Era uk.107.
Kujitambua kwa nafsi ya kweli ya ndani. Baha'u'llah and the New Era uk.108.
Maombi ni kuwasiliana na Mungu [na watu waliokufa]. Baha'u'llah and the New Era uk.110.
Watu wanatakiwa kukombolewa toka kwenye utumwa wa nafsi zao wenyewe. Baha'u'llah and the New Era uk.113.
Watu wanahitaji mpatanishi kama Kristo au Baha'u'llah kati yao na Mungu. Baha'u'llah and the New Era uk.114.
Wabaha'i wanatakiwa kuimba maneno ya Mungu kila asubuhi na jioni uk.114.
Chakula kitokanacho na wanyama hakijazuiliwa ila chakula cha siku za baadaye kitakuwa matunda na mboga za majani. Baha'u'llah and the New Era uk.125-126.
Kwa Wabaha'i vileo haviruhusiwi isipokuwa kwa sababu za kiafya. Baha'u'llah and the New Era uk.126.
Kwa Wabaha'i kucheza kamari hakuruhusiwi ila michezo mingine ya kubahatisha inaruhusiwa. Baha'u'llah and the New Era uk.126-127.
Vileo na bangi haviruhusiwi kwa Wabaha'i. Baha'u'llah and the New Era uk.128.
Kupata huduma ya madaktari kumeruhusiwa. Baha'u'llah and the New Era uk.130-131.
Wabaha'i wanaamini uponyaji wa kimiujiza kwa njia ya Roho Mtakatifu. Baha'u'llah and the New Era uk.133-134.
Wabaha'i wanataka zama nzuri hapa duniani siku za usoni. Baha'u'llah and the New Era uk.140.
Nukuu za ajabu za Muhammad. Baha'u'llah and the New Era uk.142-143.
Tafsiri isiyo sahihi ya Muhammad. Baha'u'llah and the New Era uk.145.
Wabaha'i wanatetea kutembelea sehemu za ibada za watu wengine. Baha'u'llah and the New Era uk.148.
Wabaha'i wanaamini kiurahisi kuwa nabii anaweza kutengua mafundisho ya nabii aliyetangulia. Baha'u'llah and the New Era uk.152.
Manabii wote wa Mungu hawawezi kufanya makosa. Baha'u'llah and the New Era uk.153.
Lawb-i-Aqdas (Kitabu cha Aqdas) kimeandikwa kwa ajili ya Wakristo. Baha'u'llah and the New Era uk.154.
Baba ameelezewa. Baha'u'llah and the New Era uk.154, 269.
Baha'u'llah ni nabii wa pekee. Baha'u'llah and the New Era uk.155.
Kwa wakati uliopo tuna maneno machache sana ya manabii waliotangulia. Njia za kurekodi mafundisho ya Muhammad hazitoshelezi kwa namna nyingi. Baha'u'llah and the New Era uk.157.
Baha'u'llah aliandika kuwa 'Abdu'l-Baha alikuwa mrithi wake [lakini si udhihirisho mwingine]. Baha'u'llah and the New Era uk.158.
Kibao chenye maandishi cha Tawi kimeelezwa. Baha'u'llah and the New Era uk.159.
Nyumba ya Haki ya Kimataifa imefafanuliwa kweney Agano la 'Abdu'l-Baha. Baha'u'llah and the New Era uk.160.
Wabaha'i wanaamini uwepo wa uhuru wa kuchagua. Baha'u'llah and the New Era uk.161.
Wabaha'i hawana makuhani wenye kufanya kazi hiyo tu. Jambo hili lilifaa zamani lakini si sasa. Baha'u'llah and the New Era uk.161-163.
Wabaha'i wanaunga mkono viwango vya kodi vinavyoongezeka pamoja na kipato. Baha'u'llah and the New Era uk.174-175.
Wabaha'i wanaamini kuwa kutoza riba kiasi ni sawa. Baha'u'llah and the New Era uk.177.
Utumwa wa mali zinazohamishika au viwanda hauruhusiwi. Baha'u'llah and the New Era uk.178.
Tofauti na Waislam, Wabaha'i wanaruhu mtu yoyote kurithi kiasi chochote wanachotaka. Baha'u'llah and the New Era uk.180.
Usawa wa wanawake na wanaume kwenye kila kitu hata elimu. Baha'u'llah and the New Era uk.180-181.
[Malikia wa] Zenobia na Mariamu Magdalena wameelezwa. Baha'u'llah and the New Era uk.182.
Wanawake wa Kibaha'i kwenye baadhi ya nchi wanavaa mitando ili kuzuia kuzusha vurugu. Baha'u'llah and the New Era uk.184-185.
Nukuu toka kwenye kibao chenye maandishi ya dunia. Baha'u'llah and the New Era uk.186.
Kibao chenye maandishi cha Tajalliyat kimeelezwa. Baha'u'llah and the New Era uk.188.
Maneno ya Kristo kuhusu kugeuza shavu linguine yanazuia kulipiza kisasi. Jamii ina haki ya kujilinda. Baha'u'llah and the New Era uk.189.
Maneno ya Kristo kuhusu kugeuza shavu linguine yanaonyesha kuwa alipinga ulipizaji kiasi. Lakin jamii ina haki ya kujilinda. Baha'u'llah and the New Era uk.189.
Lugha ya Kiesperanto imeelezwa. Baha'u'llah and the New Era uk.200.
Wabaha'i wanaunga mkono lugha ya ulimwengu mzima lakini hawaungi mkono Kiesperanto. Baha'u'llah and the New Era uk.202.
"Kama jumuiya ya kidini, Wabaha'i, kwa kufuata amri ya Baha'u'llah, wameachana kabisa na matumizi ya nguvu za kijeshi kwa ajili ya manufaa yao wenyewe, hata kwa malengo ya ulinzi." Baha'u'llah and the New Era uk.207. [Kinyume chake], mataifa yanaweza kupigana kuzuia uonevu au taifa lipigane lenyewe kwa lenyewe au na taifa lingine. Baha'u'llah and the New Era uk.209.
Ili ndoa iweze kufungwa, ni lazima pawe na makubaliano kwa wazazi wote. Baha'u'llah and the New Era uk.214.
Inasemekana kuwa talaka hutokea mara chache sana miongoni mwa Wabaha'i. Baha'u'llah and the New Era uk.215.
Kalenda ya Kibaha'i ina miezi 19 yenye siku 19. Baha'u'llah and the New Era uk.217-218.
Mbaha'i hawawezi akamshtaki Mbaha'i mwingine mahakamani. Baha'u'llah and the New Era uk.219.
Msaidie maskini bila kujali rangi wala imani ya kidini. Baha'u'llah and the New Era uk.220.
Wanafunga kutoka kuchomoza hadi kuzama kwa jua [kama Waislam] Baha'u'llah and the New Era uk.223.
Hairuhusiwi kueleza kwa watu mambo yote yanayotokea kwa nafsi ya mtu baaada ya kifo. Baha'u'llah and the New Era uk.230.
Ufalme wa Mungu haufungwi na muda na mahali. Ni ulimwengu mwingine kabisa. Baha'u'llah and the New Era uk.231.
Kuumbwa kwa mbingu na jehanamu ni ufananisho tu si vitu halisia. Baha'u'llah and the New Era uk.231.
Wabaha'i wanaweza kuomba kwa ajili ya wafu, na watu wasioamini nao watakuwa waamini baada ya kufa. Baha'u'llah and the New Era uk.232, 236.
Hatupaswi kutafuta kuwasiliana na roho zilizokufa. Baha'u'llah and the New Era uk.235.
Wafu nao wanaweza kuwasaidia watu waliopo hapa. Baha'u'llah and the New Era uk.235.
Maovu hayapo, isipokuwa kama upungufu au kutokuwepo kwa uzuri. Baha'u'llah and the New Era uk.237.
Mwaka 1600 KK Giordano Bruno aliuawa kwa kuchomwa moto, na Galileo akiwa amepiga magoti, alitengua usemi wake wa awali kuhusu jua. Baha'u'llah and the New Era uk.241. Hii siyo habari kamili. Wakati Bruno alifundisha kuwa dunia inalizunguka jua, Kanisa Katoliki lilimteka alipokuwa Venice kwa sababu alikuwa ni muumini wa uwepo wa Mungu kwenye kila kitu (pantheist) aliyepinga ukristo.
Zamenhoff aliteswa kwa kudhaniwa kuwa aliiunda lugha ya Kesperanto. Wanadai kuwa hata Kiesperanto "kilikuwa na wafia dini wake." Baha'u'llah and the New Era uk.242.
Mapigo ya Misri na siku ndefu ya Yoshua si matukio ya kweli. Baha'u'llah and the New Era uk.243.
Wanaamini kuwa "Ukweli hauwezi kuupinga ukweli mwingine." Baha'u'llah and the New Era uk.245.
Mungu anafahamu mambo yote lakini hatuwezi kumfahamu Mungu. Baha'u'llah and the New Era uk.245-246.
Ulimwengu na vitu vilivyomo ndani yake havina mwanzo wa muda kwa mujibu wa Baha'u'llah. Baha'u'llah and the New Era uk.249.
". . . Biblia ya Kiebrania ina maelezo wazi na yasiyokarabatiwa." Hata hivyo ilikuwa na lengo lake siku zilizopita. Baha'u'llah and the New Era uk.249-250.
Adam na Hawa na tunda ni vitu vya ufananisho tu. Baha'u'llah and the New Era uk.252.
Uovu ni kitu chenye kuleta utumwa, ni wazimu unaotenga. Baha'u'llah and the New Era uk.254.
Watu wote ni matunda ya majani ya tawi moja la kweli, maua ya bustani moja. Baha'u'llah and the New Era uk.254.
Wayahudi walimchinja Yesu. Baha'u'llah and the New Era uk.260.
"Kiti cha enzi ambacho [Kristo] anacho ni Kiti cha Enzi cha Milele kutoka hicho Kristo hutawala milele, kiti cha enzi cha mbinguni, kwani vitu vya duniani hupita lakini vitu vya mbinguni havipiti. Alitafsiri na kuzitimiza Sheria za Musa na kuzitimiliza Sheria za Manabii. Neno lake lilizishinda Mashariki na Magharibi. Ufalme wake hauna mwisho. 'Aliwainua Wayahudi waliomkubali . . . Wanyama walikuwa waishi pamoja wanamaanisha watu wa madhehebu na rangi tofauti ambao waliwahi kupigana vita lakini sasa wanatakiwa kuishi kwa upendo wakinywa pamoja Maji ya Uzima yatokayo kwenye Chemchemi ya Milele ya Kristo.'" Baha'u'llah and the New Era uk.260; imenukuliwa kutoka Wisdom of 'Abdu'l-Baha uk.48.
Ni sahihi kuichukulia Isaya 9:2-7 kuwa inamwelezea Kristo (miaka 2,000 iliyopita), lakini ni sahihi zaidi kuichukulia kuwa inamwelezea Baha'u'llah. Baha'u'llah and the New Era uk.261-262.
Toka mawio ya jua inamaanisha kuja kwa Baha'u'llah toka Iran kwenda Palestina. Baha'u'llah and the New Era uk.264.
Isa 11, n.k. inatoa unabii wa tawi lenye kumwelezea 'Abdu'l-Baha. Baha'u'llah and the New Era uk.265.
Mt 26:27; 13:40-43 ilisemwa na Kristo na inamwelezea Baha'u'llah. Baha'u'llah and the New Era uk.268.
Kitabu cha Iqan kimeelezewa. Baha'u'llah and the New Era uk.270, 274, 280.
Kufufuka hakuhusiani kwa vyovyote vile na kufufuliwa kwa mwili halisi. Baha'u'llah and the New Era uk.271, 272.
Matendo 1:11 na Yohana Mbatizaji katika roho ya Eliya vimeelezwa. Baha'u'llah and the New Era uk.272-273.
Luka 21:20-24 na Mathayo 24:4-14 kama maneno yaliyosemwa na Yesu imeelezwa. Baha'u'llah and the New Era p.274-275. Also Mt 24:29-30 uk.277-278.
Jua, mwezi na nyota ni vitu halisi sio vifananishi kwenye siku za mwisho. Baha'u'llah and the New Era uk.278-279.
Mathayo 24 na 25 zimeelezwa. Baha'u'llah and the New Era uk.280-181.
Nukuu fupi sana ya Mal 3:4, bila maelezo. Baha'u'llah and the New Era uk.283-284.
Kumb 18:22 imeelezwa. Baha'u'llah and the New Era uk.285.
Isa 55:10, 11 imeelezwa. Baha'u'llah and the New Era uk.285-286.
Mt 11:4-6 imeelezwa. Baha'u'llah and the New Era uk.286.
Uthibitisho unaodaiwa wa unabii wa jumla. Baha'u'llah and the New Era uk.286.
Surat Haykal imeelezwa, ikiwa na barua kwa wakuu wa serikali. Baha'u'llah and the New Era uk.289.
Unabii wa Ujerumani. Baha'u'llah and the New Era uk.290.
Nchi ya "Ta" kwa kiasi fulani ni Tehran, Iran. Baha'u'llah and the New Era uk.291-292.
Baha'u'llah alitoa unabii wa amani na utulivu Iran. Unabii huu tayari umeishaanza na "ishara si haba kwamba kipindi kizuri zaidi kipo karibu kuja." [kabla ya Khomeini] Baha'u'llah and the New Era uk.292.
Daniel 12:12, 13 imeelezwa. Baha'u'llah and the New Era uk.302.
Miaka 1,335 kutoka Hijra (622 BH) = 1957 BK.
Baha'u'llah and the New Era
uk.303.
Upatanisho Baha'u'llah and the New Era uk.311.
Ondoeni vyote, utumwa wa mali zinazohamishika na viwanda. Baha'u'llah and the New Era uk.312.
Mtoto pekee wa Babi alikufa akiwa mdogo. Baha'u'llah and the New Era uk.315.
Mama wa Shoghi Effendi alikuwa Ziaiyyia Khanum, ambaye alikuwa binti mkubwa wa Abd'ul-Baha, mtoto wa Baha'u'llah. Ziaiah alikuwa ndugu wa Babi. Baha'u'llah and the New Era uk.315.
Unabii wa vita kali zaidi kuliko Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baha'u'llah and the New Era uk.332.

Some Answered Questions - Maingizo 59 ambayo Hayajakamilika

'Abdu'l-Baha (Mtafsiri Laura Clifford Barney) Some Answered Questions. Baha'i Publishing Trust, 1908, 10390, 1954, 1981.
Ubah'ai ni "dini mpya na huru ya ulimwengu wote" Some Answered Questions uk.ix.
Kanuni za msingi zilizosemwa na Baha'u'llah ni kwamba ukweli wa kidini si huru bila mipaka bali ni wenye kutegemea vitu vingine; kwamba ufunuo wa kiungu ni mchakato wenye kuendelea; kwamba dini zote kubwa duniani zimetoka kwa Mungu; na kwamba misheni zao zinaonyesha hatua zinazoendelea za mchakato wa polepole wa jamii ya binadamu." Some Answered Questions uk.xii.
Hakuna kuzaliwa upya kwa nafsi kwenye mwili mwingine. Some Answered Questions uk.xii.
Muhimu zaidi, kitabu [Some Answered Questions] kimepata nafasi muhimu kwenye vitabu vitakatifu vya Imani kikiwa moja ya kazi za 'Abdu'l-Baha matamshi yaliyotolewa na 'Abdu'l-Baha mwenyewe."
Telegrafu zimeelezwa. Some Answered Questions uk.4.
Mungu alihitaji kuwa na ukamilifu wote ili aweze kuumba. Some Answered Questions uk.5.
Hitimisho lisilofuata mantiki. Madhaifu ya ulimwengu usiokuwa na uhakika ni uthibitisho wa ukamilifu wa Mungu. (Hii ni aina ya nadharia ya asili ya uhai/maisha.) Some Answered Questions uk.5.
". . . binadamu, kama akiachwa bila elimu huwa mnyama, . . . lakini kama akielimishwa huwa malaika . . ." Some Answered Questions uk.7.
Tafsiri potofu ya Mwa 1:26. Some Answered Questions uk.8, 9.
Babi ni wa ukoo wa Muhammad. Some Answered Questions uk.13 na maelezo chini ya ukurasa 1 uk.13.
Yusuf, Hajiri na Ishmael wameelezewa. Some Answered Questions uk.13.
Inadai kuwa Socrates alitembelea Syria na kujifunza toka kwa Waisrael mafundisho ya umoja wa Mungu na umilele wa nafsi. Baadaye watu wa Ugiriki walimshutumu kwa kufuru na waliamuru auawe kwa sumu. Some Answered Questions uk.14-15.
Musa alikuwa na kigugumizi, alimuua Mmisri na baada ya hapo akapandishwa cheo kuwa nabii. Some Answered Questions uk.15.
Inadaiwa kuwa wakati wa Yesu, kutofautiana kidogo tu na dini ya Kiyahudi kuliweza kumtia mtu kwenye hatari ya kifo. Some Answered Questions uk.16.
Yesu alitangua sheria za Musa. Some Answered Questions uk.16.
Nukuu ya ajabu inayodaiwa kutoka kwa Yesu. Some Answered Questions uk.17.
Safari za kijeshi za Muhammad mara zote zilikuwa za kujilinda. Some Answered Questions uk.18.
Uongo katika siku zilizoutangulia Uislam: Waarabu waliwaambia wake wao, ukizaa msichana nitakuua. Some Answered Questions uk.19.
Mwanaume anaweza kuchukua wanawake 1,000, na watu wengi walikuwa na wake zaidi ya kumi. [Hesabu hizi zinashangaza kwa sababu watu hawa walikuwa wanawaua watoto wa kike.] Some Answered Questions uk.19.
"Walikuwa kama mtu anayeshika kikombe cha sumu mkononi mwake, ambacho wakati anakaribia kukinywa rafiki yake hukivunja na hivyo humwokoa." Some Answered Questions uk.21.
"Uongo: Muhammad hakuwahi kuwapiga Wakristo." Some Answered Questions uk.21.
Wakristo hawakutakiwa kupigana kwenye majeshi ya Kiislam bali, kama fidia ya jambo hili, walitakiwa kulipa kiasi kidogo cha fedha. Some Answered Questions uk.21.
Madai ya uongo kuwa Muhammad aliugawa mwezi vipande viwili yameelezwa. Some Answered Questions uk.22.
Inadaiwa kuwa kila mtu anasema kuwa dunia ipo katikati ya ulimwengu. Some Answered Questions uk.23.
Kurani inasema kuwa jua linatembea kwenye sehemu fulani tu (Sura 36:37 na kila nyota inatembea kwenye mbingu yake yenyewe. (Sura 36:38). Some Answered Questions uk.23.
"Baha'u'llah alitokea wakati ambapo Himaya ya Uajemi ilikuwa imejawa na usiri ulio kithiri na ujinga na ilipotelea kwenye upofu mkubwa wa kushikilia mambo bila kufikiri." Some Answered Questions uk.27.
"Kwa ufupi, tutasema kuwa Uajemi ilianguka sana kiasi kwamba ikaleta majuto kwa wasafiri wote toka nje kwamba nchi hii iliyokuwa na ufahari ustaarabu mzuri sasa imeoza sana na kuharibika na kuoza sana na kushindwa kwa fedheha na watu wake wamekosa hadhi ya utu wao." Some Answered Questions uk.27.
Baha'u'llah aliandika barua kwa Napoleon III, akitoa unabii kuwa ufalme wake utachukuliwa na utaangamizwa. Ujerumani ilimshinda Napoleon mwaka 1870 BK. Some Answered Questions uk.32-33.
Baha'u'llah alidaiwa na baadhi ya watu kuwa adui wa Shah lakini hakuwa adui kweli wa Shah. Some Answered Questions uk.33.
Nabii nyingi zilidaiwa kutimia kwenye Vibao Vyenye Maandishi vya Wafalme. Some Answered Questions uk.33.
Siyyid Davudi, Msuni kutika Baghdad, aliandika kitabu kidogo kuhusu miujiza ya Baha'u'llah. Some Answered Questions uk.34.
Baha'u'llah hakuwahi kujifunza Kiarabu lakini wanazuoni walisema umahiri wake wa kuzungumza na kushawishi watu kwa Kiarabu havina ulinganifu. Some Answered Questions uk.34.
Maadui wake walidaiwa kupanga kumsulubisha na kumwangamiza Baha'u'llah. Some Answered Questions uk.35.
Giza na tetemeko la ardhi na kupasuliwa kwa pazia wakati Yesu aliposulubiwa vimeelezwa. Hata hivyo, vitu hivi havikuandikwa sehemu nyingine yoyote zaidi, ama ni vifananishi tu na havikutokea kikweli. Some Answered Questions uk.37-38.
Hesabu 14:34 imeelezewa (mwaka mmoja wa kuzunguka jangwani kwa kila moja ya siku 40 ambazo waliipeleleza Kanani) kuthibitisha kuwa siku moja ni sawa na mwaka mmoja kwenye Daniel. Some Answered Questions uk.40.
Majuma 70 yameelezwa kwenye Daniel 9:29. Some Answered Questions uk.40-43.
Dan 12:6 inamuongelea Babi, kwa kuwa alitokea siku 1,260 baada ya Hijra ya Muhammad. Some Answered Questions uk.42.
Siku (miaka) 1,290 za Baha'ullah zimeelezwa baada ya Muhammad. Some Answered Questions uk.43-44.
Baba ameelezwa. Some Answered Questions uk.43.
Kwenye Ufunuo 11, Yerusalemu imeelezwa kuwa itakanyagwa na kwa muda wa miezi 42 ikiwa inaonyesha muda kati ya Hijra ya Muhammad na kufunuliwa kwa Babi mwaka 1260 BK. Some Answered Questions uk.46-47.
Ufunuo12 imeelezwa. Some Answered Questions uk.67-72.
Vitu kama vile kufunga, maombi, ibada, ndoa na talaka, kukomesha utumwa, fidia ya mauaji, uizi, majeraha, vinaongelea vitu vya kimwili na na inabadilika kwenye kila mzunguko wa kinabii kwa mujibu wa wakati. Some Answered Questions uk.48.
Maelezo chanya ya sheira na mafundisho vya Muhammad, na ufafanuzi na maoni vya 'Ali. Some Answered Questions uk.50.
Maji yanabadilika kuwa damu kwenye Ufunuo 11 inamaanisha kuwa unabii wa Muhammad na nguvu ya 'Ali vilikuwa kama unabii wa Musa na nguvu ya Yoshua. Some Answered Questions uk.50.
Mnyama aliyewavamia manabii wawili kwenye Ufunuo 11 ni Ufalme wa [Muislam] Omayyad/Umayyad aliyepinga dini ya Muhammad na uhalisi wa 'Ali. [Wamayyad ni maimamu wa kwanza au Abu Bakr, 'Umar, Mu'awiyah, Yezid, n.k.] Some Answered Questions uk.51.
Baada ya kifo cha kishahidi cha Babi kulikuwa na tetemeko la ardhi huko Shiraz na watu wengi waliuawa, na palikuwa na mapigo mengi makubwa. Jambo hili linadaiwa kutimiza Ufunuo Rev 11:12-13. Some Answered Questions uk.55-56.
Muhammad ndiye ole wa kwanza kwenye Ufu 11:14-15 na Babi ole wa pili. Some Answered Questions uk.56-57.
Wakati wa Musa, kulikuwa na machifu wa makabila 12, wakati wa Kristo kulikuwa na mitume 12, na wakati wa Muhammad kulikuwa na maimamu 12. Namba 24 ni mara mbili ya 12 kwa Baha'u'llah. Some Answered Questions uk.57-58.
Isaya 11 imeelezwa. Some Answered Questions uk.62-66.
Yesu alijiita Mwana wa Mungu. Some Answered Questions uk.63.
Isa 11:1-10 inamwongelea Baha'u'llah. Some Answered Questions uk.62-63.
Simba kukaa pamoja na ndama wa kondoo ilitimia wakati wa Baha'u'llah ambapo watu wa dini mbalimbali walishirikiana pamoja. Some Answered Questions uk.65.
Tawi ni Baha'u'llah. Some Answered Questions uk.65.
Yerusalemu mpya inatafsiriwa kuwa ni Sheria ya Mungu. Some Answered Questions uk.68.
Jua na mwezi vinatafsiriwa kuwa ni himaya za Ottoman na uajemi. Some Answered Questions uk.68.
Vichwa saba vya shetani ni kanda nne zilizodhibitiwa na Wamayyad. Pembe kumi ni majina tofauti ya watawala wa Kimayyad. Hata kama kuna zaidi ya watawala kumi, wengi wao walikuwa na majina yanayofanana. Some Answered Questions uk.69-70.
Mfanano wa alama za nyota. Some Answered Questions uk.76.
Mfanano wa kipepeo (?) mara nyingi huvutwa kwenda kwenye mwanga. Some Answered Questions uk.77.
Roho Mtakatifu akishuka kama hua, na Mungu akionekana kama nguzo ya moto, haviwezi kuwa vitu halisia. Some Answered Questions uk.85.

Utukufu wa Yesu

(Maingizo 50)

"Kuna Yesu mmoja tu. Huyu amekuwa mkweli wakati wote, na atakuwa hivyo siku zote. Kristo ni wa pekee, habadiliki, hagawanyiki, bila kifani, na halinganishwi - 'Alfa na Omega (Ufu 1:8). Hatuwezi kuuelezea Utukufu wake kikamilifu wala kuzidisha umuhimu wake. Ni kupitia kwake tu tunaweza kumfikia Mungu. Kujua jambo hili ni kitu cha maana sana katika dini ya Kibaha'i."
 
Maoni ya kitheolojia (tuliyoyachunguza hapa) yanakazia uungu wake kama 'roho itiayo uhai', kama mmoja wa Utatu Mtakatifu, kama Mungu aliyefanyika mwili, na kama Mwana wa Mungu. Hebu tuangalie kila moja ya vipengele hivi kwa mujibu wa Biblia.
 
"Kama kielelezi cha asili ya Mungu, Kristo anaitwa 'Neno' (Logos): 'Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu (Yohana 1:1, mikazo imeongezewa). Mstari huu unaonyesha kuwa kwa namna moja Kristo aliyokuwepo kabla ya kuja hapa duniani ni sawa sawa na Mungu ('alikuwa' Mungu) na kwa namna nyingine alikuwa tofauti (alikuwako 'kwa' Mungu). Vifungu vingi kama hiki vya Biblia vinaelezea ukweli kinza huu: vingine vinamwongelea Kristo na Mungu kwa kubadilishana, wakati vingine vinawatofautisha."
 
"Ukweli wa Mungu kufanyika mwili, kama ulivyo ule wa Utatu Mtakatifu, unakuwa wazi kupitia mafundisho ya Biblia kwamba tunaiona 'sura ya Mungu asiyeonekana' (Kol. 1:15) ikiwa imeakisiwa 'kama kwenye kioo' (II Kor 3:18). Kama kioo kikamilifu cha Uhalisi wa Mungu, nafsi ya kibinadamu ya Kristo ilihusishwa na mwili wakati alipokuwa hapa duniani. Mungu kufanyika mwili kunaonyesha ukamilifu wa vigezo vya uungu.
 
"Uana wa Mungu wa Kristo haukuanza na kuzaliwa kwake na bikira. Ni asili ya sura yake kiroho ambayo, kwa mujibu wa Paulo, ilikuwepo 'kabla ya vitu vyote' na inaendelea kuwa nguvu ya uumbaji kwa njia yake 'vitu vyote hushikamanishwa' (Kol 1:17).
 
"Kutokana na mtazamo huu, kuna Kristo mmoja tu. Hapawezi kuwa na Kriso wawili, au kumi; Kristo hawezi kuwa na mtu wa kumtangulia, kumfuata, kumbadili au kuchukua nafasi yake. Yeye ni njia pekee kupitia hiyo tunaweza kumjua Mungu: 'Mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi' (Yoh 14:6).
 
"Wabaha'i wanaamini kuwa uwepo huu huu wa Mungu [Kristo] umetokea, kweye nyakati zetu, kama Baha'u'llah, mwanzilishi na mtu muhimu wa dini ya Kibaha'i, anayetimiza ahadi ya Biblia juu ya kurudi kwa Kristo. (Kabrasha la Utukufu wa Kristo)
 
'Yesu, Roho wa Mungu . . . amedhirika kwenu, mara nyingine tena, kupitia kwangu (Gleanings from the Writings of Baha'u'llah 101).
 
Kijikaratasi kiitwacho "Christianity and the Baha'i Faith" kilichoandikwa na Stonehaven Press 1997 kinasema "Kwa mtazamo huu, Baha'u'llah ni Yesu kwa namna zote zinazohusika."

For more info contact www.MuslimHope.com